hari ikawa ngumu sana, nilikuwa nakaa histel ya mikumi, kwa wale ambao wapo chuo cha saut wanaifahamu, mungu akasaidia baada ya wiki moja, kulikuwa na jamaa mmoja akahamishwa chuo na kupelekwa saut ya tabora, so kitanda kikawa waz, mim nikalala pale kama wiki mbili tu, mara majina ya bodi y mikopo yakatoka, nikawa nimepata 30% yaani 70% nijilipie. kumbuka bado sijafanya registration kama laki tano nadaiwa, wenzangu anafurahia boom, mimi nikawa nalia, tena nalia machozi, nikasema, niache tu chuo nirudi mtaani,lakini nafsi ikakataa na kunikumbusha kuwa wewe ni mtoto wa kiume, kumbuka kutoka kidato cha kwanza hadi hapa ulipofika, mwenyezimungu mkubwa bodi wakatuma pesa kama lakisaba na kitu, nikashukuru mungu, nikatoa laki tano na nusu, nikafanya registration. na nikapigwa penat juu, pia nikapewa rasmi kile kitanda alichoacha yule jamaa, mfukoni nikwa na laki mbili hivi. kidogo maisha yakaanza kuwa nafuu, nikaanza kuingia darasani,kununua vifaa na mbndaliz ,nikawa nimetumia kama 50000, inaendelea....