MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Mods: Tafadhali kabla ya kuushamisha uzi huu kwenye Jukwaa la Michezo, usomeni kwanza. Hizi ni harakati za mapinduzi. Tuko kwenye minyororo ya FIFA, tumefungwa bila kujijua. Sasa ni wakati wa ukombozi!
HISTORIA huwa na tabia ya kujirudia mara kwa mara. Ufalme wa Kirumi unakisiwa kuanza mnamo mwaka 44 BC (ulipokuwa mwanzo wa utawala wa Kaizari kama dikteta) au mwaka 27 BC (ulipokuwa mwanzo wa mfalme Augustus kama mtawala). Ufalme wa Kirumi ulifikia ukomo wake katika nyakati tofauti, kutokana na jinsi unavyoweza kuutafsiri, kwa kuwa uligawanyika katika sehemu kuu mbili.
Nusu ya Ufalme huo, ambao ulikuwa Magharibi/Ulatini (mji wa Roma ukiwa makao yake makuu) ulianguka mnamo mwaka 476 AD. Wakati haya yanatokea, nusu nyingine ya Mashariki/Ugiriki (ikiwa na mji wa Constantinople kama makao makuu) iliendelea kushamiri hadi mwaka 1453 AD. Leo tunauita ufalme huu kuwa Ufalme wa Byzantine, kuutofautisha na sehemu ya awali ya historia ya Warumi, lakini watu wa ufalme huu walijiita Warumi na waliendeleza sheria zao za Kirumi kama ilivyokuwa awali.
Kwa nini nimeanzia makala haya na historia ya Warumi na je, Warumi wanahusika vipi na mchezo huu wa soka, unaopendwa duniani kote. Nakusihi utulie, usome kwa makini makala haya, ili uelewe kinachojiri.
Nimesema kwamba soka ni utuma mamboleo, historia ikijirudia, kwani hili ni kweli tupu, lakini kuna tofauti moja kuu, ambayo nitaielezea punde.
Wakati wa awamu ya kwanza wa Ufalme wa Kirumi, watawala wake walikuwa na desturi au tuseme utamaduni wa kujistarehesha kwa ufisadi lukuki; walifanya karamu ambazo kulikuwa na chakula kingi mno, huku wakifanya ngono na wanawake ambao walikuwa watumwa, na walikuwa wakitunzwa kwa ajili ya kuwastarehesha mabwana wakubwa hao. Mtawala yeyote mwenye cheo chochote kile wa Kirumi, awe mwanajeshi wa kawaida, au kamanda wa jeshi, alikuwa na haki ya kufanya uporaji wa mali kutoka kwa Mrumi yeyote yule ambaye alikuwa na hadhi ya kawaida, ikiwa ni pamoja na ama kuwapora watoto wake na kuwafanya mali yake, wakiwa watumwa wake, na pia, kumpora mke wa Mrumi huyo, iwapo alimtamani. Mwananchi Mrumi hakuwa na haki ya kujitetea, ama kudai haki, kwani hakukuwa na vyombo vya sheria wakati huo; sheria iliyopo ilikuwa ya Jeshi la Warumi na watawala wao, ambao wao walijiona kuwa bora kuliko wengine, wakifikia kukufuru na kujiita Mabwana, wakijifananisha na Mungu. Hakika zilikuwa nyakati ngumu.
Mojawapo ya starehe ambazo watawala wa Kirumi walizipenda, ambazo zilikuja kuchochea vita nyingi za Warumi dhidi ya mataifa mengine, huku wakiipanua falme hiyo kwa uporaji na utekaji, ilikuwa katika mchezo wa Gladiators, yaani, Mashujaa. Hakika kumwita mtumwa au mhalifu (kwa mujibu wa sheria zao batili) kuwa shujaa ilikuwa dhihaka na kejeli tosha, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mchezo huu ulifanyika kwenye uwanja maalum uliojengwa kwa mchezo huo, yaani Collosseum, ambao mpaka leo mabaki yake yako jijini Roma. Kwenye uwanja huo kulikuwa na jela za aina mbili; moja ya wanyama wakali kama vile samba, chui, nyati, n.k., na ya pili kwa ajili ya wafungwa na watumwa, ambapo kila mmojawao alikuwa na sehemu yake maalum. Walitenganishwa.
