Somo la Fizikia laelekea kukosa walimu

nchasi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
564
185
Ndugu wana JF habari za majukumu ya kulijenga Taifa letu!

Katika utafiti wangu mdogo kwenye shule kadhaa za kata nimejionea mwenyewe na kugundua kuwa mbali na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na mahesabu (BIOLOGY, CHEMISTRY, PHYSICS & B/MATHS). Lakini uhaba wa walimu wa hili somo la Physics ni mkubwa mno.

Mfano shule A ina jumla ya walimu 48 ila hakuna kabisa mwl wa hilo somo na shule nyingine nyingi nadhani hata shule za ukanda wako wewe mwanaJF unaepitia uzi huu.

Inanipa wakati mgumu sana kwa sera ya Afya kuweka kigezo cha ulazima wa D kwenye hilo somo ili ajiunge na kozi za Afya kwenye vyuo vya Serikali hapa kweli watoto wa shule nyingi za Serikali ndoto zao lazima zitazimwa tu.

Nimeileta hii mada ili tujadi kwa pamoja nini kifanyike ili tupate walimu hasa wa hili somo?
 
ni kweli mkuu......walimu wa physics ni wachache
 
Tatizo ni kwamba,hata tunapofika makazini thamani ya mwalimu wa sayansi ni ndogo mno,na bado wanafanyiwa figisu za hatari badala ya kuwa encourage.
Nina mfano dhahiri, mke wa kaka yangu amekuwa akifundisha shule ya sekondari Mgulasi,iliyopo manispaa ya Morogoro.
Shemeji yangu huyu pamoja na kuwa wako 2 tu wanaofundisha fizikia shuleni kwao,lakini Mkuu wake wa shule amemfanyia zengwe za ajabu kwa sababu tu alihoji mapato na matumizi ya shule kwenye kikao.
Matokeo yake,shemeji yangu huyu aliuguliwa na mtoto,usiku(ilikuwa ghafla) akalazimika kumpeleka mtoto hospital, asubuhi akaandika barua ya kuomba ruhusa akiwa hospital,akampatia madam mwenzake ampelekee kwa Mkuu wake wa shule.
Mkuu wake alipokea barua na kuificha bila kuweka kwenye file,na akaanza kumuandikia "NO ANY INFORMATION" kwenye daftari ya mahudhurio,zilipotimia siku tano,akapeleka taarifa kwa afisa elimu,ilipofika tarehe 01/03/2016 akaletewa barua tatu na Mkuu wa shule,barua hizo zilikuwa,
1.TUHUMA ZA UTORO KAZINI
2.BARUA YA KUJIELEZA KWANINI ASICHUKULIWE HATUA
3.BARUA YA KULIMWA MSHAHARA WAKE,(NUSU MISHAHARA)
Barua zote tatu,zimeandikwa siku moja,01/03/2016.
Baada ya kupokea barua hizo alienda kwa afisa elimu wake kutafuta ufafanuzi wa jambo hilo akamtimua,alipoenda kwa mkurugenzi kutafuta haki yake hakupata fursa hiyo,aliambiwa mkurugenzi yupo busy sana.(kwa zaidi ya mwezi wiki mbili hakupata msaada wowote)
Hatimaye mwisho wa mwezi wa tatu mshahara wake ukafyekwa,akakuta kuna nusu mshahara,akaamua KUACHA KAZI,MPAKA SASA MGULASI SEKONDARI ILIYOPO MOROGORO MANISPAA YENYE WANAFUNZI 1034 INA MWALIMU MMOJA TU WA FIZIKIA,ETI KISA MWALIMU KUHOJI MAPATO NA MATUMIZI YA SHULE,KWA MWENDO HUU TUTAFIKA!!??
 
Ripoti hii kitu kwa waziri tu!
 
watapatikana wapi wakati nikifaulu physics naenda course za engeneering? hilo tatizo lipo hata vyuoni walimu wa hilo somo ni wachache, litapata walimu siku umuhimu wake ukionwa na serikali
 
Ripoti hii kitu kwa waziri tu!
Mkuu kama kumfikia Mkurugenzi tu ilikuwa na figisu figisu mpaka basi,itakuwa rahisi kiasi gani kumfikia waziri,tatizo la masomo ya sayansi litendelea kuwa kubwa mno kwa style hii ya unyanyasaji,mwenye namba ya simbachawene anitumie tafadhali,kwani watoto wetu wanakosa access ya kufundishwa kwa upuuzi wa MTU mmoja tu!
 
