Somo Jingine Kutokana na Mauaji ya Rwanda, 1994: Mapanga, Majambia na Marungu, ni Silaha za Kivita Zilizo Mbadala wa Bunduki, Mabomu na Vifaru

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,490

1747912418789.png
Screenshot_20250716_160512_Chrome.jpg

I. Usuli

“Kitendawili cha ujasiriadola ni hiki hapa: Ni kwa vipi inawezekana kuwepo kwa Taifa moja imara la watu walio sawa na huru kwa kipindi kirefu, wakiwa wanaunganishwa na Katiba moja ya nchi, wakati watu hao hao wamegawanyika katika makundi tofauti kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili?” (Rawls 1993 :xxv)

“Nadharia bora ya ujasiriadola inapaswa kutupatia utaratibu utakaotuwezesha kuhakikisha kwamba jumuiya zilizo na utofauti kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili zinaweza kuishi pamoja ndani ya jumuiya moja ya kisheria” (Galston 1991 :45)

Mwaka 2021, Rais Trump wa Amerika alishindwa uchaguzi na kugoma kukabidhi ofisi, japo Amerika ni nchi ya kidemokrasia, ambako uchaguzi wa Rais hufanyika na kutoa nafasi kwa Rais aliye madarakani kuondoka madarakani kwa amani kama akishindwa kihalali.

Mwaka 2021, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alifariki. Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alipaswa kuapishwa ili kujaza nafasi hiyo. Lakini, ilidaiwa kwamba, Katibu Mkuu Kiongozi wa wakati huo, Dkt. Bashiru Ally, aliamua kuitisha na kuongoza kikao cha watu kadhaa kilichoamua kuweka mkakati wa kumwandaa mtu mwingine mwenye sifa zilizotajwa na kikundi hicho, ili aapishwe na kuziba pengo. Uamuzi huo ulikiuka matakwa ya Katiba ya nchi, na hivyo, kwa njia ya mzunguko, kukiuka matakwa ya umma mpana wa Watanzania.

Na mwaka 2024, Rais Samia wa Tanzania aliukana ukuu wa katiba ya nchi juu ya serikali, mahakama na Bunge, kwa kutumia hoja kwamba katiba ni kitabu sawa na vitabu vingine vinavyouzwa madukani, halafu akaanza kuendesha nchi kwa kutumia katiba mbadala ya kiimla aliyoitunga yeye na wasaidizi wake wachache, na hivyo kuiweka pembeni katiba rasmi ya Tanzania ambayo ni Jamhuri ya Kiliberali na Kidemokrasia. Rais Samia wa Tanzaniaia alikula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya nchi iliyomweka madarakani tangu mwaka 2021.

Mazingira haya, kutoka Tanzania na Amerika, yanazalisha swali lifuatalo kwa wataalam wa sayansi ya ujasiriadola, usalama, haki na amani: Je, kwa ajili ya kulinda usalama, haki na amani katika nchi, ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa na jeshi la ulinzi wa wananchi dhidi ya wanasiasa kama vile Dkt. Bashiru Ally, Rais Trump na Rais Samia?

Katika muktadha wa swali hili na nukuu zilizotajwa hapo juu, makala hii inatumia historia ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 kujenga msingi wa hoja ifuatayo juu ya nafasi ya jeshi katika kukomesha siasa za kiimla katika Tanzania ya leo:

Kwamba, Kanuni ya Imani ya Utanzania inayotamkwa kikatiba, inaonyesha kwamba Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiliberali yenye wasifu wa kisiasa unaojumuisha vipengele vifuatavyo: Usawa wa heshima ya kiutu; Uhuru wa kujichagulia muundo wa mamlaka ya kiutawala; Kibali cha watawaliwa kwa watawala wao; Haki kama msingi wa amani; Serikali yenye nguvu tosha za kuleta matokeo yanayotakiwa na umma; Serikali yenye nguvu zilizowekewa ukomo; Usawa mbele ya sheria; Usawa wa fursa badala ya usawa wa matokeo; Ukuu wa ukweli wa kisayansi juu ya ukweli wa kisiasa; Uhusiano kati ya ukweli na ushahidi mpya; Mshikamano na majukumu ya kijamii, Uhuru wa kuabudu; Umoja wa Taifa unaoziweka kwapani tofauti za raia wake; Ukuu wa Katiba ya nchi juu ya serikali, bunge, mahakama; na Tunu na kanuni za maadili zinazofungua milango ya ushirikiano wa kimataifa.

Kwamba, matukio yafuatayo yanapingana na Kanuni ya Imani ya Utanzania: mauaji ya Ali KIbao, tamko la Rais Samia kwamba Katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine, kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake, kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi, kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya, kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni, kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani, kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua.

Kwamba, kama hali ilivyo katika Rwanda ya baada ya 1994, utamaduni huu mpya wa kufanya siasa za nchi kwa kutumia majeshi umetokea kwa sababu baadhi ya viongozi wakuu waliokula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya nchi wameamua kuikana Kanuni ya Imani ya Kitaifa iliyotamkwa kwa mujibu wa Katiba hiyo, na hivyo kuukataa ukweli kwamba, Katiba ya nchi yetu inalitambulisha Taifa la Tanzania kama Jamhuri ya Kiliberali na Kidemokrasia, yenye kufuata misingi ya demokrasia ya vyama vingi, ambako kunapaswa kuwa na mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations), badala ya kulitambulisha Taifa hili kama dola ya kijeshi, ambamo huwa kuna mahusiano ya kiuhasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations).

Na kwamba, kwa hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama havina hiari ispokuwa kusimama katika upande wa kulinda Kanuni ya Imani ya Utanzania inayotamkwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, na hivyo kujitenga na kazi ya kuwalinda viongozi wakuu walioamua kimakosa kuendesha nchi kwa kutumia utaratibu wa kiimla badala ya kuheshimu viapo vyao vya kulinda, kuhifadhi na kutetea Katiba ya nchi; pendekezo hili likiwa na maana kwamba mkosaji ashauriwe na wateule wake kujiuzulu kwa hiari au majenerali wamwelekeze namna ya kumaliza kipindi chake cha uongozi kwa amani, bila kuzidisha hata siku moja, mara tu baada ya uchaguzi wa Oktoba 2925.

Kwa ajili ya kufanya utetezi wa hoja hii, makala hii imegawanywa katika sehemu zifuatazo:

  1. Usuli;
  2. Utangulizi;
  3. Methodolojia;
  4. Historia fupi ya mauaji ya halaiki huko Rwanda;
  5. Hatua saba za kupanga na kutekeleza mauaji ya Rwanda;
  6. Sababu za Vyombo vya Usalama Kushindwa Kuzuia Mauaji ya Rwanda;
  7. Mafundisho Kuhusu Utu wa Binadamu katika Rwanda ya Kale;
  8. Ushiriki wa wanawake katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda
  9. Yaliyotoke Rwanda sasa yanaanza kutokea Tanzania;
  10. Kanuni ya Imani ya Utanzania, homodomia na apedomia;
  11. Muhtasari na hitimisho;
  12. Wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama; na
  13. Marejeo.

1748002273007.png

1748336691331.png

II. Utangulizi

Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Tanzania (NDC) kilianzishwa mwaka 2011. Ni Taasisi ya Elimu ya Juu inayomilikiwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo, alikizindua rasmi Chuo hiki tarehe 10 Septemba 2012.

Kulingana na tovuti yake, kwa sasa, Chuo hiki kinatoa Shahada za Uzamili katika Mafunzo ya Usalama na Mikakati (MSSS) na Diploma ya Mafunzo ya Usalama na Mikakati (DSSS).

Dira ya Chuo hiki ni kuwa taasisi yenye hadhi kubwa zaidi ya kutoa mafunzo ya usalama wa kitaifa na kimataifa kwa maafisa wakuu waliochaguliwa wa Ulinzi na Utumishi wa Umma, kuwapa ujuzi na maarifa muhimu kwa kufanya maamuzi ya busara katika mazingira magumu ya usalama wa kitaifa na kimataifa na kimkakati." (The Security Limelight: 2022, p. ii).

Kwa hiyo, mpaka sasa Taifa linao wataalam wa kutosha wenye kufahamu kuwa kikatiba, nchi yetu inapaswa kuongozwa kwa kufuata kanuni za Jamhuri ya Kiliberali inayofuata misingi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Lakini, kuna matukio kadhaa yanapingana na ukweli huu na ambayo yamenichiochea kuandika makala hii kwa ajili ya kutoa wito maalum kwao.

Kuna mauaji ya Ali KIbao, kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake, kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi, kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya, kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni, kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani, kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua..

Matukio yote haya yanafanywa na watu waliobeba bunduki ikiwa ni ishara kwamba, kwa maoni yao, kumiliki bunduki mkononi ni mwarobaini wa kutibu magonjwa yote yanayoshambulia "usalama wa Taifa."

Taswira hii inamaanisha kwamba, japokuwa Tanzania ni Jamhuri ya Kiliberali na ya Kidemokrasia, kuna mahusiano ya kihasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations) badala ya kuwepo kwa mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations).

Kwa maoni yao, basi, bunduki, mabomu, mizinga, na vifaru ni alama za kuwepo kwa "usalama" na "amani" nchini mwetu, kama tunakubaliana na fasili isemayo kwa "peace is the tranqulity of [social, political and economic] order," kama asemavyo Mtakatifu Agustino, kwenye kitabu chake kiitwacho "The City of God," sehemu ya 19 sura ya 13.

Dhana ya "amani kama utulivu wa utaratibu za kisiasa, kiuchumi na kijamii" ni ufafanuzi unaotambulika sana, hasa unaohusishwa na Mtakatifu Augustino wa Hippo.

Inasisitiza umuhimu wa jamii iliyo na utaratibu wa haki katika kufikia amani, inayojumuisha nyanja za kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

Utulivu huu, kulingana na Augustine, linahakikisha kwamba kila kitu, ikiwa ni pamoja na wanadamu, kina nafasi na kazi yake maalum katika jamii, na huchangia katika kusababisha hali ya amani.

Kwa sababu hii vibwagizo kama vile "nchi yetu ni kisiwa cha amani," "mkoa wetu uko salama" na "nchi yetu iko salama" havikomi midomoni mwao, wakati mahali pasipo na "amani ya moyo" hakuwezi kuwa na "usalama" wa kweli.

Kwa hakika, wanasahau kwamba, historia inaonyesha kuwa mapanga, mikuki, virungu, nyundo na mashoka ni silaha za vita zilizo mbadala wa bunduki, mabomu na vifaru, na kwamba, silaha hizi zikitumiwa na watu wa kawaida waliopoteza matumani zinaweza kuua watu 10,000 kwa siku, kwa miezi mitatu mfululizo, kabla ya bunduki, vifaru na mizinga havijatumika kubadilisha upepo.

Kwa maoni yangu, matukio niliyoyataja hapo juu yanawaalika wanazuoni, na hasa wale waliosomea kwenye Chuo cha Ulinzi cha Taifa la Tanzania pamoja na Vyuo vya Idara ya Usalama wa Taifa tulivyo navyo, kutafakari kwa kina, tena bila jaziba, juu ya hatari zinazoambatana na ubaguzi wenye msingi wake katika itikadi za kitabaka kama sababu ya kuanguka kwa dola.

1748451127090.png

III. Kanuni za mahusiano yenye afya kati ya raia, wanasiasa na majeshi

Kusema kwamba, kwa kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Kiliberali na ya Kidemokrasia, inapswa kuwa na wasifu wa kisiasa unaoakisi uwepo wa mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations) badala ya kuwepo kwa mahusiano ya kihasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations), ni namna nyingine ya kusema kwamba zipo nadharia nyingi zinazoongoza mahusiano kati ya raia na vyombo vya usalama, na kwamba, kila Taifa linapaswa kuchagua nadharia inalifaa kulingana na matakwa ya umma.

Hivyo, katika sehemu hii nitaeleza kwa ufupi nadharia hizo, ili kuonyesha kwamba Tanzania tunapaswa kuongozwa na nadharia inayohimiza mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama, na sio vinginevyo.

III. Methodolojia

Napendekeza kwamba, tunapaswa kuhoji na kujibu kwa ukamilifu na kwa haraka swali lifuatalo:

Tanzania ya Nyerere, ambayo ni Jamhuri ya Demokrasia ya Kiliberali, imefikaje mahala hapa ambako inatawaliwa kiimla, kinyume cha katiba ya nchi, na tunapaswa kufanya nini ili kuirudisha kwenye misingi asilia ya kikatiba kabla Taifa halijatumbukia kwenye machafuko ya kiraia?

Makala hii ni mchango wango katika kujibu swali hili. Nimetumia mfano wa anguko la dola kutokana na matukio ya uhasama wa kitabaka nchini Rwanda yaliyoanza mwaka 1959 na kuhitimishwa na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.
Kwa ajili ya kujibu swali hili, maswali madogo yafuatayo yalijibiwa kwa kuchunguza fasihi andishi yenye kuaminika zilizoorodheshwa kwenye kipengele cha "marejeo" mwishoni mwa makala hii:
  1. Wazo la kufanya mauaji ya halaiki, kama ilivyotokea nchini Rwanda, hutoka wapi, kwa maana ya nini asili ya nia ya kutekeleza mauaji ya kimbari?
  2. Kwa nini mauaji ya halaiki yalifanywa nchini Rwanda, katika wakati huo, kwa maana ya kipindi cha 1990-1994 na sio kabla au baada ya hapo?
  3. Mauaji ya halaiki ya Rwanda yalitekelezwaje, kwa maana ya nani alihamasishwa kushiriki, ni rasilimali gani zilikusanywa lini na wapi, na wauaji walitoka wapi?
  4. Kwa nini kampeni na utekelezaji wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ulifanikiwa sana kiasi cha kuwateketeza robo tatu ya Watusi wote wa Rwanda?
  5. Wanawake walishiriki vipi katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda na sababu zilizowasukuma kushiriki katika utekelezaji wa mauaji ni zipi?
  6. Tunajifunza nini kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda?
1747912499740.png

IV. Historia fupi ya mauaji ya halaiki huko Rwanda

Kulingana na kitabu cha Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007:27-34), "The Failure to Prevent Genocide in Rwanda," wakati wa pilika za Mkutano wa Berlini (1884-85) kwa ajili ya kuligawanya Bara la Afrika kati ya mamlaka tofauti za Ulaya, Rwanda iligawiwa kwa Ujerumani.

Baada ya Vita Kuu ya Pili mwaka 1918, utawala wa Wajerumani ulirithiwa na Wabelgiji. Utekelezaji wa sera za Ubelgiji ulitumia utawala wa Watutsi uliokuwepo.

Hivyo Wabelgiji waliwapa Watusi mamlaka juu ya Wahutu katika maisha ya kila siku, japo Watusi walikuwa 14% ya raia, wakati Wahutu walikuwa 85%, na Watwa wakiwa 1%.

Kwa ajili ya kuwatofautisha watu hawa, mwaka 1933, Wabeligiji walianzisha vitambulisho vya uraia vilivyowatofautisha wananchi kwa misingi ya Uhutu, Utusi na Utwa. Wahutu hawakufurahia ubaguzi huu wa kimfumo dhidi yao.

Hivyo, mwaka 1957 Wahutu waliunda chama cha siasa cha kikabila kwa ajili ya kutetea haki zao, kikaitwa “Party for the Emancipation of the Hutus (PARMEHUTU), na kutangaza “Ilani ya Amri Kumi za Wahutu” iliyowataja Watusi kama "wavamizi kutoka ng’ambo."

Mwaka 1959-61, Wahutu waliasi dhidi ya Wabeligiji na wasaidizi wao wa Kitusi, ambapo Watusi wapato 100,000 waliuwawa, na himaya ya kifalme ya Watusi kuangishwa na Wahutu.

Kisha Watusi wapatao 150,000 walikimbilia Uganda na wengine kuingia Tanzania. Kwa njia hiyo, himaya ya Watusi wa Rwanda ikawa imeangushwa kijeshi na Wahutu.

Hatimaye, mwaka 1962 Wabelgiji walitoa uhuru kwa Rwanda ikiwa chini ya uongozi wa Rais Gregoire Kayibanda, Mhutu, Rwanda ikiwa na muundo wa serikali ya Jamhuri.

Yaani, utawala wa Kifalme chini ya Watusi ulikoma na kuzaliwa kwa utawala wa Jamhuri chini ya Rais Mhutu, Kayibanda, ambaye hata hivyo, alianza kutekeleza sera za kulipiza kisasi kwa Watusi, kinyume na matakwa ya kanuni za Jamhuri.

Watusi wengi walikimbilia nchi jirani za Uganda, Burundi, Tanzania na Zaire. Wakiwa uhamishoni Watusi walikusanya nguvu pole pole katika maeneo hayo na kuunda jeshi lenye nguvu.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 jeshi la Watusi lilikuwa tayari kuivamia Rwanda na kuweka serikali ya Watusi ili kujipatia makazi ya uhakika.

Wahutu wakitishwa na uwezekano wa kurudi kwa maadui zao Watusi, walihimiza kimya kimya kuundwa kwa vikundi vya watekaji, watesaji na wauaji, ikiwa ni pamoja na kikundi cha Interahamwe.

Kazi ya vikosi hivi ilikuwa ni ama kuwafukuza au kuwaua Watusi waliobaki nchini twanda, pamoja na kuwaua Wahutu wenye msimamo wa wastani. Uhasama huu uliendelea hadi mwaka 1994 mauaji makubwa ya kimbari yalipotokea.

Saa 2.25 usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, makombora mawili ya kurushwa kutoka ardhini hadi angani yalipiga ndege iliyokuwa imewabeba Marais Juvenal Habyarimana wa Rwanda na Cyprien Ntaryamira wa Burundi, ikiwa inajaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali. Watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo waliuawa.

Viongozi wa Kihutu waliwashutumu Watusi kwa kumuua Rais wao, na raia wa Kihutu waliambiwa kwa njia ya redio na mdomo kuwa ni jukumu lao kuwaangamiza Watusi.

Hivyo, ndani ya saa chache, mashambulizi ya mauaji yalizuka nchini Rwanda ambayo, kwa muda wa miezi mitatu iliyofuata, yaani siku 90, yalisababisha vifo vya watu wapatao milioni moja, sawa na wastani wa vifo vya watu 10,000 kila siku.

Wanaume ambao walikuwa wamezoezwa kuua walikuwa washiriki wa kikosi cha mauaji ya raia kilichoitwa “Interahamwe.”

Serikali ilitoa usaidizi na wanasiasa, maafisa, wasomi na askari wenye taaluma waliwachochea wauaji kufanya kazi yao. Maafisa wa kila eneo walisaidia kuwakusanya waathiriwa na kuwaweka mahali panapofaa kwa ajili ya kuchinjwa.

Watutsi wanaume, wanawake, watoto na watoto wachanga waliuawa katika maelfu yao katika shule na makanisa. Mara nyingi wauaji walikuwa watu wanaowajua, wakiwemo majirani, wafanyakazi wenza, marafiki wa zamani, wakati mwingine hata jamaa kupitia ndoa.

Radio FM iitwayo RTLM ilitumika kutoa matangazo ya orodha ya watu wanaopaswa kuuwawa, na mahali wanakopatikana.

Kwa ujumla, mauaji ya halaiki yalitekelezwa na Wahutu dhidi ya Watusi, kwa kutumia silaha rahisi zinazopatikana katika kila kaya.

Silaha hizo ni pamoja na mapanga, marungu na majambia, nyundo, mashoka, na sululu. Baada ya jeshi, chini ya Meja Jenerali Kagame, kuingilia kati na kuwanyang'anya "silaha zao" wananchi hawa, ndipo mauaji yalikoma.

Mwaka 2003, Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa liliitangaza tarehe 7 Aprili kila mwaka kuwa ni siku ya kufanya tafakari juu ya siasa za ubaguzi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya Wahutu na Watusi nchini Rwanda. Ubaguzi huu ulikuwa chimbuko la mauaji ya KImbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Baadaye, mwaka 2004, Todd Salzman aliitikia wito wa Umoja wa Mataifa kwa kufanya tafakari kuhusu chimbuko la mauaji haya na kutusaidia kujua mengi. Makala yake imeambatanishwa mwishoni mwa andiko hili.