Wapambanaji hao waliitwa mmoja baada ya mmoja, wakipambanishwa ama na wanyama wale wakali uwanjani hapo, au wenzao ambapo ilikuwa kawaida kumwona mfungwa au mtumwa ambaye alikuwa mnyonge akipambanishwa na mwingine mwenye nguvu nyingi na mwili mkubwa, ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kutisha, huku akiwa na silaha nyingi hatari; yule mnyonge alipewa nafasi ya kuchagua silaha moja tu. Lengo lilikuwa kuhakikisha kwamba yule mnyonge anauwawa, na pindi alipoweza kumshinda mpinzani wake, kutegemea na jinsi Kaisari alivyofurahishwa, ama aliweza kuachiwa huru, au kupambanishwa na mbabe mwingine, ili starehe ya kifisadi ya kumwaga damu iendelee. Hakika Warumi walikuwa watu katili mno, na watawaliwa wao waliwaogopa mno!
Nisiwachoshe. Mmeelewa jinsi historia ya Warumi, na mchezo wao wa kifisadi kwenye uwanja wa Collosseum, ilivyokuwa. Sasa tuendelee na mada kuu.
Kwanza, natoa tamko kwamba kila uwanja wa soka duniani kote ni Collosseum, lakini isiyo na jela ya kuwaweka wapambanaji watumwa au wanyama wakali. Ni uwanja wa mapambano, kwa hali halisi, ila kwenye mpambano huo, mashujaa hawapambanishwi na wanyama wakali au wababe, bali na binadam wenzao katika mchezo wa soka, ambapo Kaisari ni FIFA.
Pili, utumwa uliopo ni kwamba wachezaji soka wanakuwa wameingia kwenye mikataba ya kulipwa pesa nyingi MNO, huku wakiwa, ama wamenunuliwa kutoka vilabu vingine vya soka au wakiwa wameajiriwa kutoka nchini mwao, kama vile barani Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na kwingineko. Wachezaji hawa wanaajiriwa wakiwa kwenye umri tofauti; wengi wao wanaajiriwa wakiwa kwenye umri mdogo, ambapo ligi maalum ambazo zinaendeshwa na kampuni kubwa, kama vile Copa Coca-Cola, ambayo inamilikiwa na kampuni ya vinywaji vyepesi (Coca-Cola), ambao ni mojawapo ya wabia wakuu wa FIFA.
Tatu, FIFA, ikishirikiana na wabia wake wa kibiashara, imekuwa na nguvu kubwa ya kutawala bila kuonekana inatawala; inasimamia ligi kadhaa za soka, kwa mfano CECAFA, CONCACAF, CAF, na nyinginezo, lakini ligi kuu kuliko zote ni ile inayoitwa Kombe la Dunia la FIFA, ambalo ndilo muhimu kuliko yote.
Nne, FIFA imetunga sheria za jinsi mchezo wa soka unavyopaswa kusimamiwa, ikiweka masharti magumu kwa wachezaji. Kwa mfano, wachezaji, hususan wale wanaonunuliwa kwa bei mbaya barani Ulaya huwekewa masharti magumu; ni lazima watumikie kipindi chote cha mikataba yao, na iwapo watataka kuivunja mikataba hiyo kwa kuhamia kwenye timu nyingine, hulazimika kufanya makubaliano na timu zao hizo kwa wakati huo na kuweka masharti ambayo yanazidi kuwaweka wachezaji hao kwenye hali ya kuwa watumwa zaidi. Licha ya kununuliwa tena kwa, pengine, dau kubwa zaidi na timu nyinginezo, wachezaji hao hulazimika kuweka mikataba ambayo inawafunga kulipa sehemu ya malipo yao ya kila mwezi kwa timu walikotoka, ama kwa muda maalum, au kwa muda ule ule wa mkataba wa awali, na kuwafanya watafute mbinu nyingine za kujikimu, kwani hulazimishwa kuishi maisha ya kifahari ambapo wanalazimika kununua magari ya bei mbaya na kumiliki nyumba za kifahari, kuwa na vimada wa bei mbaya, n.k. Kimsingi, biashara hii ya kitumwa haina tofauti na biashara ya Kishetani, kwani ni wachezaji wachache sana kwa mfano David Beckham ambao walifanikiwa kupata ushauri mzuri wa kisheria, ambapo mikataba yao haikuwa ya kitumwa, hivyo wao badala ya Warumi FIFA na washirika wao wakafanikiwa kutokana na mchezo huo.
Tano, barani Afrika, FIFA imekuwa ikitoa ruzuku ya zaidi ya dola za Kimarekani laki moja, kwa mwaka, kwa vyama vikuu vya soka, ambapo katiba za vyama au mashirikisho hayo lazima zipitishwe na FIFA. FIFA inaweka sheria kali, kwa mfano Serikali hairuhusiwi kuingilia masuala ya soka na ni marufuku vilabu au mtu yeyote kupeleka masuala ya soka mahakamani, kwa sababu yoyote ile. Hili ni kweli hata hapa nchini kwetu Tanzania. FIFA inafanya hivi ili kuhakikisha kwamba mashirikisho haya yanasimamia vizuri makusanyo ya mapato yake, kwa mfano, kwenye malipo ya ununuzi na uuzwaji wa wachezaji kupitia mawakala maalum, na pia kwenye harakati za kuajiri wachezaji chipukizi wanaoonekana kuwa na vipaji, ili kuwapeleka kwenye ligi za Marekani Kaskazini na Bara Ulaya.
