Sorry for disturbing..

Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,661
2,931
Mwaka 2015 nilihamishiwa kampuni B kutoka kampuni A zilizokuwa zinamilikiwa na mzawa wa Tanzania hapa hapa, nilitolewa A kuja B baada ya B kuwa na upungufu wa wafanyakazi katika fani yangu ya IT. kila siku nilitakiwa kufika kazini saa moja nanusu asubuhi tayari kwa majukumu ya siku nzima, nilijiwekea ka utaratibu wa kutoka nyumbani nilipokuwa ninaishi ilala bungoni saa kumi na mbili na robo na kwanza kabla ya kufika job nilitulia kwenye kijiwe kimoja cha kahawa maeneo ya posta karibu na Haidar plaza, kutoka hapo nilifululiza mpaka imalaseko supermarket kwa ajili kujipatia vitafunwa vya asubuhi (sijui kama hadi leo wanauza) siku moja wakati ninafika pale imaleseko tayari kwa kupambana na foleni isiyo rasmi kufikia vitafunwa gafla nikahisi kitu laini kinanigusa bega, kuangalia ni binti mmoja mrembo haswa akaanza "sorry for disturbing... siwezi ku fight kufika kule can you buy me...."? wazo la kwanza nililokuwa nalo nilijuwa huyu dada ana nia ya kunidhalilisha mbele ya umati wa watu, lakini baada ya kumuangalia kwa jicho kali nikagundua udhaifu wa kimaumbile aliokuwa nao, kwamba anajiona yupo in very high status na hio hakuzoe mambo ya foleni na misuguano kama ile, nikakubali kumsaidia, hatimae zamu yangu ikafika na nikapata huduma ya kwangu na kwake pia akanishukuru sana sana na hapo ndio nikajua kweli inawezekana anatoka katika familia ya wenye nazo kutokana na kivazi alichovyaa handbag aliyobeba saa na mambo kama hayo akanishukuru na tukatoka nje, kila mtu na safari yake, wiki tatu baadae jumapili moja nikiwa maeneo ya coco beach gafla nikasikia sauti ya mtu akiniita kakaa, kakaa kugeuka nikakutana na mtoto labda wa 7yrs old hivi akaniambia unaitwa mle kwenye gari lile pale, nikashangaa sana, kwenda kufika ni gari BMW i kuchungulia.... uso kwa uso na mdada mmoja matata sana akiwa amevaa tshirt nyeupe na short ya jeans nikashangaa maana sikuwa ninamjua ingawa sura yake haikuwa ngeni, alivyoniona mshangao wangu akacheka sana "mimi ni yule dada ulienisaidia kupata vitafunwa pale imalaseko" memory ikarudi na sasa tukaanza kupiga story za hapa na pale, mwisho wa siku akafunga gari na tukaanza kusogea kutafuta viti kivulini na kukaa, akaniambia nimekuja hapa special kuna birthday ya rafiki yangu itafanyika hapa na kama hutojali naomba nikualike rasmi kama rafiki yangu, nikakataa, maana nilikuwa na program zangu za mapumziko na siku hio sikutaka usumbufu hata kidogo. Nikampa kampani hadi group la wasichana 8 na mwanaume 1 lilipofika nao wakiwa na magari makali nikamuaga na kuondoka kuwaacha wanedelee na ratiba zao. wakati nimekaa sehemu peke yangu nikijivinjari kwa crisp za mihogo na cocacola gafla nilizungukwa na kundi la wanaume 4 mmoja akauvuta siti karibu yangu kisha akatoa kisu kirefu taratibu akakizungusha mpaka mpaka kwenye mbavu, nikahisi maumivu kwa mbali lakini siku panic kabisa, kisha mmoja kati ya wale wengine waliobaki ki muonekano alikuwa ndio boss waoambae akaanza kutoa hutuba "kaka sisi hatuna kesi na wewe, ila yule dada ni mchumba wangu ukiendelea nakuua na sitanii" wakaondoka eneo lile kwa speed nikashangaa sana. Nilichogundua baadae yule dada alikuwa ni binti wa waziri flani serikalini lakini alikuja kuolewa na jambazi ambapo baadae alikuja kuuwawa kwenye tukio moja la ujambazi arusha na hadi ninaweka uzi huu dada amehama nchi kwa aibu. wakati waTz wakimkumbuka Baba wa taifa, mimi ninakumbukumbu ya tukio lile la Alhamis ya tarehe 15 october 2015
 
siku hizi JF kuna competition ya kuwa wa mwanzo ku comment kwa maneno mawili matatu, tumejaaliwa na ugeni huu.
 
Pole mkuu, kheri walikuachia uhai wako.
 
Wakati naanza kusoma nilijua mwishoni itaishia kama zali LA mentali......! Kumbe Hamna.....

Nimepoteza muda....
 
Huyo dada yuko wapi huko nje nimtafute Mimi, maana kitambo cjapa misukosuko hadi mwili unawasha...au mdada mwingine aliyeolewa na lijambazi kama wamfahamu, nina hasira sana na majambazi wasiojulikana
 
ahahahaha kweli nimeamini hapa wabongo hatutaki shulee
 
Back
Top Bottom