Kwa ufupi, Salzman(2004) anasema kuwa ukimya wa Kanisa Katoliki pamoja na uamuzi wake wa kusimama upande wa watawala wa Watusi waliokuwa wanafanya ukandamizaji dhidi ya Wahutu ulichukua miaka 30 kabla ya Kanisa Katoliki kugundua na kukiri hadharani kuwa linaumwa ugonjwa wa kushirikiana na tabaka la watawala wakatili.

Anaongeza kusema kwamba, wakati Kanisa Katoliki lilipogundua na kukiri ukweli huo hadharani tayari lilikuwa limechelewa sana kuweza kuchukua hatua stahiki za kuzuia mauaji ya halaiki yaliyotokea mwaka 1994.

Jambo jingine kubwa tunajifunza kutokana na mauaji ya Rwanda ni kwamba uovu huenea pale watawala wanapoubariki.

Katika mfululizo wa mahojiano na wakulima kumi ambao walikuwa wauaji wa umati katika mauaji ya kila siku ya Rwanda, Jean Hatzfeld (2005), katika kitabu chake, “Machete Season: The Killers of Rwanda Speak,” anatoa taswira ya wazi ya mojawapo ya visa vya uhalifu vilivyokithiri vya kisasa.

Wakulima hawa, ambao waligeuka kwa urahisi na haraka wakawa wauaji wa watu wengi, hawakuhitaji kutokujulikana ili kutoa kifunua uovu wao walioutenda.

Badala yake, wanasema wazi kuwa, zamu zao za kutenda maovu zilisitawi chini ya maagizo kutoka kwa mamlaka za mitaa, kwa kuungwa mkono sana na jumuiya yao na wale walio karibu nao, na wakati huo huo wakiendelea na maisha yao ya kawaida sana, ya nyumbani, tena maisha mema. Kuhusu jambo hili, mmoja wa wauaji wa wakulima wengi alisema haya:
"Baadhi ya wakosoaji wanadai kwamba tulibadilika na kuwa wanyama wa mwituni, kwamba tulipofushwa na ukatili. Hiyo ni hila ya kupotosha ukweli. Ninaweza kusema hivi:
“Nje ya mabwawa ya damu, maisha yetu yalionekana kuwa ya kawaida kabisa. Tuliimba kwenye njia, tulikuwa na chaguo letu huku tukiwa na akili timamu.
“Tulizungumza juu ya bahati yetu nzuri, tuliondoa madoa yetu ya damu kwenye pua zetu na kufurahia kupika kwenye beseni. katika maisha mapya yaliyokaribia kuanza kwa kula mguu wa nyama ya ng'ombe.
“Usiku tulikuwa na fursa ya kufanya tendo la ndoa na wake zetu, na tuliwakemea watoto wetu wakorofi.”

Kuna simulizi la kihistoria lenye kusisimua kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda. Limesimuliwa na Immaculee Ilibagiza (2007), kupitia kitabu chake, "Left to Tell: Discovering God amidst the Rwandan Holocaust". Imaculee anasema:
“Sauti zao zilikuwa kavu, kakamavu, na zenye kudhamiria. ‘Yuko hapa, tunajua yuko hapa mahali fulani. Mtafute, mtafute Immaculée.’ Kulikuwa na sauti nyingi, wauaji wengi. Niliweza kuwaona akilini mwangu.”
“Marafiki na majirani zangu wa zamani, ambao siku zote walikuwa wananisalimia kwa upendo na fadhili, wakipita katikati ya nyumba wakiwa wamebeba mikuki na mapanga na kuita jina langu.” ‘Nimeua mende 399,’ akasema mmoja wa wauaji. ‘Immaculée atakuwa wa 400. Ni nambari nzuri kuua’.
"Nilijiinamia kwenye kona ya bafu letu dogo la siri bila kusogeza hata msuli. Kama wale wanawake wengine saba waliojificha nami ili kuokoa maisha yetu, nilishusha pumzi pole pole ili wauaji wasinisikie nikipumua." (Utangulizi, uk.1)
1747912562498.png

V. Hatua saba za kupanga na kutekeleza mauaji ya Rwanda

Kulingana na Jean Mukimbiri (2005), mauaji ya halaiki ya Rwanda yalipangwa na kutekelezwa katika hatua saba.

Mosi, ni kutengeneza matabaka (classification/redefinition): Hapa kuna kubainisha tabaka la watu wanaopaswa kuuwawa kwa kutumia sifa maalum za kimaumbile, na hivyo kufanikisha dhana ya "sisi dhidi ya wao". Ilani ya Wahutu ya mwaka 1957 ilitumika kufanya kazi hii nchini Rwanda kwa kuwataja Watusi kama "wavamizi kutoka ng'ambo."

Pili, ni kutengeneza vitambulisho maalum kama alama ya utofautisho rasmi (registration/symbolisation): Tabaka la watu wanaolengwa walipewa vitambulisho vyenye majina maalum, ambapo kwa mujibu wa sensa iliyofanyika vitambulisho vya uraia vilitofautisha Wahutu (85%), Watusi (14%) na Watwa (1%).

Tatu, ni kudhalilisha utu wa walengwa Watusi (dehumanisation): Watusi walibatizwa majina yanayowaondoa kwenye kundi la watu na kuwaweka kwenye kundi la wanyama, wadudu au virusi, kama vile "panya" na "mende." Huu ulikuwa mkakati wa kuwaandaa wauaji kisaikilojia ili waamini kwamba kuua "mende" sio jinai wala dhambi, maana "mende" sio watu.

Nne, ni kuporwa mali na ardhi (confiscation): Watusi walinyang'anywa ardhi na mali na zikagawiwa kwa Wahutu; na waliondolewa kwenye mpango wa pensheni, lengo likiwa kuwadhoofisha kiuchumi.

Tano, ni ubaguzi wa rejareja wa kiuchumi, kisiasa na kijamii (sporadic exclusion): Watusi walibaguliwa katika nafasi za uteuzi wa kiserikali, kwenye vyuo walinyimwa fursa ya kupanda madaraja ya kitaaluma kama vile kutoka udaktari kwenda uprofesa, kwenye ajira nako walienguliwa kila walipoomba kazi.

Sita, ni ubaguzi wa kimfumo kwa ajili ya kuwatenga walengwa na jamii baki (systematic isolation): Wakati huko Ujerumani zilijengwa kambi za mauaji, Rwanda kambi za mauaji zilikuwa makanisa, viwanja vya mpira, na mashule. Redio zilitumika kuwalaghai walengwa waende maeneo hayo kwa ajili ya usalama wao kumbe walikuwa wanajipeleka machinjioni.

Na saba, ni utekelezaji wa mauaji (extermination): Vikosi vya Interahamwe vilitekeleza mauaji chini ya mwongozo wa viongozi wakuu wa serikali. Tayari vilikuwa vimepewa mafunzo na vitendea kazi mapema kwa ajili hii.

Kutokana na mtiririko huu wa matukio ni wazi kwamba, mauaji ya halaiki yanaweza kuzuilika kama kuna utashi wa kisiasa kutoka kwa watu ambao bado wanaongozwa na hulka ya kiu ya haki. Nchini Rwanda walikosekana watu wa aina hii kwa kipindi cha miaka 40, yaani tangu 1926 mpaka 1994. Hili ni somo kubwa.

1747912613959.png

VI. Sababu za Vyombo vya Usalama Kushindwa Kuzuia Mauaji ya Rwanda
Kulingana na Walter Dorn, Jonathan Matloff na Jennifer Matthews (2000), mambo matatu yalikuwa muhimu kwa ajili ya kuzuia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Mambo hayo ni uwezo wa kijasusi kwa ajili ya kupata taarifa za onyo la mapema na hivyo kupanga kuzuia; uwezo wa kuchukua hatua za kuzuia, yaani, kuingilia kati; na utashi wa kisiasa wa kutumia hizi njia mbili.

Wanaongeza kuwa, kwa sehemu kubwa, jambo la tatu ndilo ilikosekana Rwanda, kwani mambo mawili ya kwanza yalikuwepo nchini humo.

Ni kwa sababu hii, Swaraj Parameswaran (2024) na Chimene Benningshof (2023), wanasema kuwa, kukosekana kwa utayari wa kusoma alama za nyakati, kutafsiri kwa usahihi na kubaini hatari ya mauaji iliyokuwa inakuja lilikuwa kosa kubwa kuliko kosa la kushindwa kuyazuia mauaji hayo mara tu yalipotokea.

Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007: 63-79), katika kitabu chao, "The Failure to Prevent Genocide in Rwanda," wameeleza kwa ufasaha ukosefu wa utashi wa kisiasa kwa kubainisha taarifa za kijasusi zilizokuwepo Rwanda kabla ya mauaji, taarifa ambazo, kama zingefanyiwa kazi, zingeweza kusaidia kuzuia au kupunguza mauaji hayo.

Kuibuka kwa Wahutu wenye msimamo mkali

Utekaji nyara wa kijeshi, mauaji, uporaji wa Interahamwe ukiwalenga Watusi uliendelea kutoka 1991 hadi 1993.

Mwaka 1992 mauaji ya Watusi yalitambuliwa na wanadiplomasia wa kigeni, ambapo Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Shirika la Amnesty International waliweka mauaji ya Watutsi nchini Rwanda kwenye ajenda zao na kuitaja serikali ya Rwanda na kuwajibika kwa ukatili huo.

Mnamo Agosti 1993, makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Wahutu na Watusi yalifikiwa mjini Arusha nchini Tanzania, na haya yakaitwa Mapatano ya Arusha.

Kama sehemu ya Mapatano haya, Serikali ya Mpito ya Mseto ilipaswa kuundwa, uchaguzi huru wa kitaifa ufanyike, wakimbizi wa Kitutsi warejeshwe makwao nchini Rwanda, na jeshi la Rwanda lingeundwa ambalo lilikuwa na Wahutu na Watutsi.

Lakini, vurugu ziliendelea kabla, wakati na baada ya mazungumzo ya amani ya Arusha kuanzia 1992 hadi 1993, ambapo, Katibu Mkuu wa chama cha Habyarimana alikejeli Makubaliano ya Arusha.

Kwa ajili ya kuvuruga mchakato wa amani chini ya Mapatano ya Arusha, chama tawala kiliwaua kwa umati takriban Watusi 300 wanaoishi Ruhengeri na Gisenyi katika siku za mwisho za Januari 1993.

Kisha, shambulio la ghafla la RPF lilifuata, ambapo, mamia ya watu wakauawa, na wengine kuikimbia nchi.

Ripoti za wanadiplomasia kwa ulimwengu wa nje

Katika miaka iliyotangulia mauaji ya kimbari, jumuiya ya wanadiplomasia nchini Rwanda, maofisa waliokuwa katika mazungumzo ya Arusha na maafisa wa nje ya nchi wanaoshughulikia Rwanda walijua kuhusu kuwepo kwa "Akazu."

Huu ulikuwa mtandao wa karibu wa Wahutu wenye msimamo mkali ambao walikuwa na kikosi chao cha mauaji. Pia Akazu walijukana kama “Mtandao Zero.”

Wanachama wa mtandao wa Akazu walitoka katika familia ya Wahutu iliyoimarishwa vyema ya mke wa Habyarimana, Agathe Kanzinga. Watu muhimu sana wa Akazu walikuwa mashemeji watatu wa Habyarimana, Protais Zigiranyirazo, Kanali Pierre-Celestin Rwagafilitia na Seraphin Rwabukumba.

Mtandao wa Akazu ulikuwa na mawasiliano ndani ya halmashauri za mitaa, wilaya, balozi za Rwanda na watumishi wengi waandamizi wa serikali na maafisa wa kijeshi.

Mapema mwaka wa 1991, tathmini ya kijasusi, iliyoandikwa na wakala wa Ufaransa, ilibainisha mduara wa ndani wa mamlaka ambao ulitawaliwa na Agathe na familia yake.

Kulingana na wakala huyo, mduara wa ndani ulikuwa na lengo la kubakiza mamlaka; aina yoyote ya mazungumzo au jaribio la kulazimisha demokrasia ingechochea upinzani wao, na katika majibu yao wangeeneza hofu. Uchambuzi huu ulitumwa kwa nchi wafadhili mbalimbali.

Katika majira ya Masika ya 1992 Johan Swinnen, balozi wa Ubelgiji nchini Rwanda, aliripoti kwa wizara yake mjini Brussels kuhusu kuwepo kwa "kundi la siri" ambalo lilikuwa "linapanga kuwaangamiza Watutsi."

Ripoti kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu

Katika miaka ya kabla ya mauaji ya kimbari ya 1994, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kama mashirika ya misaada na mashirika ya haki za binadamu, yalizidi kufanya kazi nchini Rwanda. Waliripoti juu ya mauaji katika sehemu tofauti za nchi na ushiriki wa wanajeshi na viongozi wa eneo hilo.

Mnamo Mei 1992 Amnesty International ilitoa ripoti iliyohusu mateso ya Watutsi na wapinzani wa serikali kati ya 1990 na 1992.

Ripoti hiyo ilizungumzia "kunyongwa kwa njia isiyo ya haki kwa zaidi ya Watutsi 1,000 tangu 1990, kuenea kwa mateso na aina nyingine za unyanyasaji, kutoweka kwa mahabusu, kukamatwa kwa watu wengi na kuzuiliwa au kufunguliwa kesi holela kwa zaidi ya watu 8,000."

Mnamo Januari 1993 muungano wa vyama vya haki za binadamu vya Rwanda ulitoa wito kwa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kuunda tume ya kuchunguza hali ya Rwanda.

Tume hii ilitumia wiki tatu nchini Rwanda, ikiwahoji mashahidi, waathiriwa na familia na kukusanya ushuhuda kuhusu matukio katika miaka miwili iliyopita.

Ripoti hiyo ilichapishwa mapema mwaka wa 1993 na ilizungumzia kuhusu mauaji yanayoungwa mkono na serikali dhidi ya Watusi, mauaji ya Watusi wasiopungua 2,000 na kuwekwa kizuizini kwa Watusi zaidi ya 10,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Tume hiyo ilisema kuwa ngazi ya juu ya mamlaka, akiwemo Rais Habyarimana, inawajibika kwa ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na wanajeshi, wanamgambo na raia.

Ripoti kutoka kwa mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa, Bacre Waly Ndiaye, alifanya uchunguzi nchini Rwanda mwezi Aprili 1993, baada ya kufahamishwa kuhusu madai ya ukiukaji wa haki ya kuishi.

Aliripoti kuhusu unyongaji wa watu unaofanywa kinyume cha sheria. Aliongelea kuhusu "mauaji ya halaiki yanayowezekana." Ripoti ya Ndiaye ilichapishwa Agosti 1993 na Februari 1994 iliwasilishwa rasmi wakati wa kikao cha 50 cha Tume ya Haki za Kibinadamu.

Maonyo ya Human Rights Watch mwaka 1993 na 1994

Shirika la Human Rights Watch lilitoa ripoti mbili zinazohusu hali mbaya nchini Rwanda: moja Juni 1993 na nyingine Januari 1994.

Ripoti ya Juni 1993 ilieleza kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Rwanda tangu Oktoba 1990. Watutsi na watu wote walioitwa "washiriki wa RPF” waliishi katika ukosefu wa usalama kila mara, wakishambuliwa majumbani mwao au kudhulumiwa.

Ripoti ya pili ya HRW, iliyochapishwa miezi miwili na nusu kabla ya kuzuka kwa mauaji ya kimbari, iliitwa "Msimu wa Silaha Rwanda." Ripoti hiyo ilitoa mtazamo wa kina wa utitiri wa silaha kutoka mataifa ya kigeni nchini kwenda Rwanda.

Maonyo ya CIA ya Amerika mnamo 1993 na 1994

Kabla ya mauaji ya halaiki, CIA ilichapisha ripoti mbili ambazo zilihusu ghasia kubwa na zinazoweza kutokea nchini Rwanda na matokeo yake.

Utafiti wa CIA mnamo Januari 1993 ulizungumza juu ya "uwezekano wa vurugu kubwa za kikabila" na ripoti mnamo Desemba 1993 ilizungumza kuhusu tani milioni 40 za silaha ndogo ndogo ambazo zilihamishwa kutoka Poland hadi Rwanda kupitia Ubelgiji.

Propaganda za chuki kupitia magazeti

Sehemu muhimu za propaganda za chuki dhidi ya Watusi zilifanyika kupitia habari na makala za magazetini.

Gazeti la “Kangura,” jina likimaanisha "waamshe wengine," lilikuwa gazeti la kibaguzi zaidi nchini Rwanda. Lilianza kuchapisha miaka minne kabla ya kuzuka kwa mauaji ya halaiki na likawa na vurugu zaidi katika matamshi yake kuelekea Aprili 1994.

Gazeti hilo lilikuwa na matoleo mawili, moja kwa Kinyarwanda na jingine kwa Kifaransa. Kangura lilifadhiliwa na watu wa ngazi za juu za utawala wa Habyarimana. Lilikuza taifa la Wahutu kwa kuchochea chuki na jeuri ya kikabila dhidi ya Watusi.

Mnamo Desemba 1990, gazeti la Kangura lilichapisha makala yenye tamko la "Amri Kumi za Wahutu," ikiwa ni "Wito kwa Dhamiri ya Wahutu" dhidi ya ukatili wa Watusi.

Amri hizo zilionyesha Watusi kama maadui, watu waovu, wasio waaminifu na wenye tamaa kubwa. Amri zilisisitiza juu ya haja ya kudumisha "usafi wa Kihutu na kuepuka uchafuzi wa kinasaba kutoka kwa Watutsi."

Katika ukamilifu wake, Amri Kumi za Wahutu, zilizochapishwa gazetini mwaka 1990, zilisomeka kama ifuatavyo:

  1. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba mwanamke wa Kitutsi, hata awe nani, anafanya kazi kwa maslahi ya kabila lake la Kitutsi. Kama matokeo, tutazingatia msaliti Mhutu yeyote anayeoa mwanamke Mtutsi, kuajiri mwanamke wa Kitutsi kama suria, kuajiri mwanamke wa Kitutsi kama katibu au kumchukua chini ya ulinzi.
  2. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba binti zetu Wahutu wanafaa zaidi na waangalifu zaidi katika jukumu lao kama mwanamke, mke, na mama wa familia. Ni makatibu wazuri, wazuri na waaminifu zaidi.
  3. Wanawake wa Kihutu, watakuwa macho na kujaribu kuwarudisha waume zao, kaka, na wana wao wa kiume kwenye akili zao.
  4. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba kila Mtutsi si mwaminifu katika biashara. Lengo lake pekee ni ukuu wa kabila lake. Matokeo yake, Mhutu yeyote anayefanya yafuatayo ni msaliti: anashirikiana na Watutsi katika biashara; anawekeza pesa zake au pesa za serikali katika biashara ya Watutsi; kukopesha au kukopa pesa kutoka kwa Mtutsi; inatoa upendeleo kwa Watutsi katika biashara kama vile kupata leseni za kuagiza, mikopo ya benki, maeneo ya ujenzi, masoko ya umma, nk.
  5. Nyadhifa zote za kimkakati, kisiasa, kiutawala, kiuchumi, kijeshi na kiusalama zinapaswa kukabidhiwa kwa Wahutu pekee.
  6. Sekta ya elimu ikijumuisha wanafunzi wa shule, wanafunzi na walimu lazima wawe Wahutu walio wengi.
    Wanajeshi wa Rwanda wanapaswa kuwa Wahutu pekee. Uzoefu wa vita vya Oktoba 1990 umetufundisha somo. Hakuna mwanajeshi atakayeoa mtutsi.
  7. Wahutu waache kuwahurumia Watutsi.
  8. Wahutu, popote walipo, lazima wawe na umoja na mshikamano na wawe na wasiwasi na hatima ya ndugu zao Wahutu. Wahutu wa ndani na nje ya Rwanda lazima daima watafute marafiki na washirika kwa ajili ya Wahutu, kuanzia na ndugu zao Wahutu. Ni lazima wakabiliane na propaganda za Watutsi kila mara. Wahutu lazima wawe imara na macho dhidi ya adui wao wa kawaida wa Kitutsi.
  9. Mapinduzi ya Kijamii ya 1959, Kura ya Maoni ya 1961, na Itikadi ya Wahutu, lazima ifundishwe kwa kila Mhutu katika kila ngazi. Kila Mhutu lazima aeneze itikadi hii kwa upana. Mhutu yeyote anayemtesa ndugu yake Mhutu kwa sababu ya kusoma, kueneza na kufundisha itikadi hii ni msaliti.
Hivyo, gazeti la Kangura lilieneza dhana kwamba "Watusi walikuwa wakitayarisha vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wahutu ambavyo havitaacha mtu yeyote" na kwamba jeshi la "RPF ilitaka kuanzisha tena ufalme wa Watutsi na kuwafanya Wahutu kuwa watumwa."
Mhariri mkuu wa gazeti la Kangura, Hassan Ngeze, alipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu mwaka 2003 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda na alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela.

