Soko la CCM Katoro, Geita limeuzwa?

Soko la CCM Katoro, Geita limeuzwa?

Mkurya mweupe

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2023
Posts
250
Reaction score
830
Nilikuwa maeneo ya Katoro ,soko kuu la ccm, nimeona wafanyabiashara wa eneo hilo na machinga wa soko wakilaumu kuwa wamepewa notisi ya siku 49 kupisha mwekezaji mpya wa kujenga hilo soko, ambae amepewa idhini ya ujenz wa hilo soko bila kupewa ushindani wa watu au wawekezaji kushindania, hivo wafanyabiashara wa eneo hilo na baadhi ya viongozi wa CCM wanahisi kuwa kuna harufu ya rushwa imepatikana katika kumpata mwekezaji mpya wa hilo soko, maana yeye anadai gharama yake ya kuingia kwenye chumba ni 5M, wakati hilo eneo lilikuwa linatumika kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wa tabaka la chini ambao mitaji yao wengi ni 1M au chini ya hapo.

Pia kwa upande mwingine wanashangaa kwanini notisi ya kutoka eneo hilo imetolewa kwa muda mfupi sana kinyume na Sheria ,hivo kuonekana kuna harufu ya rushwa na baadhi ya viongozi wa chama wamekuwa wakiwaambia wafanyabiashara kutotii agizo hili, wakidai kwamba baadhi ya viongozi wa chama ,wamepokea rushwa ili zoezi ili likamilike bila wao kuhusishwa na hawajui lolote lilitokea

Hata diwani mmoja wa eneo hili alipoulizwa na wafanyabiashara amesema kuwa huu ni mradi wa watu wameshapiga hela

Kwahyo Chama Cha Mapinduzi muingilie kati hili suala hili ukwl wa zabuni hii ufahamike au wafanyabiashara wapewe elimu Kama Kuna ukarabati unataka kufanyika kumpisha mwekezaji ambae atamiliki majengo hayo kwa miaka 5 kama uongozi wa soko unavyosema ,na Kama rushwa imetumika ifatiliwe kwa umakini ,mpaka hatua za kumpata huyo mwekezaji mpya wa soko.

Maana wafanyabiashara wa hili eneo tokea ule mkutano wa Lissu wanasema kuwa soko la ccm Katoro limeuzwa kwa mtu na wao kukosa nafasi ya kuendelea kufanya kazi eneo ,na hvo kumilikiwa na mtu mmoja ambae akimaliza ujenz ataamua kodi yake iwe kiasi gani?

Hivyo wanahusishwa kuwa soko la ccm limeuzwa Kama ambavyo bandari inadaiwa kuuzwa na hvo kuwanyima fursa wafanyabiashara wadogo takribani 1,000 eneo la kufanyia kazi ,na hvo wanaenda kupoteza maeneo ya kufanyia kazi na pia utakuwa mwanzo wa kuua mitaji yao.

Nimepata kushuhudia baadhi ya viongozi wa Ccm wenyewe wakipita kwa wafanyabiashara kuhamasisha kugomea zoez hili wakidai kuwa wakubwa wao wamepokea rushwa kubwa kutoka kwa mwekezaji ambaye amepewa soko hilo kuliboresha bila hata ya kumshindanisha na mtu yoyote ,hata mabango waliyoweka ya kutafuta mwekezaji wanadai yaliwekwa ikiwa tayari mwekezaji huyo ashapatikana hvo walibandika tangazo hilo kama njia ya kuwazuga wafanyabiashara, pia walihakikisha wanaweka kiwango kikubwa kwa mfanyabiashara ambae atataka kuboresha chumba chake kiasi Cha kutoa ni ,5M ,wakati wafanyabiashara hao asilimia 98 ,mitaji yao haifiki milion tano ,hivyo Chama Cha Mapinduzi kwa kushirikiana na vyombo husika ,tunaomba mhakikishe mnatatua hili tatizo.

Na jana mwenyekiti wa hilo soko alianza kuwahamasisha machinga watoke ndani ya eneo hilo ,akijua wao ndo wana nguvu sana na kuwapeleka kuwatelekeza kwa nje ambapo ndo fremu mpya zinajengwa na hvo zikiisha wanakuwa hawana pa kwenda maana wanakuwa wamekaa mbele ya fremu za mwekezaji mpya ,hivyo akiwini kuwapa machinga eneo hilo anaamini wafanyabiashara wengine itakuwa rahisi kuwaondosha bila kujali lolote(divide and rule) ,na hvo dili lao kukamilika.

