Somo na funzo la ziada kwenye msiba wa Dr. Reginald Mengi

Somo na funzo la ziada kwenye msiba wa Dr. Reginald Mengi

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,273
Historia ya bilionea mtanzania Dr. Reginald Mengi ilifungwa rasmi juzi 09/05/2019 baada ya kuzikwa katika kijiji alichozaliwa na kukulia. Kuna somo kubwa ambalo Mengi ametuachia wote waliokwenda kumzika na sisi tuliyekuwa tunaangalia kupitia televisheni na kusikiliza katika redio. Somo hilo ni kuthamini na kujali mahali alipozaliwa pamoja na kuwa wazazi wake wote walishafariki.

Mengi alijenga nyumba zenye hadhi kubwa kama ilivyo hadhi yake kiuchumi pamoja na kuweka mazingira mazuri sana ya kijijini kwake mazingira ambayo ni nadra sana hata katika baadhi ya miji mikubwa. Kila mmoja aliliridhika na nyumba na mazingira aliyoyakuta kijijini kwa Mengi kama ilivyo thamani yake kiuchumi.

Somo na funzo kubwa kwa wote wakiwemo wafanyabiashara, viongozi, na watafutaji wengine wote ambao mpo katika mikoa mingine hasa mijini ni kuthamini vijijini kwetu tuliko toka. Unaweza ukaona mazingira ya nyumbani kwa Mengi kuliko kijijini ni mazuri kuliko hata pengine ya hapa Dar ambapo ndipo alipokuwa anaishi.

Kuna watu wakisha toka vijijini kwao na kufanikiwa mijini huwa wanasahau kwao mpaka kuna kuwa pori. Wanajenga mijumba ya nguvu mijijni lakini kwenye vijiji vyao vya asili hali ni kama porini kunabaki mahame wengi utakuta visingizio eti wazazi wake wote walishafariki hivyo hawaoni haja. Hawa ndio unakuta hata wakifa inakuwa aibu wanapopelekwa kuzikwa kwao ndipo marafiki, wafanyabiashara na wafanyakazi wenzao wanapopigwa na mshangao wanapokwenda kukuta mazingira ya hovyo kabisa vijijini mwao na kushangaa namna maisha yao mijini yalivyo ya juu halafu kwao kwa asili ni aibu tupu. Hawa ndio hata wakifa kwa aibu wanataka wazikwe huko waliko au familia inaamua kuwazika mijini. Kwa Dar wengi wanapenda kubanana makaburi Kinondoni ambako ndiko wanaona kwenye hadhi yao kwasababu kwao aibu tupu. Jamani Kinondoni kumejaa jengeni vizuri kwenu mwende mkazikwe kwenu kama Mengi mnang''ang'ania makaburi ya Kinondoni ambako kumejaa mwisho mnajikuta mnazikwa juu ya makaburi ya wenzenu ambao walishazikwa miaka mingi iliyopita.

Nawapongeza sana wachaga kwa kujali vijiji vyao kitu ambacho huwa kinawapa hata motisha ya kurudi kwao kila mwaka siyo kama baadhi ya wengine kurudi kwao ni kama jela wanabaki mijini iwe Pasaka, Chrismas, Idd, mwaka mpya nk mpaka wanakufa na kuzikwa huko huko wanaishi kama wakimbizi wasio na kwao hata watoto wao wana zaa hawajui asili ya wazazi wao wanaishia kuongea kiswahili na kiingereza tu. Hata utamaduni wa kurudi nyumbani mara kwa mara huwa unachochea maendeleo na kuleta umoja wa familia na ukoo kwa ujumla. Hebu jamani tuweke mazingira ya vijijini kwetu vizuri kulingana na uwezo wetu kama wewe ni wa mamilioni weka nyumba ya hadhi yako kijijijni kwenu hujui lini tutakuja, kama wewe ni wa mabilioni basi tukija tuone kama tulivyoona kwa mengi, kama wewe ni wa kuunga unga kama mimi basi hata nyumba nzuri ya vumba viwili au vitatu nzuri tuikute. Watu wakija kama siyo wewe uliyekufa inaweza kuwa mkeo au mwanao watathaminisha mazingira watakayo yakuta na maisha yako huko uliko mjini na kukupa marksi unazostahili. Kama ni aibu utavuna aibu kama siyo wewe ni familia yako kama ni sifa utavuna sifa hata kama umekufa kama ilivyo kwa Dr. Mengi.

RIP Mengi: I CAN, I MUST, I WILL

1094324
 
Back
Top Bottom