Propaganda za chuki kupitia redio

Sehemu muhimu za propaganda za chuki dhidi ya Watusi zilifanyika kupitia matangazo ya redio pia.

Redio maarufu ya kueneza chuki, "Radio Television Libre des Milles Collines (RTLMC)" ilianzishwa na Wahutu wenye msimamo mkali kama "sauti ya itikadi kali."

Kwa sababu ya mtindo wake usio rasmi wa utangazaji, pamoja na muziki wa kufoka na lugha ya mitaani, kituo kilivutia wasikilizaji wengi na tofauti.

Kama ilivyokuwa kwa gazeti la Kangura, Redio ya RTLMC ilifadhiliwa na Wahutu wenye msimamo mkali. Wanachama wote wa Akazu walikuwa wanahisa wa RTLMC, huku Habyarimana akiwa ndiye mwenye hisa nyingi zaidi.

Madhumuni ya redio hiyo yalikuwa kuanzisha kampeni ya kuwachafua Watusi na kueneza ujumbe hasi dhidi ya maafikiano ya Arusha.

Redio ya RTLMC ilizidi kuwa na vurugu katika utangazaji wake. Kwa mfano, tarehe 26 Novemba 1993, RTLMC ilitoa wito wa kuuawa kwa viongozi wa upinzani, na kuangamizwa kwa Waziri Mkuu Agathe Uwilingiyamana na Waziri Mkuu mteule Twagiramungu.

Marc Nees, ambaye alifanya kazi kama afisa wa ujasusi wa jeshi la Ubelgiji nchini Rwanda kuanzia Novemba 1993 hadi Machi 1994, alisema katika ushahidi wake mbele ya Seneti ya Ubelgiji kwamba:

"Nina hakika kwamba kama tungesimamisha RTLMC tungekuwa na nafasi zaidi ya kuzuia mauaji ya kimbari, au angalau kuyapunguza."

Ushahidi wa mdomo kutoka kwa Msiri

Taarifa za kijasusi zilizokuwa muhimu na zenye kuaminika zilikuja kwa njia ya mdomo kutoka kwa msiri mmoja, Januari 1994.

Huyu alikuwa ni Afisa Usalama aliyekuwa anafanya kazi kwa ukaribu na Rais Habyarimana, akiwa amepewa jukumu la kutoa mafunzo maalum kwa kikundi cha Interahamwe. Alijitambulisha kwa jina la “Jean Pierre.”

Piere alimfahamisha Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, UNAMIR, Dallaire, kwamba, dhamiri yake ilikuwa inamsuta maana amepewa kazi asiyotaka kuifanya.

Kazi yake ilikuwa ni kusambaza silaha kwenye vitongoji vya Kigali, kuandaa orodha ya watusi wote wanaokaa kwenye vitongoji hivyo, na kuwa tayari kuwaua pale atakapopewa amri ya kufanya hivyo.

Alikuwa tayari kufichua maeneo yaliko mghala ya silaha alizokuwa anasambaza, lakini kwa sharti kwamba apewe hifadhi ya kisiasa nje ya Rwanda.Kwa mujibu wa Piere, mtandao wa Interahamwe aliokuwa amekwishatengeneza na kukabiodhi silaha ulikuwa na uwezo wa kuua wati 1,000 kwa kila dakika mbili.

Wakati Piere alikuwa tayari kushiriki mapambano dhidi ya jeshi la RPF, hakuwa tayari kutekeleza mauaji ya Watusi wasio na hatia.

Piere alifafanua kwamba, viongozi waliokuwa nyuma ya mpango huo ni pamoja na viongozi wa chama tawala cha Rais Habyarimana.

Majumuisho muhimu

Kwa taarifa hii, ukweli ulikuwa wazi kwamba kuna mauaji ya halaiki yanaandaliwa na watawala, ambao kwa sababu hiyi wasingeweza kuwa sehemu ya kutyazuia.

Na kwa ujumla, utafiti wa Shirika la Human Rights Watch (1999), wenye kichwa cha maneno "Leave None to Tell the Story: Genocide in Rwanda," umeeleza vizuri sana ushiriki wa vyombo vya dola na wanasiasa katika mauji ya Rwanda ya mwaka 1994.

Muundo mzima wa serikali ya Wahutu kuanzia Ikulu mpaka serikali ya mtaa ulishiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mauaji. Kwa hiyo, mauaji ya Rwanda yana mengi ya kutufundisha hata leo, hasa hapa Tanzania.

Kwa sehemu kubwa, Idara ya Usalama wa Taifa ya Rwanda, Jeshi la Wananchi la Rwanda na Jeshi la Polisi la Rwanda, ni vyombo ambavyo viliungana pamoja katika kupanga na kutekeleza mauaji ya Watusi.

Hivyo, fundisho moja kubwa ni kwamba, vyombo vya ulinzi na usalama vinavyofuata amri za watawala wakati amri hizo zinakiuka misingi ya utu, na kusigina Katiba ya nchi, yenye kuongelea utaifa badala ya ukabila, vinaweza kulitumbukiza Taifa katika vita ya wenywe kwa wenyewe.

1748184028496.png

VII. Mafundisho Kuhusu Utu wa Binadamu Katika Rwanda ya Kale

Kila jamii inayo mafundisho yake kuhusu hulka ya utu wa Kimungu, utu wa malaika, utu wa binadamu, na utu wa majini. Hapa naongelea hulka ya utu wa binadamu, yaani, hulka ya “mtu” aitwaye “binadamu.”

Mafundisho kuhusu hulka ya utu wa kibinadamu huwavutia na kuwaunganisha watu wengi kwa sababu yanahusu maumbile yao wenyewe.

Hivyo, tangu zamani watu tofauti wamejaribu kujiuliza na kujibu maswali kama vile: Mtu anayo hulka ya namna gani? Mtu ana thamani gani? Mtu alitoka wapi? Mtu atakwenda wapi? Uhai wa mtu ulitoka wapi? Na mambo mengine mengi yanayohusiana na uwepo wa watu.

Taaluma inayohusika na kujibu maswali haya huitwa anthropolojia, na inayo matawi mengi kulingana na mwegemeo wake wa kihistoria.

Kwa ujumla, kuna “anthropolojia ya kisayansi,” “anthropolojia ya Kikristo,” “anthropolojia ya Kiislamu,” “anthropolojia ya Kihindi,” “anthropolojia ya Kibantu,” “anthropolojia ya Kiarabu,” “anthropolojia ya Kizungu,” “anthropolojia ya Kigriki,” “anthropolojia ya Kipolandi,” “anthropolojia ya Kinyarwanda,” na orodha inaendelea.

Kinachotuhusu hapa ni “anthropolojia ya kinyarwanda.” Kulingana na Philip Verwimp(2013:6), anthropolojia ya kinyarwanda ilikuwa ni ya kitabaka.

Yaani, baadhi ya Watusi walifundishwa kuwa wao ni wana wa uzao bora wa Ham na kuwa Wahutu ni wana wa uzao uliolaaniwa wa Shem.

Hivyo, Watusi wakawa wanawaona Wahutu kama watu walio na haki kidogo kuliko haki walizo nazo Watusi. Kwa mujibu wa Biblia, Ham na Shem ni Wana wa Noah (Mwanzo 9:20-27).

Walisahau fundisho jingine muhimu la Biblia lisemalo kwamba Wahutu na Watusi "wameumbwa kwa mfano wa Mungu mmoja." Hata Wamisionari wa Kanisa Katoliki walisahau kusisitiza ukweli huu.

Ukweli ni kwamba, viongozi wa Rwanda, Watusi na Wahutu, kwa nyakati tofauti, walifanya makosa ya kukweza:
  1. mauti juu ya maisha;​
  2. uwongo juu ya ukweli;​
  3. ujinga juu ya maarifa;​
  4. haki juu ya dhuluma;​
  5. utumwa juu ya uhuru;​
  6. ukoloni juu ya ukombozi;​
  7. unyama juu ya utu;​
  8. uhuni juu ya ustaarabu;​
  9. uadui juu ya urafiki;​
  10. chuki juu ya upendo;​
  11. hofu juu ya matumaini;​
  12. dharau juu ya heshima;​
  13. udini, ukabila, ukanda na uchawa juu ya Utaifa;​
  14. mabavu juu ya maridhiano;​
  15. maombolezo misibani juu ya shangwe za harusini;​
  16. ubaya juu ya wema;​
  17. umaskini juu ya utajiri;​
  18. mbinu haramu juu ya mbinu halali;​
  19. malengo ya muda mfupi juu ya malengo ya muda mrefu;​
  20. malengo haramu juu ya malengo halali; na​
  21. kwa ujumla walikwenza tunu hasi juu ya tunu chanya.​
Katika muktadha huu, jambo muhimu sana ambalo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vya Rwanda vilishindwa kuelewa ni nafasi ya tunu za kiutu katika maisha ya watu viliopaswa kuwalinda.

Nitaeleza kwa kifupi sana. KIla mfumo wa maadili unazo sehemu kuu tatu zifuatazo:
  1. Seti ya tunu chanya za kiutu;
  2. Seti ya majukumu na haki; na
  3. Chimbuko la tunu, majukumu na haki.
Mosi, kuna seti ya tunu za kiutu ambazo huonyesha ni malengo gani yanayopaswa kufukuziwa na watu kwa ajili ya kufanikisha ustawi wao, mfano ni afya, elimu, uhuru, usawa, mali, na ukweli.

Yaani, tunu za kiutu huwawezesha wananchi kujua malengo gani wayafukuzie kwa sababu yanawasaidia kustawi, malengo yapi wayaepuke kwa sababu yanawazuia kupata ustawi, watu gani wafungamane nao, na watu gani wawaepuke.

Pili, kuna seti ya haki na majukumu, yenye kujumuisha makatazo na miongozo ya kiutendaji inayoeleza matendo gani yanaruhusiwa na matendo yapi yanakatazwa.

Seti ya kanuni za haki na majukumu hutaja mbinu za kukuza na kuhami tunu za kiutu. Mbinu zinazohujumu tunu za kiutu huitwa mbinu haramu, wakati mbinu zinazostawisha tunu za kiutu huitwa mbinu halali.

Na tatu, kuna msingi wa tunu, haki na majukumu tajwa, mara nyingi, msingi huo ukiwa unatokana na mtazamo wa jamii kuhusu swali lifuatalo: Utu ni kitu gani, viumbe gani ni watu kamili, na viumbe gani sio watu kabisa? Jawabu kwa swali hili ndio huzaa tunu, haki na majukumu katika jamii husika.

Nitatoa mifano minne kuhusu ututuri wa mafundisho ya jamii kuhusu “mtu” aitwaye “mwanadamu,” ili kuonyesha jinsi yanavyopingana.

Mosi, kama tulivyoona, baadhi ya Watusi wanaojioni kuwa ni wana wa uzao bora wa Ham n kuwaona Wahutu kama wana wa uzao uliolaaniwa wa Shem, wanawaona Wahutu kama watu walio ha haki kidogo kuliko haki walizo nazo Watusi. Hii ndio sababu ya vita ya halaika huko Rwanda.

Pili, baadhi ya Wazungu wanawaona Waafrika kama vile wako kundi moja na sokwe, hivyo wanaona Mwafrika anazo haki chache kuliko Mzungu. Hii ndio sababu kuu ya ukoloni wa mwafrika.

Na tatu, baadhi ya Waarabu wanawaona Waafrika kama vile wako karibu sana na nyani, hivyo wanaona Mwafrika anazo haki chache zaidi kuliko Mwarabu. Hii ndio sababu kuu ya biashara ya utumwa wa mwafrika. Na mifano inaendelea.

Na nne, baadhi ya Waislamu wanawaona Makafiri kama vile ni watu wa daraja la pili walio na haki chache kuliko walizo nazo Waislamu. Hii ndio sababu ya mateso ya Wakristo katika nchi nyingi za Kiislamu.

Kwa sababu hizi zote, jamii yoyote inayokweza tunu hasi juu ya tunu chanya, na kuinua mbinu haramu juu ya mbinu halali, inakuwa imekufa kimaadili, maana haiwezi tena kutofautisha kati ya haki na dhuluma, na hivyo kushindwa kutofautisha kati ya ufalme wa watu (homodomia) na ufalme wa nyani (apedomia).

Tunaweza kuongelea ufalme wa "apedomia" dhidi ya ufalme wa "homodomia," kama alivyowahi kufanya hayati Mtikila, katika hotuba yake moja.

Na ufalme wa apedomia ndiyo ilikuwa sifa kuu ya jamii ya Rwanda kati ya mwaka 1959 na 1994. Tangu wakati huo, Rais Kagame amekuwa katika jitihada za kuikarabati Rwanda ili iondoke kwenye ufalme wa nyani (apedom) na kuingia kwenye ufalme wa watu (human kingdom).

Kutokana na haya yote, somo moja linaibuka. Kila mtaala na kila muhtasari wa elimu ya kitaifa lazima iwasaidie watoto wote kupata jawabu sahihi kwa swali lifuatalo: Utu ni kitu gani, viumbe gani ni watu kamili, na viumbe gani sio watu kabisa?

Yaani, ni lazima iwepo anthropolojia ya kitaifa, yenye uwezo wa kuzikosoa anthropolojia baki, kama ikibidi. Somo la uraia linapaswa kufanya kazi hii. Mwandishi Juan Manuel Burgos(2022) ametoa mfano mzuri wa maudhui ya kuanza nayo.
1747912662627.png

VIII. Ushiriki wa wanawake katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda
Unyanyasaji wa wanawake wakati wa vurugu na vita limekuwa lengo kuu la tafiti nyingi zinazochunguza uhusiano ambao hujitokeza kati ya jinsia na migogoro ya kivita.

Kwa jadi na historia pana, wanawake wamekuwa wakichukuliwa kama wahanga. Lakini, kuna historia inaonyesha ukweli tofauti. Wapo wanawake ambao ama walisaidia watekelezaji wa mauaji, au walifanya utekelezaji wa mauaji moja kwa moja, au waliidhinisha mauaji. Mfano mzuri inapatikana nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Leila Fielding (2014), katika kitabu chake, “Female Genocidaires during the Rwandan Genocide,” huko Rwanda, baadhi ya wanawake hawakutoa tu msaada na kutia moyo wanaume wa Kihutu kufanya uhalifu, bali pia walishiriki moja kwa moja.

Walikuwa wahanga na wahalifu waliofanya mashambulizi na kuchochea ubakaji, wakiwa mawakala wa uovu na alama ya mauti.

Leila Fielding (2014:13) anasema kuwa, kuna wanawake waliokuwa madiwani, walimu na watendaji wa vijiji walioshiriki katika utekelezaji wa mauaji, akimtaja diwani Rose Karaushara wa Kigali aliyeamuru mauaji wa Watusi 5,000.

Aidha, Leila Fielding (2014:19) anafafanua kuwa, mwaka 2002, karibu watu 100,000 walikuwa mahabusu wakisubiri usikilizwaji wa kesi za mauaji ya halaiki, watu 3,000 kati yao wakiwa ni wanawake.

Kati yao, Leila Fielding (2014:26) anaeleza, wanawake 47 walishiriki mauaji kwa kuweka mipango, kuchochea, na kuratibu. Walikuwa na vyeo mbalimbali kwenye vyama vya siasa, jeshini, na kwenye madhehebu ya dini.

Aidha, Leila Fielding (2014:26) anasimulia kisa cha Pauline Nyiramasuhuko, aliyekuwa Waziri wa Familia na na Masuala Wanawake, kama mfano uliokithiri wa mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na wanawake.

Yeye alihamasisha ubakaji na ngono za mateso dhidi ya wanawake Watusi nchini Rwanda. Anafafanuliwa na mashahidi kama mtu aluyekuwa amevaa kombati za kijeshi na kubeba a bunduki akiwa anaamuru vitendo vya mauaji ya kimbari.

Mwenendo wa Nyiramasuhuko ulijumuisha kuweka vizuizi barabarani ili kubaini, kuwateka nyara, kuwabaka na kuwaua watutsi.

Alikuwa akisafiri mara kwa mara katika eneo lake la asili wa Butare katika gari aina ya peugot wakati wa mauaji ya halaiki, likiendeshwa na mwanawe ambaye alikuwa mwanachama mashuhuri wa Interhamwe, na alitumia kipaza sauti kuchochea ubakaji na mauaji ya wanawake wa Kitutsi.

Pauline alishtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, moja kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na lingine kama ukiukaji wa Mkataba wa Geneva wa Uhalifu wa Kivita.

IX. Yaliyotoke Rwanda sasa yanaanza kutokea Tanzania

Lakini, maajabu ni kwamba, yaliyotokea nchini Rwanda kati ya miaka ya 1959 hadi 1994 yanatokea katika Tanzania ya leo, chini ya serikali ya awamu ya sita.

Mnyukano uliopo kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kwa upande mmoja, na misimamo inayochukuliwa na vyombo vya usimamizi wa sekta ya usalama, kwa upande mwingine, ni sura mbili ya hali hiyo.

Kama ilivyokuwa wakati wa uhasama kati ya Wahutu na Watusi huko Rwanda enzi zile, sisi hapa Tanzania tunashuhudia "ubaguzi haramu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii wenye sura ya hawa ni CCM na wale ni Chadema," hasa kwa kutumia kigezo cha tofauti ziliozo katika itikadi za vyama.

Katika mchakato wa kutekeleza ubaguzi dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani chama tawala na serikali yake wanakweza itikadi za vyama juu ya tunu za Kitaifa katika namna ambayo inaonyesha kwamba, ama kwa kujua au kwa kutojua, wanajenga kwa mkono wa kushoto na kubomoa kwa mkono wa kulia.

Vyombo vya dola vya Tanzania vimeigiza tabia ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Rwanda ya miaka ya 1990. Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa sasa inawaruhusu kufanya kazi zote bila kutofautisha kati kazi za polisi wala kazi za JWTZ.

Kwa usahihi, naona kuwa, matukio yafuatayo yanapingana na Kanuni ya Imani ya Utanzania:
  1. Kubinafsishwa kinyemelea kwa Bandari ya Dar es Salaam,
  2. Mauaji ya Ali Mohamed Kibao,
  3. Tamko la Rais Samia kwamba Katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine,
  4. Kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake,
  5. Kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi,
  6. Kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya,
  7. Kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema,
  8. Polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni,
  9. Kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani,
  10. Kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na
  11. Kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua.
  12. Baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwaita baadhi ya Watanzania wanaofanya uanaharakati wa kupoigania haki za watu "kenge," kama alivyotamka Tauhida Galos, Mbunge wa Viti Maalum, Mjini Magharibi, Zanzibar.

1748335457086.png

Mbunge Tauhida anaamini kwamba hata kenge wakitekwa kenge wengine hawastahili hata kuwaulizia au kupiga kelele kuhusu kenge wenzao kupotea.

Kwa maoni yangu, tangu Rais Samia alipotamka kwamba katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine alikuwa amebatilisha kiapo chake na kuanza safari ya kuweka muundo mpya wa kiutawala anaoutaka yeye, na kujenga timu ya kumsaidia kufikia azima yake hiyo.

Lakini, kazi ya kwanza ya vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa ni kulinda katiba ya nchi kwa kulinda "muundo wa serikali" uliotamkwa na wananchi na kuingizwa kwenye katiba ya nchi ambayo haiwezi kubadilishwa na Mahakama, Bunge wala serikali kupitia Baraza la Mawaziri.

