Soma vitabu hivi uijue historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, TANU na uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,916
30,259
Ibn Hazim Media Centre imechapa vitabu vinne vidogo vidogo kwa usomaji wa haraka na kufanya jumla ya vitabu vinne kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.
  1. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam.
  2. Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam
  3. Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaaam
  4. Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre, 2019 Dar es Salaam
Kitabu cha kwanza katika mfululizo huu uliopewa anuani ya "Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika," ni historia ya Tewa Said Tewa, Sheikh Rashid Sembe na Zuberi Mtemvu na kitabu cha pili ni historia ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Peter Mhando.

Kitabu cha tatu kinaeleza historia ya Gerezani ambako ndiyo ilikuwa ngome ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Mwandishi anawachukua wasomaji wake katika safari ya miguu mtaa kwa mtaa wakipiga hodi nyumba kwa nyumba kwani chini ya kila paa kuna historia.

Kitabu cha nne kimeeleza historia ya marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu ambae katika maisha yake jina lake lilisimama kama nembo inayoeleza na kuthibitisha changamoto
zilizokuja na uhuru:

WATU MASHUHURI.jpg

1574564499084.png

DAR ES SALAAM NA WAZALENDO WAKE.jpg

1574564404134.png
 
Attachments

  • WATU MASHUHURI KITABU CHA PILI.jpg
    WATU MASHUHURI KITABU CHA PILI.jpg
    7.2 KB · Views: 10
  • SHEIKH ILUNGA KITABU.png
    SHEIKH ILUNGA KITABU.png
    7 KB · Views: 11
TAYARI TUNAFAHAMU NYERERE NDIYE ALIYETULETEA UHURU. HAYO MENGINE YATAKUKONDESHA SANA. TULISHASOMA VITABU NA KUSIKIA KWA WATU WA ZAMANI NYERERE NDIYE ALIYELETA UHURU TUNASHUKURU HE WAS SMART.
 
Komeo...
Kuwa Nyerere ndiye aliyeongoza harakati za kudai uhuru hakuna anaepinga.

Mimi nilichofanya katika historia hii ni kuenda mbali zaidi na kueleza historia kabla ya Nyerere ili kukamilisha historia kamili ya uhuru wa Tanganyika.

Ndipo katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes nikaanza na baba yake Kleist Sykes na marafiki zake akina Mzee bin Sudi na Ibrahim Hamisi walipounda African Association mwaka wa 1929 na sababu ni kuwa kutokana na chama hiki ndipo TANU ikaundwa mwaka wa 1954 na wanae wawili Abdul na Ally pamoja na Nyerere wakiwa kati ya wazalendo 17 wa TANU walioasisi chama hiki.

Sasa ikiwa utatafakari utajiuliza kwa nini ukoo huu wa Sykes unaunganishwa na harakati za uhuru kutoka kwa baba yao mwaka wa 1929?

Huu ni mfano mdogo mmoja tu.

Ukitaka kuingia kwa undani katika hili utagundua kuwa Nyerere alipofika Dar es Salaam 1952 alipokelewa na Abdul Sykes na mwaka wa 1953 Nyerere akagombea urais wa TAA dhidi ya Abdul katika Ukumbi wa Arnautoglo na Nyerere akashinda.

Lakini ili uelewe vipi Nyerere aliweza kuingizwa kwenye uongozi wa TAA 1953 kabla ya kufika katika uchaguzi inakubidi uelezwe mkutano wa Nansio nyumbani kwa Hamza Mwapachu kati ya Abdul, Hamza na Ali Mwinyi Tambwe nk. nk.

Katika haya halikadhalika kuna mengi ya kuelezwa nk. nk.

Unafika safari ya UNO mwaka wa 1955 na kujiuzulu kazi Nyerere na kwenda kuishi na Abdul Sykes nyumbani kwake nk. nk.

Jiulize imekuwaje Nyerere hakuwa mbali na Abdul Sykes toka afike Dar es Salaam 1952 hadi uhuru unapatikana?

Unaijua historia hii?

Ikiwa historia hii inakukera unataka harakati za kudai uhuru wasitajwe wazalendo wengine ila atajwe Nyerere peke yake hii ni bahati mbaya.
 
Unafanya vizuri kuhifadhi na kuwapatia elimu jamii, ila husiingize udini kama kwamba Nyerere alichukia waislamu. Cha muhimu ni kutokuwa biased.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAYARI TUNAFAHAMU NYERERE NDIYE ALIYETULETEA UHURU. HAYO MENGINE YATAKUKONDESHA SANA. TULISHASOMA VITABU NA KUSIKIA KWA WATU WA ZAMANI NYERERE NDIYE ALIYELETA UHURU TUNASHUKURU HE WAS SMART.
Katika harakati za uhuru, Nyerere alikuja baadae kidogo. Yeye zaidi aliunga juhudi za watu wa kanda ya Ziwa. Harakati kali za kudai uhuru zilichagizwa na kuchachamaa kwa kasi zaidi katika eneo la kanda ya ziwa. Soma vizuri historia.
 
Back
Top Bottom