Kadri WanaCHADEMA wanavyojitokeza humu jamvini kutetea hoja ya kwanini akina Mbowe waendelee kubakia madarakani ndivyo wanavyozidi kuipa nguvu hoja ya MAGAMBA ya kwanini CHADEMA wasiaminiwe kupewa Nchi.
Hivi tunaposema kwamba CHADEMA itakufa bila ya akina Mbowe hii inaashiria nini? Hii inaashiria kuwa CHADEMA kama taasisi bado haijawa imara kwa maana ya kujenga misingi, miundo na mifumo thabiti ya namna kupata viongozi bora wa kuaminika, namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kisiasa instead imejengwa kuwa Taasisi dhaifu ambayo political survival yake inategemea uwepo wa Viongozi flani tu wachache.
Sasa tuangalie muda Uongozi wa sasa umekuwa madarakani na kasi yake katika kukijenga Chama kama Taasisi imara,Hivi tujiulize ni sahihi kuendelea kuwa Uongozi huu ambao kasi yake kukijenga Chama imekuwa ni ya kusua sua au tunahitaji Uongozi mpya uimarishe mifumo ya Chama na kukifanya kuwa Chama kisichotegemea watu wachache kutimiza malengo yake mbalimbali yana hopefully kiwe tayari kuing'oa CCM madarakani 2015.
Tech Wiz,
Suala la uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia
Wanaojadili kuhusu term limits hawajengi hoja kuonyesha ni namna gani ukosefu wa ukomo wa uongozi ndani ya vyama unaua demokrasia.
Chama cha Congress cha nchini India 'The Largest democracy" in the world hakijawahi kuwa na ukomo wa Uongozi.Sonia Gandhi ameongoza Congress kwa muda mrefu
Nchini Afrika Kusini chama cha ANC hakina term limits.
Chama cha Labour nchini Ireland kimeweka kigezo cha kushindwa uchaguzi kama kigezo cha kubadili uongozi
Prof.Petracca wa Irvene huko Canada amejadilli kwa kina hoja hii na kukusanya analysisi ya scholars wengi kuhusu term limits na demokrasia
Term limits pia inaweza kuwa ni kigezo cha kuua democracy maana unamnyima mgombea na wapiga kura haki ya kumchagua wanayemtaka
Playing devil's advocate side:Mbona tunakubali term limits kwa urais halafu kwa wabunge hatupigi kelele?
Nchini Marekani uchaguzi uliopita Mitt Romney alibeba ajenda ya analyst Denmit ya kutaka bunge la Congress liwekewe term limit kupitia constitutional amendments.
Mapendekezo ni house of Reps iwe na term 3 yaani 6 years na Senate iwe na 2 terms yaani 12 years
Sasa tukirudi kwa suala la CHADEMA kuhusu term limit kama inavyoshupaliwa hapa basi kuna uwezekano wa kufanyika kama ilivyokua kwa Vladmir Putin kule Russia.Alikua Rais for 10 years kisha akashuka na kuwa powerful PM kabla ya kurudi tena kugombe urais.Sasa hapo malengo na dhamira ya kubadili uongozi imetimia?
So the really Democracy ni uchaguzi ndio utakaoamua