Kwa hiyo, tangu siku ile Rais Samia alipotangaza kuukataa ukuu wa kitabu kinachoitwa "Katiba ya nchi" na kuiweka katika daraja moja na vijitabu vingine vinavyoweza kubadilishwa kiholela na mtu yeyote, vyombo vya ulinzi na usalama vilipaswa kujitenga naye na kusimama upande wa katiba ya nchi. Lakini hilo halikutokea na halijatokea mpaka leo.

Huko Rwanda, badala ya kusimama na wananchi wa Kihutu waliokuwa wanateswa na wanasiasa wa Kitusi, viongozi wa Kanisa Katoliki walisimama upande wa watesaji wa Kitusi, wakiwa wanatumia mbinu haramu ya uenjilishaji katika kufukuzia malengo mazuri ya kidini.

Huu ulikuwa ni umachiaveli ukitekelezwa na Kanisa, ama kwa kujua au kwa kutojua. Vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania vinalo somo kubwa kutoka Rwanda. Havipaswi kurudia makosa yaliyofanywa na Kanisa Katoliki.

X. Kanuni ya Imani ya Utanzania, homodomia na apedomia

Kuna tofauti kubwa kati ya matukio ya Rwanda ya miaka ya 1994 na Kanuni ya Imani ya Utanzania. Katiba yetu inataja tunu, haki na majukumu muhimu, na hivyo kutoa mwongozo thabiti kuhusu tofauti kati ya ufalme wa watu (homodomia) na ufalme wa nyani (apedomia).

1747912711644.png

Nafupisha Kanuni ya Imani ya Tanzania hapa chini kwa msaada wa maandishi ya Christopher Wolfe(2006:144-47), katika kitabu chake, "Natural Law Liberalism," na pia kwa msaada wa Bican Sahin (2010), katika kitabu chake, Toleration: The Liberal Virtue." Kwa mujibu wa maandiko haya, Kanuni ya Imani ya Utanzania inaweza kufupishwa kama ifuatavyo:
  1. Usawa wa heshima ya kiutu (human dignity): Watu wote wenye mwili hai unaojumuisha mifupa, nyama na damu inayobeba umeme wa akili na utashi wanastahili kuthaminiwa utu wao kwa usawa, hata kama hakuna watu wawili wanaoweza kuwa na kiwango kile kile cha umeme wa akili na utashi. Hii maana yake ni kwamba ni marufuku kumtumia mtu kama nyenzo ya kufanikisha malengo ya mtu baki bila kuzingatia ukweli kwamba mtu huyo anayo akili, utashi na malengo binafsi yanayopaswa kuzingatiwa mara zote.​
  2. Uhuru wa kujichagulia muundo wa utawala (self-determination): Muundo wa utawala uliopo nchini lazima utokane na maamuzi huru ya watu wanaotawaliwa ukiwa unaonyesha wanataka watawaliwe vipi na hawataki kutawaliwa namna gani.​
  3. Kibali cha watawaliwa kwa watawala (consent of the governed): Watawala wanapaswa kutokana na ridhaa ya watu wanaotawaliwa kupitia chaguzi huru na za haki, zinazofanyika mara kwa mara.​
  4. Haki binafsi na majukumu ya kijamii (individual rights and social responsibilities): Kama jamii inataka kuwa na amani ya kweli lazima kila mtu akubali kwamba kila mtu na kila taasisi inazo haki binafsi na majukumu kwa jamii pana, ambapo majukumu hayo yanamaanisha wajibu wa kuheshimu haki za binadamu baki. Mantiki hapa ni kwamba, haki huzaa amani, amani ni tunda la haki, na haki ni chimbuko la amani.​
  5. Serikali yenye nguvu tosha za kuleta matokeo yanayotakiwa na umma (effective and efficient government): Kuna serikali yenye nguvu za kutosha kutekeleza majukumu iliyokabidhiwa, kwa maana ya uwezo wa kukusanya kodi; kuzuia uhalifu; kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.​
  6. Serikali yenye nguvu zilizowekewa ukomo (limited government): Kuna serikali iliyowekewa mipaka ya kutosha ili kuizuia isivunje haki za raia, ambapo mipaka ifuatayo inahusika: uchaguzi wa mara kwa mara kwa ajili ya kuiwajibisha serikali isiyotekeleza wajibu wake; bunge lenye meno ya kuing'ata serikali; mahakama yenye makucha ya kuikwaruza serikali; wananchi wenye mamlaka ya kumpumzisha kiongozi hata kabla ya msimu mwingine wa uchaguzi kufika (power of recall); taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa; tume huru ya haki za binadamu yenye makucha; na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali yenye meno.​
  7. Usawa mbele ya sheria (equality before the law): Kuna usawa mbele ya sheria kutokana na matakwa ya sheria kuchukua nafasi ya amri zinazotokana na mihemuko binafsi ya watawala, ambapo watu wote na taasisi zote zina hadhi sawa mbele ya sheria, sheria zinatumika kutoa hukumu sawa kwa matukio yote yaliyo sawa, na sheria zinatumika kutoa hukumu tofauti kwa matukio yote yaliyo tofauti.​
  8. Usawa wa fursa badala ya usawa wa matokeo (equality of opportunity): Serikali inalo jukumu la kumweka kila raia huru dhidi ya vikwazo vya kisheria, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambazo ili kwa njia hiyo kumwongezea yamkini ya kufanikisha, kulingana na juhudi binafsi, malengo binafsi aliyojiwekea.​
  9. Ukuu wa ukweli wa kisayansi juu ya ukweli wa kisiasa (superiority of scientific truth over socially constructed truth): Kuna ukuu wa ukweli unaotokana na uchunguzi wa kisayansi dhidi ya ukweli unaojengeka katika jamii kutokana na maamuzi ya vikao vya viongozi au watu maarufu katika jamii.​
  10. Uhusiano kati ya ukweli na ushahidi mpya (Openness of truth to new evidence): Ukweli wa kisiasa, kiuchumi na kijamii unavuvumka kulingana na upatikanaji wa ushahidi mjaraba mpya, bila kujali kwamba ushahidi mpya unapingana na taarifa za kiufunuo yaliyoko kwenye misahafu mbalimbali ya kidini.​
  11. Mshikamano na majukumu ya kijamii (solidarity and social duties): Watu huunda jumuiya kwa ajili ya kutengeneza nguvu za pamoja ili kufanikisha mahitaji ambayo hayawezekani nje ya ushirikiano wa kijumuiya. Hivyo, pamoja na uwepo wa haki binafsi, kila mtu anayo majukumu ya kijamii, ambapo kila mtu anakuwa na wajibu kwa jamii pale anapohitajika kuchangia katika kufanikisha maslahi ya watu wote. Hii ni dhana ya mshikamano.​
  12. Uhuru wa kuabudu (freedom of worship): Mamlaka ya nchi haipaswi kuanzisha dini rasmi wala kufungamana na dini yoyote na kuifanya dini ya kitaifa; kila mwananchi anao uhuru wa ama kunzisha dini mpya, au kuchagua dini waitakayo au kuzikataa dini zote; kuna daraja la ushirikiano kati ya dini na siasa katika mafundisho ya kidini ambayo yanazingatia kanuni za urazini (rational theism); na kuna ukuta unaotenganisha dini na siasa pale ambapo ushirikiano hauwezekani kwa sababu ya mafundisho ya kidini ambayo yanayokiuka kanuni za urazini kutokana na kukweza mapokeo yenye mikanganyiko ya kimantiki juu ya urazini (dogmatic theism).​
  13. Umoja wa Taifa unaoziweka kwapani tofauti za raia wake (superiority of national unity over individual differences): Umoja wa kitu kimoja chenye sehemu nyingi zilizo tofauti hutokana na uwepo wa seti ndogo ya sifa chache zinazofanya kazi kama uzi wa kuziunganisha sehemu kadhaa zilizo na utofauti. Katika siasa za kuendesha nchi inayohusisha watu wanaotofautiana kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili, uzi huo huitwa tunu na majumu ya kitaifa. Hivyo, kwa ajili ya kulinda umoja wa Taifa tunapaswa kukubaliana juu ya uwepo wa soko huru la mawazo tofauti ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kijinsia, kimaadili na kidini, isipokuwa mawazo yale yanayomomonyoa, kudhoofisha au kuua kabisa tunu na majukumu ya kitaifa. Kanuni ya uvumilivu inayo nafasi kubwa katika soko huria la mawazo.​
  14. Ukuu wa Katiba ya nchi juu ya serikali, bunge, mahakama (constitutional supremacy): Katiba ya nchi ni muhtasari wa maamuzi ya pamoja ya watawaliwa, wenye kueleza namna wanavyotaka watawaliwe, katiba hiyo ikiwa inataja tunu na majukumu ya kitaifa yaliyo na nguvu za veto juu ya maamuzi ya serikali, bunge na mahakama.​
  15. Tunu na kanuni za maadili zinazofungua milango ya ushirikiano wa kimataifa (universal values which are friendly to international cooperation): Kutokana na imani juu ya usawa wa hadhi ya kiutu, unaotokana na uwepo wa hazina ya akili na utashi katika mwili wa kila kiumbe chenye kromozomu 46, inawezekana kubuni kanuni za ushirikiano wa kimataifa bila kujali mipaka ya nchi moja moja, na kanuni hizo zinaitwa haki asilia za binadamu.​
1748321810605.png

XI. Muhtasari na hitimisho

Katika makala hii nimeichunguza historia pana ya mauaji ya Rwanda kama ilivyotafitiwa na kina Philip Verwimp(2013), Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007), Salzman (2004), Hatzfeld (2005), Ilibagiza (2007) na wengine ili kujibu maswali yafuatayo:
  1. Wazo la kufanya mauaji ya halaiki, kama ilivyotokea nchini Rwanda, hutoka wapi, kwa maana ya nini asili ya nia ya kutekeleza mauaji ya kimbari?
  2. Kwa nini mauaji ya halaiki yalifanywa nchini Rwanda, katika wakati huo, kwa maana ya kipindi cha 1990-1994 na sio kabla au baada ya hapo?
  3. Mauaji ya halaiki ya Rwanda yalitekelezwaje, kwa maana ya nani alihamasishwa kushiriki, ni rasilimali gani zilikusanywa lini na wapi, na wauaji walitoka wapi?
  4. Kwa nini kampeni na utekelezaji wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ulifanikiwa sana kiasi cha kuwateketeza robo tatu ya Watusi wote wa Rwanda?
  5. Tunajifunza nini kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda?
Kwa maoni yangu, hitimisho kutokana na majibu kwa maswali haya ni kwamba, dawa ya kuepukana na utamaduni wa mauaji ya halaiki, kama yaliyotokea huko Rwanda, ni kusimama kwenye Kanuni ya Imani ya Utanzania, yaani misingi ya Jamhuri ya Kiliberali, kama ilivyotamkwa kwenye katiba ya nchi yetu tangu mwaka 1977.

1748177928412.png

XII. Wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama

Kihistoria, nchini Tanzania, uhusiano kati ya jeshi na siasa, kwa maana ya uhusiano wa kiraia na kijeshi, umekuwa na sifa ya mchanganyiko wa kipekee wa ushirikiano na udhibiti wa kiraia, na kusababisha utulivu wa kiasi.

Wakati jeshi limejumuishwa katika jumuiya za kiraia kupitia miundo kama vile Jeshi la Kujenga Taifa na Wanamgambo wa Wananchi, na wanajeshi wanaofanya kazi wanaweza hata kugombea nyadhifa za kisiasa, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pia limekuwa chini ya uangalizi wa kiraia na halijapata mapinduzi au vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo, napenda kusema kuwa, katika hali ya sasa, jeshi lazima lichukue hatua za makusudi za kusimamia nidhamu ya wanasiasa wa kitaifa, hasa mkuu wa nchi.

Nasema hivi kwa kuwa, naona kwamba mfumo wa vyombo vinavyosimamia sekta ya usalama (security sector governance system) unaumwa ugonjwa wa "umachiaveli," ugonjwa ambao ulikuwa unavisumbua vyombo vya ulinzi na Usalama vya Rwanda katika miaka ya 1959 mpaka 1994.

Tunaisoma historia ili kubaini makosa yaliyofanyika zamani, ili kwa njia hiyo tuweze kuzisoma vizuri alama za nyakati tulizomo, na hatimaye, kuweka mipango iliyo salama kwa ajili ya kesho salama.

Na kutokana na usomaji wangu wa historia naona kuwa ni makosa makubwa kwa Tanzania kuruhusu Mzungu, Mwarabu au Mtusi kukalia kiti cha Urais, Uwaziri, au kiti cha Ukurugenzi wa Idara nyeti, hapa nchini Tanzania.

Namna yao ya kufikiri, kuhukumu na kutenda inapingana kabisa na Kanuni ya imani ya Utanzania, kama ilivyofupishwa hapo juu.

Na kwa kweli, hakuna haja ya taasisi nyeti katika Taifa letu kuongozwa na watu wenye tatizo la ukomo wa kimaarifa usioweza kuboreshwa ("irredeemable cognitive closure") wakati wapo Watanzania wengi wasio na tatizo hilo. Vyombo vya ulinzi na usalama vijisahihishe kabla ya uchaguzi mkuu ujao kwa kumshauri Rais Samia kukaa pembeni.

Uongozi wake wa maumivu ya miaka kumi, chini ya serikali ya awamu ya tano na awamu ya sita umetosha kutusaidia kumwelewa, kumpima na kumhukumu kwa haki, na hukumu.

Na hukumu ni kwamba: Rais Samia hana sifa ya kuitwa mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu wala rais wa nchi inayoitwa Tanzania. Mawazo, maneno na matendo yake yanapingana wazi wazo na Kanuni ya Imani ya Utanzania.

Wapo Watanzania wengi wenye sifa stahiki na wako tayari kupokea kijiti cha Urais. Wakati wa Samia kukaa pembeni ni sasa.

Namalizia makala hii kwa kutumia msemo wa KIlatini kwamba, "verbum sapienti sat est," yaani "enough has been said for the wise."

XIII. Marejeo:

  1. Aurel Croissant, David Kuehn and David Pion-Berlin (2024), Research Handbook on Civil–Military Relations (Northampton, USA:Edward Elgar Publishing, Inc),
  2. A. Walter Dorn, Jonathan Matloff and Jennifer Matthews (2000), "Preventing the Bloodbath: Could the UN have Predicted and Prevented the Rwanda Genocide?," Journal of Conflict Studies, XX.1, pp.9-52. URL: Preventing the Bloodbath - Could the UN have Predicted and Prevented the Rwanda Genocide? [Accessed on 10 May 2025]
  3. Bican Sahin (2010), Toleration: The Liberal Virtue (New York: Lexington Books)
  4. Chimene Benningshof (2023), The Role of Intelligence in the Failure To Prevent Genocide: A Comparative Analysis of Rwanda and Srebrenica. Mster of Arts Thesis, International Relations. Faculty of Humanities, Leiden University.
  5. Christopher Wolfe(2006), Natural Law Liberalism (New York: Cambridge University Press). Kitabu kimeanbatanishwa.
  6. Daniel John Pundu (2022), “Succession Politics as a Threat to Peace and Security in Africa: The Case for Constitutionalism and Democratization,” The Security Limelight (A Special Newsletter of the National Defense College of Tanzania), p.57-62. URL: https://www.ndctz.go.tz/uploads/documents/sw-1676552022-SUCCESSION POLITICS AS A THREAT TO PEACE AND SECURITY IN AFRICA-DR. DANIEL PUNDU.pdf [Accessed on 10 May 2025]
  7. Human Rights Watch (1999), Leave None to Tell the Story: Genocide in Rwanda, URL: https://www.refworld.org/reference/countryrep/hrw/1999/en/97537 [Accessed on 10 May 2025]
  8. Immaculee Ilibagiza (2007), Left to Tell: Discovering God amidst the Rwandan Holocaust ( Carlsbad , Califonia: Hay House ). Kitabu kimeambatanishwa.
  9. Jean Hatzfeld (2005), Machete Season: The Killers of Rwanda Speak (New York: Farrar, Straus, Giroux).
  10. Jean Mukimbiri(2005), "The Seven Stages of the Rwandan Genocide," Journal of International Criminal Justice, 3.4:823–836. URL: The Seven Stages of the Rwandan Genocide [Accessed on 10 May 2025]
  11. John Rawls (1993), Political Liberalism (New York: Columbia University Press)
  12. Juan Manuel Burgos(2022), Personalist Anthropology: A Philosophical Guide to Life (Delaware, USA: Vernon Press)
  13. Kevin F. Krupski(2023), "Who’s the Boss? Defining the Civil-Military Relationship in the Twenty-First Century," Military Review, 103.1: 26-33.
  14. Klaus Bachmann (2023), A History of Rwanda: From the Monarchy to Post-genocidal Justice (New York: Routledge)
  15. Leila Fielding (2014), Female Genocidaires during the Rwandan Genocide: When women kill ( Hamburg: Anchor Academic Publishing)
  16. Linder Melvern(2004), Conspiracy to Murder: The Rwandan Genocide (London/New York: Verso)
  17. Marie Eve Desrosiers(2023), Trajectories of Authoritarianism in Rwanda: Elusive Control before the Genocide (New York: Cambridge University Press)
  18. National Defense College (September 2022), Security Limelight (A Special Newsletter of the National Defense College of Tanzania).
  19. Susan Thomson (2017), Rwanda: From Genocide to Precarious Peace (New Haven and London: Yale University Press)
  20. Swaraj Parameswaran (2024), "Preventing or stopping the genocide: What was the main diplomatic failure in Rwanda?," URL: Preventing or stopping the genocide: What was the main diplomatic failure in Rwanda? [Accessed on 10 May 2025]
  21. Todd Salzman (2004), The church’s failure in Rwanda, URL: CATHOLICS & COLONIALISM | Commonweal Magazine [Accessed on 10 May 2025]
  22. William Galston (1991), Liberal Purposes: Goods, Virtues and Diversity in the Liberal State (Cambridge: Cambridge University Press)
  23. Philip Verwimp(2013), Peasants in Power: The Political Economy of Development and Genocide in Rwanda (New York/London: Springer Dordrecht Heidelberg)
  24. Viambatanisho vya Picha muhimu
1747505149827.png

Hayati Rais Juvénal Habyarimana

1747505335984.png
 
Attachments

Myasikie tu hayo mauaji.

Muumba awape amani jirani zetu hawa.
Mkuu acha kabisa
Acha kabisa ....
Watu hawajajua kabisa hayo mambo yanavyo play aiseeee hali ilikua tete

Mara kumi ku deal na watu wanaotaka amani ipotee mapema kabisa..

Pia hakuna rais anayetak kukaa madarakan mazima hapa nchini.
Why tuanze kufanyiana mambo ya ajabu
 
Huyo Dada aliyendika hicho kitabu amepitia mengi mabaya sana, nawajua wengi. Na wapo wengi. Its a Generational Trauma kwao

=====

Ila nasikia majambia/mapanga yaliyotumika huko yalipita Bandari ya Daresalaam. Raisi Mwinyi alikasirika sana lakini dameji ilikuwa ishatokea
 
Kuna movie hapa ya idriss elba nimetoka kuichek daah hilo tukio la mapanga nj kweli kabisa
 
Somo gani la kujifunza kutoka kwako wakati hujui hata kuandika.

Like seriously ni mtu gani mwenye level ya Doctorate, ambae inawezekana anaujumbe wa kuelimisha.

Wakati ujumbe wenyewe upo represented kama umeandikwa na mtoto wa primary, nani anamuda wa kusoma maandishi ya njano na grey text.

Sasa wewe Dr gani atakuandika hujui.

Halafu hayo mambo ya Rwanda, tulisha maliza hayatuhusu.
 
