Soma mtazamo huu na uchangie; Very interesting!

Trance M

Senior Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
183
Reaction score
37
Katika kupitapita kwenye website nikakutana na huu mtazamo. Kwa kweli nimeona una tija na si vibaya tukashare wote ili tusiwe na mpasuko wa kidini.

Ndugu zangu.
Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.

Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo Kristo) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.

Siuoni mfumo Kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo Kristo, siuoni kwa kuwa hii nchi ni ya Wakristo, Wapagani, Waislamu, Wahindu na dini nyingine.
Siuoni mfumo Kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina Omari Mahita, na Said Mwema wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauaji ya Waislamu wenzetu na ndugu zetu Wakristo.
Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo Kristo nikimwangalia JK na Makamu wake. Siuoni mfumo Kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi Shein na Seif Shariff Hamad. Siuoni mfumo kristo nikimwangalia Chande Othman yule jaji mkuu na Othman Rashid, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Si uoni hata nikiungalia kwenye Wizara na Taasisi nyingine za Serikali.

Wanaoongela mfumoKristo hawana uthibitisho wa kutosha kuhalalisha madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinachopiga macho pazia mchana wa jua kali.
Kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu, lazima tutambue kuwa adui wa Waislamu siyo Wakristo, Wapagani, Wahindu au dini nyingine zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.

Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia za amani kupata suluhu.
Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa Uislamu kwa Tanzania.

1. Adui namba moja kwa Waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa Kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu.
Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia. Mtakuwa mashahidi hata shule tulizonazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya Kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa Masheikh walioiva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanaoendana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa dini.

2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya CCM kupata uhalali wa kutawala kwa kura za Waislam.
Lazima tujue kuwa CCM wametutumia vya kutosha na kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano, Wametudanganya swala la Mahakama ya Kadhi wakati wa kampeni za 2010, Waislamu waliotaka tuwe na Kadhi kwa kauli hadaa ya CCM wakapiga kura za kuhadaiwa lakini baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa kudanganywa. Tuunge mkono chama ambacho hakitatugawa lakini pia ambacho hakitatugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.

3. BAKWATA imekuwa ni kama taasisi ya CCM. Wanamuweka wanayemtaka wao.
Lazima tupiganie BAKWATA iwe chombo huru cha Waislamu na tuwaweke viongozi wenye maono mapana tunaotaka sisi, na siyo CCM, hii itasaidia kurejesha imani kwa BAKWATA. Napendekeza vigezo vya kuiongoza BAKWTA viwe ni kwa kiwango cha PhD kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia, lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo Kikuu cha MUM kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa BAKWATA ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe Shahada moja na kuendelea.

