Special Diploma UDOM, Aibu kwa serikali

Kuna wakati nishakuwa mwalimu wa hayo masomo katika level ya o_level. Najua mwalimu wa masomo ya Hisabati, Physics na Chemistry anatakiwa awe vipi ili kumfanya mwanafunzi wake aelewe. Nilikwenda pale Udom mwezi uliopita kwa shughuli za kikazi nikabahatika kukutana na hawa vijana na nikabahatika kuangalia mtaala wanaotumia. Kwanza ukweli ni kwamba pale mostly ni wale wenye div 3 ambao hawakubahatika kupata fursa ya kwenda kidato cha 5.
Ninachokiamini hawa vijana ili kuwa competent kulikuwa na haja ya kupitia elimu ya advance kwa masomo husika, Nadhani nisingekuwa na haya maoni iwapo wengekuwa wanachukuliwa vijana waliohitimu kidato cha 6 kwa PCM wakakosa nafasi ya kuendelea na chuo.

Naamini kwa wale wanaosoma degree pale UDOM wanaweza kuelezea zaidi ni aina gani ya vijana tunawatengeneza pale.
 
Nakubaliana na hili wazo. Ungepigwa msaragambo wa watu wote ambao hawajafanya kozi za ualimu lakini wamefanya masomo ya sayansi na kufaulu vizuri katika level yoyote yaani O-level, advance au hata vyuoni kwao wawekewe utaratibu maaalumu waende vyuo kwa refresh course wangesaidia. Tatizo hata motivation kwenye ualimu ipo chini sana. serikali anapaswa kujitadhimini. Ila swala la mtu kuingia na passmark ndogo kiukwel huwa halitadhimini utendai wake wa kazi,. Nakumbuka nikiwa chuoni nasoma degree ya kwanza ya ualimu tulikuwa walimu wengi wa primary tunaojiendeleza kuliko wa sekondary ambao wengi wao sifa wanazo ila wamechoka. Kiukweli taaluma inataka bidii binafsi na sio kujivunia ulichopata level za chini. Walimu wa primary wapo wanajiendeleza wengine wan Masters, PhD mpaka maprofesa like hao hao wa sekondary.
 


wana old moshi xul kumbe tupo wengi humu....hahahah akina mzee omary wa DH
 
Samahani mkuu mie mwenyewe nilipata dv four form six nikiwa naufaulu wa advanced mathematics tu ambayo nilipata E lakini cjawahi bahatika kupata nafasi ya kujiunga na chuo cha elimu cha serikali sijui waweza nisaidia maana kidato cha nne nilifaulu vizuri sana sema a level mambo yaliingiliana nikaharibu
 

Linatengenezwa jipu la koo
 
Acha uongo vijana waliochaguliwa ni wale walioshindwa kwenda advance na viGPA zao z mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…