I. Usuli

“Kitendawili cha ujasiriadola ni hiki hapa: Ni kwa vipi inawezekana kuwepo kwa Taifa moja imara la watu walio sawa na huru kwa kipindi kirefu, wakiwa wanaunganishwa na Katiba moja ya nchi, wakati watu hao hao wamegawanyika katika makundi tofauti kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili?” (Rawls 1993 :xxv)

“Nadharia bora ya ujasiriadola inapaswa kutupatia utaratibu utakaotuwezesha kuhakikisha kwamba jumuiya zilizo na utofauti kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili zinaweza kuishi pamoja ndani ya jumuiya moja ya kisheria” (Galston 1991 :45)

Mwaka 2021, Rais Trump wa Amerika alishindwa uchaguzi na kugoma kukabidhi ofisi, japo Amerika ni nchi ya kidemokrasia, ambako uchaguzi wa Rais hufanyika na kutoa nafasi kwa Rais aliye madarakani kuondoka madarakani kwa amani kama akishindwa kihalali.

Na mwaka 2021, Rais Samia wa Tanzaniaia alikula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya nchi iliyomweka madarakani, lakini baadaye mwaka 2024 Samia aliukana ukuu wa katiba juu ya serikali, mahakama na Bunge, kwa kutumia hoja kwamba katiba ni kitabu sawa na vitabu vingine vinavyouzwa madukani, halafu akaanza kuendesha nchi kwa kutumia katiba mbadala ya kiimla aliyoitunga yeye na wasaidizi wake wachache, na hivyo kuiweka pembeni katiba rasmi ya Tanzania ambayo ni Jamhuri ya Kiliberali na Kidemokrasia.

Mazingira haya, kutoka Tanzania na Amerika, yanazalisha swali lifuatalo kwa wataalam wa sayansi ya ujasiriadola, usalama, haki na amani: Je, kwa ajili ya kulinda usalama, haki na amani katika nchi, ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa na jeshi la ulinzi wa wananchi dhidi ya marais wa aina ya Trump na Samia?

Katika muktadha wa swali hili na nukuu zilizotajwa hapo juu, makala hii inatumia historia ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 kujenga msingi wa hoja ifuatayo juu ya nafasi ya jeshi katika kukomesha siasa za kiimla katika Tanzania ya leo:

Kwamba, Kanuni ya Imani ya Utanzania inayotamkwa kikatiba, inaonyesha kwamba Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiliberali yenye wasifu wa kisiasa unaojumuisha vipengele vifuatavyo: Usawa wa heshima ya kiutu; Uhuru wa kujichagulia muundo wa mamlaka ya kiutawala; Kibali cha watawaliwa kwa watawala wao; Haki kama msingi wa amani; Serikali yenye nguvu tosha za kuleta matokeo yanayotakiwa na umma; Serikali yenye nguvu zilizowekewa ukomo; Usawa mbele ya sheria; Usawa wa fursa badala ya usawa wa matokeo; Ukuu wa ukweli wa kisayansi juu ya ukweli wa kisiasa; Uhusiano kati ya ukweli na ushahidi mpya; Mshikamano na majukumu ya kijamii, Uhuru wa kuabudu; Umoja wa Taifa unaoziweka kwapani tofauti za raia wake; Ukuu wa Katiba ya nchi juu ya serikali, bunge, mahakama; na Tunu na kanuni za maadili zinazofungua milango ya ushirikiano wa kimataifa.

Kwamba, matukio yafuatayo yanapingana na Kanuni ya Imani ya Utanzania: mauaji ya Ali KIbao, tamko la Rais Samia kwamba Katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine, kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake, kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi, kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya, kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni, kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani, kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua.

Kwamba, kama hali ilivyo katika Rwanda ya baada ya 1994, utamaduni huu mpya wa kufanya siasa za nchi kwa kutumia majeshi umetokea kwa sababu baadhi ya viongozi wakuu waliokula kiapo cha kulinda, kuhifadhi na kutetea katiba ya nchi wameamua kuikana Kanuni ya Imani ya Kitaifa iliyotamkwa kwa mujibu wa Katiba hiyo, na hivyo kuukataa ukweli kwamba, Katiba ya nchi yetu inalitambulisha Taifa la Tanzania kama Jamhuri ya Kiliberali na Kidemokrasia, yenye kufuata misingi ya demokrasia ya vyama vingi, ambako kunapaswa kuwa na mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations), badala ya kulitambulisha Taifa hili kama dola ya kijeshi, ambamo huwa kuna mahusiano ya kiuhasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations).

Na kwamba, kwa hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama havina hiari ispokuwa kusimama katika upande wa kulinda Kanuni ya Imani ya Utanzania inayotamkwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, na hivyo kujitenga na kazi ya kuwalinda viongozi wakuu walioamua kimakosa kuendesha nchi kwa kutumia utaratibu wa kiimla badala ya kuheshimu viapo vyao vya kulinda, kuhifadhi na kutetea Katiba ya nchi; pendekezo hili likiwa na maana kwamba mkosaji ashauriwe na wateule wake kujiuzulu kwa hiari au majenerali wamwelekeze namna ya kumaliza miaka yake kumi ya uongozi kwa amani, bila kuzidisha hata siku moja.

Kwa ajili ya kufanya utetezi wa hoja hii, makala hii imegawanywa katika sehemu zifuatazo:

  1. Usuli;
  2. Utangulizi;
  3. Methodolojia;
  4. Historia fupi ya mauaji ya halaiki huko Rwanda;
  5. Hatua saba za kupanga na kutekeleza mauaji ya Rwanda;
  6. Sababu za Vyombo vya Usalama Kushindwa Kuzuia Mauaji ya Rwanda;
  7. Mafundisho Kuhusu Utu wa Binadamu katika Rwanda ya Kale;
  8. Ushiriki wa wanawake katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda
  9. Yaliyotoke Rwanda sasa yanaanza kutokea Tanzania;
  10. Kanuni ya Imani ya Utanzania, homodomia na apedomia;
  11. Muhtasari na hitimisho;
  12. Wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama; na
  13. Marejeo.

II. Utangulizi

Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Tanzania (NDC) kilianzishwa mwaka 2011. Ni Taasisi ya Elimu ya Juu inayomilikiwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo, alikizindua rasmi Chuo hiki tarehe 10 Septemba 2012.

Kulingana na tovuti yake, kwa sasa, Chuo hiki kinatoa Shahada za Uzamili katika Mafunzo ya Usalama na Mikakati (MSSS) na Diploma ya Mafunzo ya Usalama na Mikakati (DSSS).

Dira ya Chuo hiki ni kuwa taasisi yenye hadhi kubwa zaidi ya kutoa mafunzo ya usalama wa kitaifa na kimataifa kwa maafisa wakuu waliochaguliwa wa Ulinzi na Utumishi wa Umma, kuwapa ujuzi na maarifa muhimu kwa kufanya maamuzi ya busara katika mazingira magumu ya usalama wa kitaifa na kimataifa na kimkakati." (The Security Limelight: 2022, p. ii).

Kwa hiyo, mpaka sasa Taifa linao wataalam wa kutosha wenye kufahamu kuwa kikatiba, nchi yetu inapaswa kuongozwa kwa kufuata kanuni za Jamhuri ya Kiliberali inayofuata misingi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Lakini, kuna matukio kadhaa yanapingana na ukweli huu na ambayo yamenichiochea kuandika makala hii kwa ajili ya kutoa wito maalum kwao.

Kuna mauaji ya Ali KIbao, kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake, kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi, kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya, kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni, kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani, kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua..

Matukio yote haya yanafanywa na watu waliobeba bunduki ikiwa ni ishara kwamba, kwa maoni yao, kumiliki bunduki mkononi ni mwarobaini wa kutibu magonjwa yote yanayoshambulia "usalama wa Taifa."

Taswira hii inamaanisha kwamba, japokuwa Tanzania ni Jamhuri ya Kiliberali na ya Kidemokrasia, kuna mahusiano ya kihasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations) badala ya kuwepo kwa mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations).

Kwa maoni yao, basi, bunduki, mabomu, mizinga, na vifaru ni alama za kuwepo kwa "usalama" na "amani" nchini mwetu, kama tunakubaliana na fasili isemayo kwa "peace is the tranqulity of [social, political and economic] order," kama asemavyo Mtakatifu Agustino, kwenye kitabu chake kiitwacho "The City of God," sehemu ya 19 sura ya 13.

Dhana ya "amani kama utulivu wa utaratibu za kisiasa, kiuchumi na kijamii" ni ufafanuzi unaotambulika sana, hasa unaohusishwa na Mtakatifu Augustino wa Hippo.

Inasisitiza umuhimu wa jamii iliyo na utaratibu wa haki katika kufikia amani, inayojumuisha nyanja za kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

Utulivu huu, kulingana na Augustine, linahakikisha kwamba kila kitu, ikiwa ni pamoja na wanadamu, kina nafasi na kazi yake maalum katika jamii, na huchangia katika kusababisha hali ya amani.

Kwa sababu hii vibwagizo kama vile "nchi yetu ni kisiwa cha amani," "mkoa wetu uko salama" na "nchi yetu iko salama" havikomi midomoni mwao, wakati mahali pasipo na "amani ya moyo" hakuwezi kuwa na "usalama" wa kweli.

Kwa hakika, wanasahau kwamba, historia inaonyesha kuwa mapanga, mikuki, virungu, nyundo na mashoka ni silaha za vita zilizo mbadala wa bunduki, mabomu na vifaru, na kwamba, silaha hizi zikitumiwa na watu wa kawaida waliopoteza matumani zinaweza kuua watu 10,000 kwa siku, kwa miezi mitatu mfululizo, kabla ya bunduki, vifaru na mizinga havijatumika kubadilisha upepo.

Kwa maoni yangu, matukio niliyoyataja hapo juu yanawaalika wanazuoni, na hasa wale waliosomea kwenye Chuo cha Ulinzi cha Taifa la Tanzania pamoja na Vyuo vya Idara ya Usalama wa Taifa tulivyo navyo, kutafakari kwa kina, tena bila jaziba, juu ya hatari zinazoambatana na ubaguzi wenye msingi wake katika itikadi za kitabaka kama sababu ya kuanguka kwa dola.

View attachment 3349042

III. Kanuni za mahusiano yenye afya kati ya raia, wanasiasa na majeshi

Kusema kwamba, kwa kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Kiliberali na ya Kidemokrasia, inapswa kuwa na wasifu wa kisiasa unaoakisi uwepo wa mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (friendly civil-military relations) badala ya kuwepo kwa mahusiano ya kihasama kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama (confrontational civil-military relations), ni namna nyingine ya kusema kwamba zipo nadharia nyingi zinazoongoza mahusiano kati ya raia na vyombo vya usalama, na kwamba, kila Taifa linapaswa kuchagua nadharia inalifaa kulingana na matakwa ya umma.

Hivyo, katika sehemu hii nitaeleza kwa ufupi nadharia hizo, ili kuonyesha kwamba Tanzania tunapaswa kuongozwa na nadharia inayohimiza mahusiano ya kirafiki kati ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama, na sio vinginevyo.

III. Methodolojia

Napendekeza kwamba, tunapaswa kuhoji na kujibu kwa ukamilifu na kwa haraka swali lifuatalo:

Tanzania ya Nyerere, ambayo ni Jamhuri ya Demokrasia ya Kiliberali, imefikaje mahala hapa ambako inatawaliwa kiimla, kinyume cha katiba ya nchi, na tunapaswa kufanya nini ili kuirudisha kwenye misingi asilia ya kikatiba kabla Taifa halijatumbukia kwenye machafuko ya kiraia?

Makala hii ni mchango wango katika kujibu swali hili. Nimetumia mfano wa anguko la dola kutokana na matukio ya uhasama wa kitabaka nchini Rwanda yaliyoanza mwaka 1959 na kuhitimishwa na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Kwa ajili ya kujibu swali hili, maswali madogo yafuatayo yalijibiwa kwa kuchunguza fasihi andishi yenye kuaminika zilizoorodheshwa kwenye kipengele cha "marejeo" mwishoni mwa makala hii:
  1. Wazo la kufanya mauaji ya halaiki, kama ilivyotokea nchini Rwanda, hutoka wapi, kwa maana ya nini asili ya nia ya kutekeleza mauaji ya kimbari?
  2. Kwa nini mauaji ya halaiki yalifanywa nchini Rwanda, katika wakati huo, kwa maana ya kipindi cha 1990-1994 na sio kabla au baada ya hapo?
  3. Mauaji ya halaiki ya Rwanda yalitekelezwaje, kwa maana ya nani alihamasishwa kushiriki, ni rasilimali gani zilikusanywa lini na wapi, na wauaji walitoka wapi?
  4. Kwa nini kampeni na utekelezaji wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ulifanikiwa sana kiasi cha kuwateketeza robo tatu ya Watusi wote wa Rwanda?
  5. Wanawake walishiriki vipi katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda na sababu zilizowasukuma kushiriki katika utekelezaji wa mauaji ni zipi?
  6. Tunajifunza nini kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda?

IV. Historia fupi ya mauaji ya halaiki huko Rwanda

Kulingana na kitabu cha Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007:27-34), "The Failure to Prevent Genocide in Rwanda," wakati wa pilika za Mkutano wa Berlini (1884-85) kwa ajili ya kuligawanya Bara la Afrika kati ya mamlaka tofauti za Ulaya, Rwanda iligawiwa kwa Ujerumani.

Baada ya Vita Kuu ya Pili mwaka 1918, utawala wa Wajerumani ulirithiwa na Wabelgiji. Utekelezaji wa sera za Ubelgiji ulitumia utawala wa Watutsi uliokuwepo.

Hivyo Wabelgiji waliwapa Watusi mamlaka juu ya Wahutu katika maisha ya kila siku,
japo Watusi walikuwa 14% ya raia, wakati Wahutu walikuwa 85%, na Watwa wakiwa 1%.

Kwa ajili ya kuwatofautisha watu hawa, mwaka 1933, Wabeligiji walianzisha vitambulisho vya uraia vilivyowatofautisha wananchi kwa misingi ya Uhutu, Utusi na Utwa. Wahutu hawakufurahia ubaguzi huu wa kimfumo dhidi yao.

Hivyo, mwaka 1957 Wahutu waliunda chama cha siasa cha kikabila kwa ajili ya kutetea haki zao, kikaitwa “Party for the Emancipation of the Hutus (PARMEHUTU), na kutangaza “Ilani ya Amri Kumi za Wahutu” iliyowataja Watusi kama "wavamizi kutoka ng’ambo."

Mwaka 1959-61, Wahutu waliasi dhidi ya Wabeligiji na wasaidizi wao wa Kitusi, ambapo Watusi wapato 100,000 waliuwawa, na himaya ya kifalme ya Watusi kuangishwa na Wahutu.

Kisha Watusi wapatao 150,000 walikimbilia Uganda na wengine kuingia Tanzania. Kwa njia hiyo, himaya ya Watusi wa Rwanda ikawa imeangushwa kijeshi na Wahutu.

Hatimaye, mwaka 1962 Wabelgiji walitoa uhuru kwa Rwanda ikiwa chini ya uongozi wa Rais Gregoire Kayibanda, Mhutu, Rwanda ikiwa na muundo wa serikali ya Jamhuri.

Yaani, utawala wa Kifalme chini ya Watusi ulikoma na kuzaliwa kwa utawala wa Jamhuri chini ya Rais Mhutu, Kayibanda, ambaye hata hivyo, alianza kutekeleza sera za kulipiza kisasi kwa Watusi, kinyume na matakwa ya kanuni za Jamhuri.

Watusi wengi walikimbilia nchi jirani za Uganda, Burundi, Tanzania na Zaire. Wakiwa uhamishoni Watusi walikusanya nguvu pole pole katika maeneo hayo na kuunda jeshi lenye nguvu.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 jeshi la Watusi lilikuwa tayari kuivamia Rwanda na kuweka serikali ya Watusi ili kujipatia makazi ya uhakika.

Wahutu wakitishwa na uwezekano wa kurudi kwa maadui zao Watusi, walihimiza kimya kimya kuundwa kwa vikundi vya watekaji, watesaji na wauaji, ikiwa ni pamoja na kikundi cha Interahamwe.

Kazi ya vikosi hivi ilikuwa ni ama kuwafukuza au kuwaua Watusi waliobaki nchini twanda, pamoja na kuwaua Wahutu wenye msimamo wa wastani. Uhasama huu uliendelea hadi mwaka 1994 mauaji makubwa ya kimbari yalipotokea.

Saa 2.25 usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, makombora mawili ya kurushwa kutoka ardhini hadi angani yalipiga ndege iliyokuwa imewabeba Marais Juvenal Habyarimana wa Rwanda na Cyprien Ntaryamira wa Burundi, ikiwa inajaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali. Watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo waliuawa.

Viongozi wa Kihutu waliwashutumu Watusi kwa kumuua Rais wao, na raia wa Kihutu waliambiwa kwa njia ya redio na mdomo kuwa ni jukumu lao kuwaangamiza Watusi.

Hivyo, ndani ya saa chache, mashambulizi ya mauaji yalizuka nchini Rwanda ambayo, kwa muda wa miezi mitatu iliyofuata, yaani siku 90, yalisababisha vifo vya watu wapatao milioni moja, sawa na wastani wa vifo vya watu 10,000 kila siku.

Wanaume ambao walikuwa wamezoezwa kuua walikuwa washiriki wa kikosi cha mauaji ya raia kilichoitwa “Interahamwe.”

Serikali ilitoa usaidizi na wanasiasa, maafisa, wasomi na askari wenye taaluma waliwachochea wauaji kufanya kazi yao. Maafisa wa kila eneo walisaidia kuwakusanya waathiriwa na kuwaweka mahali panapofaa kwa ajili ya kuchinjwa.

Watutsi wanaume, wanawake, watoto na watoto wachanga waliuawa katika maelfu yao katika shule na makanisa. Mara nyingi wauaji walikuwa watu wanaowajua, wakiwemo majirani, wafanyakazi wenza, marafiki wa zamani, wakati mwingine hata jamaa kupitia ndoa.

Radio FM iitwayo RTLM ilitumika kutoa matangazo ya orodha ya watu wanaopaswa kuuwawa, na mahali wanakopatikana.

Kwa ujumla, mauaji ya halaiki yalitekelezwa na Wahutu dhidi ya Watusi, kwa kutumia silaha rahisi zinazopatikana katika kila kaya.

Silaha hizo ni pamoja na mapanga, marungu na majambia, nyundo, mashoka, na sululu. Baada ya jeshi, chini ya Meja Jenerali Kagame, kuingilia kati na kuwanyang'anya "silaha zao" wananchi hawa, ndipo mauaji yalikoma.

Mwaka 2003, Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa liliitangaza tarehe 7 Aprili kila mwaka kuwa ni siku ya kufanya tafakari juu ya siasa za ubaguzi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya Wahutu na Watusi nchini Rwanda. Ubaguzi huu ulikuwa chimbuko la mauaji ya KImbari ya mwaka 1994 nchini humo.

Baadaye, mwaka 2004, Todd Salzman aliitikia wito wa Umoja wa Mataifa kwa kufanya tafakari kuhusu chimbuko la mauaji haya na kutusaidia kujua mengi. Makala yake imeambatanishwa mwishoni mwa andiko hili.

Kwa ufupi, Salzman(2004) anasema kuwa ukimya wa Kanisa Katoliki pamoja na uamuzi wake wa kusimama upande wa watawala wa Watusi waliokuwa wanafanya ukandamizaji dhidi ya Wahutu ulichukua miaka 30 kabla ya Kanisa Katoliki kugundua na kukiri hadharani kuwa linaumwa ugonjwa wa kushirikiana na tabaka la watawala wakatili.

Anaongeza kusema kwamba, wakati Kanisa Katoliki lilipogundua na kukiri ukweli huo hadharani tayari lilikuwa limechelewa sana kuweza kuchukua hatua stahiki za kuzuia mauaji ya halaiki yaliyotokea mwaka 1994.

Jambo jingine kubwa tunajifunza kutokana na mauaji ya Rwanda ni kwamba uovu huenea pale watawala wanapoubariki.

Katika mfululizo wa mahojiano na wakulima kumi ambao walikuwa wauaji wa umati katika mauaji ya kila siku ya Rwanda, Jean Hatzfeld (2005), katika kitabu chake, “Machete Season: The Killers of Rwanda Speak,” anatoa taswira ya wazi ya mojawapo ya visa vya uhalifu vilivyokithiri vya kisasa.