4. Kutokufuata mafundisho ya mtume.
Mtume wetu Muhammad S.A.W alikuwa mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na kukumbushana mema na kukatazana mabaya. Uislamu haujajengwa kwenye misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya. Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya tutawaepuka wale wanaoutumia Uislamu wetu kama daraja ambalo baadaye hutuchafua wote. Mfano, wale walioingia kuchoma na kuvunja Makanisa na kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya Kanisa na mikate.
“Uislamu ni unadhifu” hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu kipenzi Muhammad S.W.A.
Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili tumuenzi kipenzi chetu.
—
Mohamedi ‘Moudy’ Mtoi
Twitter: mohamediMtoi
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Mtoi mimekuelewa vizuri na nimegundua kuwa kwa mtazamo wako ni kwamba waislamu Tanzania hawako sahihi katika kile wanachodai kuwa wanafanyiwa dhuluma hasa kile wanachopigia kilele yaani Mfumo Kristo.Umejaribu kutoa au kuelezea kwa mifano nafasi ambazo waislam wameshika ktk serikali,labda nikupongeze kwa kuweka wazi ktk yale ambayo unayajua juu madai ya waislam na pia kujaribu kuanisha maadui wa waislam. Labda mimi nikushauri kwanza utafute vitabu hivi Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara kilichoandikwa na Dr. Sivalon, Muslims and the State in Tanzania na Mwembachai Killings vilivyoandikwa na Prof.Hamza Njozi. Vile vile fuatilia kwa uchache habari ya MOU yaani Memondarum of Understanding ambayo serikali imeingia mkataba na kuwapatia taasisi za kidini(kikristo) mamilioni ya shilingi kuendesha taasisi zao. Rejea pia kauli ya Membe na Pengo juu Tanzania kujiunga na OIC. Kimsingi ukiangalia kwa umaikindi kuna chembembe za udini ambazo zimekuwepo toka kabla na baada ya uhuru. Kwa kauli ya Nyerere aliahidi kulipa KANISA nafasi nzuri ktk serikali ya Tanzania.Kuwa na viongozi wakubwa waislam si kigezo kikubwa cha kusema kuwa hakuna mfumo hebu angalia kiasilimia utakuta ni asilimia ndogo mno. Chukulia mf. ni waislamu wangapi ni Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wa wizara mbalimbali na taasisi na idara, wakuu wa shule, walimu wakuu na walimu. Na ukichunguza ni waislamu wangapi wana uwezo wa kushika nyazifa mbalimbali.Mimi kwa ushauri wangu serikali iyaangalie madai ya waislamu na sio kuyafumbia macho. Mwisho nakubaliana na wewe katika wale maadui wa uislamu hasa BAKWATA ni kikwazo kikubwa ktk harakati za waislamu toka ilipoundwa mwaka 1968 baada ya kuivunja East Africa Muslim Welfare Society(EAMWS) ambayo ilikuwa ni nguzo ya umoja wa waislamu Afrika Mashariki ambayo makao makuu yake yalikuwa Tanzania yaani Tanganyika by then pale Changombe.Ndugu yangu tusome historia itatusaidia kujua asili ya mambo au matatizo yanayotukabili.
 
Sawa kabisa,
 
Mtazamo wangu wakati mwingine huwa nafikiri sisi watu weusi haya mambo ya dini hizi 2 nikama hazituhusu vile! Pili huwa nfikiri kuwa sisi watu weusi kimsingi kama kuna pepo na moto basi sisi ni wa peponi kabisa na moto hautuhusu! FIKIRIA kwamba kabla hawajafika wageni hapa Afrika sisi tulikuwa dini gani? Kabla hawajfika wao hapa Afrika hakukuwa na Mkristo wala Muislamu! Na si miaka mingi tangu wafike hapa Afrika! Sasa swli linakuja kama ni kweli sisi binaadamu Dini ndio zitakazotupeleka peponi je babu zetu waliokufa kabla hizi dini ngeni hazijafika bala hili wameenda upande gani?! Kwa kuwa wao hawakuwa waislam wala wakristo. Uislamu na Ukristo tunaougombania sisi si dini zetu hizi,ni dini za wageni hizi. Na wlaiotuletea imani hizi wooote kimsingi hawakuja Afrika kutuletea dini bali walikuwa wanakuja kwa maslahi ya biashara zao nadini walitumia kutuzuga tu tutulie, na watu hawa walitutesa saana sana na kututumia kama ng'ombe wa kulimia sisi! Na mungu kwa nini alituumba sisi Waafrika tukiwa na mapungufu makubwa ya akili? Akaruhusu waafrika tuteswe na hawa waleta dini na ameruhusu waendelee kututesa mpakamilele? Tunaitwa nyani mpaka leo, wanazoa tu malighafi zetu milele,yaani sisi ndio duni kuliko mabara yooote, kwa nini dini zao hazijatusaidia hili? Na kwanini hakuna nabii na mtume mweusi katika dini zote mbili? WAAFRIKA kwetu ni peponi tu kama kutakuwapo kweli, mungu hawezi kuwa katili hivyo,atutese duniani kisha akatutese na huko: HIVYO KUWAZA JUU YA UISLAMU AU KUWAZA JUU YA UKRISTO kwa mwfrika ni kupoteza muda tu!!
 
Katika kupitapita kwenye website nikakutana na huu mtazamo. Kwa kweli nimeona una tija na si vibaya tukashare wote ili tusiwe na mpasuko wa kidini.

Ndugu zangu.
Tunapokuwa tunajiuliza mhemuko wa udini unatoka wapi au nani wameusababisha na kuuasisi, si vibaya tukajua maadui wakuu kwa upande wetu Waislamu.

