Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,050
- 12,966
Salam.
Nimetembelea Mwanza hivi karbuni baada ya miaka michache kupita. Last time nilifika pale 5 years ago.
Mji umebadilika sana, miundombinu imeboresheka na mingine kuongezeka mfano Rock city mall, iko bomba kuliko mlimani city, nimeona pia barabara ya kwenda uwanja wa ndege ikipanuliwa ziwe mbili.
Tatizo moja nililoliona Mwanza itakuja kua kama Dar very soon, tatizo lake ina njia tatu za kuingia na kutoka, ile njia ya Musoma, njia ya Nyegezi(Shinyanga) na njia ya kwenda uwanja wa ndege, hii haiendi mbali zaidi ya Igombe.
Mji unapanuka na kuongeza idadi ya watu miundombinu ikiwa ile ile, mvua ikinyesha kidogo mafuriko mjini kati kama vile Jangwani, mji unakua haupitiki, mfumo wa maji taka ni hovyo.
Nashangaa kwa nini serikali haitaki kuliona hilo mapema ihamishe ofisi zake nje ya mji ili kuja kuondoa usumbufu baadae.
Mwanza watu bado wana utamaduni wa kula nyumbani, migahawa ya maana ni michache sana, unaweza kutoka uwanja wa ndege kupata mgahawa wa maana hadi mjini, fast food and take away centres bado chache sana. Bado u-local ni mwingi sana maana baskeli bado zinatapakaa city centre za wauza maziwa nk.
Kwa ujumla safari yangu ya Mwanza ilikua nzuri sana ilikua ya kupendeza na ilikua ya mafanikio. Ntarudi kula sato, by the way mimi ni mlake zone.