Soko la Kayanga wilayani Karagwe laungua moto, Zimamoto watoka Bukoba kuzima moto

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Soko la Kayanga wilaya ya Karagwe limeungua lote. Zimamoto kutoka Bukoba mjini ndio wamefika na kuanza kuzima moto.

- Moto umedhibitiwa kwa ushirikiano wa fire kutoka Bukoba na Kiwanda cha Sukari Kagera. Moto ulikuw umeanza kusambaa kwenye maduka jirani na soko.

Maoni yangu:

Haya ni masikitiko makubwa kwa viongozi wa wilaya kubwa kama hii kukosa gari la zima moto na vifaa vingine vya uokozi.Inabidi tufike sehemu serikali nayo iache kupendelea baadhi ya mikoa.Mikoa na wilaya zote zina wananchi wanaohitaji huduma sawa.

Sasa ona wilaya inakosa gari la zima moto wakati mkoa mwingine kuna magari mpaka taabu japokuwa nayo magumashi.

Poleni sana ndugu zangu wanyambo, nalikumbuka soko letu.

1460406152982.jpg
 
160412015949_fire_tanzania_640x360_bbc_nocredit.jpg

Zaidi ya maduka 150 yameteketea kwa moto
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza vibanda vya maduka zaidi ya 150 katika mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera magharibi mwa Tanzania. Moto huo ambao ulianza Jumatatu majira ya sa 2:00 usiku umeteketeza mali na bidhaa za aina mbalimbali kama mchele, sukari, nguo, simu, pamoja na bidhaa zingine.

Gloria Kilio ambaye alikuwa akiuza vyakula vya nafaka, amesema stoo zake zote tatu (3) za nafaka zimeungua, “Stoo zilikuwa na magunia ya unga, mchele na sukari lakini vyote vimeteketea,” amesema Gloria huku akilia. Anasema wakati moto unatokea alikuwa tayari amekwisha kwenda nyumbani na kuwaacha wafanyakazi wake wakimalizia kufunga vibanda.

Wafanyabiashara wengi wanasema walikuwa na mikopo na wengi wao hawana bima ya mali zao. Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao: “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta,: anasema Jonas na kuongeza, “kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.” Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki.

160412020147_moto_tanzania_640x360_bbc_nocredit.jpg

Wafanyabiashara wamedai kupata hasara kutokana na ajali hiyo.Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi yamekwishateketea.

Diwani wa kata ya Kanoni wilaya karagwe Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewastua na ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo. Anasema tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha. “Mara nyingi katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi yao yako serikali kuu.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinwiro amesema kuwa Serikali ya wilaya yake itapata gari la zima moto hivi karibuni, “Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.

Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenye kibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.

Chanzo: BBC
 
Kwanza nawapa pole mliopoteza Mali zenu. Tatizo ni ubovu wa miundombinu au hujuma? Isiwe kama ya mwanjelwa mbeya au mtambani kinondoni.
 
a97370c4820690b0762e4b5f7f90a985.jpg

Moto mkubwa umezuka na kuteketeza vibanda vya maduka zaidi ya 150 katika mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera magharibi mwa Tanzania. Moto huo ambao ulianza Jumatatu majira ya sa 2:00 usiku umeteketeza mali na bidhaa za aina mbalimbali kama mchele, sukari, nguo, simu, pamoja na bidhaa zingine.

Gloria Kilio ambaye alikuwa akiuza vyakula vya nafaka, amesema stoo zake zote tatu (3) za nafaka zimeungua, “Stoo zilikuwa na magunia ya unga, mchele na sukari lakini vyote vimeteketea,” amesema Gloria huku akilia. Anasema wakati moto unatokea alikuwa tayari amekwisha kwenda nyumbani na kuwaacha wafanyakazi wake wakimalizia kufunga vibanda.

Wafanyabiashara wengi wanasema walikuwa na mikopo na wengi wao hawana bima ya mali zao. Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao: “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta,: anasema Jonas na kuongeza, “kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.” Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki.

Wafanyabiashara wamedai kupata hasara kutokana na ajali hiyo
Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto.

Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi yamekwishateketea.

Diwani wa kata ya Kanoni wilaya karagwe Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewastua na ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo. Anasema tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha. “Mara nyingi katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi yao yako serikali kuu.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinwiro amesema kuwa Serikali ya wilaya yake itapata gari la zima moto hivi karibuni, “Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.

Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenye kibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.
 
Pole wote mlioathirika kwa namna moja au nyingine Na janganhili la moto.
 
Maduka 150, wanachangishwa 30,000 kila mwezi kwa ajili ya janga la moto na hawana gari la kuzimia moto!

Kwa hesabu za haraka haraka, wanachangishwa millioni 54 kwa mwaka.

Viongozi hapo ni lazima wawalipe wote waliokuwa wanachangishwa na waende jela bila huruma kwa miaka isiyopungua mitatu kila mmoja.

Viongozi kama hao ndiyo wanairudisha hii nchi nyuma.
 
Hao viongozi waligeuza hao wafanyabiashara mradi wao kwa kukusanya 30,000 kwa kisingizio cha zimamoto, na kama hilo soko lilianza miaka mitano iliyopita inamaana wamekusanya kiasi cha zaidi ya shilingi 250 milioni na gari la zimamoto amna, hawa sio majipu tena ni zaidi ya majipu.
 
Miundombinu bora kwenye Soko la Kayaga nayo ni kikwazo kigine ambacho kama ajali ya moto ikitokea kuuzima kweka itakuwa ni vugumu.
Poleni sana wana Kayaga.
 
Huyu DC kweli kaniacha hoi. Yaani watu wameunguliwa na mali zao, hawana kitu, wanakabiliwa na madeni halafu anasema wilaya itapata gari la zima moto kwamba kakutana na Kamishna wa zimamoto!! Yaani hayo ni maneno ya kumwambia mtu aliyeunguliwa na mali zake, na biashara kwa kukosekana huduma ya gari la la kuzimia moto?

Wilaya ya Karagwe ilianzishwa rasmi miaka minne hivi kabla ya uhuru, mwaka 1957(8), miaka yote hiyo haina gari la kuzimia moto, je ni kwa nini?
Je Kupata gari hilo ni hisani, yaani mpaka DC akambembeleze Kamishna wa Zimamoto? Ni wakuu wangapi watapata nafasi hiyo?
 
Kama mlikuwa mnachangishwa ushuru wa fire,jikusanyeni andaaa risiti zenu,tafuta mwanasheria mzuri muwadai fire fidia
 
aina zote za moto ni hatari sana sema hapa kwetu michango ya moto ni mingi kuriko njia za kudhibiti moto..hata kwa kutoa elimu au kuwa na baadhi ya vifaa vya kuzima moto unapoanza kwa huu ambao sio wa mafuta au umeme..
 
Ni wakati wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa tatizo hili la kuungua kwa masoko
Naona masoko mengi yanafanana kwa jinsi yalivyojengwa, masoko yalijengwa enzi za mkoloni kwa wakati huo watu walikuwa wachache lakini soko linakidhi Mara tatu ya wanaotumia.

Leo hii watumiaji wameongezeka na mbanano umezidi kiasi hata pa kupita mtu unakosa. Pesa nyingi zinaliwa za halmashauri kwa kisingizio cha kukarabati masoko na unakuta badala ya kulikuza wanapiga hela tu yaani ubunifu ni ZERO na tamaa ya wachache ndio inatuangusha wengi.

Walipwe wahangwa wote maana tunajua watapewa hela ya mbuzi tu.
 
Back
Top Bottom