Ukimjua adui ni rahisi kupambana naye na ni nusu ya ushindi kwenye vita ya kutafuta haki au usawa au kuondoa tunao uita unyanyasaji kwa waislamu au mfumo kristo kama wengine wanavyopenda kuita (Mimi sio muumini wa dhana ya mfumo Kristo) maana nimeona wakati wote Waislamu wenzangu wakishika nafasi kubwa Serikalini, kwenye mashirika ya umma na hata mashirika binafsi.

Siuoni mfumo Kristo kama unavyoitwa au kama baadhi ya Waislamu wenzangu wengine wanavyotaka kuaminisha umma wa Kiislamu juu ya hii dhana.
Nasema sioni kwa kuwa bado naamini katika uwezo na si mfumo Kristo, siuoni kwa kuwa hii nchi ni ya Wakristo, Wapagani, Waislamu, Wahindu na dini nyingine.
Siuoni mfumo Kristo kwa kuwa nimeshuhudia watu kama kina Omari Mahita, na Said Mwema wakiwa viongozi wa vyombo ambavyo mara kadhaa vimesababisha mauaji ya Waislamu wenzetu na ndugu zetu Wakristo.
Mtanisamehe bure wenye mtazamo tofauti na wangu lakini siuoni mfumo Kristo nikimwangalia JK na Makamu wake. Siuoni mfumo Kristo nikimuangalia wajina wangu Mohamedi Shein na Seif Shariff Hamad. Siuoni mfumo kristo nikimwangalia Chande Othman yule jaji mkuu na Othman Rashid, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Si uoni hata nikiungalia kwenye Wizara na Taasisi nyingine za Serikali.

Wanaoongela mfumoKristo hawana uthibitisho wa kutosha kuhalalisha madai yao ambayo kwa sasa nayaita hayana mashiko bali yametawaliwa na ukame wa maono na kiangazi cha fikra kinachopiga macho pazia mchana wa jua kali.
Kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu, lazima tutambue kuwa adui wa Waislamu siyo Wakristo, Wapagani, Wahindu au dini nyingine zinazopatikana kwenye huu ulimwengu.

Lazima tujue kuwa sisi ni ndugu tunaohitaji kuishi kwa upendo na kuvumiliana bila kuathiri imani zetu, na ikitokea lazima tutafute njia za amani kupata suluhu.
Kwa mtazamo wangu hawa ndio maadui wakubwa wa Uislamu kwa Tanzania.

1. Adui namba moja kwa Waislamu ni kutokuwa na mashule na vyuo vingi vyenye kutoa elimu bora kwa vijana wa Kiislamu na hata wale wa upande wa pili wanaokuja kuitafuta elimu.
Najua kuna watu watapinga sana lakini ukweli mchungu lazima tuuseme ili tupate pa kuanzia. Mtakuwa mashahidi hata shule tulizonazo hazifanyi vizuri sana kwenye mitihani ya Kitaifa lakini pia hata mashule yetu hayana mfumo wa kuandaa Masheikh walioiva kwenye elimu dunia na akhera. Mimi napendekeza harakati zetu ziwe kwenye kujenga mashule ya viwango pamoja na kuajiri walimu bora bila kujali dini zao ili kuwaandaa vijana bora wanaoendana na kasi ya sayansi na teknolojia kuelekea soko la ajira ya ushindani na pia viongozi bora wa dini.

2. Ni kukubali kufanywa nyezo ya CCM kupata uhalali wa kutawala kwa kura za Waislam.
Lazima tujue kuwa CCM wametutumia vya kutosha na kutudanganya vya kutosha, sasa tuseme basi! Mfano, Wametudanganya swala la Mahakama ya Kadhi wakati wa kampeni za 2010, Waislamu waliotaka tuwe na Kadhi kwa kauli hadaa ya CCM wakapiga kura za kuhadaiwa lakini baada ya matokeo wakatugeuka! Huku ni kuonekana kuwa tu-malofa wa kudanganywa. Tuunge mkono chama ambacho hakitatugawa lakini pia ambacho hakitatugawa na kuharibu umoja wetu wa kitaifa.

