Sophia Simba - Mwanamama anayenishangaza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sophia Simba - Mwanamama anayenishangaza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Mar 10, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana jioni kulikuwa na mjadala uliokuwa unaendeshwa na BBC Swahili, miongoni mwa wachangiaji alikuwa ni Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto Mh Sophia Simba... Nilishangaa kwa jinsi alivyokuwa hawezi kujenga hoja zake na jinsi ambavyo anaonekana hajui sawa sawa wajibu na majukumu ya wizara yake.

  Kilichonishangaza zaidi ni idadi ya vyeo alivyonavyo huyu mwanasiasa machachari - yeye ndiye mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa CCM, pia ni mbunge wa kuteuliwa... naamini nafasi zote hizi zilishindaniwa na watu wengine na yeye akaibuka kidedea, lakini ajabu yake ni kwamba katika wazungumzaji wa jana yeye ndiye alionekana asiyena uwezo wa kujenga hoja kuliko wachangiaje wote (hata yule dada wa kijijini alionekana kuzijua changamoto za wizara ya wanawake kuliko waziri mwenyewe).

  Swali langu je ina maana kwenye umoja wa akina mama wa CCM hakuna mwanamke aliyeonyesha nia ya kugombea nafasi aliyonayo Sophia mwenye uwezo kuliko yeye? Je na katika wanasiasa wanawake wa CCM hakuna anayeweza kuongoza wizara ya Jinsia Wanawake na Watoto vizuri zaidi ya Sophia Simba?

  Ni aibu kwa Tanzania kuwa na mawaziri wenye uwezo duni wa kujenga hoja kama ule ulioonyeshwa na Waziri Sophia jana.. ni aibu!
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wapo, ila tatizo lililopo ni je ni wanamtandao? Hivi umewahi kujiuliza ni kwanini Kikwete kawa Rais lakini Magufuli kawa waziri. Au ni kwanini Sita siyo Spika wa bunge japo uwezo wake ni mkubwa kuliko ana makinda?
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  nilishawahi kusikia aligawa ''uchumi'' kwa muheshimiwa!! aagh nilikuwa napita tu..nitarudi baadae
   
 4. m

  matawi JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tanzania hata ngombe anaweza kuwa kiongozi ili mradi Rosti tamu aamue
   
Loading...