Wakulima hawa, ambao waligeuka kwa urahisi na haraka wakawa wauaji wa watu wengi, hawakuhitaji kutokujulikana ili kutoa kifunua uovu wao walioutenda.

Badala yake, wanasema wazi kuwa, zamu zao za kutenda maovu zilisitawi chini ya maagizo kutoka kwa mamlaka za mitaa, kwa kuungwa mkono sana na jumuiya yao na wale walio karibu nao, na wakati huo huo wakiendelea na maisha yao ya kawaida sana, ya nyumbani, tena maisha mema. Kuhusu jambo hili, mmoja wa wauaji wa wakulima wengi alisema haya:
"Baadhi ya wakosoaji wanadai kwamba tulibadilika na kuwa wanyama wa mwituni, kwamba tulipofushwa na ukatili. Hiyo ni hila ya kupotosha ukweli. Ninaweza kusema hivi:
“Nje ya mabwawa ya damu, maisha yetu yalionekana kuwa ya kawaida kabisa. Tuliimba kwenye njia, tulikuwa na chaguo letu huku tukiwa na akili timamu.
“Tulizungumza juu ya bahati yetu nzuri, tuliondoa madoa yetu ya damu kwenye pua zetu na kufurahia kupika kwenye beseni. katika maisha mapya yaliyokaribia kuanza kwa kula mguu wa nyama ya ng'ombe.
“Usiku tulikuwa na fursa ya kufanya tendo la ndoa na wake zetu, na tuliwakemea watoto wetu wakorofi.”

Kuna simulizi la kihistoria lenye kusisimua kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda. Limesimuliwa na Immaculee Ilibagiza (2007), kupitia kitabu chake, "Left to Tell: Discovering God amidst the Rwandan Holocaust". Imaculee anasema:
“Sauti zao zilikuwa kavu, kakamavu, na zenye kudhamiria. ‘Yuko hapa, tunajua yuko hapa mahali fulani. Mtafute, mtafute Immaculée.’ Kulikuwa na sauti nyingi, wauaji wengi. Niliweza kuwaona akilini mwangu.”
“Marafiki na majirani zangu wa zamani, ambao siku zote walikuwa wananisalimia kwa upendo na fadhili, wakipita katikati ya nyumba wakiwa wamebeba mikuki na mapanga na kuita jina langu.” ‘Nimeua mende 399,’ akasema mmoja wa wauaji. ‘Immaculée atakuwa wa 400. Ni nambari nzuri kuua’.
"Nilijiinamia kwenye kona ya bafu letu dogo la siri bila kusogeza hata msuli. Kama wale wanawake wengine saba waliojificha nami ili kuokoa maisha yetu, nilishusha pumzi pole pole ili wauaji wasinisikie nikipumua." (Utangulizi, uk.1)

V. Hatua saba za kupanga na kutekeleza mauaji ya Rwanda

Kulingana na Jean Mukimbiri (2005), mauaji ya halaiki ya Rwanda yalipangwa na kutekelezwa katika hatua saba.

Mosi, ni kutengeneza matabaka (classification/redefinition): Hapa kuna kubainisha tabaka la watu wanaopaswa kuuwawa kwa kutumia sifa maalum za kimaumbile, na hivyo kufanikisha dhana ya "sisi dhidi ya wao". Ilani ya Wahutu ya mwaka 1957 ilitumika kufanya kazi hii nchini Rwanda kwa kuwataja Watusi kama "wavamizi kutoka ng'ambo."

Pili, ni kutengeneza vitambulisho maalum kama alama ya utofautisho rasmi (registration/symbolisation): Tabaka la watu wanaolengwa walipewa vitambulisho vyenye majina maalum, ambapo kwa mujibu wa sensa iliyofanyika vitambulisho vya uraia vilitofautisha Wahutu (85%), Watusi (14%) na Watwa (1%).

Tatu, ni kudhalilisha utu wa walengwa Watusi (dehumanisation): Watusi walibatizwa majina yanayowaondoa kwenye kundi la watu na kuwaweka kwenye kundi la wanyama, wadudu au virusi, kama vile "panya" na "mende." Huu ulikuwa mkakati wa kuwaandaa wauaji kisaikilojia ili waamini kwamba kuua "mende" sio jinai wala dhambi, maana "mende" sio watu.

Nne, ni kuporwa mali na ardhi (confiscation): Watusi walinyang'anywa ardhi na mali na zikagawiwa kwa Wahutu; na waliondolewa kwenye mpango wa pensheni, lengo likiwa kuwadhoofisha kiuchumi.

Tano, ni ubaguzi wa rejareja wa kiuchumi, kisiasa na kijamii (sporadic exclusion): Watusi walibaguliwa katika nafasi za uteuzi wa kiserikali, kwenye vyuo walinyimwa fursa ya kupanda madaraja ya kitaaluma kama vile kutoka udaktari kwenda uprofesa, kwenye ajira nako walienguliwa kila walipoomba kazi.

Sita, ni ubaguzi wa kimfumo kwa ajili ya kuwatenga walengwa na jamii baki (systematic isolation): Wakati huko Ujerumani zilijengwa kambi za mauaji, Rwanda kambi za mauaji zilikuwa makanisa, viwanja vya mpira, na mashule. Redio zilitumika kuwalaghai walengwa waende maeneo hayo kwa ajili ya usalama wao kumbe walikuwa wanajipeleka machinjioni.

Na saba, ni utekelezaji wa mauaji (extermination): Vikosi vya Interahamwe vilitekeleza mauaji chini ya mwongozo wa viongozi wakuu wa serikali. Tayari vilikuwa vimepewa mafunzo na vitendea kazi mapema kwa ajili hii.

Kutokana na mtiririko huu wa matukio ni wazi kwamba, mauaji ya halaiki yanaweza kuzuilika kama kuna utashi wa kisiasa kutoka kwa watu ambao bado wanaongozwa na hulka ya kiu ya haki. Nchini Rwanda walikosekana watu wa aina hii kwa kipindi cha miaka 40, yaani tangu 1926 mpaka 1994. Hili ni somo kubwa.

VI. Sababu za Vyombo vya Usalama Kushindwa Kuzuia Mauaji ya Rwanda
Kulingana na Walter Dorn, Jonathan Matloff na Jennifer Matthews (2000), mambo matatu yalikuwa muhimu kwa ajili ya kuzuia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Mambo hayo ni uwezo wa kijasusi kwa ajili ya kupata taarifa za onyo la mapema na hivyo kupanga kuzuia; uwezo wa kuchukua hatua za kuzuia, yaani, kuingilia kati; na utashi wa kisiasa wa kutumia hizi njia mbili.

Wanaongeza kuwa, kwa sehemu kubwa, jambo la tatu ndilo ilikosekana Rwanda, kwani mambo mawili ya kwanza yalikuwepo nchini humo.

Ni kwa sababu hii, Swaraj Parameswaran (2024) na Chimene Benningshof (2023), wanasema kuwa, kukosekana kwa utayari wa kusoma alama za nyakati, kutafsiri kwa usahihi na kubaini hatari ya mauaji iliyokuwa inakuja lilikuwa kosa kubwa kuliko kosa la kushindwa kuyazuia mauaji hayo mara tu yalipotokea.

Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007: 63-79), katika kitabu chao, "The Failure to Prevent Genocide in Rwanda," wameeleza kwa ufasaha ukosefu wa utashi wa kisiasa kwa kubainisha taarifa za kijasusi zilizokuwepo Rwanda kabla ya mauaji, taarifa ambazo, kama zingefanyiwa kazi, zingeweza kusaidia kuzuia au kupunguza mauaji hayo.

Kuibuka kwa Wahutu wenye msimamo mkali

Utekaji nyara wa kijeshi, mauaji, uporaji wa Interahamwe ukiwalenga Watusi uliendelea kutoka 1991 hadi 1993.

Mwaka 1992 mauaji ya Watusi yalitambuliwa na wanadiplomasia wa kigeni, ambapo Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Shirika la Amnesty International waliweka mauaji ya Watutsi nchini Rwanda kwenye ajenda zao na kuitaja serikali ya Rwanda na kuwajibika kwa ukatili huo.

Mnamo Agosti 1993, makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Wahutu na Watusi yalifikiwa mjini Arusha nchini Tanzania, na haya yakaitwa Mapatano ya Arusha.

Kama sehemu ya Mapatano haya, Serikali ya Mpito ya Mseto ilipaswa kuundwa, uchaguzi huru wa kitaifa ufanyike, wakimbizi wa Kitutsi warejeshwe makwao nchini Rwanda, na jeshi la Rwanda lingeundwa ambalo lilikuwa na Wahutu na Watutsi.

Lakini, vurugu ziliendelea kabla, wakati na baada ya mazungumzo ya amani ya Arusha kuanzia 1992 hadi 1993, ambapo, Katibu Mkuu wa chama cha Habyarimana alikejeli Makubaliano ya Arusha.

Kwa ajili ya kuvuruga mchakato wa amani chini ya Mapatano ya Arusha, chama tawala kiliwaua kwa umati takriban Watusi 300 wanaoishi Ruhengeri na Gisenyi katika siku za mwisho za Januari 1993.

Kisha, shambulio la ghafla la RPF lilifuata, ambapo, mamia ya watu wakauawa, na wengine kuikimbia nchi.

Ripoti za wanadiplomasia kwa ulimwengu wa nje

Katika miaka iliyotangulia mauaji ya kimbari, jumuiya ya wanadiplomasia nchini Rwanda, maofisa waliokuwa katika mazungumzo ya Arusha na maafisa wa nje ya nchi wanaoshughulikia Rwanda walijua kuhusu kuwepo kwa "Akazu."

Huu ulikuwa mtandao wa karibu wa Wahutu wenye msimamo mkali ambao walikuwa na kikosi chao cha mauaji. Pia Akazu walijukana kama “Mtandao Zero.”

Wanachama wa mtandao wa Akazu walitoka katika familia ya Wahutu iliyoimarishwa vyema ya mke wa Habyarimana, Agathe Kanzinga. Watu muhimu sana wa Akazu walikuwa mashemeji watatu wa Habyarimana, Protais Zigiranyirazo, Kanali Pierre-Celestin Rwagafilitia na Seraphin Rwabukumba.

Mtandao wa Akazu ulikuwa na mawasiliano ndani ya halmashauri za mitaa, wilaya, balozi za Rwanda na watumishi wengi waandamizi wa serikali na maafisa wa kijeshi.

Mapema mwaka wa 1991, tathmini ya kijasusi, iliyoandikwa na wakala wa Ufaransa, ilibainisha mduara wa ndani wa mamlaka ambao ulitawaliwa na Agathe na familia yake.

Kulingana na wakala huyo, mduara wa ndani ulikuwa na lengo la kubakiza mamlaka; aina yoyote ya mazungumzo au jaribio la kulazimisha demokrasia ingechochea upinzani wao, na katika majibu yao wangeeneza hofu. Uchambuzi huu ulitumwa kwa nchi wafadhili mbalimbali.

Katika majira ya Masika ya 1992 Johan Swinnen, balozi wa Ubelgiji nchini Rwanda, aliripoti kwa wizara yake mjini Brussels kuhusu kuwepo kwa "kundi la siri" ambalo lilikuwa "linapanga kuwaangamiza Watutsi."

Ripoti kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu

Katika miaka ya kabla ya mauaji ya kimbari ya 1994, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), kama mashirika ya misaada na mashirika ya haki za binadamu, yalizidi kufanya kazi nchini Rwanda. Waliripoti juu ya mauaji katika sehemu tofauti za nchi na ushiriki wa wanajeshi na viongozi wa eneo hilo.

Mnamo Mei 1992 Amnesty International ilitoa ripoti iliyohusu mateso ya Watutsi na wapinzani wa serikali kati ya 1990 na 1992.

Ripoti hiyo ilizungumzia "kunyongwa kwa njia isiyo ya haki kwa zaidi ya Watutsi 1,000 tangu 1990, kuenea kwa mateso na aina nyingine za unyanyasaji, kutoweka kwa mahabusu, kukamatwa kwa watu wengi na kuzuiliwa au kufunguliwa kesi holela kwa zaidi ya watu 8,000."

Mnamo Januari 1993 muungano wa vyama vya haki za binadamu vya Rwanda ulitoa wito kwa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kuunda tume ya kuchunguza hali ya Rwanda.

Tume hii ilitumia wiki tatu nchini Rwanda, ikiwahoji mashahidi, waathiriwa na familia na kukusanya ushuhuda kuhusu matukio katika miaka miwili iliyopita.

Ripoti hiyo ilichapishwa mapema mwaka wa 1993 na ilizungumzia kuhusu mauaji yanayoungwa mkono na serikali dhidi ya Watusi, mauaji ya Watusi wasiopungua 2,000 na kuwekwa kizuizini kwa Watusi zaidi ya 10,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Tume hiyo ilisema kuwa ngazi ya juu ya mamlaka, akiwemo Rais Habyarimana, inawajibika kwa ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na wanajeshi, wanamgambo na raia.

Ripoti kutoka kwa mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa, Bacre Waly Ndiaye, alifanya uchunguzi nchini Rwanda mwezi Aprili 1993, baada ya kufahamishwa kuhusu madai ya ukiukaji wa haki ya kuishi.

Aliripoti kuhusu unyongaji wa watu unaofanywa kinyume cha sheria. Aliongelea kuhusu "mauaji ya halaiki yanayowezekana." Ripoti ya Ndiaye ilichapishwa Agosti 1993 na Februari 1994 iliwasilishwa rasmi wakati wa kikao cha 50 cha Tume ya Haki za Kibinadamu.

Maonyo ya Human Rights Watch mwaka 1993 na 1994

Shirika la Human Rights Watch lilitoa ripoti mbili zinazohusu hali mbaya nchini Rwanda: moja Juni 1993 na nyingine Januari 1994.

Ripoti ya Juni 1993 ilieleza kuendelea kwa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Rwanda tangu Oktoba 1990. Watutsi na watu wote walioitwa "washiriki wa RPF” waliishi katika ukosefu wa usalama kila mara, wakishambuliwa majumbani mwao au kudhulumiwa.

Ripoti ya pili ya HRW, iliyochapishwa miezi miwili na nusu kabla ya kuzuka kwa mauaji ya kimbari, iliitwa "Msimu wa Silaha Rwanda." Ripoti hiyo ilitoa mtazamo wa kina wa utitiri wa silaha kutoka mataifa ya kigeni nchini kwenda Rwanda.

Maonyo ya CIA ya Amerika mnamo 1993 na 1994

Kabla ya mauaji ya halaiki, CIA ilichapisha ripoti mbili ambazo zilihusu ghasia kubwa na zinazoweza kutokea nchini Rwanda na matokeo yake.

Utafiti wa CIA mnamo Januari 1993 ulizungumza juu ya "uwezekano wa vurugu kubwa za kikabila" na ripoti mnamo Desemba 1993 ilizungumza kuhusu tani milioni 40 za silaha ndogo ndogo ambazo zilihamishwa kutoka Poland hadi Rwanda kupitia Ubelgiji.

Propaganda za chuki kupitia magazeti

Sehemu muhimu za propaganda za chuki dhidi ya Watusi zilifanyika kupitia habari na makala za magazetini.

Gazeti la “Kangura,” jina likimaanisha "waamshe wengine," lilikuwa gazeti la kibaguzi zaidi nchini Rwanda. Lilianza kuchapisha miaka minne kabla ya kuzuka kwa mauaji ya halaiki na likawa na vurugu zaidi katika matamshi yake kuelekea Aprili 1994.

Gazeti hilo lilikuwa na matoleo mawili, moja kwa Kinyarwanda na jingine kwa Kifaransa. Kangura lilifadhiliwa na watu wa ngazi za juu za utawala wa Habyarimana. Lilikuza taifa la Wahutu kwa kuchochea chuki na jeuri ya kikabila dhidi ya Watusi.

Mnamo Desemba 1990, gazeti la Kangura lilichapisha makala yenye tamko la "Amri Kumi za Wahutu," ikiwa ni "Wito kwa Dhamiri ya Wahutu" dhidi ya ukatili wa Watusi.

Amri hizo zilionyesha Watusi kama maadui, watu waovu, wasio waaminifu na wenye tamaa kubwa. Amri zilisisitiza juu ya haja ya kudumisha "usafi wa Kihutu na kuepuka uchafuzi wa kinasaba kutoka kwa Watutsi."

Katika ukamilifu wake, Amri Kumi za Wahutu, zilizochapishwa gazetini mwaka 1990, zilisomeka kama ifuatavyo:

  1. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba mwanamke wa Kitutsi, hata awe nani, anafanya kazi kwa maslahi ya kabila lake la Kitutsi. Kama matokeo, tutazingatia msaliti Mhutu yeyote anayeoa mwanamke Mtutsi, kuajiri mwanamke wa Kitutsi kama suria, kuajiri mwanamke wa Kitutsi kama katibu au kumchukua chini ya ulinzi.
  2. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba binti zetu Wahutu wanafaa zaidi na waangalifu zaidi katika jukumu lao kama mwanamke, mke, na mama wa familia. Ni makatibu wazuri, wazuri na waaminifu zaidi.
  3. Wanawake wa Kihutu, watakuwa macho na kujaribu kuwarudisha waume zao, kaka, na wana wao wa kiume kwenye akili zao.
  4. Kila Mhutu anapaswa kujua kwamba kila Mtutsi si mwaminifu katika biashara. Lengo lake pekee ni ukuu wa kabila lake. Matokeo yake, Mhutu yeyote anayefanya yafuatayo ni msaliti: anashirikiana na Watutsi katika biashara; anawekeza pesa zake au pesa za serikali katika biashara ya Watutsi; kukopesha au kukopa pesa kutoka kwa Mtutsi; inatoa upendeleo kwa Watutsi katika biashara kama vile kupata leseni za kuagiza, mikopo ya benki, maeneo ya ujenzi, masoko ya umma, nk.
  5. Nyadhifa zote za kimkakati, kisiasa, kiutawala, kiuchumi, kijeshi na kiusalama zinapaswa kukabidhiwa kwa Wahutu pekee.
  6. Sekta ya elimu ikijumuisha wanafunzi wa shule, wanafunzi na walimu lazima wawe Wahutu walio wengi.
    Wanajeshi wa Rwanda wanapaswa kuwa Wahutu pekee. Uzoefu wa vita vya Oktoba 1990 umetufundisha somo. Hakuna mwanajeshi atakayeoa mtutsi.
  7. Wahutu waache kuwahurumia Watutsi.
  8. Wahutu, popote walipo, lazima wawe na umoja na mshikamano na wawe na wasiwasi na hatima ya ndugu zao Wahutu. Wahutu wa ndani na nje ya Rwanda lazima daima watafute marafiki na washirika kwa ajili ya Wahutu, kuanzia na ndugu zao Wahutu. Ni lazima wakabiliane na propaganda za Watutsi kila mara. Wahutu lazima wawe imara na macho dhidi ya adui wao wa kawaida wa Kitutsi.
  9. Mapinduzi ya Kijamii ya 1959, Kura ya Maoni ya 1961, na Itikadi ya Wahutu, lazima ifundishwe kwa kila Mhutu katika kila ngazi. Kila Mhutu lazima aeneze itikadi hii kwa upana. Mhutu yeyote anayemtesa ndugu yake Mhutu kwa sababu ya kusoma, kueneza na kufundisha itikadi hii ni msaliti.
Hivyo, gazeti la Kangura lilieneza dhana kwamba "Watusi walikuwa wakitayarisha vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wahutu ambavyo havitaacha mtu yeyote" na kwamba jeshi la "RPF ilitaka kuanzisha tena ufalme wa Watutsi na kuwafanya Wahutu kuwa watumwa."
Mhariri mkuu wa gazeti la Kangura, Hassan Ngeze, alipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu mwaka 2003 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda na alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela.

Propaganda za chuki kupitia redio

Sehemu muhimu za propaganda za chuki dhidi ya Watusi zilifanyika kupitia matangazo ya redio pia.

Redio maarufu ya kueneza chuki, "Radio Television Libre des Milles Collines (RTLMC)" ilianzishwa na Wahutu wenye msimamo mkali kama "sauti ya itikadi kali."

