Something is wrong somewhere

Forgo

Member
Apr 7, 2016
27
60
Kuna wakati unaweza ukaona vyema Ikulu kuongozwa na genge la wahuni wenye hofu ya Mungu na maadili kwa wananchi kuliko ikaongozwa na Mtu mmoja anayejipa ufalme na ukuu wa miliki zote hadi zisizo halali kwake na kujifanya yeye ndiye Sheria ya nchi na kwa neno lake mnatii.

Utambuzi wa mihimili mitatu (Serikali, Bunge na Mahakama) upo mmoja ambao wenyewe umechimbiwa chini zaidi! La hasha! yote ni kwasababu ya mamlaka ya Katiba mbovu tuliyonayo sasa na kwa ubovu huo ameibuka anayeweza kuitumia mamlaka hiyo awezavyo.

Kama Taifa tumefikia mahala ambapo tunafanya siasa za chuki, siasa za visasi na ubaguzi tukiongozwa na wakuu wenye mamlaka!, tumefikia kuishi kwa hofu kila mahali juu ya mtu mmoja aliyeamua kwa hiari yake kutumia uozo wa Katiba ya nchi kama njia ya kujipa Ukuu na Utukufu kwa dunia hii ya tatu!.

Sote tunafahamu adui wa Mtanzania ni Ujinga, Umasikini na Maradhi. Sasa ujinga umezaa Uwoga na tumefika mahala mjukuu amezaliwa Chuki. Kwa hapa kama Taifa hatuwezi kutoka salama bila ya machafuko na umwagaji damu (Japo siombei hayo).

Waliokuwa na dhamana ya kuukomesha ujinga walibeba unafiki na kuulea, sasa umekomaa na tungoje matunda ya unafiki wa wasomi wetu, viongozi wa dini na viongozi wa serikali na kila mmoja kwa nafasi yake avune alichopanda kwa jitihada za kufikishana hapa tulipo sasa.

Ukoloni mamboleo kuishi kwa uhuru wa bandela ilihali ni makabulu walele kwa watanzania wenzetu!, dhambi hii haitotuacha salama.

"When dictatorship is a fact then revolution becomes right" - Victor Hugo.

Muda utasema kwetu tutarudi lini.
 
Umesema ukweli unaouma.Ni bora Wahuni wenye kumuogopa Mungu kuliko unafiki anayejifanya wanamuogopa Mungu.

Tukisema hakuna msafi huko.Sasa baada ya kuona na yeye ni Mchafu ameanza vita na Wapiga kura.Chuki,visasi na Ubaguzi.

Watanzania wajinga tunatakiwa tuamini ati ukitumia Colgate na Chumvi basi madawa ya Kulevya hayataonekana kwenye damu yako!Sishangai Research ilifanywa na MTU asiye na cheti hata cha darasa la saba,lakini tunatakiwa tuamini upuuzi huna kunawapuuzi wenzake wakajumuika naye ili wampigie Makofi.

Wapuuzi wenzake ambao pia ni wakqepa kodi lakini kwa Sababu ni wenzake kulipa kodi siyo issue.

Hapa ndipo tulipofika.
 
Mpaka sasa wabunge wameshashindwa kwenye kutetea na kukemea kila mwenendo usiofaa wa nchi.
Naomba wapeleke muswada ambao utalegeza sheria za kumiliki silaha (bunduki) iwe kama Marekani.

Gwajima ana yake, Makonda anazunguka na bullet proof vest.

Mimi nikiwa na yangu nitajua cha kufanya.
 
Wauza unga siku hizi wakisikia neno MAKONDA wanatimua mbio mithili ya nyumbu aliyekatwa mkia

Mvua zinanyesha jaman shikeni majembe mkalime sasa,
Mvua inanyesha Sinza halafu Mwananyamala hainyeshi. Ile iliyosababisha mafuriko Sinza ilikazana kidogo baadaye ikakata unalimaje sasa kama mvua inabagua pa kunyesha?
 
kweli nchi ipo pabaya hadi akina lizaboni makada wa chama wamefyata mkia.

jamaa anaolodhesha majina ya wake zenu awakalbishe ikulu kwa chai ya jioni
 
Mvua inanyesha Sinza halafu Mwananyamala hainyeshi. Ile iliyosababisha mafuriko Sinza ilikazana kidogo baadaye ikakata unalimaje sasa kama mvua inabagua pa kunyesha?
Mtajijua, ila mkuu alishasema watu walime, kwqnza dar hakuna mashamba nendeni Lindi na mtwara
 
Afadhali hata mwenzako kaandika. Wewe umesubiri aandike ndio uje kuhoji....kweli ccm ina chuo cha kuzalisha majuha!
Una assume kwamba nimesubiri aandike.

Halafu ume assume kwamba mimi ni CCM.

Yote si kweli.

Nani ju.ha hapa sasa?
 
Back
Top Bottom