Swash Bizo
Senior Member
- Jan 29, 2011
- 141
- 93
Kaka,solar panel 60W original ya uhakika
hi wanajamii wenzangu........
ninanuza solar panel 60W original ya uhakika ikiwa na charger controler yake na betri ya 140N pamoja na inverter ya 500w na waya mbili za 30mita
bei ni 800 tu kwa vyote hivyo.
nimevuta umeme ndio maana ninaviuza vitu hivi.
contact: 0757 983670 AU PM.......for serious buyers only..!!!
Kaka,
60W maana yake nini, inawasha bulb moja ya watts 60 tu, na ukitaka kuwasha bulb ya jikoni itabidi ile ya sebuleni tukazime mpaka tumalize kupika, unless tuna viji bulb vya watts tano tano ndani vingiii, sio? Ama nakosea?
Hiyo bei iko ktk dola, au Tsh? Kama ni tsh naomba nikutumie kwa mpesa kabisa nisichelewe.
Usiuze, tafuta mtaalam wa umeme akuungie relay switch(sawa na contacter switch za motor) Battery zikiwa na charge relay switch inakata supply ya Tanesco, umeme wa battery unatumika,Charge ya battery ikupungua relay switch inaunga umeme wa Tanesco automatically. Hivi utaokoa gharama za umeme wa Tanesco kwa kiwango fulani.
Kaka,
60W maana yake nini, inawasha bulb moja ya watts 60 tu, na ukitaka kuwasha bulb ya jikoni itabidi ile ya sebuleni tukazime mpaka tumalize kupika, unless tuna viji bulb vya watts tano tano ndani vingiii, sio? Ama nakosea?
Usiuze, tafuta mtaalam wa umeme akuungie relay switch(sawa na contacter switch za motor) Battery zikiwa na charge relay switch inakata supply ya Tanesco, umeme wa battery unatumika,Charge ya battery ikupungua relay switch inaunga umeme wa Tanesco automatically. Hivi utaokoa gharama za umeme wa Tanesco kwa kiwango fulani.
Hapana!umeme ni very complicated kaka........
Hapana!
Huu ni umeme wa form TWO! Usinambie umeme ni kitu very complicated! Unapokutana na mtu kwenye mtandao mimi huwa naogopa sana kumwambia hicho kitu ni kigumu, kigumu kwako, hujui yeye amesahihisha dissertation ngapi za umeme!
Hebu tuone unatuuzia nini hapa. Umesema kwamba nikitaka naweza kununua bulb za energy saver za watts 12, badala ya 60w. Kwa hiyo chochote nitakachofanya hii mashine itawasha taa ndogo ndogo za watts 12 zisizozidi jumla watts 60, mwisho! I said as much! Nilisema hivyo awali. Na mtu mwenye bulb ya watts 60 kama anazo mbili itabidi azime ya sebuleni akawashe ya jikoni apike akimaliza azime akawashe radio. Na akiwasha taa ya chumbani huku sebuleni wageni kiza! You can't escape that fact, au nieleze nakosea wapi.
In other words siwezi kuthubutu kuwasha jokofu la watts 600!
Siwezi kuwasha hata ka flat panel TV kadogo dogo ka nchi 27 ka watts 130.
Siwezi kuthubutu kuwasha jiko la umeme.
Kwa hiyo hii mashine sana sana ni ya kwenda nayo camp nje ya mji kucharge mashine ya kunyolea ndevu na kisimu kidogo cha Techno.
Huwezi kutengeneza watts ambazo hazipo, simple physics, I mean, there is no physics here at all here. Usinambie umeme ni kitu complicated kana kwamba nachemka halafu siwezi kuelewa unachosema, which is smokescreen anyway. Ndio maana nchi yetu tunalea jamii inayojinyima elimu, hatuna elimu, tunaingizwa mikenge na makampuni ya kufua umeme kwa sababu tunashindwa kudadavua mambo madogo ya megawatt hours ya ma mashine zao hafifu wanazotuletea!
Kaka, hapo utakuwa umetengeza nishati. Haiwezekani. Inverter sio chanzo cha umeme.Kumbuka umeme huu hucharge battery na battery hutoa current kubwa kwenda kwenye 500W ....Ni appliances zile ambazo ni less than or equal to 500W zaweza tumika.
Tukiitendea haki hiyo Joules law of conservation of energy ni input energy ni solar panel ya 60W times time to be exposed to sun utakachopata kinaitwa energy(60W ni Power na sio energy). Uki expose kwa 0.1 second unapata 1 Joule of energy sasa hapo ndipo pakuanzia na hiyo kwenye output zako unaweza ukawa na jokofu la 600w unaweza kulitumi kwa 1/10 of the time to charge. Yaani lisaa 1.1 kwa siku. Ila kwa ushauri solar ya Watt 120 na battery 2 za N100 unweza kutumia TV na taa kama 10. Kuna watundu wanweza ku recycle huo umeme ukarecharge battery kwakuongeza baadhi ya vitu kwenye inverter.Kaka, hapo utakuwa umetengeza nishati. Haiwezekani. Inverter sio chanzo cha umeme.
Chanzo cha umeme wako kikiwa 60watts basi hakuna mtambo mwingine wowote duniani ambao utafungwa hapo kutengeneza watts ziwe hata 61, achilia mbali 500W, bila kuwa na chanzo kingine. Sijui unanielewa? Huwezi ku run chombo cha Watts 500 kwenye power source ya 60W, elemental Physics, ambayo ni Principle of Conservation of Energy. I mean this if fundamental stuff my brother. Hata yeye mwenyewe mwenye mali amekuba kwamba hiki kifaa anachouza huwezi ku run chombo kinachozidi watts 60, kanambie nikatafute vitaa taa vya watts 12 au vya watts tisa tisa!
Lakini hii ni sayansi, si dini na mi si mhubiri, naweza kuwa wrong, kaa nakosea show me the physics.
Na hapo umezungumzia kama umeme hautumiki. Yaani utakuwa unachaji betri kwa masaa hayo 11 bila kuweka load.Ukifunga moja-kwa-moja toka kwenye panel bila betri utapata dc 12v, <5A, <60W, hii ni sahihi. Ukifunga betri, 12V, 5A kwa masaa ~11(H) =~55AH zinajaa kwenye betri. Betri alilo nalo ni kubwa anatumia ~1/3 ya uwezo kama charger inaruhusu anaweza ongeza panel nyingine. 55AH kwa 12V ni ~660W ambazo waweza kuzitumia utakavyo.