Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Soka inapelekwa wapi? Sasa kufunga mabao ndiyo suala la hadhi kubwa na si kuzuia mabao yasifungwe, kuunganisha timu na kutoa pasi za mabao. Kukiwa na utaratibu wa kutoa tuzo, mindset zetu zinatuelekeza kwa aliyefunga mabao yaliyoipa mafanikio timu. Hatufikiri sana kuhusu waliozuia timu isifungwe na waliotoa pasi za uhakika za mabao. Eti kuna tuzo ya bao bora (best goal) lakini hakuna tuzo ya uokoaji bora (best save) na ya pasi ya mwisho bora (best assist). Kwa mwendo huu, miaka ijayo tutakosa makipa, walinzi na viungo wa kutosha kwani kila kijana atapenda kuwa striker ili apate hadhi kubwa na tuzo. Manuel Neuer alistahili kuwa mchezaji bora 2014 lakini kwa bahati mbaya ni mzuia magoli na si mfunga magoli. Alizuia magoli mengi kufungwa na hakufunga goli tofauti na Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli mengi na hakuzuia goli kufungwa!