3. BAKWATA imekuwa ni kama taasisi ya CCM. Wanamuweka wanayemtaka wao.
Lazima tupiganie BAKWATA iwe chombo huru cha Waislamu na tuwaweke viongozi wenye maono mapana tunaotaka sisi, na siyo CCM, hii itasaidia kurejesha imani kwa BAKWATA. Napendekeza vigezo vya kuiongoza BAKWTA viwe ni kwa kiwango cha PhD kwa kuangalia uwezo wa elimu akhera na elimu dunia, lakini pia pamoja na uwezo wa kuongoza na kusimamia mambo. Chuo Kikuu cha MUM kinaweza kusaidia kuratibu kupatikana wataalamu na watendaji wengine wa BAKWATA ambao nao kiwango cha chini cha kuanzia kiwe Shahada moja na kuendelea.

4. Kutokufuata mafundisho ya mtume.
Mtume wetu Muhammad S.A.W alikuwa mwema, mwingi wa hekima na busara. Lazima tuyafuate mafundisho yake na kukumbushana mema na kukatazana mabaya. Uislamu haujajengwa kwenye misingi ya uhasama, vurugu, fujo, chuki na mambo mengine mabaya. Uislamu umejengwa kwenye misingi ya usafi wa matendo mema, kumcha Mungu, ukarimu, na kuhurumia na kuwajali wengine. Tukiyafanya haya tutawaepuka wale wanaoutumia Uislamu wetu kama daraja ambalo baadaye hutuchafua wote. Mfano, wale walioingia kuchoma na kuvunja Makanisa na kuiba sadaka, baadhi ya vifaa vya Kanisa na mikate.
¡°Uislamu ni unadhifu¡± hii ni moja ya tafsiri ya hadithi za mtume wetu kipenzi Muhammad S.W.A.
Tuyafuate mafundisho yake kwa matendo ili tumuenzi kipenzi chetu.
¡ª
Mohamedi ¡®Moudy¡¯ Mtoi
Twitter: mohamediMtoi

Nina mashaka kuwa wewe ni muislamu na ikiwa wewe ni muislamu basi ni mtu ambaye huumizi kichwa katika kuliendea jambo, unakurupuka, yaani uko shallow mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Mtazamo wangu wakati mwingine huwa nafikiri sisi watu weusi haya mambo ya dini hizi 2 nikama hazituhusu vile! Pili huwa nfikiri kuwa sisi watu weusi kimsingi kama kuna pepo na moto basi sisi ni wa peponi kabisa na moto hautuhusu! FIKIRIA kwamba kabla hawajafika wageni hapa Afrika sisi tulikuwa dini gani? Kabla hawajfika wao hapa Afrika hakukuwa na Mkristo wala Muislamu! Na si miaka mingi tangu wafike hapa Afrika! Sasa swli linakuja kama ni kweli sisi binaadamu Dini ndio zitakazotupeleka peponi je babu zetu waliokufa kabla hizi dini ngeni hazijafika bala hili wameenda upande gani?! Kwa kuwa wao hawakuwa waislam wala wakristo. Uislamu na Ukristo tunaougombania sisi si dini zetu hizi,ni dini za wageni hizi. Na wlaiotuletea imani hizi wooote kimsingi hawakuja Afrika kutuletea dini bali walikuwa wanakuja kwa maslahi ya biashara zao nadini walitumia kutuzuga tu tutulie, na watu hawa walitutesa saana sana na kututumia kama ng'ombe wa kulimia sisi! Na mungu kwa nini alituumba sisi Waafrika tukiwa na mapungufu makubwa ya akili? Akaruhusu waafrika tuteswe na hawa waleta dini na ameruhusu waendelee kututesa mpakamilele? Tunaitwa nyani mpaka leo, wanazoa tu malighafi zetu milele,yaani sisi ndio duni kuliko mabara yooote, kwa nini dini zao hazijatusaidia hili? Na kwanini hakuna nabii na mtume mweusi katika dini zote mbili? WAAFRIKA kwetu ni peponi tu kama kutakuwapo kweli, mungu hawezi kuwa katili hivyo,atutese duniani kisha akatutese na huko: HIVYO KUWAZA JUU YA UISLAMU AU KUWAZA JUU YA UKRISTO kwa mwfrika ni kupoteza muda tu!!

