Somo la kitunguu saumu: Nguvu yake, tiba na maajabu

Mshana ndugu yangu mi kibarua changu ni kusafirisafiri je nikichukua vitunguu swaumu vikubwa kama vitano vikamenywa na kutwangwa,kisha nikachanganya na asali kama vikombe viwili vya chai na ndimu kama tano,alafu nikachukua mchanganyiko huo nikaweka kwenye chupa ili nikisafiri niwe nachukua kiasi nakunywa kwa maji ya moto je kuna ubaya au nisawa tu?
 
Mshana ndugu yangu mi kibarua changu ni kusafirisafiri je nikichukua vitunguu swaumu vikubwa kama vitano vikamenywa na kutwangwa,kisha nikachanganya na asali kama vikombe viwili vya chai na ndimu kama tano,alafu nikachukua mchanganyiko huo nikaweka kwenye chupa ili nikisafiri niwe nachukua kiasi nakunywa kwa maji ya moto je kuna ubaya au nisawa tu?
Ni sahihi lakini isizidi massa 48,utatengeneza mvinyo mmoja mkali sana
 
Si unaonainatanua mishipa iliyosinyaa?
Unachifanya unachukua asali maji ya moto na kitunguu saumu robo lita ya maji moto kitunguu saumu vipande viwili asali vijiko vitatu daily kwa mwezi mzima
Vipi nikiwa nakatakata vipande vidogo halafu nameza Bila kutafuna?
 
Hii ndio nimeprove, kuna kipindi niliona sipigi zile show za fally ipupa, mzee mmoja akanishauri hiyo kitu nilikuwa napiga vipande vyangu kumi kama ni vikubwa , kama ni vile vidogo namenya chote, then natwanga, nachukua na asali vijiko viwili vikubwa na mix na maji moto,,,, hapo ni asubuhi kabla hujapiga hata msawaki, nilifanya hilo zoezi mwezi mzima,, aiseeh baada ya hapo kila show lazima kari la fire lipaki mlangoni
Hayo maji moto ni kiasi gani mkuu
 
4433ec83c0c29b46fd775e22e1defa9c.jpg


Kwanza nipende kumshukuru sana Lavan Island yeye ndio chachu ya mada hii...nilikuwa sina ufahamu wa kutosha kuhusu kitunguu saumu japo nilikuwa najua kuwa ni kinga nzuri kwa mtoto anayetaka usiku na kulialia, lakini kumbe kitunguu saumu ni kinga hatari kwa mambo ya kishirikina na viumbe roho wabaya

83805480c0069b5dac86d76530537f6b.jpg


Kitunguu saumu kwa jina la kitaalam Allium sativum sio kiboko ya wachawi tu bali pia ni kinga ya magonjwa mengi na hata wadudu waharibifu.

Hiki kiungo kimacholeta Ladha kwenye vyakula vingi kilianza kutumika zamani sana kwenye nchi nyingi duniani

Wamisri waliamini katika majini yanayonyonya damu watoto wakitumia kichane cha vitunguu saumu kuwa kinga watoto wao..sehemu za China Malaysia nk wazazi hutumia kuwapaka watoto kitunguu saumu kwenye paji la uso kama kinga ya nguvu za giza.

Kule Romania wao husaga na kupakaza kwenye milango na madirisha ya nyumba zao , mageti na hata kwenye pembe za ng'ombe wakiamini nguvu ya kitunguu saumu kwenye Kufukuza wachawi na viumbe roho wabaya.

Lakini pia ili kumlinda marehemu aliyekuwa na dalili za kugeuka jini au kuzuia asichukuliwe kishirikina walimlisha/walimwekea vipande kadhaa vya kitunguu saumu mdomoni...na hii pia ni kinga hata ya kuzuia roho yake isiweze kurudi mwilini

Huo ulikuwa ni upande wa giza lakini unapokuja kwenye afya ya kawaida ya mwili kitunguu saumu huongeza kinga mwilini, huku kikipunguza cholesterol kwa kiwango kikubwa mno huku kikisaidia kutanua mishipa ilisinyaa, zaidi hii kitu ni kinga bora sana ya cancer na hata mgonjwa mwenye dalili za cancer . BP kisukari nk nk...ukiweza kabla ya kulala tafuna kipande kimoja cha kitunguu saumu kile kisicho na harufu kali

Maajabu ya kitunguu saumu ni kwamba inakuwaje kitu kidogo namna hii kinakuwa na nguvu ya ajabu hata kuwa kinga kwenye nguvu nyingi za giza? Kimoja kinachosemwa saana ni ile harufu yake . . . majini mashetani na hata wachawi na washirikina wakiwemo wanga wana mzio mkali na harufu ya kitunguu saumu na vitu vichachu..hii ndio sababu pekee iliyoweza kutolewa mpaka sasa.

Lakini pia maajabu mengine ni ile nguvu ya Kufukuza hata wadudu waharibifu majumbani na mashambani kiasi cha kuvutia watengeneza madawa ya wadudu kukitumi.

Kuna watu baadhi si wachawi wala si washirikina lakini hupenda kutumia mchanganyiko wa Biblia takatifu kitunguu saumu na mafuta ya mzeituni kuwasaidia watu wenye magonjwa ya ajabu yanayohusishwa na nguvu za giza kwahiyo jamani pamoja na kuwa kiungo kimacholeta Ladha kwenye vyakula vingi lakini pia ni kinga ya magonjwa mengi na hata nguvu za giza

ef08580701efcecb9f1b952283712432.jpg
Mshan jr. Naomba msaad wako tafadhar nina mama yngu anasumbuliwa san na majini wakati mwingine yanampiga vibao usiku nakumpa vitisho vikali mara kichwa kina muuma mara mapigo ya moyo kwenda mbio yana yanamletea mawenge sana kuna kipindi akienda kwa ustadh anasomewa yanatulia yanachukua muda kurudi sasa afanyeje ili yasimsumbue tena maana ikifika usiku anaogopa hata kulala lzima wazee watie timu kumpa shurba zao na mateso mengine. Asante
 
Mshan jr. Naomba msaad wako tafadhar nina mama yngu anasumbuliwa san na majini wakati mwingine yanampiga vibao usiku nakumpa vitisho vikali mara kichwa kina muuma mara mapigo ya moyo kwenda mbio yana yanamletea mawenge sana kuna kipindi akienda kwa ustadh anasomewa yanatulia yanachukua muda kurudi sasa afanyeje ili yasimsumbue tena maana ikifika usiku anaogopa hata kulala lzima wazee watie timu kumpa shurba zao na mateso mengine. Asante
Pole hiyo nyumba yenu ni lango la shetan naamisha kuna zindiko mliweka la Uganga kulinda nyumba dhidi ya wachawi

Mganga mkuu wa mapepo ni Yesu uamin usiamin Mungu tu hata mimi nahaha na mdogo wangu hapa Vita kunasiku utakubaliana nami
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom