Mfumo wa ununuaji wa sonara ungeachwa uendelee halafu TRA apange utaratibu mzuri wa kukusanya kutoka kwa sonara na chain itakayoanzia hapo mpaka kwenye end product.
Serikali ikae chini na hawa Makota wakubwa maana wengi wanafahamika ikubaliane mfumo ambao wao nao watalipa kodi na chain yote kutoka kwao kwenda kwenye end product au nje ya nchi!
Ila kabla ya kwenda kujenga hilo soko serikali ilipaswa kutoa dodoso za kukusanyia taarifa kwa wachimbaji wadogo na wakubwa ili kujua namna chain ya biashara ya dhahabu imekaa!
Kuwa na mfumo ni jambo moja, kuwa na mfumo unaofanya kazi kwa ufanisi ni jambo jingine!
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa.
Kodi hizi za Kuwaachia TRA wakadirie tu zimewaumiza wafanyabiashara sana.
Zinawafanya maafisa wa TRA kuwa Miungu watu na kupanua wigo wa Rushwa.
Utaratibu aliouanzisha Mh. Rais kwa wafantabiashara wadogo nadhini ni mzuri sana.
Watu walitakiwa wauchangamkie mana una lengo zuri sana.
Na pia unapunguza rushwa na ubabaishaji mwingi.
Utaratibu huo ulitakiwa uhamie kwa wafanyabiashara wote kulingana na ukubwa wa mtaji.
Siasa iwekwe pembeni.
Mfano uliotaja kwa masonara ni wa kweli ,na pia ni rahisi kudili na kodi kwao ikiwemo Leseni ya biashara.
Maushuru yanakua mengi na yanapewa majina mengi sana mpaka inakua ni tabu kulipika.
Kodi ingewekwa kwenye Leseni ya mmiliki wa Mashimo ya wachimbaji wadodgo wa dogo tu.
Mana sio kila siku anapata. Kisha iende kwenye Leseni ya wafanyabiashara wa wadogo ,mabroka na wale wakubwa . Kila mmoja apewe Kiwango chake cha kulipia Leseni mpaka kule kwenye sonara.
Hizi kodi kodi nyingine ndio zinazosababisha Rushwa kwa maafisa wa TRA.
Matokeo yake ni kuwa na Maafisa wa TRA wanaomiliki Mali nyingi na zenye thamani kubwa kwa ujumla wake kuliko Mali wanazomiliki walipa kodi. Ikiwa na maana hela nyingi zinapotea kwenye Rushwa ili wasiwakomoe wafanya biashara kwa kuwakadiria kiwango cha juu.
Sheria zinapokua nyingi zinasababisha wigo wa Rushwa uwe mkubwa badala ya tija kwa taifa na wananchi waliowekeza mitaji na nguvu zao.
Nchi inakua na matajiri wasiozalisha wala kurumia nguvu zao kumiliki Mali zaidi ya Rushwa. Ni bora kuwapa unafuu wafanyabiashara wa kitanzania kisheria ili mitaji yao ikue waongeze wigo wa ajira na TRA wapate kodi kwenye income tax ,kuliko huu mfumo mbovu wa makodi mengi ya kukisia tu na kuwafanya wafanyabiashara wafilisike huku maafisa wa TRA wakijilimbikizia Mali na kujenge mijengo isiyozalisha wala kutoa ajira kwa watoto wa maskini wa Tanzania.
Wakati mwingine naona kuwa ni bora kuwa na wafanyabiashara wakwepa kodi kuliko maafisa wa TRA wala Rushwa.
Mfanyabiashara mkwepa kodi anaweza akakuza mtaji na biashara ikapanuka na akaongeza wigo wa ajira tofauti na TRA mla Rushwa na hasara kwa taifa na wafanyabiashara pia.
Sent using
Jamii Forums mobile app