SOMO: LUGHA MAHABATI...

Dr Sai

Member
Oct 2, 2019
41
52
Hi guys,
Hope weekend ipo poowah kabisa...!!

Ety jamani mnajua kuwa, "Mahusiano yana lugha?"

Basi kama ulikuwa hulijui hilo. Leo Dr sai anakwambia kwamba
"Ndio, mahusiano yana lugha".

Kama tunavyoelewa, mahusiano yamegawanyika kwenye matawi kadha wa kadha. Yapo mahusiano ya urafiki, mapenzi, undugu, familia n.k
Lakini leo, sisi tutajikita zaidi kwenye mahusiano ya kimapenzi tu. Hivyo tutapata nafasi ya kuangalia LUGHA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI, ambayo ndio msingi mkuu zalishi wa ndoa na familia zetu.

Basi twende tukaone, lugha ya mahusiano ya kimapenzi ni nini? Au ni kitu gani?.

Kwa kifupi, lugha ya mahusiano ya kimapenzi inaitwa MAHABATI. Mahabati ni lugha inavyotumika kuwasilisha hisia za moyo wa mtu, kwa njia ya mazungumzo au/na matendo.

Sasa hapo ulipo jiulize, je ulishawahi kuitumia hii lugha?.

Bila shaka, utapata jibu la NDIO!!?!

Basi leo tunaenda kuangalia, NI KWA NAMNA GANI, TUNAWEZA KUITUMIA HII LUGHA YA MAHABATI, KATIKA MINAJIRI YA KUWATENGENEZA WENZI WETU WA MAISHA. Yaani wake/waume zetu...

Nianze na jinsia pendwa ya kike. Maana jinsia hii, ndio jinsia namba moja lengwa kwenye mada yetu ya leo.

Siku hizi wadada wengi, wamekuwa na ridandasi ya kuzikimbia ndoa zao. Na wengine kupendelea kuchagua mwanaume, aliyeopo kwenye reli ya mafanikio, nafasi au muonekano fulani attractive. Huku tukiona wale wanaume wenzangu na mimi wa kwetu pakavu, yaani tusio na uwezo wa kifedha au wale tusio kuwa na mionekano swafi ya kuvutia, tunakosa kabisa vipaumbele kwenye vichwa vya hawa walimbwende wetu!!

Maskini hii hali, haiishii kwa wanawake ambao hawajaolewa tu! Bali hali hii imewatawala hata baadhi ya wanawake, waliopo kwenye ndoa zao!!

Sio ajabu kuwasikia wanawake hao wakisema:-
"Natamani ningeolewa na yule mbaba..."
"Huyu wa kwangu, kanipata bahati mbaya tu....kwanza muone alivyo alivyo..."
"Loh! fulani hataniweza mie, kwanza muone mtu mwenyewe..hayupo romantic kabisa..."
Na wengine wanadiliki hata kusema wazi kabisa "Mimi mwanaume atakayetaka awe nami, lazima awe na gari, nyumba...." Nk

Kwa kweli mambo hayo, sio ya kuyashangaa katika dunia ya leo. Maana ni moja ya mataluma ya kizazi kipya....

Ila leo nataka tukumbushane kwamba, hiyo sio tabia nzuri kabisah! Hata nyie wanawake wenyewe, hope mnaniunga mkono katika hili. Maana ni mara nyingi tu, mmekuwa mashaidi wa kuona wenzenu wanakutana na mabalaah, kwenye scenarios za namna hiyo....wengine wanakuja kugundua, wanatembea na mume za watu. Wengine wanavunja ndoa zao. Wapo pia wanaochezewa tu na kuwekwa kando, then anaolewa mwingine.....n.k

Basi leo, naomba wewe mwanamke unayepata nafasi ya kunisikiliza hapa, useme
"INATOSHA, KWANZIA SASA NAMTENGENEZA WA KWANGU...KUWA VILE NIPENDAVYO"

Ndio! unatakiwa umtengeze mwanaume wako, haijalishi ulimkuta/yupo vipi. Kumbuka hakuna mkate mgumu, mbele ya chai. Hata kama hachani nywele, ana nguo moja tu, anatembea kwa baiskeli, maskini, hakuridhishi....nk
Am sure yote hayo yanaweza kubaki kuwa historia, endapo ukaamua iwe historia!.

Basi kuanzia leo, we tambua UNAWEZA KUMBADILISHA MWANAUME WAKO, KUWA VILE UPENDAVYO......KWA KUTUMIA LUGHA YA MAHABATI.

Kama ulikiwa ulifahamu hilo, basi leo ndio ufahamu hivyo. Kwakweli hakuna kitu kina nguvu kubwa, kwenye ulimwengu wa mapenzi, kama LUGHA YA MAHABATI. Lugha hiyo ndio kila kitu, kwenye ulimwengu wa mapenzi...haijalishi hupo kwenye mahusino ya uchumba au ndoa!