Kwa sababu ya mtindo wake usio rasmi wa utangazaji, pamoja na muziki wa kufoka na lugha ya mitaani, kituo kilivutia wasikilizaji wengi na tofauti.

Kama ilivyokuwa kwa gazeti la Kangura, Redio ya RTLMC ilifadhiliwa na Wahutu wenye msimamo mkali. Wanachama wote wa Akazu walikuwa wanahisa wa RTLMC, huku Habyarimana akiwa ndiye mwenye hisa nyingi zaidi.

Madhumuni ya redio hiyo yalikuwa kuanzisha kampeni ya kuwachafua Watusi na kueneza ujumbe hasi dhidi ya maafikiano ya Arusha.

Redio ya RTLMC ilizidi kuwa na vurugu katika utangazaji wake. Kwa mfano, tarehe 26 Novemba 1993, RTLMC ilitoa wito wa kuuawa kwa viongozi wa upinzani, na kuangamizwa kwa Waziri Mkuu Agathe Uwilingiyamana na Waziri Mkuu mteule Twagiramungu.

Marc Nees, ambaye alifanya kazi kama afisa wa ujasusi wa jeshi la Ubelgiji nchini Rwanda kuanzia Novemba 1993 hadi Machi 1994, alisema katika ushahidi wake mbele ya Seneti ya Ubelgiji kwamba:

"Nina hakika kwamba kama tungesimamisha RTLMC tungekuwa na nafasi zaidi ya kuzuia mauaji ya kimbari, au angalau kuyapunguza."

Ushahidi wa mdomo kutoka kwa Msiri

Taarifa za kijasusi zilizokuwa muhimu na zenye kuaminika zilikuja kwa njia ya mdomo kutoka kwa msiri mmoja, Januari 1994.

Huyu alikuwa ni Afisa Usalama aliyekuwa anafanya kazi kwa ukaribu na Rais Habyarimana, akiwa amepewa jukumu la kutoa mafunzo maalum kwa kikundi cha Interahamwe. Alijitambulisha kwa jina la “Jean Pierre.”

Piere alimfahamisha Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, UNAMIR, Dallaire, kwamba, dhamiri yake ilikuwa inamsuta maana amepewa kazi asiyotaka kuifanya.

Kazi yake ilikuwa ni kusambaza silaha kwenye vitongoji vya Kigali, kuandaa orodha ya watusi wote wanaokaa kwenye vitongoji hivyo, na kuwa tayari kuwaua pale atakapopewa amri ya kufanya hivyo.

Alikuwa tayari kufichua maeneo yaliko mghala ya silaha alizokuwa anasambaza, lakini kwa sharti kwamba apewe hifadhi ya kisiasa nje ya Rwanda.Kwa mujibu wa Piere, mtandao wa Interahamwe aliokuwa amekwishatengeneza na kukabiodhi silaha ulikuwa na uwezo wa kuua wati 1,000 kwa kila dakika mbili.

Wakati Piere alikuwa tayari kushiriki mapambano dhidi ya jeshi la RPF, hakuwa tayari kutekeleza mauaji ya Watusi wasio na hatia.

Piere alifafanua kwamba, viongozi waliokuwa nyuma ya mpango huo ni pamoja na viongozi wa chama tawala cha Rais Habyarimana.

Majumuisho muhimu

Kwa taarifa hii, ukweli ulikuwa wazi kwamba kuna mauaji ya halaiki yanaandaliwa na watawala, ambao kwa sababu hiyi wasingeweza kuwa sehemu ya kutyazuia.

Na kwa ujumla, utafiti wa Shirika la Human Rights Watch (1999), wenye kichwa cha maneno "Leave None to Tell the Story: Genocide in Rwanda," umeeleza vizuri sana ushiriki wa vyombo vya dola na wanasiasa katika mauji ya Rwanda ya mwaka 1994.

Muundo mzima wa serikali ya Wahutu kuanzia Ikulu mpaka serikali ya mtaa ulishiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mauaji. Kwa hiyo, mauaji ya Rwanda yana mengi ya kutufundisha hata leo, hasa hapa Tanzania.

Kwa sehemu kubwa, Idara ya Usalama wa Taifa ya Rwanda, Jeshi la Wananchi la Rwanda na Jeshi la Polisi la Rwanda, ni vyombo ambavyo viliungana pamoja katika kupanga na kutekeleza mauaji ya Watusi.

Hivyo, fundisho moja kubwa ni kwamba, vyombo vya ulinzi na usalama vinavyofuata amri za watawala wakati amri hizo zinakiuka misingi ya utu, na kusigina Katiba ya nchi, yenye kuongelea utaifa badala ya ukabila, vinaweza kulitumbukiza Taifa katika vita ya wenywe kwa wenyewe.

View attachment 3345440

VII. Mafundisho Kuhusu Utu wa Binadamu Katika Rwanda ya Kale
Kila jamii inayo mafundisho yake kuhusu hulka ya utu wa Kimungu, utu wa malaika, utu wa binadamu, na utu wa majini. Hapa naongelea hulka ya utu wa binadamu, yaani, hulka ya “mtu” aitwaye “binadamu.”

Mafundisho kuhusu hulka ya utu wa kibinadamu huwavutia na kuwaunganisha watu wengi kwa sababu yanahusu maumbile yao wenyewe.

Hivyo, tangu zamani watu tofauti wamejaribu kujiuliza na kujibu maswali kama vile: Mtu anayo hulka ya namna gani? Mtu ana thamani gani? Mtu alitoka wapi? Mtu atakwenda wapi? Uhai wa mtu ulitoka wapi? Na mambo mengine mengi yanayohusiana na uwepo wa watu.

Taaluma inayohusika na kujibu maswali haya huitwa anthropolojia, na inayo matawi mengi kulingana na mwegemeo wake wa kihistoria.

Kwa ujumla, kuna “anthropolojia ya kisayansi,” “anthropolojia ya Kikristo,” “anthropolojia ya Kiislamu,” “anthropolojia ya Kihindi,” “anthropolojia ya Kibantu,” “anthropolojia ya Kiarabu,” “anthropolojia ya Kizungu,” “anthropolojia ya Kigriki,” “anthropolojia ya Kipolandi,” “anthropolojia ya Kinyarwanda,” na orodha inaendelea.

Kinachotuhusu hapa ni “anthropolojia ya kinyarwanda.” Kulingana na Philip Verwimp(2013:6), anthropolojia ya kinyarwanda ilikuwa ni ya kitabaka.

Yaani, baadhi ya Watusi walifundishwa kuwa wao ni wana wa uzao bora wa Ham na kuwa Wahutu ni wana wa uzao uliolaaniwa wa Shem.

Hivyo, Watusi wakawa wanawaona Wahutu kama watu walio na haki kidogo kuliko haki walizo nazo Watusi. Kwa mujibu wa Biblia, Ham na Shem ni Wana wa Noah (Mwanzo 9:20-27).

Walisahau fundisho jingine muhimu la Biblia lisemalo kwamba Wahutu na Watusi "wameumbwa kwa mfano wa Mungu mmoja." Hata Wamisionari wa Kanisa Katoliki walisahau kusisitiza ukweli huu.

Ukweli ni kwamba, viongozi wa Rwanda, Watusi na Wahutu, kwa nyakati tofauti, walifanya makosa ya kukweza:
  1. mauti juu ya maisha;
  2. uwongo juu ya ukweli;
  3. ujinga juu ya maarifa;
  4. haki juu ya dhuluma;
  5. utumwa juu ya uhuru;
  6. ukoloni juu ya ukombozi;
  7. unyama juu ya utu;
  8. uhuni juu ya ustaarabu;
  9. uadui juu ya urafiki;
  10. chuki juu ya upendo;
  11. hofu juu ya matumaini;
  12. dharau juu ya heshima;
  13. udini, ukabila, ukanda na uchawa juu ya Utaifa;
  14. mabavu juu ya maridhiano;
  15. maombolezo misibani juu ya shangwe za harusini;
  16. ubaya juu ya wema;
  17. umaskini juu ya utajiri;
  18. mbinu haramu juu ya mbinu halali;
  19. malengo ya muda mfupi juu ya malengo ya muda mrefu;
  20. malengo haramu juu ya malengo halali; na
  21. kwa ujumla walikwenza tunu hasi juu ya tunu chanya.
Katika muktadha huu, jambo muhimu sana ambalo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vya Rwanda vilishindwa kuelewa ni nafasi ya tunu za kiutu katika maisha ya watu viliopaswa kuwalinda.

Nitaeleza kwa kifupi sana. KIla mfumo wa maadili unazo sehemu kuu tatu zifuatazo:
  1. Seti ya tunu chanya za kiutu;
  2. Seti ya majukumu na haki; na
  3. Chimbuko la tunu, majukumu na haki.
Mosi, kuna seti ya tunu za kiutu ambazo huonyesha ni malengo gani yanayopaswa kufukuziwa na watu kwa ajili ya kufanikisha ustawi wao, mfano ni afya, elimu, uhuru, usawa, mali, na ukweli.

Yaani, tunu za kiutu huwawezesha wananchi kujua malengo gani wayafukuzie kwa sababu yanawasaidia kustawi, malengo yapi wayaepuke kwa sababu yanawazuia kupata ustawi, watu gani wafungamane nao, na watu gani wawaepuke.

Pili, kuna seti ya haki na majukumu, yenye kujumuisha makatazo na miongozo ya kiutendaji inayoeleza matendo gani yanaruhusiwa na matendo yapi yanakatazwa.

Seti ya kanuni za haki na majukumu hutaja mbinu za kukuza na kuhami tunu za kiutu. Mbinu zinazohujumu tunu za kiutu huitwa mbinu haramu, wakati mbinu zinazostawisha tunu za kiutu huitwa mbinu halali.

Na tatu, kuna msingi wa tunu, haki na majukumu tajwa, mara nyingi, msingi huo ukiwa unatokana na mtazamo wa jamii kuhusu swali lifuatalo: Utu ni kitu gani, viumbe gani ni watu kamili, na viumbe gani sio watu kabisa? Jawabu kwa swali hili ndio huzaa tunu, haki na majukumu katika jamii husika.

Nitatoa mifano minne kuhusu ututuri wa mafundisho ya jamii kuhusu “mtu” aitwaye “mwanadamu,” ili kuonyesha jinsi yanavyopingana.

Mosi, kama tulivyoona, baadhi ya Watusi wanaojioni kuwa ni wana wa uzao bora wa Ham n kuwaona Wahutu kama wana wa uzao uliolaaniwa wa Shem, wanawaona Wahutu kama watu walio ha haki kidogo kuliko haki walizo nazo Watusi. Hii ndio sababu ya vita ya halaika huko Rwanda.

Pili, baadhi ya Wazungu wanawaona Waafrika kama vile wako kundi moja na sokwe, hivyo wanaona Mwafrika anazo haki chache kuliko Mzungu. Hii ndio sababu kuu ya ukoloni wa mwafrika.

Na tatu, baadhi ya Waarabu wanawaona Waafrika kama vile wako karibu sana na nyani, hivyo wanaona Mwafrika anazo haki chache zaidi kuliko Mwarabu. Hii ndio sababu kuu ya biashara ya utumwa wa mwafrika. Na mifano inaendelea.

Na nne, baadhi ya Waislamu wanawaona Makafiri kama vile ni watu wa daraja la pili walio na haki chache kuliko walizo nazo Waislamu. Hii ndio sababu ya mateso ya Wakristo katika nchi nyingi za Kiislamu.

Kwa sababu hizi zote, jamii yoyote inayokweza tunu hasi juu ya tunu chanya, na kuinua mbinu haramu juu ya mbinu halali, inakuwa imekufa kimaadili, maana haiwezi tena kutofautisha kati ya haki na dhuluma, na hivyo kushindwa kutofautisha kati ya ufalme wa watu (homodomia) na ufalme wa nyani (apedomia).

Tunaweza kuongelea ufalme wa "apedomia" dhidi ya ufalme wa "homodomia," kama alivyowahi kufanya hayati Mtikila, katika hotuba yake moja.

Na ufalme wa apedomia ndiyo ilikuwa sifa kuu ya jamii ya Rwanda kati ya mwaka 1959 na 1994. Tangu wakati huo, Rais Kagame amekuwa katika jitihada za kuikarabati Rwanda ili iondoke kwenye ufalme wa nyani (apedom) na kuingia kwenye ufalme wa watu (human kingdom).

Kutokana na haya yote, somo moja linaibuka. Kila mtaala na kila muhtasari wa elimu ya kitaifa lazima iwasaidie watoto wote kupata jawabu sahihi kwa swali lifuatalo: Utu ni kitu gani, viumbe gani ni watu kamili, na viumbe gani sio watu kabisa?

Yaani, ni lazima iwepo anthropolojia ya kitaifa, yenye uwezo wa kuzikosoa anthropolojia baki, kama ikibidi. Somo la uraia linapaswa kufanya kazi hii. Mwandishi Juan Manuel Burgos(2022) ametoa mfano mzuri wa maudhui ya kuanza nayo.

VIII. Ushiriki wa wanawake katika kutekeleza mauaji ya halaiki ya Rwanda
Unyanyasaji wa wanawake wakati wa vurugu na vita limekuwa lengo kuu la tafiti nyingi zinazochunguza uhusiano ambao hujitokeza kati ya jinsia na migogoro ya kivita.

Kwa jadi na historia pana, wanawake wamekuwa wakichukuliwa kama wahanga. Lakini, kuna historia inaonyesha ukweli tofauti. Wapo wanawake ambao ama walisaidia watekelezaji wa mauaji, au walifanya utekelezaji wa mauaji moja kwa moja, au waliidhinisha mauaji. Mfano mzuri inapatikana nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa Leila Fielding (2014), katika kitabu chake, “Female Genocidaires during the Rwandan Genocide,” huko Rwanda, baadhi ya wanawake hawakutoa tu msaada na kutia moyo wanaume wa Kihutu kufanya uhalifu, bali pia walishiriki moja kwa moja.

Walikuwa wahanga na wahalifu waliofanya mashambulizi na kuchochea ubakaji, wakiwa mawakala wa uovu na alama ya mauti.

Leila Fielding (2014:13) anasema kuwa, kuna wanawake waliokuwa madiwani, walimu na watendaji wa vijiji walioshiriki katika utekelezaji wa mauaji, akimtaja diwani Rose Karaushara wa Kigali aliyeamuru mauaji wa Watusi 5,000.

Aidha, Leila Fielding (2014:19) anafafanua kuwa, mwaka 2002, karibu watu 100,000 walikuwa mahabusu wakisubiri usikilizwaji wa kesi za mauaji ya halaiki, watu 3,000 kati yao wakiwa ni wanawake.

Kati yao, Leila Fielding (2014:26) anaeleza, wanawake 47 walishiriki mauaji kwa kuweka mipango, kuchochea, na kuratibu. Walikuwa na vyeo mbalimbali kwenye vyama vya siasa, jeshini, na kwenye madhehebu ya dini.

Aidha, Leila Fielding (2014:26) anasimulia kisa cha Pauline Nyiramasuhuko, aliyekuwa Waziri wa Familia na na Masuala Wanawake, kama mfano uliokithiri wa mauaji ya kimbari yaliyotekelezwa na wanawake.

Yeye alihamasisha ubakaji na ngono za mateso dhidi ya wanawake Watusi nchini Rwanda. Anafafanuliwa na mashahidi kama mtu aluyekuwa amevaa kombati za kijeshi na kubeba a bunduki akiwa anaamuru vitendo vya mauaji ya kimbari.

Mwenendo wa Nyiramasuhuko ulijumuisha kuweka vizuizi barabarani ili kubaini, kuwateka nyara, kuwabaka na kuwaua watutsi.

Alikuwa akisafiri mara kwa mara katika eneo lake la asili wa Butare katika gari aina ya peugot wakati wa mauaji ya halaiki, likiendeshwa na mwanawe ambaye alikuwa mwanachama mashuhuri wa Interhamwe, na alitumia kipaza sauti kuchochea ubakaji na mauaji ya wanawake wa Kitutsi.

Pauline alishtakiwa kwa makosa mawili ya ubakaji, moja kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na lingine kama ukiukaji wa Mkataba wa Geneva wa Uhalifu wa Kivita.

IX. Yaliyotoke Rwanda sasa yanaanza kutokea Tanzania

Lakini, maajabu ni kwamba, yaliyotokea nchini Rwanda kati ya miaka ya 1959 hadi 1994 yanatokea katika Tanzania ya leo, chini ya serikali ya awamu ya sita.

Mnyukano uliopo kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kwa upande mmoja, na misimamo inayochukuliwa na vyombo vya usimamizi wa sekta ya usalama, kwa upande mwingine, ni sura mbili ya hali hiyo.

Kama ilivyokuwa wakati wa uhasama kati ya Wahutu na Watusi huko Rwanda enzi zile, sisi hapa Tanzania tunashuhudia "ubaguzi haramu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii wenye sura ya hawa ni CCM na wale ni Chadema," hasa kwa kutumia kigezo cha tofauti ziliozo katika itikadi za vyama.

Katika mchakato wa kutekeleza ubaguzi dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani chama tawala na serikali yake wanakweza itikadi za vyama juu ya tunu za Kitaifa katika namna ambayo inaonyesha kwamba, ama kwa kujua au kwa kutojua, wanajenga kwa mkono wa kushoto na kubomoa kwa mkono wa kulia.

Vyombo vya dola vya Tanzania vimeigiza tabia ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Rwanda ya miaka ya 1990. Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa sasa inawaruhusu kufanya kazi zote bila kutofautisha kati kazi za polisi wala kazi za JWTZ.

Kwa usahihi, naona kuwa, matukio yafuatayo yanapingana na Kanuni ya Imani ya Utanzania:
  1. Kubinafsishwa kinyemelea kwa Bandari ya Dar es Salaam,
  2. Mauaji ya Ali Mohamed Kibao,
  3. Tamko la Rais Samia kwamba Katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine,
  4. Kutekwa na kupotezwa kwa Deo Soka na wenzake,
  5. Kuteswa na kujeruhiwa kwa wafuasi wa Chadema wakiwa wanaelekea mahakamani Kisutu kwenye kesi,
  6. Kutekwa na kupotezwa kwa Mdude Nyagali huko Mbeya,
  7. Kubuniwa kwa kesi hewa ya uhaini dhidi ya Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema,
  8. Polisi kuziteka ofisi za Makao Makuu ya Chadema huko Mikocheni,
  9. Kuwindwa kwa watia nia wa Chadema katika ngazi ya ubunge na udiwani,
  10. Kutekwa na kupotezwa kwa Shedrack Yusuph Chaula aliyechana picha ya Rais, na
  11. Kuvamiwa kwa makao makuu ya Kanisa Katoliki huko Kurasini jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya kumnyamazisha Padre Kitima kwa kumwua.
  12. Baadhi ya viongozi wa kisiasa kuwaita baadhi ya Watanzania wanaofanya uanaharakati wa kupoigania haki za watu "kenge," kama alivyotamka Tauhida Galos, Mbunge wa Viti Maalum, Mjini Magharibi, Zanzibar.

View attachment 3347375

Mbunge Tauhida anaamini kwamba hata kenge wakitekwa kenge wengine hawastahili hata kuwaulizia au kupiga kelele kuhusu kenge wenzao kupotea.

Kwa maoni yangu, tangu Rais Samia alipotamka kwamba katiba ya nchi ni kitabu tu kama vitabu vingine alikuwa amebatilisha kiapo chake na kuanza safari ya kuweka muundo mpya wa kiutawala anaoutaka yeye, na kujenga timu ya kumsaidia kufikia azima yake hiyo.

Lakini, kazi ya kwanza ya vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa ni kulinda katiba ya nchi kwa kulinda "muundo wa serikali" uliotamkwa na wananchi na kuingizwa kwenye katiba ya nchi ambayo haiwezi kubadilishwa na Mahakama, Bunge wala serikali kupitia Baraza la Mawaziri.

Kwa hiyo, tangu siku ile Rais Samia alipotangaza kuukataa ukuu wa kitabu kinachoitwa "Katiba ya nchi" na kuiweka katika daraja moja na vijitabu vingine vinavyoweza kubadilishwa kiholela na mtu yeyote, vyombo vya ulinzi na usalama vilipaswa kujitenga naye na kusimama upande wa katiba ya nchi. Lakini hilo halikutokea na halijatokea mpaka leo.

