Somo: Rudi mpenzi

Somo: Rudi mpenzi

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Habari, kuna wengine huko waliko ni usiku, usiku mwema!
Rudi mpenzi! Ushawahi kuiskia kauli hii? Unajua sababu ya kauli hii?
Wengi hujutia maamuzi ya talaka.

Zaidi ya nusu ya talaka tunazozishuhudia huku uswahilini kwetu, mitaani, makazini, na kwingineko, huleta majuto makubwa kwa watalaka, wengi hawajui tu, nimegundua hilo (kwa dhamira ya kuelewana hapa, naomba talaka iongezeke maana, kuachana kwa wapenzi). Nimegundua kwamba baada ya hali ya mambo kutulia, wengi wa watalaka hujutia maamuzi yao ya awali.

Sababu kubwa ya majuto haya, ni hisia kwamba mtalaka ana-m-miss mwenza wake! Ukweli wa mambo unaonyesha kuwa kauli "nipe talaka/ ntakupa talaka" hutolewa wakati wa hasira za juu sana, wakati ambao mhusika amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiria na kufanya maamuzi.

Hali ya mambo inapotulia, huja kubainika baadae kuwa ule ulikuwa uamuzi mgumu sana kuuchukua, ni uamuzi wa ajabu, ni kama muamuzi hakupepesa macho mara mbili, na ukweli unakuwa kwamba tayari maji yameshamwagika.

Iko hivi jamani, unaweza usijutie papo kwa papo baada ya kutoa ama kupewa talaka, lakini changamoto za maisha baada ya talaka, upweke ama hata imani kuwa "nilikurupuka" humuingiza mtalaka katika majuto. Lakini pia wapo wale wanaojikaza kisabuni, anaumia moyoni lakini kwa ndugu na jamaa zake, anatamka kuwa hana mpango nae tena, kuwa ni bora sasa anaishi mwenyewe, kiukweli anatamani warejeane sio leo, bali ni sasa hivi.

Kitu kizuri ni kuwa, baadhi ya wahanga wameweka bayana juu ya majuto yao ya baada ya talaka, na wamebaki na moyo wa "sawa tu, wacha maisha yaendelee, wapo ambao wamethubutu, wamechukua hatua, tumewaskia ama kuwasoma wakiwatafuta wenza wao wapate muafaka!" Katika hawa kuna waliofanikiwa, na bahati mbaya pia kuna walioshindwa kwa sababu tofauti, kurudisha pendo lililopotea.

Kuna sababu 10 za majuto kwa watalaka:


  1. Hisia kwamba bado nampenda "aliekuwa mtu wangu" - hii unaeza kuita ni kiherehere ama kuigaiga ama kufata mkumbo, kama si kujifanya mjuaji!
  2. Upweke - Ni kama kupima maji ya mto kwa mguu, hakuwa ameangalia namna gani aliweza kuinvest katika uhusiano wao, nguvu iliotumika wakati wa kuinvest ktk penzi, ndio na nguvu ya madhara ya kumwagana itakavyokuwa.
  3. Sababu ya talaka haikuwa nzito kivile - hawa wapo wengi sana. kitu kidogo tu, wanakimbilia ktk kauli zinazoashiria kuachana. baada ya muda, huja kushangaa kwamba wakati yeye kadai kuachana kisa mwenza ni mlevi, kuna mtu anamsimulia kuwa yeye kamfumania mwenza wake na wamesameheana na maisha yanaendelea
  4. Wivu baada ya kujua aliekuwa wako kapata mwingine - Hapa ulidhani hatampata kama wewe, hapana, anaweza kumpata zaidi yako! walisema wasemaji: mapenzi kama kiti cha basi, ukishuka tu, anaka mwenzio! Na siku hizi imekuwa mbaya zaidi, kabla hujashuka kuna mwenzio ameshapanda na amekaa! Ni kwamba ukishuka unapunguza idadi ya mizigo tu.
  5. Uhusiano mbaya kati ya mwenza wako na watoto wenu - Talaka ama kuachana ni moja ya majibu mabaya sana ya mgogoro wa mahusiano, lakini hii inakuwa mbaya zaidi kama wahusika walishahusika kuleta watoto duniani. Kuachana kukitokea, lazima kuna mtalaka mmoja atakuwa mbali na watoto, hapa ndio penye majuto.
If marriage means you fell in love, does divorce mean you climbed out?



 
Back
Top Bottom