Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,045
Tanzania haishiwi vioja. Punde kupitia kupitia taarifa ya Habari ya Mlimani TV nimemwona Jaji Mkuu-Chande, Lau Kego Masha-IMMA Advocates na mwakilishi wa UDSM wakizindua mpango wa kuwajengea uwezo wanasheria wetu wapatao 170 katika sheria za mikataba. Lengo ni kuhakikisha eti wanasheria wetu hawaingii mkenge kwenye mikataba hasa ya kimataifa. Suala zima ni jema lakini hofu yangu ni uwezo na unadhifu wa IMMA katika masuala ya ufungaji wa Mikataba yenye tija kwa Taifa. Isijekuwa badala ya kujenga uwezo, tunaimarisha kizazi cha ufisadi kwa kutoa mbinu za ki-DEEP GREEN FINANCE