Sometimes mambo yanakwama hautamani kuamshwa ukilala

fact only

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
1,826
Reaction score
2,851
Hellow JF.

Unakuta.
Unajiheshimu/Umejitunza vizuri unakuja kuoa/olewa na Malaya sugu.

Umepambana umejinyima ukalima nyanya zako vizuri siku unaenda shambani nyanya zimeungua nusu shamba.

Umesoma vizuri mpaka chuo lakini hauoni fursa wala haupati ajira(kulala/kula yako ya shidashida). Upo kwa SHEMEJI YAKO NA JAMII INAKUSIMANGA KILA KUKICHA.

Umepanga fremu ya biashara mwaka unaisha hakuna ulichokipata mpaka unakosa kodi yakulipia tena Fremu.

Mshahara wako na majukumu yako vitu viwili tofauti kabisa(madeni kila kona) familia zina kutazama wewe kama mkombozi.

Umekomaa kwenye mafunzo ya ujeshi/polisi na umefanya vizuri kabisa lakini kila siku wanaitwa wengine hata ulio wazidi uwezo.

Wakuu sometimes ukilala hautamani kuamshwa kabisa.
 
Amini nyakati ngumu hazidumu
usijifananishe wala Kujilinganisha na mwingine
Jaribu kufanya mambo mengine kama jambo unalofanya limegoma

Usisikilize sana maneno mtaani
Jifunze kwa wengine unaowaamini

Usikate tamaa, ukitaka kufahamu hili angalia ndege anavyotengeza kiota ndio utashangaa kutoka kajani kamoja hadi kuwa kiota sio mchezo.

ukijipata ishi kawaida kama ulivyozoea bajeti yako.
 
Sio unajipata unaanza kutamani wakina Giggy(reckless life).
 
Hellow JF.

Unakuta.
Unajiheshimu/Umejitunza vizuri unakuja kuoa/olewa na Malaya sugu.

Umepambana umejinyima ukalima nyanya zako vizuri siku unaenda shambani nyanya zimeungua nusu shamba.

Umesoma vizuri mpaka chuo lakini hauoni fursa wala haupati ajira(kulala/kula yako ya shidashida). Upo kwa SHEMEJI YAKO NA JAMII INAKUSIMANGA KILA KUKICHA.

Umepanga fremu ya biashara mwaka unaisha hakuna ulichokipata mpaka unakosa kodi yakulipia tena Fremu.

Mshahara wako na majukumu yako vitu viwili tofauti kabisa(madeni kila kona) familia zina kutazama wewe kama mkombozi.

Umekomaa kwenye mafunzo ya ujeshi/polisi na umefanya vizuri kabisa lakini kila siku wanaitwa wengine hata ulio wazidi uwezo.

Wakuu sometimes ukilala hautamani kuamshwa kabisa.
Inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom