Songwe: Kimondo SC yashushwa madaraja mawili na faini ya milioni 2

mjwanga petro

New Member
Sep 22, 2014
4
8
TIMU ya Kimondo Super SC imeshushwa madaraja mawili (hadi ligi ya Mkoa) na matokeo ya mechi zake zote ilizocheza katika kundi B ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yamefutwa kwa kushindwa kufika uwanjani kucheza mechi dhidi ya JKT Mlale bila sababu za msingi.

Mechi hiyo namba 47 ilitakiwa kuchezwa Januari 28 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea lakini Kimondo haikutokea uwanjani wala kutoa taarifa yoyote hadi Februari 1 ilipotuma taarifa Bodi ya Ligi (TPLB) na kutoa sababu ambazo hazikukubaliwa na Kamati.

Pia Kimondo imetozwa faini ya Sh 2 milioni ambapo kati ya hizo Sh 1 milioni itachukuliwa na TPLB wakati Sh 1 milioni italipwa JKT Mlale. Adhabu dhidi ya Kimondo ni utekelezaji wa Kanuni ya 28(1) na (2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
 
Back
Top Bottom