Mkuu una point hapa.
 
Sababu nyingine inayowarudisha nyuma waislamu ni kutokuwa na ndoa imara. Ndoa inapovunjika watoto wanapata taabu sana. Kuna jamii ambazo zaidi ya 80% ya ndoa zimevunjika! (PEngine hata zaidi.) Mwanamke anapoachwa huondoka na mtoto (watoto) . Kwa kuwa wengi wao hawajasoma hujaribu kazi kama za mama ntilie, kuuza matunda nk. Wakati huo huo akitafuta baba mwingine wa kuchukua nafasi ya yule aliyemwacha. Hapo maendeleo ya mtoto huwa mashakani sana.
Mwito kwa vijana wa kiislamu; Malezi mema ya mtoto ni kulelewa na baba na mama. Kuhakikisha hili angalieni maendeleo ya watu wanaoheshimu ndoa zao kama Moshi, Kagera, Mbeya, Arusha nk. Huo ndio u
kweli.
 
Nina mashaka kuwa wewe ni muislamu na ikiwa wewe ni muislamu basi ni mtu ambaye huumizi kichwa katika kuliendea jambo, unakurupuka, yaani uko shallow mkuu.

MDAU JR nadhani ungempinga kwa hoja za maana na mifano ingekuwa na tija. Hapo unaonesha wewe ndio upo shallow. Jaribu kutetea hoja yako.
 
Last edited by a moderator:
Sababu nyingine inayowarudisha nyuma waislamu ni kutokuwa na ndoa imara. Ndoa inapovunjika watoto wanapata taabu sana. Kuna jamii ambazo zaidi ya 80% ya ndoa zimevunjika! (PEngine hata zaidi.) Mwanamke anapoachwa huondoka na mtoto (watoto) . Kwa kuwa wengi wao hawajasoma hujaribu kazi kama za mama ntilie, kuuza matunda nk. Wakati huo huo akitafuta baba mwingine wa kuchukua nafasi ya yule aliyemwacha. Hapo maendeleo ya mtoto huwa mashakani sana.
Mwito kwa vijana wa kiislamu; Malezi mema ya mtoto ni kulelewa na baba na mama. Kuhakikisha hili angalieni maendeleo ya watu wanaoheshimu ndoa zao kama Moshi, Kagera, Mbeya, Arusha nk. Huo ndio u
kweli.

Mkuu seremi umezungumzia suala la ndoa katika uislam kuwa ndio tatizo kubwa linaloleta matatizo katika uislam. Mimi sikuungi mkono moja kwa moja kwa kuwa wapo waislam waliostaarishwa na elimu na kuamua kuwa na mke mmoja na hivyo kukuza watoto katika malezi bora. Suala la ndoa siku hizi ni janga si kwa waislam tu bali hata kwa wakristo.

Nadhani suala la msingi hapa ni kuweka kipaumbele katika ELIMU tena ile ya dunia na kwa kiasi flani elimu ya dini. Muumini akishaelimika atastaaribika na maisha yake yatakuwa ya kistaarabu.

Katika ulimwengu wa leo tunashuhudia teknolojia ikitawala ulimwengu hivyo hakuna mbadala wa maendeleo zaidi ya elimu. Ukijaribu kuangalia wakristo walio wengi wameelimika ukilinganisha na upande wa pili. Hii ni kutokana na kuweka kipaumbele katika elimu. Sikatai kuona watoto wa kiislam wakienda madrasa hata nyakati za asubuhi badala ya kuwa shule kwa wakati huo bali nakataa hizo juhudi za elimu ya ahera kupewa kipaumbele zaidi ya elimu ya dunia. Ukiangalia wakristo pia wana mafundisho kama kipaimara Komunio lakini hufanywa baada ya wanafunzi kutoka shuleni (shule ya dunia).

Nadhani ndugu zangu waislam ifikie kipindi tukubaliane na ukweli japo ni mchungu kuwa bila kuweka kipaumbele katika elimu dunia na kubakia katika elimu ahera hakika mfumo kristo hautakwisha.
 
