Msukuma Msomi
Senior Member
- Feb 6, 2017
- 173
- 149
Majuzi nilienda mkoa flani kikazi, basi kwenye Lodge niliyofikia nikakuta mzee mmoja wa kizungu ambae ni mteja wa mara kwa mara hapo. Yeye ameishi Tanzania muda mrefu na huwa anakuja na kuondoka, kwao ni US, mara ya kwanza kukanyaga Tanzania ni 1984.
Basi tukatokea kuzoeana maana kila asubuhi tunakutana Restaurant kwaajili ya chai, na ndipo kila tukikutana either kwenye breakfast au lunch au dinner, akawa ananipigia mastori dizaini kama vichekesho hivi lakini ni kweli vilitokea, na anaongea kiswahili vizuri japo kwa lafudhi ya kizungu:
Basi tukatokea kuzoeana maana kila asubuhi tunakutana Restaurant kwaajili ya chai, na ndipo kila tukikutana either kwenye breakfast au lunch au dinner, akawa ananipigia mastori dizaini kama vichekesho hivi lakini ni kweli vilitokea, na anaongea kiswahili vizuri japo kwa lafudhi ya kizungu:
- ...siku moja kuna Masai aliingia kwenye kilabu cha pombe kule Arusha, begani kwakwe kulikuwa na Kasuku, kasuku yule alikuwa na rangi nzuri sana! Basi mhudumu wa baa akamuuliza Maasai; "huyo Kasuku mzuri sana, umemtoa wapi?"...kabla Maasai hajajibu, Kasuku akawahi na kutamka (kwa toni ya juu); "Longido!".
- ..."siku moja nilienda Babati kujumuika na wamishenari wa kanisa, sasa bado nilikuwa najifunza kiswahili. Ilipofika muda wa kula, pale walikuwa wanapika ugali wa aina mbili; wa mahindi na ugali wa ngano (ugali wa ngano unakaa zaidi tumboni)...basi akaja dada kutoka jikoni kuniuliza nakula nini?...nikamwambia: "naomba ugali wa ngono!"....yule dada alishtuka halafu akapiga kelele kuelekea jikoni kushtaki. Nikaona mama mkubwa ametoka, mkononi kashika kisu, na mkono mwingine sufuria...wakati huo wamishenari na mapadri wote wako chini wanagalagala kwa kucheka....yule mama akauliza kwa hasira: " umemwambia nini mwanangu??"...ndio wamishenari wakanitete kwamba nilikosea kiswahili.
- ..."siku moja nilikuwa kwenye kambi ya vijana kule Arusha, kiteto. Bado nilikuwa sijui kiswahili vizuri, na wale vijana walikuwa na utani mwingi ingawa mimi nilikuwa makini kujifunza kiswahili. Basi asubuhi mmoja, nikaamuliza kijana mmoja; "naomba uniambie jina la chakula tulichokula jana, ni kitamu sana!" yule kijana akajibu; "unataka kula chakula cha jana?"....nikajibu "ndio". Kijana akanisogelea na kuniambia, "nenda jikoni, waambie naomba kipolo!!"....nikapata wasiwasi kwasababu nilipokuwa naenda jikoni, wale vijana walikuwa wakiniangalia kwa shauku! Ikabidi niulize mtu mwingine "kipolo ni nini!?" ndio nikajua wamenidanganya!