Huko Rwanda, badala ya kusimama na wananchi wa Kihutu waliokuwa wanateswa na wanasiasa wa Kitusi, viongozi wa Kanisa Katoliki walisimama upande wa watesaji wa Kitusi, wakiwa wanatumia mbinu haramu ya uenjilishaji katika kufukuzia malengo mazuri ya kidini.

Huu ulikuwa ni umachiaveli ukitekelezwa na Kanisa, ama kwa kujua au kwa kutojua. Vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania vinalo somo kubwa kutoka Rwanda. Havipaswi kurudia makosa yaliyofanywa na Kanisa Katoliki.

X. Kanuni ya Imani ya Utanzania, homodomia na apedomia

Kuna tofauti kubwa kati ya matukio ya Rwanda ya miaka ya 1994 na Kanuni ya Imani ya Utanzania. Katiba yetu inataja tunu, haki na majukumu muhimu, na hivyo kutoa mwongozo thabiti kuhusu tofauti kati ya ufalme wa watu (homodomia) na ufalme wa nyani (apedomia).

Nafupisha Kanuni ya Imani ya Tanzania hapa chini kwa msaada wa maandishi ya Christopher Wolfe(2006:144-47), katika kitabu chake, "Natural Law Liberalism," na pia kwa msaada wa Bican Sahin (2010), katika kitabu chake, Toleration: The Liberal Virtue." Kwa mujibu wa maandiko haya, Kanuni ya Imani ya Utanzania inaweza kufupishwa kama ifuatavyo:
  1. Usawa wa heshima ya kiutu (human dignity): Watu wote wenye mwili hai unaojumuisha mifupa, nyama na damu inayobeba umeme wa akili na utashi wanastahili kuthaminiwa utu wao kwa usawa, hata kama hakuna watu wawili wanaoweza kuwa na kiwango kile kile cha umeme wa akili na utashi.​
  2. Uhuru wa kujichagulia muundo wa utawala (self-determination): Muundo wa utawala uliopo nchini lazima utokane na maamuzi huru ya watu wanaotawaliwa ukiwa unaonyesha wanataka watawaliwe vipi na hawataki kutawaliwa namna gani.​
  3. Kibali cha watawaliwa kwa watawala (consent of the governed): Watawala wanapaswa kutokana na ridhaa ya watu wanaotawaliwa kupitia chaguzi huru na za haki, zinazofanyika mara kwa mara.​
  4. Haki na amani (human rights, justice and peace): Kama jamii inataka kuwa na amani ya kweli lazima kila mtu akubali kwamba kila mtu na kila taasisi inao wajibu wa kuheshimu haki za binadamu. Haki huzaa amani, amani ni tunda la haki, haki ni chimbuko la amani.​
  5. Serikali yenye nguvu tosha za kuleta matokeo yanayotakiwa na umma (effective and efficient government): Kuna serikali yenye nguvu za kutosha kutekeleza majukumu iliyokabidhiwa, kwa maana ya uwezo wa kukusanya kodi; kuzuia uhalifu; kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.​
  6. Serikali yenye nguvu zilizowekewa ukomo (limited government): Kuna serikali iliyowekewa mipaka ya kutosha ili kuizuia isivunje haki za raia, ambapo mipaka ifuatayo inahusika: uchaguzi wa mara kwa mara kwa ajili ya kuiwajibisha serikali isiyotekeleza wajibu wake; bunge lenye meno ya kuing'ata serikali; mahakama yenye makucha ya kuikwaruza serikali; wananchi wenye mamlaka ya kumpumzisha kiongozi hata kabla ya msimu mwingine wa uchaguzi kufika (power of recall); taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa; tume huru ya haki za binadamu yenye makucha; na ofisi ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali yenye meno.​
  7. Usawa mbele ya sheria (equality before the law): Kuna usawa mbele ya sheria kutokana na matakwa ya sheria kuchukua nafasi ya amri zinazotokana na mihemuko binafsi ya watawala, ambapo watu wote na taasisi zote zina hadhi sawa mbele ya sheria, sheria zinatumika kutoa hukumu sawa kwa matukio yote yaliyo sawa, na sheria zinatumika kutoa hukumu tofauti kwa matukio yote yaliyo tofauti.​
  8. Usawa wa fursa badala ya usawa wa matokeo (equality of opportunity): Serikali inalo jukumu la kumweka kila raia huru dhidi ya vikwazo vya kisheria, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambazo ili kwa njia hiyo kumwongezea yamkini ya kufanikisha, kulingana na juhudi binafsi, malengo binafsi aliyojiwekea.​
  9. Ukuu wa ukweli wa kisayansi juu ya ukweli wa kisiasa (superiority of scientific truth over socially constructed truth): Kuna ukuu wa ukweli unaotokana na uchunguzi wa kisayansi dhidi ya ukweli unaojengeka katika jamii kutokana na maamuzi ya vikao vya viongozi au watu maarufu katika jamii.​
  10. Uhusiano kati ya ukweli na ushahidi mpya (Openness of truth to new evidence): Ukweli wa kisiasa, kiuchumi na kijamii unavuvumka kulingana na upatikanaji wa ushahidi mjaraba mpya, bila kujali kwamba ushahidi mpya unapingana na taarifa za kiufunuo yaliyoko kwenye misahafu mbalimbali ya kidini.​
  11. Mshikamano na majukumu ya kijamii (solidarity and social duties): Watu huunda jumuiya kwa ajili ya kutengeneza nguvu za pamoja ili kufanikisha mahitaji ambayo hayawezekani nje ya ushirikiano wa kijumuiya. Hivyo, pamoja na uwepo wa haki binafsi, kila mtu anayo majukumu ya kijamii, ambapo kila mtu anakuwa na wajibu kwa jamii pale anapohitajika kuchangia katika kufanikisha maslahi ya watu wote. Hii ni dhana ya mshikamano.​
  12. Uhuru wa kuabudu (freedom of worship): Mamlaka ya nchi haipaswi kuanzisha dini rasmi wala kufungamana na dini yoyote na kuifanya dini ya kitaifa; kila mwananchi anao uhuru wa ama kunzisha dini mpya, au kuchagua dini waitakayo au kuzikataa dini zote; kuna daraja la ushirikiano kati ya dini na siasa katika mafundisho ya kidini ambayo yanazingatia kanuni za urazini (rational theism); na kuna ukuta unaotenganisha dini na siasa pale ambapo ushirikiano hauwezekani kwa sababu ya mafundisho ya kidini ambayo yanayokiuka kanuni za urazini kutokana na kukweza mapokeo yenye mikanganyiko ya kimantiki juu ya urazini (dogmatic theism).​
  13. Umoja wa Taifa unaoziweka kwapani tofauti za raia wake (superiority of national unity over individual differences): Umoja wa kitu kimoja chenye sehemu nyingi zilizo tofauti hutokana na uwepo wa seti ndogo ya sifa chache zinazofanya kazi kama uzi wa kuziunganisha sehemu kadhaa zilizo na utofauti. Katika siasa za kuendesha nchi inayohusisha watu wanaotofautiana kwa misingi ya jinsia, rangi, kabila, dini, itikadi za kisiasa, na maadili, uzi huo huitwa tunu na majumu ya kitaifa. Hivyo, kwa ajili ya kulinda umoja wa Taifa tunapaswa kukubaliana juu ya uwepo wa soko huru la mawazo tofauti ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kijinsia, kimaadili na kidini, isipokuwa mawazo yale yanayomomonyoa, kudhoofisha au kuua kabisa tunu na majukumu ya kitaifa. Kanuni ya uvumilivu inayo nafasi kubwa katika soko huria la mawazo.
  14. Ukuu wa Katiba ya nchi juu ya serikali, bunge, mahakama (constitutional supremacy): Katiba ya nchi ni muhtasari wa maamuzi ya pamoja ya watawaliwa, wenye kueleza namna wanavyotaka watawaliwe, katiba hiyo ikiwa inataja tunu na majukumu ya kitaifa yaliyo na nguvu za veto juu ya maamuzi ya serikali, bunge na mahakama.​
  15. Tunu na kanuni za maadili zinazofungua milango ya ushirikiano wa kimataifa (universal values which are friendly to international cooperation): Kutokana na imani juu ya usawa wa hadhi ya kiutu, unaotokana na uwepo wa hazina ya akili na utashi katika mwili wa kila kiumbe chenye kromozomu 46, inawezekana kubuni kanuni za ushirikiano wa kimataifa bila kujali mipaka ya nchi moja moja, na kanuni hizo zinaitwa haki asilia za binadamu.​

XI. Muhtasari na hitimisho

Katika makala hii nimeichunguza historia pana ya mauaji ya Rwanda kama ilivyotafitiwa na kina Philip Verwimp(2013), Fred Grunfeld na Anke Huijboom (2007), Salzman (2004), Hatzfeld (2005), Ilibagiza (2007) na wengine ili kujibu maswali yafuatayo:

  1. Wazo la kufanya mauaji ya halaiki, kama ilivyotokea nchini Rwanda, hutoka wapi, kwa maana ya nini asili ya nia ya kutekeleza mauaji ya kimbari?
  2. Kwa nini mauaji ya halaiki yalifanywa nchini Rwanda, katika wakati huo, kwa maana ya kipindi cha 1990-1994 na sio kabla au baada ya hapo?
  3. Mauaji ya halaiki ya Rwanda yalitekelezwaje, kwa maana ya nani alihamasishwa kushiriki, ni rasilimali gani zilikusanywa lini na wapi, na wauaji walitoka wapi?
  4. Kwa nini kampeni na utekelezaji wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ulifanikiwa sana kiasi cha kuwateketeza robo tatu ya Watusi wote wa Rwanda?
  5. Tunajifunza nini kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda?
Kwa maoni yangu, hitimisho kutokana na majibu kwa maswali haya ni kwamba, dawa ya kuepukana na utamaduni wa mauaji ya halaiki, kama yaliyotokea huko Rwanda, ni kusimama kwenye Kanuni ya Imani ya Utanzania, yaani misingi ya Jamhuri ya Kiliberali, kama ilivyotamkwa kwenye katiba ya nchi yetu tangu mwaka 1977.

View attachment 3345252

XII. Wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama

Mwisho niseme kuwa, katika hali ya sasa, naona kuwa mfumo wa vyombo vinavyosimamia sekta ya usalama (security sector governance system) unaumwa ugonjwa wa "umachiaveli," ugonjwa ambao ulikuwa unavisumbua vyombo vya ulinzi na Usalama vya Rwanda katika miaka ya 1959 mpaka 1994.

Tunaisoma historia ili kubaini makosa yaliyofanyika zamani, ili kwa njia hiyo tuweze kuzisoma vizuri alama za nyakati tulizomo, na hatimaye, kuweka mipango iliyo salama kwa ajili ya kesho salama.

Na kutokana na usomaji wangu wa historia naona kuwa ni makosa makubwa kwa Tanzania kuruhusu Mzungu, Mwarabu au Mtusi kukalia kiti cha Urais, Uwaziri, au kiti cha Ukurugenzi wa Idara nyeti, hapa nchini Tanzania.

Namna yao ya kufikiri, kuhukumu na kutenda inapingana kabisa na Kanuni ya imani ya Utanzania, kama ilivyofupishwa hapo juu.

Na kwa kweli, hakuna haja ya taasisi nyeti katika Taifa letu kuongozwa na watu wenye tatizo la ukomo wa kimaarifa usioweza kuboreshwa ("irredeemable cognitive closure") wakati wapo Watanzania wengi wasio na tatizo hilo. Vyombo vya ulinzi na usalama vijisahihishe kabla ya uchaguzi mkuu ujao kwa kumshauri Rais Samia kukaa pembeni.

Uongozi wake wa maumivu ya miaka kumi, chini ya serikali ya awamu ya tano na awamu ya sita umetosha kutusaidia kumwelewa, kumpima na kumhukumu kwa haki, na hukumu.

Na hukumu ni kwamba: Rais Samia hana sifa ya kuitwa mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu wala rais wa nchi inayoitwa Tanzania. Mawazo, maneno na matendo yake yanapingana wazi wazo na Kanuni ya Imani ya Utanzania.

Wapo Watanzania wengi wenye sifa stahiki na wako tayari kupokea kijiti cha Urais. Wakati wa Samia kukaa pembeni ni sasa.

Namalizia makala hii kwa kutumia msemo wa KIlatini kwamba, "verbum sapienti sat est," yaani "enough has been said for the wise."

XIII. Marejeo:
  1. Aurel Croissant, David Kuehn and David Pion-Berlin (2024), Research Handbook on Civil–Military Relations (Northampton, USA:Edward Elgar Publishing, Inc),
  2. A. Walter Dorn, Jonathan Matloff and Jennifer Matthews (2000), "Preventing the Bloodbath: Could the UN have Predicted and Prevented the Rwanda Genocide?," Journal of Conflict Studies, XX.1, pp.9-52. URL: Preventing the Bloodbath - Could the UN have Predicted and Prevented the Rwanda Genocide? [Accessed on 10 May 2025]
  3. Bican Sahin (2010), Toleration: The Liberal Virtue (New York: Lexington Books)
  4. Chimene Benningshof (2023), The Role of Intelligence in the Failure To Prevent Genocide: A Comparative Analysis of Rwanda and Srebrenica. Mster of Arts Thesis, International Relations. Faculty of Humanities, Leiden University.
  5. Christopher Wolfe(2006), Natural Law Liberalism (New York: Cambridge University Press). Kitabu kimeanbatanishwa.
  6. Daniel John Pundu (2022), “Succession Politics as a Threat to Peace and Security in Africa: The Case for Constitutionalism and Democratization,” The Security Limelight (A Special Newsletter of the National Defense College of Tanzania), p.57-62. URL: https://www.ndctz.go.tz/uploads/documents/sw-1676552022-SUCCESSION POLITICS AS A THREAT TO PEACE AND SECURITY IN AFRICA-DR. DANIEL PUNDU.pdf [Accessed on 10 May 2025]
  7. Human Rights Watch (1999), Leave None to Tell the Story: Genocide in Rwanda, URL: https://www.refworld.org/reference/countryrep/hrw/1999/en/97537 [Accessed on 10 May 2025]
  8. Immaculee Ilibagiza (2007), Left to Tell: Discovering God amidst the Rwandan Holocaust ( Carlsbad , Califonia: Hay House ). Kitabu kimeambatanishwa.
  9. Jean Hatzfeld (2005), Machete Season: The Killers of Rwanda Speak (New York: Farrar, Straus, Giroux).
  10. Jean Mukimbiri(2005), "The Seven Stages of the Rwandan Genocide," Journal of International Criminal Justice, 3.4:823–836. URL: The Seven Stages of the Rwandan Genocide [Accessed on 10 May 2025]
  11. John Rawls (1993), Political Liberalism (New York: Columbia University Press)
  12. Juan Manuel Burgos(2022), Personalist Anthropology: A Philosophical Guide to Life (Delaware, USA: Vernon Press)
  13. Kevin F. Krupski(2023), "Who’s the Boss? Defining the Civil-Military Relationship in the Twenty-First Century," Military Review, 103.1: 26-33.
  14. Klaus Bachmann (2023), A History of Rwanda: From the Monarchy to Post-genocidal Justice (New York: Routledge)
  15. Leila Fielding (2014), Female Genocidaires during the Rwandan Genocide: When women kill ( Hamburg: Anchor Academic Publishing)
  16. Linder Melvern(2004), Conspiracy to Murder: The Rwandan Genocide (London/New York: Verso)
  17. Marie Eve Desrosiers(2023), Trajectories of Authoritarianism in Rwanda: Elusive Control before the Genocide (New York: Cambridge University Press)
  18. National Defense College (September 2022), Security Limelight (A Special Newsletter of the National Defense College of Tanzania).
  19. Susan Thomson (2017), Rwanda: From Genocide to Precarious Peace (New Haven and London: Yale University Press)
  20. Swaraj Parameswaran (2024), "Preventing or stopping the genocide: What was the main diplomatic failure in Rwanda?," URL: Preventing or stopping the genocide: What was the main diplomatic failure in Rwanda? [Accessed on 10 May 2025]
  21. Todd Salzman (2004), The church’s failure in Rwanda, URL: CATHOLICS & COLONIALISM | Commonweal Magazine [Accessed on 10 May 2025]
  22. William Galston (1991), Liberal Purposes: Goods, Virtues and Diversity in the Liberal State (Cambridge: Cambridge University Press)
  23. Philip Verwimp(2013), Peasants in Power: The Political Economy of Development and Genocide in Rwanda (New York/London: Springer Dordrecht Heidelberg)
  24. Viambatanisho vya Picha muhimu

Hayati Rais Juvénal Habyarimana

View attachment 3337373
Aisee hii piece of read is very Nice.

Nitaipa muda wa kutosha kupitia neno kwa neno.

Asante Dr Mama Amon.
 
Somo gani la kujifunza kutoka kwako wakati hujui hata kuandika.

Like seriously ni mtu gani mwenye level ya Doctorate, ambae inawezekana anaujumbe wa kuelimisha.

Wakati ujumbe wenyewe upo represented kama umeandikwa na mtoto wa primary, nani anamuda wa kusoma maandishi ya njano na grey text.

Sasa wewe Dr gani atakuandika hujui.

Halafu hayo mambo ya Rwanda, tulisha maliza hayatuhusu.
Mwenzetu kwani una kiwango gani cha Elimu ?
Hata umeshindwa kutambua andiko la kiwango cha PhD ?
 
Una akili mingi sana,watawala wa kiafrika hawapendi watu wanaotumia akili zao vyema
 
Pamoja na kiapo cha watumishi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama cha kuilinda na kuitetea katiba, je kuja mechanism yoyote rasmi ya kufanya hivyo pale rais anapoivunja katiba?

Hili ni swali tulijiuliza wakati wa JPM, and to be honest, utawala wa JPM ndio ulikuwa na mfanano mkubwa zaidi na yaliyukuwa yanatokea Rwanda mwanzoni mwa miaka ya 90.

Mpaka watu wakawa wanahisi huenda jamaa ni Mhutu, zile hazikuwa tabia za kitanzania kabisa.

Sasa tunaye mzanzibari ambaye ameamua kufuata nyayo za JPM, je anadhibitiwa vipi pale inapoonekana anakwenda kinyume na kiapo chake?
 
Somo gani la kujifunza kutoka kwako wakati hujui hata kuandika.

Like seriously ni mtu gani mwenye level ya Doctorate, ambae inawezekana anaujumbe wa kuelimisha.

Wakati ujumbe wenyewe upo represented kama umeandikwa na mtoto wa primary, nani anamuda wa kusoma maandishi ya njano na grey text.

Sasa wewe Dr gani atakuandika hujui.

Halafu hayo mambo ya Rwanda, tulisha maliza hayatuhusu.
MSomi nakuona unakosoa mwandiko badala ya kukosoa na kujaribu kutoa suluhisho la kile kinachotokea machoni mwetu
 
Huyu mtu ana matatizo sina shaka mada yake ina nondo na elimu ya kutufundisha:

Shida yake moja, kila mara anaambiwa aache kuweka yellow and grey texts anapoandika. It makes difficult to read kwa baadhi ya members kusoma.

Yeye aelewi vinginevyo I have no doubt message yake ni nzuri, lakini kusoma inakuwa shida keshaelezwa watu wengine wana poor vision.

Ndio msingi wa kumwambia hajui kuandika
 
Huyu mtu ana matatizo sina shaka mada yake ina nondo na elimu ya kutufundisha:

Shida yake moja, kila mara anaambiwa aache kuweka kuweka yellow and grey texts anapoandika. It makes difficult to read kwa baadhi ya members kusoma.

Yeye aelewi vinginevyo I have no doub bosst message yake ni nzuri, lakini kusoma inakuwa shida keshaelezwa watu wengine wana poor vision.

Ndio msingi wa kumwambia hajui kuandika
Nishakuelewa boss. Mwenye Uzi pia hakikisha kabla ya huu mwaka kwisha uwe umejifunza kuandika vizuri na hasa swala la kutuchanganyia rangirangi
 
Back
Top Bottom