Tatizo ni kwamba,hata tunapofika makazini thamani ya mwalimu wa sayansi ni ndogo mno,na bado wanafanyiwa figisu za hatari badala ya kuwa encourage.
Nina mfano dhahiri, mke wa kaka yangu amekuwa akifundisha shule ya sekondari Mgulasi,iliyopo manispaa ya Morogoro.
Shemeji yangu huyu pamoja na kuwa wako 2 tu wanaofundisha fizikia shuleni kwao,lakini Mkuu wake wa shule amemfanyia zengwe za ajabu kwa sababu tu alihoji mapato na matumizi ya shule kwenye kikao.
Matokeo yake,shemeji yangu huyu aliuguliwa na mtoto,usiku(ilikuwa ghafla) akalazimika kumpeleka mtoto hospital, asubuhi akaandika barua ya kuomba ruhusa akiwa hospital,akampatia madam mwenzake ampelekee kwa Mkuu wake wa shule.
Mkuu wake alipokea barua na kuificha bila kuweka kwenye file,na akaanza kumuandikia "NO ANY INFORMATION" kwenye daftari ya mahudhurio,zilipotimia siku tano,akapeleka taarifa kwa afisa elimu,ilipofika tarehe 01/03/2016 akaletewa barua tatu na Mkuu wa shule,barua hizo zilikuwa,
1.TUHUMA ZA UTORO KAZINI
2.BARUA YA KUJIELEZA KWANINI ASICHUKULIWE HATUA
3.BARUA YA KULIMWA MSHAHARA WAKE,(NUSU MISHAHARA)
Barua zote tatu,zimeandikwa siku moja,01/03/2016.
Baada ya kupokea barua hizo alienda kwa afisa elimu wake kutafuta ufafanuzi wa jambo hilo akamtimua,alipoenda kwa mkurugenzi kutafuta haki yake hakupata fursa hiyo,aliambiwa mkurugenzi yupo busy sana.(kwa zaidi ya mwezi wiki mbili hakupata msaada wowote)
Hatimaye mwisho wa mwezi wa tatu mshahara wake ukafyekwa,akakuta kuna nusu mshahara,akaamua KUACHA KAZI,MPAKA SASA MGULASI SEKONDARI ILIYOPO MOROGORO MANISPAA YENYE WANAFUNZI 1034 INA MWALIMU MMOJA TU WA FIZIKIA,ETI KISA MWALIMU KUHOJI MAPATO NA MATUMIZI YA SHULE,KWA MWENDO HUU TUTAFIKA!!??
Wazazi hapa ndo waungane waingilie kati. Kimsingi hapo mwalimu hana shida yeyote kazi atapata sehemu nyingine. Kamati za shule na wazazi waingilie kati haiwezekani mtu mmoja awachezee akili kwa tamaa zake labda kama hao wazazi na walimu hawajitambui
 
uhaba utapungua baada ya higher diploma wakimaliza masomo yo mwakani!!!
kweli kabisa maana wengi waliolisoma advance hawakua na hamu tena ya kulisoma chuo kwa sababu wengi walioenda education waliona hamna haja ya kusoma kitu kigumu wakati ajila hipo 1 kwa 1 hata wakisoma mengine,atleast hao waliotoka olevel wakenda kulisomea diploma alkuwapa mawazo sana.
 
Tatizo ni kwamba,hata tunapofika makazini thamani ya mwalimu wa sayansi ni ndogo mno,na bado wanafanyiwa figisu za hatari badala ya kuwa encourage.
Nina mfano dhahiri, mke wa kaka yangu amekuwa akifundisha shule ya sekondari Mgulasi,iliyopo manispaa ya Morogoro.
Shemeji yangu huyu pamoja na kuwa wako 2 tu wanaofundisha fizikia shuleni kwao,lakini Mkuu wake wa shule amemfanyia zengwe za ajabu kwa sababu tu alihoji mapato na matumizi ya shule kwenye kikao.
Matokeo yake,shemeji yangu huyu aliuguliwa na mtoto,usiku(ilikuwa ghafla) akalazimika kumpeleka mtoto hospital, asubuhi akaandika barua ya kuomba ruhusa akiwa hospital,akampatia madam mwenzake ampelekee kwa Mkuu wake wa shule.
Mkuu wake alipokea barua na kuificha bila kuweka kwenye file,na akaanza kumuandikia "NO ANY INFORMATION" kwenye daftari ya mahudhurio,zilipotimia siku tano,akapeleka taarifa kwa afisa elimu,ilipofika tarehe 01/03/2016 akaletewa barua tatu na Mkuu wa shule,barua hizo zilikuwa,
1.TUHUMA ZA UTORO KAZINI
2.BARUA YA KUJIELEZA KWANINI ASICHUKULIWE HATUA
3.BARUA YA KULIMWA MSHAHARA WAKE,(NUSU MISHAHARA)
Barua zote tatu,zimeandikwa siku moja,01/03/2016.
Baada ya kupokea barua hizo alienda kwa afisa elimu wake kutafuta ufafanuzi wa jambo hilo akamtimua,alipoenda kwa mkurugenzi kutafuta haki yake hakupata fursa hiyo,aliambiwa mkurugenzi yupo busy sana.(kwa zaidi ya mwezi wiki mbili hakupata msaada wowote)
Hatimaye mwisho wa mwezi wa tatu mshahara wake ukafyekwa,akakuta kuna nusu mshahara,akaamua KUACHA KAZI,MPAKA SASA MGULASI SEKONDARI ILIYOPO MOROGORO MANISPAA YENYE WANAFUNZI 1034 INA MWALIMU MMOJA TU WA FIZIKIA,ETI KISA MWALIMU KUHOJI MAPATO NA MATUMIZI YA SHULE,KWA MWENDO HUU TUTAFIKA!!??

alijibu hizo barua, taratibu za kiutumishi zinajulikana. atakuwa mjinga endapo atasarender kaz yake kwa hyo shda ndogo sana, otherwise awe ameanza kaz HIV juzi. kiubinadamu always do the best ufuate taratibu, alitakiwa kuomba ruhusa kwa mwajir wake co MKUU wa shule, MKUU wa shule alitakiwa kumpitishia ruhusa tu!! poleni basi mshaurin vyema. coz inaonekana kaacha kaz kwa jazba...
 