Sita, sasa tunashuhudia jinsi ambavyo vilabu vya soka vimekuwa vikilazimishwa kushiriki biashara hii haramu, ya kuwanunua na kuwauza wachezaji wao kwa bei mbaya; dau likiwa kubwa zaidi, ndivyo wachezaji wanavyojikuta wameingia kwenye mikataba ambayo inawafunga kimaisha, wakiishi katika mazingira tete, na kulazimika kuvitumikia vilabu hivyo kwa muda wote wa mkataba, kwani wakiamua kuondoka, lazima warudishe malipo ya mkataba wa klabu hizo kwa uongozi. Kwa mfano, iwapo mchezaji wa klabu hapa nchini analipwa kiasi cha Shs 2,000,000 kwa mwezi, kama muda wake wa kuchezea klabu hiyo umebakia miezi 6 au mwaka, anaweza ama kulazimika kulipa kiasi hicho cha mwezi au sehemu yake, kwa kipindi chote kilichobakia. Wakati mwingine, kutokana na makubaliano ya wachezaji hao na vilabu ambavyo wanataka kuhamia, fedha hizi huweza kulipwa na vilabu hivyo, KABLA ya kulipa dau la kumnunua mchezaji huyo.
Uchambuzi/Tathmini: Hivi tulianza lini kuwageuza binadam wenzetu hapa nchini kuwa bidhaa kama nyanya sokoni, unakwenda, unapatana na mchuuzi, mnafikia bei, unaondoka na nyanya zako nyumbani? Hatuoni kwamba, kwanza, huu ni utumwa, na pili, tunamkufuru Mungu?
Mchezo huu wa kuwauza na kuwanunua wacheza soka umeanza miaka ya karibuni; isingewezekana kufanyika hivyo kwani FIFA haikuwa imeandaa mazingira ya kuwapo kwa hali hiyo. Ilipaswa kuanzia ngazi za chini, kwa mfano, kwenye ligi ya Copa Coca-Cola, ambapo mwaka 2008, timu ya taifa ya vijana (Ngorongoro Heroes) ilishinda kombe hilo nchini Brazil, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki. Hivi hatukuona kwamba tumeingizwa mkenge? Kuna tetesi kwamba FIFA walipeleka maagizo maalum kwa timu shiriki za fainali za Copa Coca-Cola nchini Brazil, mwaka huo, kuiachia Ngorongoro Heroes kushinda kombe hilo ili kuimarisha dhana hapa nchini kwamba sasa tumeingia rasmi katika soka la kimataifa. Mkenge mkubwa tulivalishwa! Miaka mingine yote ambayo Ngorongoro Heroes imekuwa ikishiriki kwenye fainali za Copa Coca-Cola imekuwa ikishindwa vibaya; hamuoni ajabu?
Sisi Waafrika tuna tatizo moja tu; bado tunawaona watu weupe kuwa sawa na miungu watu, na sasa wametuingiza kwenye biashara hii haramu ya utumwa mamboleo kupitia soka. Sasa binadamu amekuwa bidhaa ya kununua na kuuzwa. Hivi hakuna mchezaji hata mmoja anayejiuliza: Kama huyu ana uwezo wa kunilipa na/au kuninunua kiasi chote hiki cha pesa, yeye anapata kiasi gani?
Vilabu vya soka vya, kwa mfano, Uingereza, vina nguvu kubwa. Klabu ya Manchester United, licha ya kumiliki kituo chake cha luninga ambapo michezo yake yote hurekodiwa na kurushwa, na wale wanaotaka kuiona kulazimika kulipia gharama kubwa kuiona, lakini bado inamiliki uwanja wake wa soka, Old Trafford, ambapo ndani yake wapenzi na washabiki wanaweza kukuta na kununua bidhaa mbali mbali zinazoitangaza timu hiyo, kama vile jezi, mipira, kofia, fulana, n.k., ambazo huuzwa kwa mamilioni kila mwaka. Hapa nchini kuna wafanyabiashara wanaonunua bidhaa hizo na kuja kuwauzia washabiki wa timu za Uingereza, kwani wameona kwamba soka la hapa nchini halina mvuto. Kila wakati timu hizo zinapokuwa na mechi, mashabiki hao wa Ligi ya Uingereza (FA Cup) hukutana kwenye vilabu vya pombe, ambapo hukaa na kutazama mechi hizo na kunywa kiwango kikubwa cha pombe, ambapo mara nyingi watengenezaji na wauzaji wa pombe wanajulikana hudhamini maonesho ya mechi hizo kwenye baa hizo, ambapo mashabiki hao hushawishiwa kushiriki kwa wingi ili kuwawezesha kununua na kunywa pombe hizo kwa wingi, huku wakidai tafadhali kunywa kistaarabu. Kuna ustaarabu gani katika unywaji wa pombe?
