Soko la Mwanjelwa CHADEMA Msituangushe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Soko la Mwanjelwa CHADEMA Msituangushe!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Oct 30, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ujenzi wa soko la Mwanjelwa umekamilika kwa asilimia 99 na kazi iliyobakia ni jinsi gani au mtindo gani utatumika kuliwezesha soko hilo lianze kazi tena. CHADEMA ina nguvu sana Mbeya Mjini na Mbunge wake Joseph Mbilinyi anakubalika sana kwa watu. lakini kama hawataingiza nguvu zao kwenye kusimamia watu watakaoingia kwenye Soko jipya la Mwanjelwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kupoteza umaarufu kwa wananchi wa kawaida wa Mbeya Mjini.

  Baada ya Soko la Mwanjelwa kuungua waliokuwa wafanyabiashara wake walihamishiwa eneo la SIDO na wengi wao waliunguliwa vitu vyao na kupata hasara kubwa sana. Lakini mpango wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na baadhi ya madiwani wanataka watakaoingia kwenye soko Jipya la Mwanjelwa wawe ni wafanyabiashara wenye mtaji wa wastani wa shilingi 3,000,000 na si chini wa hapo.

  Kuna uwezekano mkubwa sana wale waliokuwa wafanyabishara kwenye soko hilo na kuunguliwa vitu vyao ambao kwa sasa hawana mtaji huo unaotakiwa kushindwa kurudi kwenye soko la Mwanjelwa. Kwa maana nyingine hawa ni wanyonge ambao wanatakiwa kutetewa na CHADEMA kama chama na Joseph Mbilinyi kama mbunge wao. Hapa CCM wanataka kufanya ufisadi na uonevu dhidi ya wafanyabiashara hao basi CHADEMA isimame upande wa wafanyabiashara.
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mh. Sugu fanyia kazi suala hili haraka sana. USHAURI wangu: Kipaumbele wapewe kwanza wale walikuwemo kwenye soko na kuunguliwa bidhaa zao.

  Kama nafasi zitabaki basi ndiyo wapewe wafanyabiashara hao wenye mitaji ya > Tsh. 3 Milioni
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa kama mtaji wako below 3mil si ubaki sido tuu bse hayo mabanda yataendelea kuwepo tuu!
   
 4. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mi nashindwa kuelewa unalitakia nini jiji la mbeya kama unatoa ushauri kama huu... Soko la mwanjelwa jipya ni bora kama likipatiwa wafanyabiashara wenye mtaji wa hata 10million. hayo ndio maendeleo. huwezi kujaza machinga sido, soweto, mwanjelwa, uyole, etc mpaka lini? tunahitaji kuona mji wetu unasonga mbele pia.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,170
  Trophy Points: 280
  wekeni picha tafadhali
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unajua kwamba Halmashauri ya Mbeya inaweza kuwawekea dhamana kwenye taasisi za fedha wafanyabiashara waliokuwepo awali ili wapatiwe mitaji itakayowawezesha kufanya biashara kwenye Soko la Mwanjelwa badala ya kuwatupa!!
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Usijali sana manake mchakato bado unaendelea!!!!
   
 8. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu kwa ninavyojua wengi waliopata madhara ktk soko la mwanjelwa walikuwa ni wenye mitaji inayozidi hata ml.5 na ndio maana wengi wao wali fail hata kuokoa baadhi ya mali zao.
  Hata hivyo kwa sasa soko limejengwa kisasa zaidi ya mwanzo hivyo basi uwezekano wa kumeza wafanyabiashara wote wa mwanzo upo.
   
 9. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  SIDO wataondolewa nakumbuka waliwahi kuambiwa wasijenge majengo ya kudumu.
   
 10. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Mbeya tuna watu bogus Na ninazani ni pamoja na wewe???? utanisamehe sana uvumilivu umenitoka kwani siasa hizi za kichina mtaacha lini???

  By the way who is Sugu kwenye utendaji, mbeya ni lini tutaacha ujinga huu, leo nimeona uzinduzi wa barabara huko rombo na nimemuona mbunge wa huko ndugu selasini very positive kitu ambacho kwa CDM ya mbeya hatuwezi na kama hii ndiyo aina ya washauri wa mbunge tumekwisha.

  Tafadhali kama huna issue ukae kimya usituingize tuanze tena kujichomea lami na kuibiana wenyewe kwa wenyewe huu ni uhuni wa hali ya juu.
   
 11. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Kwa ninavyojua hii inatokana na uelewa mdogo wa kutojua majukumu ya mbunge kikatiba na maana ya halmashauri kwa msingi wa uendeshaji wake? hapo kwenye RED usikute akafanya hivyo hivyo haswa ukizingatia mtu mwenyewe ni dietless
   
Loading...