Mkuu kama kumfikia Mkurugenzi tu ilikuwa na figisu figisu mpaka basi,itakuwa rahisi kiasi gani kumfikia waziri,tatizo la masomo ya sayansi litendelea kuwa kubwa mno kwa style hii ya unyanyasaji,mwenye namba ya simbachawene anitumie tafadhali,kwani watoto wetu wanakosa access ya kufundishwa kwa upuuzi wa MTU mmoja tu!
huyo shemejio kaonewa lakini ishu nyingine una swallow tu pride yako, yanapita maisha yanaendelea, kisichokuua kinakukomaza
 
Walimu wa Sayansi ni JANGA kiufupi sio kwamba vijana hawapo sio wapo wengi tu ila hawaoni umuhimu wa kuua ndoto zao kwenda kwenye ualimu ambapo treatment ni sawa na mwalimu wa arts mwenye F ya mathematics...Vijana wanaona ni bora waende FTC au Vyuo vya Ufundi japo wamefaulu masomo ayo....leo hii ni ukweli usiofichika ukitembelea mashule ya mijini walimu wengi ni wanawake wamejaa maofisini uku wote wakiwa Arts....Sio Science tu ata masomo ya ufundi walimu wa masomo ayo mfano motor vehicle, fitting n turning,Brick work n carpentry, electrical installation n electronics nk nk mashule km Bwiru boys tech, iyunga,mbeya tech nk nk masomo ayo yamekufa kibudu....Nchi hii itajaa wanasheria na walimu wa arts tu km hakuna jitihada za kuokoa Taifa hili
 
1.Ukiwa mwalimu usiachekuwa na mkopo 2. Ukiwa mwalimu usiombe ruhusa kwa mkuu, omba DEO au DED kupitia kwa mkuu
 
alijibu hizo barua, taratibu za kiutumishi zinajulikana. atakuwa mjinga endapo atasarender kaz yake kwa hyo shda ndogo sana, otherwise awe ameanza kaz HIV juzi. kiubinadamu always do the best ufuate taratibu, alitakiwa kuomba ruhusa kwa mwajir wake co MKUU wa shule, MKUU wa shule alitakiwa kumpitishia ruhusa tu!! poleni basi mshaurin vyema. coz inaonekana kaacha kaz kwa jazba...
Kama umenipata vizuri ni kwamba aliandika barua ya ruhusa akiwa hospital na akampatia madam mwenzake aiwasilishe,lakini Mkuu wake wa shule inaonekana alimpa matumaini madam aliyeagizwa kuwa hakuna tatizo kwa kuwa anauguliwa,kumbe moyoni ndo ilikuwa target ya kumzima mdomo na kuwatisha wengine ili wasihoji hoji habari ya fedha za shule!!
 
Fizikia ni somo nnalolipenda sana, ni kwa vile Kazi nnnayofanya hainiruhusu kuwa na Kazi nyingine ya ziada hata kwa kujitolea bure ningefundisha, kwa ufupi naipenda sana physics, haina longolongo, ni concepts tupu. Mechanics ya A level ndio hasa nilikua najichukulia umaarufu kwa kukata maswali ya UP. Ntamkumbuka sana Pdiddy (Mwl. Msami wa Old Moshi) na Kaka ( Luhwagho Ifunda).

Sio tu kwamba tutaksbiliwa na uhaba wa waalimu, muda sio mrefu njaa ya mainjinia (wahandisi) italisumbua sana taifa letu. Maslahi yanaathiri sana watu wasome au wafanye Kazi gani. Licha ya ugumu wa masomo ya Sayansi, maslahi take ni madogo sana, hivyo kusoma hayo masomo inabaki kuwa ni interest au hobby ya mtu binafsi.
Kuna haja ya kuwa na motisha ili kuinusuru hii sekta.
 
MOTISHA KWA WALIMU WA SCIENCE HASA WA HILI SOMO NI MUHIMU SANA BILA HIVYO UKWELI MASHULE MENGI YATAJAA WALIMU WA MASOMO YA ARTS NA WATOTO WATAIGA MISEMO YA WALIMU WAO ''KWA NINI NIPATE SHIDA YA KUKOMAA NA SOMO GUMU LA PHYSICS WAKATI HUKU KWENYE MTEREMKO KUPO NA MSHAHARA NI ULEULE''
 
Back
Top Bottom