Somo La Leo Kutoka kwa Mzee Mwanakijiji

Somo La Leo Kutoka kwa Mzee Mwanakijiji

Chamoto

Platinum Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
9,883
Reaction score
22,309
Nimekuwepo hapa JF kwa muda ila mara nyingi huwa na soma tuu (lurker). Katika watu ambao hupenda kusoma makala zao ni Mzee Mwanakijiji. Nadhani kila mtu anamfahamu ila ningependa kumshukuru kwa kutukumbusha kitu kimoja ambacho ni mfano wa kuigwa kwa wengi hapa jamvini..

Huyu jamaa anaongoza kwa kubandika makala hapa na makala zake ni nzuri ila si wote wanofurahishwa na makala zake. Huyu Mzee huwa ana "hit home" kiasi kwamba mara nyingi hupata majibu mabaya na yenye hasira kutoka kwa wasiopendezwa na hoja zake.

Cha ajabu kila anapopata hayo mapigo huyu Mzee huwashukuru hao waliomponda kwa kubonyeza "thanks button". Yaani nilikuwa najiuliza ni kwanini huwa anafanya hivyo? Katika kutafakari nikakumbuka katika maandiko tunaambiwa tushukuru kwa kila jambo.

Asante Mzee Mwanakijiji kwa kutukumbusha hilo.
 
Chamoto

umenena ... kwani ukipigwa kofi shavu la kushoto na geuza tena shavu la kulia ....
 
Ni kweli kabisa

Cha baridi tusitaniane hapa, wewe kweli mtu kakupiga mkofi then umgeuzie shavu la kushoto nalo akutandike? Nenda hata kwa kakobe kampige kofi uone...haya ni maandishi yapo tu kwenye bible na hakuma mtu anayeyatekeleza
 
Lol naona leo unausongo na mimi, haya bwana

Ila ni kweli kwa binadamu ni vigumu kurudisha mema lakini tukimshirikisha Mungu yeye atatuwezesha. Maana yake ni kuwa kama mtu amekutendea kosa huhitaji kurudisha kosa. Ukipitia makala za mwanakijiji na kuona jinsi baadhi wanavyo mkejeli nadhani ungenielewa.
 
Ikifika mahali mpaka kamati inakulaumu ujue ni impact yake imekwenda mbali, huyu jamaa huandika habari zinazogonga vichwa vya watu tena za kiuchunguzi! Nampongeza sana MKJ
 
Ikifika mahali mpaka kamati inakulaumu ujue ni impact yake imekwenda mbali, huyu jamaa huandika habari zinazogonga vichwa vya watu tena za kiuchunguzi! Nampongeza sana MKJ
Yaani umegongo penyewe kabisa.
 
Back
Top Bottom