Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,670
1d6bb09df98228f1e8166e9fcc51ab57.jpg




Nimeiona kwny JF twitter:

=========
UPDATES:

Waliofukuzwa Uanachama wa CCM kuanzia leo:
1. Sophia Simba
2. Ramadhan Madabida
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na
5. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga



IMG_4028.jpg

IMG_4029.jpg

IMG_4030.jpg

IMG_4031.jpg

IMG_4032.jpg


=====
KWA UFUPI:

Machi 11, 2017 - Dodoma

Habari kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.

Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavangu, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.

Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Leizer amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Mollel, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Awadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.

Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.

IMG_4036.JPG

IMG_4037.JPG

IMG_4034.JPG

IMG_4035.JPG
 
Mabadiliko ndani ya CCM ni lazima yatokee khasa baada ya miaka 40 tangu kuundwa kwake.

Nafasi katika halmashauri kuu zimepunguzwa kutoka 388 hadi 158, wakati nafasi katika kamati kuu zimepunguzwa kutoka 34 hadi 24.

Mabadiliko kama haya au kwa kiingereza "reforms " ni muhimu, khasa ukiwa na kiongozi anaejali kupunguza matumizi na kuleta nidhamu na uwajibikaji hata katika chama chake.

Pia mabadiliko kama haya kutakiwezesha chama cha CCM kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kuondokana na wanachama wasohitajika lakini wanaolipwa fedha za mishahara bure.

Ila kumvua uanachama Sophia Simba ni uamuzi sahihi na balozi Nchimbi kukaa nje akiwa balozi ni adhabu tosha.

Kwa umri alokuwa nao mama Sophia Simba alipaswa kuchunga kauli zake na ile kauli yake aloitoa kwenye harakati za kuchuja wagombea uraisi mwaka 2015 ya kwamba, yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona mgombea mwenye sifa kama Edward Lowasa akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba wote wanaomchafua Edward Lowasa ni wajinga na wapumbavu.

Hii ni sawa na mtu kutapika kabisa halafu baadae anakuja kula matapishi yake mwenyewe.
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.
 
Back
Top Bottom