Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,227
- 157,421
MAMLAKA HUSIKA SHUGHULIKIENI TATIZO HILI LA SONGWE AIRPORT - MBEYA.
Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 12 mwezi Disemba mwaka jana 2016 tukiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo tulikuwa tunasubiri kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania kwenda Mbeya, mjadala mkubwa na abiria wenzangu tuliokuwa pale ulikuwa ni kuhofia namna ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe yaani Songwe Airport uliopo mkoani Mbeya. Nakumbuka tulikuwa tunasafiri kwa ndege mpya ya serikali kati ya zile mbili zilizokuwa zimetoka kuzinduliwa na Raisi Magufuli, ndege aina ya "Bombadier". Na nakumbuka ilikuwa ndo siku yangu ya kwanza kuzipanda ndege hizi za aina hii tangu zinunuliwe na serikali yetu.
Ninakumbuka siku hiyo aliyeuanzisha mjadala ule alikuwa ni mmoja wa abiria mwenzangu ambaye nahisi kama alikuwa ni Mchewa wa nchini Malawi (kutokana na ongea yake), huyu Mmalawi aliyekuwa anaongea Kiswahili kwa shida alikuwa anatuambia kuwa kuna siku ndege aliyokuwa ameipanda kutoka Dar es Salaam ilisumbuka sana kutua pale Songwe Airport kwasababu ya ukungu mzito uliowafanya rubani na wasaidizi wake kushindwa kuona vyema. Ukungu wenye kuleta giza ilikuwa shida.....
Kwasababu siku ile ya tarehe 12/12/2016 kulikuwa na hali ya kiukungukungu na kimvua kwa mbali jijini Dar es Salaam, basi wengi wa abiria tukawa tumejawa na wasiwasi kuwa kuna uwezekano Mbeya kukawa na "mshikemshike" wakati wa kutua. Namshukuru Mungu kuwa tuliondoka Dar es Salaam na hiyo ndege aina ya "Bombadier" na kusafiri salama na baada ya muda tukatua Uwanja wa Songwe mkoani Mbeya bila shida, tulikukuta Mbeya kukiwa kukavu bila ukungu wa aina yoyote. Tukamshukuru Mungu!!
Siku chache baadaye (sikumbuki ilikuwa ni tarehe ngapi), nikapata habari kuwa Ndege toka Dar es Salaam imeshindwa kutua Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa kile kilichoitwa waongoza ndege kushindwa kumudu ukungu uliokuwepo uwanjano siku hiyo, hivyo ikalazimika isitue Songwe na kurudi Dar es Salaam ikiwa na abiria wote waliokuwemo kwenye hiyo ndege. Nasikia wakaja kusafiri siku nyingine......
Asubuhi hii ya leo ninaambiwa kuwa ndege mali ya kampuni ya FastJet iliyokuwa imetoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ikiwa na abiria ndani yake imeshindwa kutua Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukungu uliokuwepo uwanjani hapo, uliosababisha rubani na wasaidizi wake kushindwa kutua na ndege uwanjani hapo. Hivyo naambiwa ndege ya leo (FastJet) imelazimika kutotua Songwe na kurudi jijini Dar es Salaam ikiwa na abiria ndani, abiria wamerudishwa Dar es Salaam wakisubiri utaratibu mwingine watakaoambiwa.
Mimi Lusako kama mwana Mbeya na kama Mtanzania natoa pole kwa Wanambeya na Watanzania wenzangu na hata wageni wa nje (kama wapo) waliokumbwa na kadhia hii ya leo. Lakini pia natoa pole kwa wamiliki wa ndege yaani kampuni ya FastJet kwa kadhia hii, maana na nyie lazima mtakuwa mmepata hasara kwa kurusha ndege toka Dar mpaka Mbeya kwa kutumia mafuta yenu (bei ya mafuta ya ndege si mchezo). Poleni nyote, abiria na kampuni ya FastJet.
Wito wangu kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa viwanja vya ndege hususani Uwanja wa Ndege wa Songwe, ni kuwa ninawaomba mlishughulikie tatizo hili. Tafuteni namna yoyote iwe ya kiteknolojia au vyoyote mtakavyoona inafaa kumaliza tatizo hili. Wekeni hata taa za kupambana na giza linalosababishwa na ukungu. Ninajua zipo taa za aina hiyo, tunaomba ziwekwe kwenye uwanja huo ili kuondoa kadhia hii.
Hali hii ikiachwa iendelee hivi ilivyo ninaogopa itazitisha Kampuni zinazomiliki Ndege, zitaanza kuhofia kuleta ndege zao mkoani Mbeya kwa kuogopa kupata hasara kama hizi nilizozielezea hapo juu. Ninaziomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi hili, Mbeya tunazihitaji sana hizi ndege. Hivyo tunaomba msiwavunje moyo wawekezaji walioamua kutulea ndege hizi huko "kukaja". Tafadhali mamlaka husika, chukueni hatua stahiki za kukabiliana na tatizo hili sugu.
Kwa leo mimi ninamalizia hapa, une mmalile. Kazi kwenu!!