Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Bw Ahmed Isse Awad amesema Somalia kamwe haitajiunga na jumuiya yoyote inayoipinga Qatar.
Awad alisema hayo jana mjini Doha alipohudhuria kongamano, na kusisitiza kuwa Somalia haitafungamana na upande wowote juu ya mgogoro wa nchi za ghuba. Mapema jana, Awad alikutana na naibu waziri mkuu wa Qatar ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, na walijadili njia za kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili na utatuzi wa masuala ya kikanda wanayoyafuatilia kwa pamoja.
Qatar ni miongoni mwa nchi chache zinazotoa msaada kwa Somalia, na imeanzisha miradi ya maendeleo na miundombinu nchini humo.
Swahili.cri