Last edited by a moderator:
mtoi umetumwa na bakwata ?. Dhuluma zote hizi bado unaleta ----- hapa. mfumo kristo hupo muulize membe atakujibu vizuri kilichompata kuhusu kuanzishwa kwa oic
 
Sawa kabisa,

Hapa umenena mkuu sultan. Zamani sana wakati nikiwa nasoma primary kulikuwa na vikundi vya dini mbalimbali vikileta sinema zikionesha mafundisho ya yesu kristo na wakati mwingine sinema za mtume Mohamad SAW zikielezea athari za kutokumwabudu Mungu na maisha baada ya kifo jambo ambalo ndilo linalochukua attention kubwa za waumini wa dini zote mbili. Kwakweli nilifurahia sana utotoni kwani sinema zilikuwa na mafundisho ya kusisimua.

Nilipomaliza chuo ndipo niliookomaa kiakili na kupata ufahamu juu ya suala zima la imani hasa baada ya kuanza kusoma historia ya ukombozi wa mwafrika, Imani na dini zetu kwa ujumla.

Nilikuja kuwa na masuali mengi ambayo hayajajibiwa vizuri Moja wapo ni hilo ulilohoji juu ya hukumu ya mababu zetu waliotangulia mbele za haki kabla ya dini kuwafikia. Pili ni jinsi waarabu na wazungu walivyotugeuza watumwa huku wao ndio waliotuletea hizi dini zinayosisitiza upendo. Tatu ni maisha baada ya kifo bado ni imani kali kwa pande zote mbili.

Tunasoma kuwa zamani waafrika na hasa Tanganyika tulikuwa ni wamoja na tulikuwa na ibada zetu za kijadi (kuabudu wanyama, miti nk) na tuliishi kwa mshikamano. Iweje leo waliotuletea dini wametuacha nayo na wao kufuata mambo ya kidunia? Tufuate lipi tuache lipi? Tunaona uarabuni watu wanavyochinjana pia tunaona ulaya na marekani watu wanavyopora rasilimali zetu kwa manufaa yao.

Nadhani tusigombane sana kutokana na masuala ya kidini kwani huo sio utamaduni wetu.
 
Sababu nyingine inayowarudisha nyuma waislamu ni kutokuwa na ndoa imara. Ndoa inapovunjika watoto wanapata taabu sana. Kuna jamii ambazo zaidi ya 80% ya ndoa zimevunjika! (PEngine hata zaidi.) Mwanamke anapoachwa huondoka na mtoto (watoto) . Kwa kuwa wengi wao hawajasoma hujaribu kazi kama za mama ntilie, kuuza matunda nk. Wakati huo huo akitafuta baba mwingine wa kuchukua nafasi ya yule aliyemwacha. Hapo maendeleo ya mtoto huwa mashakani sana.
Mwito kwa vijana wa kiislamu; Malezi mema ya mtoto ni kulelewa na baba na mama. Kuhakikisha hili angalieni maendeleo ya watu wanaoheshimu ndoa zao kama Moshi, Kagera, Mbeya, Arusha nk. Huo ndio u
kweli.

ukweli mtupu
 
Mkuu seremi umezungumzia suala la ndoa katika uislam kuwa ndio tatizo kubwa linaloleta matatizo katika uislam. Mimi sikuungi mkono moja kwa moja kwa kuwa wapo waislam waliostaarishwa na elimu na kuamua kuwa na mke mmoja na hivyo kukuza watoto katika malezi bora. Suala la ndoa siku hizi ni janga si kwa waislam tu bali hata kwa wakristo.

Nadhani suala la msingi hapa ni kuweka kipaumbele katika ELIMU tena ile ya dunia na kwa kiasi flani elimu ya dini. Muumini akishaelimika atastaaribika na maisha yake yatakuwa ya kistaarabu.

Katika ulimwengu wa leo tunashuhudia teknolojia ikitawala ulimwengu hivyo hakuna mbadala wa maendeleo zaidi ya elimu. Ukijaribu kuangalia wakristo walio wengi wameelimika ukilinganisha na upande wa pili. Hii ni kutokana na kuweka kipaumbele katika elimu. Sikatai kuona watoto wa kiislam wakienda madrasa hata nyakati za asubuhi badala ya kuwa shule kwa wakati huo bali nakataa hizo juhudi za elimu ya ahera kupewa kipaumbele zaidi ya elimu ya dunia. Ukiangalia wakristo pia wana mafundisho kama kipaimara Komunio lakini hufanywa baada ya wanafunzi kutoka shuleni (shule ya dunia).