Sisi Waafrika tunaweza kulikata konde la nyuma kati yetu na FIFA, kuiasi, na kuanzisha Ligi ya Soka ya Afrika, ambayo haitakuwa na masharti ya kitumwa na kifisadi kama hizo zinazoendeshwa na FIFA. Potelea mbali ruzuku zao lukuki kwa mashirikisho yetu ya soka kama vile TFF! Tukiamua tunaweza. Lakini kwanza tuwe na nia. Mimi ni muumini wa Pan Africanism, ambayo sera yake kuu ni Afrika ya Waafrika, kwa Waafrika. Viongozi wetu waliotangulia, Patrice Lumumba, Kwameh Nkrumah, Mwalimu Nyerere, waliasisi Pan Africanism wakiamini kwamba itafika siku kizazi kimojawapo cha Waafrika kitaamua Afrika iwe ya Waafrika. Inawezekana.
Leo kuna hiki kitu kinaitwa Airtel Rising Stars, ligi ya vijana wadogo kabisa wake kwa waume ambayo ina lengo moja tu kuu: Kuwaajiri wanasoka vijana wadogo kabisa na kuwalea ili waive na waingie rasmi kwenye utumwa huu wa soka la Ulaya. Leo hii, mchezaji Mtanzania, Shomari Kapombe ameruhusiwa na TFF kwenda kufanya majaribio nchini Sweden, ikiwa ni mwendelezo wa mpango huo huo wa kifisadi wa kuendeleza utumwa huu mamboleo. Wala tusishangae, japokuwa tumekuwa tukiwaona Watanzania wanaofanikiwa kupata mikataba ya kucheza soka barani Ulaya kuwa wameula, kumbe tumewasindikiza kwa shangwe, hoi hoi na vigelegele, kuingia rasmi kwenye utumwa huu wa kifisadi kabisa!
Tanzania ilikuwa mojawapo ya Nchi Zilizokuwa katika Mstari wa Mbele (Front Line States) katika ukombozi wa Bara Afrika. Ilichangia kwa kiasi kikubwa katika ukombozi wan chi nyingi Barani Afrika, ambazo zilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa nchi za Magharibi, kwa ufanisi mkubwa. Tanzania ina asili ya mapinduzi; sio tu ya kifikra, lakini ya kiuchumi na kiutamaduni pia.
Hebu tujiulize. Tutashtakiwa na nani iwapo tutaikata mirija yote inayotufunga na FIFA, na kuanzisha ligi zetu wenyewe za soka? Kwani ni lazima tuamini kwamba kufika na kucheza kwenye ligi ya soka ya Kombe la Dunia la FIFA ndio kilele cha mafanikio yetu? Hii ni dhana potofu na ya kitumwa, kwani hayo ni malengo yanayotokana na utamaduni wa kimagharibi, ambao sisi Waafrika hatufanani nao. Wahenga walisema: Mdharau kwao ni mtumwa! HAKIKA tumeukubali utumwa, lakini tukiamua tunaweza.
Najua wengi hamjiamini kwamba inawezekana. Lakini tujiulize: Wamiliki halali wa Bara Afrika ni nani zaidi ya Waafrika wenyewe? Kama huo ndio ukweli, hakika, hakuna kinachotuzuia kukatilia mbali minyororo yote inayotufunga na FIFA na kuachana nayo, na hatimaye kuanzisha Ligi Kuu ya Soka ya Afrika, ikiwa ni pamoja na kuanzisha Kombe la Soka la Afrika. Dunia ya nini? Afrika inatosha sana. Kama ni udhamini wa Coca-Cola, si haba, kuna kampuni nyingi za kutosha kutudhamini sisi wenyewe, za Kiafrika, si hizi za kigeni kama zinazodhamini Ligi Kuu ya Taifa, na nyinginezo.
Narudia: Tukiamua tunaweza. Tanzania inaweza kusimamia mapinduzi haya na kuwaunganisha Waafrika. Suala ni lini tuanze kwani tumechelewa sana na hali yazidi kuwa mbaya.
Chaguo ni letu: Kuukubali utumwa mamboleo au kuutafuta uhuru wetu kwa mara nyingine.
TUNAWEZA! TUJIAMINI! TUJIPANGE!
AMANDA AWETHU! A LUTA CONTINUA!