Wasalaam ndugu zangu,
Leo katika pita pita zangu huku na huku kuangalia vichwa vya magazeti nimekutana na hii "Prof Mhongo kutia saini mkataba wa Tanzania kuuza mihogo China" kwenye gazeti lao linaloitwa UHURU. Well, nikajiuliza tu Prof Mhongo anasaini kama nani maana hayuko kwenye Wizara ya Kilimo, Biashara wala Mambo ya Nje baadae nikaona hili swali halina tija kwangu wala uzao wangu nikabaki kuiangalia hii kama fursa ila nikabaki na maswali yafuatayo ambayo naomba kama kuna mwenye taarifa ya ziada tujulishane.
1. Ni aina gani (specie) ya mihogo itakuwa exported kwenda China na mbegu zake zinapatikana wapi?
2. Bei ya mihogo China imekaa vipi tulinganishe na bei zetu hapa nchini tukijumlisha na gharama za usafirishaji?
3. Hii biashara ya kuexport mihogo kwenda China ndo sasa itaanza baada ya huu mkataba au imekuwepo kabla?
4. China wanahitaji hii mihogo kwa matumizi gani? Kama ni unga si bora kusaga hapa hapa na kupack kama sehemu ya value addition na tuka-export unga wenyewe?
Chonde chonde kwa mwenye taarifa yoyote inayojibu hayo au taarifa nyingine yoyote ya biashara ya mihogo nje ya nchi tushirikishane.
Nawasilisha.