Spain ni nchi nzuri kwa kufanya biashara

Ngondonyoni

Senior Member
Feb 16, 2016
120
74
Ndugu wanaJF,

Nipo Spain kwa muda. Ni nchi nzuri na Kubwa ndani ya Ulaya. Watanzania wengi wanaijua sababu ya mchezo wa mpira, Real Madrid, Barcelona FC na kadhalika. Lakini watanzania wengi pia hawajui ni nchi pia nzuri kwa kufanya biashara kama unajipanga vizuri.

Hapa nakutana na wasenegal wengi, waghana, wacameroon, wacongo waafrika wa magharibi kibao na siyo wote wakimbizi wa uchumi ila ni watafutaji wa biashara. Wote tunajua umaarufu wa vigae (tiles) wa Spain. Pía vyakula vyao kama wine, tapas, chorizo.... Lakini si wengi wanajua pia kwamba unaweza kupata spare parts zilizotumika na used na new machinery, na mambo mengi wabongo tumezoea kutafuta Uingereza Uholanzi au Ujerumani.

Nafasi za biashara zipo kwa wale wanaotaka. Mimi binafsi natafuta huko na huko na nawakaribisha mniulizie chochote kuhusu Spain. Ukitafuta makampuni au bidhaa, ukitafuta kujua zaidi kuhusu import na export toka Spain... naelewa lugha na sheria za hapa. Na kama unakuwa serious kibiashara tutaelewana pia.

Hasta luego
 
Naomba unicheki whatsapp bas boss +255786623636
 
ghalama ya kwenda na kurudi, kama mtu ameamua kusurvey.
Una source yoyote kwa mtu anaependa kujifunza Kihispaniola kwa wepesi.
Natamani kujua mengi pia...
Vipi kuhusu mazao ya kilimo/Asali huko
 
Gharama inategemea msimu na kampuni. Bei nzuri tumia Turkish airlines, binafsi napenda pía Emirates na Qatar sababu ukitafuta vizuri unaweza kupata ofa za usd 700-850
Kuhusu lugha kwa kweli saizi sijui lakini jana nimeisoma thread moja hapa ya kozi za lugha ya hispanola
Mazao ya kilimo wanalima sana Ngano na mahindi, matunda ya aina yote mpaka mengine ya kitropiki kama ndizi na parachichi, mboga.... asalí ya hapa ni nzuri sana. Lakini wanatafuta nta ya Africa pia
 
Naomba ufafanuzi kuhusu import na export, sanasana sheria zao. Pia masoko mfano kwa bidhaa kutoka Tanzania
 
Hakuna shida. Kutoka Tanzania tunaweza kuleta mazao, nta, sisal, alizeti, crustaceans, nk.
Hizo alizeti zinatakiwa package za kg ngapi ngapi na usafirishaji ukoje pia naomba kuuliza vitu vya culture kama viatu na vikapu vinaweza kupata soko huko?
 
Back
Top Bottom