Naomba kuwasilisha .
Asanteni.
 
Madiwani wa eneo hili ambao ni CCM ,wanawaambia wafanyabiashara wagome wakishagoma wao watakuwa nyuma yao ,maana kwao ni ngumu kuanza hvo wanasema wafanyabiashara wakiashaanza wao watatoka kuwatetea na baadhi ya viongozi wa chama wamekuwa wakipita kwa wafanyabiashara kuwaomba wasikubali kutoka kwani hili zoezi ni dili la watu wachache sana waliohusika kupigwa hela na huyo mwekezaji ili alichukue eneo hilo la ccm ambalo ni maarufu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ,
 
Kanuni za uandishi zizingatiwe..
Hukuwahi kusoma ili ufikishe ujumbe ,mfano tangazo unaweza kosea hata grammar ili mtu ajenge wazo hapohapo likae mfano hata sokoni ,ningeamua niandike Nsokoni la ccm ,ni kuvuta attention ya watu ,inaruhusiwa kabisa.
 
Napafahamu vizuri hapo pia nawafahamu baazi ya wafanya biashara wa soko Hilo kifupi pale janja janja imetawala eneo Hilo Kuna Mzee mmoja pale nasikia aliwahi sumbuwana nao sana mpaka mahakamani ila Kwa Sasa nasikia Mungu kamtwaa kama sikosei huyo Mzee aliwahi KUWA MWALIM akasitafu jina lake kama sikosei anaitwa ndegea.
 
Ndiyo huyo mzee walimfanyia janja akadhulumiwa eneo lake ,cha kushangaza zaidi kuna mtu alipewa eneo hilo ajenge fremu ,lakini na yeye kwakuwa kaja mwekezaji mpya na yeye anadaiwa ampishe huyo mwekezaji wakati ana fremu zaidi ya 15 na mwaka hana
 
Hukuwahi kusoma ili ufikishe ujumbe ,mfano tangazo unaweza kosea hata grammar ili mtu ajenge wazo hapohapo likae mfano hata sokoni ,ningeamua niandike Nsokoni la ccm ,ni kuvuta attention ya watu ,inaruhusiwa kabisa.

Chukulia poa. Kubari kukosea mkuu.

Unapoandika Uzi onyesha kuwa umekusudia kutoa elimu na kufikisha ujumbe Kwa wasomaji.

Asante Kwa muda wako na Uzi wako. Kama upo Katoro tuonane nipo buseresere hapa.
 
Chukulia poa. Kubari kukosea mkuu.

Unapoandika Uzi onyesha kuwa umekusudia kutoa elimu na kufikisha ujumbe Kwa wasomaji.

Asante Kwa muda wako na Uzi wako. Kama upo Katoro tuonane nipo buseresere hapa.
Jadili content ya hoja iliyowasilishwa .
 
Kanuni za uandishi zizingatiwe..
Nikupe elimu kidogo kuna kitu kinaitwa ''poetic licence" ndo utajua uandishi niliotumia unaruhusiwa Ila kwakuwa Elimu yako ni ndogo bado huwez kuelewa vitu kama hivi .......bado umekariri kanuni za uandishi wa darasa la pili ,soma umuhimu wa "poetic licence " ndo urudi tena hapa tujadili.
 
Chukulia poa. Kubari kukosea mkuu.

Unapoandika Uzi onyesha kuwa umekusudia kutoa elimu na kufikisha ujumbe Kwa wasomaji.

Asante Kwa muda wako na Uzi wako. Kama upo Katoro tuonane nipo buseresere hapa.
Mkuu nitakuja unikodishie Baiskeli hapo ,asante sana
 
Nikupe elimu kidogo kuna kitu kinaitwa ''poetic licence" ndo utajua uandishi niliotumia unaruhusiwa Ila kwakuwa Elimu yako ni ndogo bado huwez kuelewa vitu kama hivi .......bado umekariri kanuni za uandishi wa darasa la pili ,soma umuhimu wa "poetic licence " ndo urudi tena hapa tujadili.
Sawa.
Wewe mwenye elimu kubwa. Lakini ichokiandika ni upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom