Soldering station huwa bei gani?

cobra poison

Member
Sep 14, 2016
32
12
453f334efaeed0d2d650d86f901364a2.jpg

Soldering station ni bei gani na wapi zinapatikana
 
453f334efaeed0d2d650d86f901364a2.jpg

Soldering station ni bei gani na wapi zinapatikana

Inategemea na product make, ila hiyo hapo juu kwenye picha yako sio nzuri , zina compressor kwenye heater ya hot gun.

angalia hii hicha hapa chini hiyo LUCKY 852D ambayo ina compressor ndani ya hiyo main unit yake. bei ni wastani wa 170,000/-
 
Attachments

  • LUKEY1.jpg
    LUKEY1.jpg
    46 KB · Views: 192
  • LUKEY2.jpg
    LUKEY2.jpg
    51.2 KB · Views: 160
hii ndo inayotumika kunyofolea vifaa vya kwenye circuit ya simu kama ac ???
 
hii ndo inayotumika kunyofolea vifaa vya kwenye circuit ya simu kama ac ???
Sio AC ni IC. . inakuwa na solder gun ya kawaida isipokuwa ina adjustable temperature. Pia ina hot Air gun ambayo inatumika kuchoma vitu vyenye pin ndogo, kukausha unyevu, kuyeyusha wax au gundi, ku shape plastic insulator etc
 
mkuu nimezima fegi(saluti) wewe itakua ni nyoko kwenye hizi ishu

swali la nyongeza tafadhali lakini liko nje ya mada :

nina galaxy s3 nikichomeka charge inaonyesha kialama cha kuingia charge lakini asilimia hazipandi badala yake zinashuka kama vile haijachomekwa charge ; na nikichomeka charge ikiwa nimeizima inatokea battery kama vile inataka kuonyesha inaingia halafu inazima mazima ..

Ufumbuzi wa hili tatizo unaweza kua ni nini???

N:B Tatizo hili halikuepo kabla na nimejaribu kubadilisha battery lakini hamna kilichobadilika
 
Baadhi ya pin za hiyo port ya kuchajia zimevunjika au zimechomoka kutoka kwenye pcb (saket). Chunguza kwa makini kama hiyo port inatingishika, unaweza kuitingisha kwa sindano au toothpick.
 
Baadhi ya pin za hiyo port ya kuchajia zimevunjika au zimechomoka kutoka kwenye pcb (saket). Chunguza kwa makini kama hiyo port inatingishika, unaweza kuitingisha kwa sindano au toothpick.
asante mkuu ntajaribu kuchunguza

swali la nyongeza:
kwanini nikijaza battery kwa kobe battery inadrain faster tofauti na ilivokua awali ? pia nini kinasababisha simu kunyonya charge? na mfano nikiflash hii simu je kuna uwezekano wowote wa hili tatizo kwisha?
 
Uwezekano mkubwa hilo tatizo ni la Hardware na sio software. Hivyo kuflash hakutasaidia. ( ila kama una uhakika port ipo sawa na battery ipo sawa yaani kwa ujumla kama hakuna tatizo la hardware flashing inaweza kuwa suluhisho). Dalili zote zinaonesha hilo ni tatizo la hardware.

Kuhusu Kobe. Kobe nyingi hazina acuracy , unakuta Kobe inatoa voltage zaidi volt 5 . zingine zinatoa 9V hata kama zimeandikwa 5v. Sasa kwakuwa battery za lithium ni INTELLIGENCE (yaani zina akili ) basi battery itajilinda kwa kujifanya imejaa ili kuepuka uharibifu. Lakini kiuhalisia battery inakuwa bado haijafika 100% . Huwa kinachosema kama battery imejaa au bado huwa ni controller iliyopo ndani ya battery ambayo kazi yake ni PROTECTION dhidi ya umeme unaoingia na kutoka kwenye battery pamoja kuitambulisha simu aina ya battery iliyopo kwenye simu.

Saket hii inaweza kutoa taarifa za uongo endapo;
1. Battery imechajiwa na voltage zisizo sahihi.
2. Battery imewekwa mahali penye joto au imepata joto sana kuliko kiwango kinachoruhusiwa.

3. Battetry imechajiwa na current ndogo na imekaa kwenye chaji kwa muda mrefu sana. N.k
 
Back
Top Bottom