Kama ni dawa, basi lugha ya mahabati ni zaidi ya muharubaini!
Inatibu:-
1: Ugonjwa wa kutokusikilizana na mwenzio.
2: Kutokufikishwa kileleni...
3: Ugonjwa wa kujisahau, kutimiza wajibu.
4: Virusi vya alshabab, kutwa kupigana!
5: Ugonjwa wa kukosa mtoto...
6: Ugonjwa wa umaskini...
7: Ugonjwa wa kutokujipenda, rafurafu...
8: Kukosekana kwa vitamin A romantic...
9: Virusi vya usaliti...
10: Kukosekana kwa amani na furaha.
11: Kuibiwa mali yako....
12: Kila umpendaye, ni mume wa mtu!
13: Mwanaume umtakae, umpati...!!
14: Virusi vya kujikatia tamaa ya kuolewa! Nk

Hakika nakwambia, hayo ni baadhi tu ya matatizo, yanayoweza kutibika, kwa kutumia dawa ya LUGHA YA MAHABATI.

Najua hapo ulipo umeanza kujiuliza, "nitawezaje, kuitumia hii dawa ya lugha ya mahabati?"

Jibu ni rahisi sana, lugha ya mahabati inatumiwa hivi:-
1: Kujidekeze kimahaba mbele ya mwenzio.
2: Mpe mwenzio maneno matamu ya sifa.
3: Mfanye ajione hakuna kama yeye...
4: Muonyeshe kuwa yeye, ana bahati sana...
5: Muonyeshe unamsikiliza na kumtii...
6: Mpikie chakula kile anachokipendaga...
7: Onyesha kumuhitaji mwenzio kimwili...
8: Mpe haki yake ya tendo...
9: Muite jina lake halisi na sio baba nanii...
10: Usinune nune, mbele ya mwenzako...
11: Zungumza na mwenzio kimahaba, juu ya maisha yenu na familia.
12: Mpe pia mwenzio, nafasi ya rafiki....
13: Kuwa na sura mwangavu...
14: Kubali kutongozwa, ila usikubali mategemeo ya kila anaye kutongoza.
15: Acha kumdharau mwanaume, hata awe amevaa magunia.
16: Ondoa vigezo kama fedha, mali na nafasi. Kuwa vipaumbele vya kutafuta mwenza wako...
17: Jiepushe na debates za gender!
Nk

Hakika zipo namna nyingi za kuitumia lugha ya mahabati. Haijalishi tayari upo kwenye ndoa, uchumba au bado huja bahatika.....lugha ya mahabati haina ubaguzi, hakika inaweza kutumika na yoyote yule. Nadhani kadili siku zitavyokuwa zinaenda, ndivyo tutakuwa tunajuzana njia nyingine ni zipi kwa marefu na mapana.

Lakini mpaka hapo, nadhani leo umeona kwamba unaweza kutatua changamoto, zinazokukumba katika ulimwengu wa mapenzi. Tena simply tu, utajikuta unafanikiwa kufunua chapter ya upendo, furaha na amani katika mahusiano yako!

"Mungu akupe nini sasa?!! Gunia la chawa?!!"

Basi nami mpaka hapo, sina la ziada. Hivyo naomba niwaachie ngoma yenu, wenye shughuri, ili nanyi mjipindue kadili muwazavyo...

#....MAFANIKIO YOYOTE YA MWANAUME, YUPO MWANAMKE NYUMA YAKE.....#

Sakayo Shunie SweetieLee Mzigua90 financial services Karma Hornet Depal naina19 Kasie Atoto adorabella Saint anne Jovvan @Keetah Madame B na wengine wote....

Nawatakia kila la kheri.
Merci.
 
Kwahyo hao uliowatagi ndo wana sauti za mahaba sauti za kumtoa nyoka pangoni sauti za kuibua makinikia yaliyofichwa sauti za kukamatisha wahujumu uchumi?
 
Hapana,
Tatizo kubwa ni kukosekana kwa ufahamu, juu ya mambo ya msingi katika maisha ya mwanadamu. And bad enough muda huo huo, utandawazi na kampeni za kijinsia, zinazidi kushamiri na kufunika macho ya watu.....

All in all tuendelee tu kuelimishane taratibu, huku tukizidi kumtanguliza Muumba katika maisha yetu.

Ni hayo tu...
 
Ooh very sorry Mr.
Unajua sikufahamu kabisa, kwamba naongea na nani. Siunajua tena, I'd hizi ni ngumu sana kuzinote!

Naomba uniwie radhi sana chief.
Mimi Dada tena Dr
Ila Mimi siuzikagi sjui kwa nn

Haya bana ngoja nisogezesogeze sku kila la kher mkuu
 
Ahsante mtoa mada kwa somo zuri, binafsi nitalifanyia kazi nitakuletea na kadi ya mwaliko..!!
 
"KWENYE KILA MAFANIKIO YA MWANAUME KUNA MWANAMKE NYUMA YAKE"
huyo 'mwanamke' ni Mama yake sio wewe Magidalena Mwakipesile.
 
Back
Top Bottom