Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Hiki kisa ni kweli kilitokea. Kuna baba mmoja alikwenda kusoma Ujerumani. Akiwa kule alipata mpenzi wa kizungu. Baada ya muda walibahatika kupata mtoto wa kiume. Mama hakuwa tayari kuishi Tanzania na mzee alikunywa maji ya bendera. Hivyo baada ya kumaliza masomo mzee alirudi nyumbani na kukabidhiwa ofisi na nyumba ya serikali. Yule Baba alioa na maisha yakasonga.
Kule Ujerumani mtoto alilelewa na mama yake. Alidekezwa kupita maelezo kwakua alikuwa ndiyo kila kitu kwa mama yake. Yeye ndiye aliamua wale nini, hakuambiwa hapana kila alichotaka kwa mama yake ilikuwa ni ndiyo. Mtoto hakusikiliza walimu, ilikuwa shida sana kupokea neno hapana kutoka kwa mwalimu. Alikuwa mkaidi sana. Kufika umri wa miaka saba mtoto walimu walimnawa mikono. Social Services walimwambia mama yake mtoto anatafutiwa nafasi kwenye shule ya watoto watukutu.
Mama alimwarifu baba yake huku Tanzania. Mtoto alipandishwa ndege Baba yake alimpokea airport. Wamefika nyumbani kwanza aliweza kuongea na Baba yake tu Kijerumani. Ilibidi ajifunze Kiswahili kwani enzi hizo hakukuwa na hata English medium.
Baba yake alimpa ratiba ya kazi zake za kufanya.
1. Asubuhi unatandika kitanda chako na kukunja pyajama kabla hujakwenda shule.
2. Wewe ndiye muoshaji vyombo wa nyumba baada ya watu kumaliza kula.
3. Jioni ukitoka shule unamwagilia bustani ya mboga, walilima nyanya, mchicha nk
4. Saa 12.00 uwe umeshaoga na uko mezani na madaftari yako tayari kwa Baba kukagu kazi za shule.
Jumamosi unasafisha chumba chako na kufua nguo zako kabla ya kusaidia kazi nyingine kama kuosha gari nk. Baada yapo aliruhusiwa kucheza mpira na wstoto wenzake.
Siku za kwanza kulikuwa na bakora nyingi na mtoto akililia kurudi kwa mama yake. Mzee alimjibu Ujerumani utoiona ukimaliza form six na pass ya university entry.
Yule mtoto alimaliza na div one form six. Alirudi kwa mama yake akiwa mwanaume mwenye busara mama alitokwa na machozi.
Baba yake aliweka muda mwingi kwa malezi ya kijana huyu, Baba aliacha kunywa pombe na kila siku alimfundisha mwanae mpaka elimu ya juu ndiyo alikodisha mwakimu weekends.