Nadhani ndugu zangu waislam ifikie kipindi tukubaliane na ukweli japo ni mchungu kuwa bila kuweka kipaumbele katika elimu dunia na kubakia katika elimu ahera hakika mfumo kristo hautakwisha.

Hapa umenena, Elimu ni tatizo kwa wengi waislamu na wamekazana kusema mfumo kristo kwa kuwa viongizi wengi walioshikilia serikali na maendeleo ki ujumla ni wakristo.
Kihistoria wakristo walithamini saana elimu hata mababu wa kikristo ndio waliowasomesha watoto wao ambao kwa sasa wengi wao ni viongozi na wenye maendeleo.
Kwa upande wa waislamu mababu zao walikazania saana elimu akhera (madrasa) na kuwa sheikh ndo lengo kuu. Na kwa sasa ndio hawa wanaolalamikia mfumo kristo.
Ukweli utabaki pale pale... Kwa dunia ya sasa bila elimu dunia hufiki popote hasa kwenye upande wa uongozi! Cha msingi ni kubadilika na kukubali kuwa ELIMU ndo kila kitu ifanywe iwe ni lazima kwa kila mtu.
Na siku zoote mtu anayelalamikia mifumo ya kidini kama ndio kikwazo chunguza saaana Elimu na malezi yake yaliyomkuza hutobishana nae.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu the-true-wash kumbe tuna mtazamo mmoja. Nashukuru kwamba watu wengi wanalitambua hili kuwa ni tatizo na adui mkubwa wa waislam. Nadhani sasa ni muda muafaka wa kufanya mabadiliko. Mabadiliko haya yanaanzia katika kiini ambacho ni masheikh na viongozi wakuu wa kiislam kwa kuhubiri maendeleo hasa ya Elimu ya dunia.

Waumini wakipata mafundisho mazuri kutoka kwa masheikh yenye mwelekeo mzuri wa mageuzi katika suala la elimu ya dunia nadhani wazazi hawatopoteza mda kuwapeleka watoto wao madrasa kwa mda mrefu. Sikatai watoto kupata elimu ya kiroho lakini nataka pawepo kipaumbele zaidi katika elimu ya dunia. Pia uchaguzi wa masheikh uzingatie suala la elimu ya akhera na elimu ya dunia. Elimu iwe ni kigezo kwa yeyote anayehitaji uongozi kwenye msikiti.
 
Last edited by a moderator:
mtoi umetumwa na bakwata ?. Dhuluma zote hizi bado unaleta ----- hapa. mfumo kristo hupo muulize membe atakujibu vizuri kilichompata kuhusu kuanzishwa kwa oic

OIC haiwezi kuanzishwa katika nchi isiyo na dini.
 
Huyo si muislam na anapretend kua ye ni muislam but si muislam,,....na hajitambui ata kidogo,,.....pumbaless hakuna logic hapo,,....mara nyingine bora uwe kimya kuliko kuongea pumba ambazo ata ukimpa bata hatozila,,....brainless ideas,,....!!
 
Mkuu seremi umezungumzia suala la ndoa katika uislam kuwa ndio tatizo kubwa linaloleta matatizo katika uislam. Mimi sikuungi mkono moja kwa moja kwa kuwa wapo waislam waliostaarishwa na elimu na kuamua kuwa na mke mmoja na hivyo kukuza watoto katika malezi bora. Suala la ndoa siku hizi ni janga si kwa waislam tu bali hata kwa wakristo.

Nadhani suala la msingi hapa ni kuweka kipaumbele katika ELIMU tena ile ya dunia na kwa kiasi flani elimu ya dini. Muumini akishaelimika atastaaribika na maisha yake yatakuwa ya kistaarabu.

Katika ulimwengu wa leo tunashuhudia teknolojia ikitawala ulimwengu hivyo hakuna mbadala wa maendeleo zaidi ya elimu. Ukijaribu kuangalia wakristo walio wengi wameelimika ukilinganisha na upande wa pili. Hii ni kutokana na kuweka kipaumbele katika elimu. Sikatai kuona watoto wa kiislam wakienda madrasa hata nyakati za asubuhi badala ya kuwa shule kwa wakati huo bali nakataa hizo juhudi za elimu ya ahera kupewa kipaumbele zaidi ya elimu ya dunia. Ukiangalia wakristo pia wana mafundisho kama kipaimara Komunio lakini hufanywa baada ya wanafunzi kutoka shuleni (shule ya dunia).

Nadhani ndugu zangu waislam ifikie kipindi tukubaliane na ukweli japo ni mchungu kuwa bila kuweka kipaumbele katika elimu dunia na kubakia katika elimu ahera hakika mfumo kristo hautakwisha.
Familia imara na thabiti ndio msingi wa mambo yote mazuri uyaonayo duniani.unapo zungumzia ELIMU, tambua kuwa inaanza na elimu ya awali halafu msingi,sekondari na hatimae chuo kikuu.ndoa ikivunjika wanao ishia kupata taabu ni watoto.hawapati mahitaji muhimu kama mavazi,malazi, chakula na hata elimu bora.
Binafsi nimepata kufanyia utafiti juu ya matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa mikoa ya LINDI, MTWARA NA PWANI.Matokeo ya utafiti ule yalinishangaza sana.zaidi ya asilimia 95 ya wasichana wote wanao hitimu kidato cha nne hawaendi kidato cha tano.Zaidi ya asilimia 85 ya wavulana wote wanahitimu kidato cha nne hawaendi kidato cha tano.Lakini pia mikoa hii yote kwa pamoja ina shule za sekondari chache kuliko mkoa wa kilimanjaro au Mbeya. hali ikiwa hivyo maana yake ni kwamba wasomi kutoka mikoa hii yenye waislamu wengi itazalisha wasomi wachache kuliko Kilimanjaro au Mbeya.MSINGI WA TATIZO HILI NI KUWA KARIBU ASILIMIA 80 YA WANAFUNZI WOTE WA LINDI, MTWARA NA PWANI wanalelewa na mzazi mmoja au wanakaa na babu zao au nyanya zao!weak familiea means weak or poor upbringing.
 
Pia nashindwa kuelewa kwann waislamu walalamike kuwa kuwa kuna mfumo kristo wakati vyuo vya kikristo havibagui wala havikuchagulii mavazi, tofauti na vyuo vya kiislamu, mf.Pale Chuo kikuu cha kiislamu morogoro wakristo hawajichagulii mavazi wote kama ni wasichana wanavaa kama waislamu, pale Songea Muslim pia hivyo hivyo, huo sio unyanyasaji kwa wakristo hawa? Mbona waislamu ktk vyuo vya kikristo wapo huru!!.Hivyo waislamu tusipende kulalamika without doing research.Elimu mbovu mnaipata kutokana na kuangalia udin kuliko kuangalia nan ana uwezo gan.
 
Nina mashaka kuwa wewe ni muislamu na ikiwa wewe ni muislamu basi ni mtu ambaye huumizi kichwa katika kuliendea jambo, unakurupuka, yaani uko shallow mkuu.

naona kama wewe uko shallow zaidi yake, maana hukuweza kujengea hoja walau kipengele kimoja
 
Huyo si muislam na anapretend kua ye ni muislam but si muislam,,....na hajitambui ata kidogo,,.....pumbaless hakuna logic hapo,,....mara nyingine bora uwe kimya kuliko kuongea pumba ambazo ata ukimpa bata hatozila,,....brainless ideas,,....!!
Marnah sijakuelewa ulivyomshambulia bwana Mtoi bila kuwa na sababu au hoja ya msingi. Nadhani wewe ndio baadhi ya wachache mliokosa elimu au kama unayo basi hujaelimika.

Mkosoe bwana Mtoi kwa hoja na si kumuita brainless au mtoa pumba. Hapo unabaki wewe kuwa brainless kwa kuwa hakuna ulichochangia badala ya kujishushia heshima yako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom