Msanii, pole sana..
Mwanawane ngoja nikwambie tu kuwa, kwa kweli huhitaji crack gene ku-crack anti-virus software... kufanya hivyo ni kujitia matatani mwenyewe... ni sawa na kesi ya mbuzi kuipeleka kwa chui ili atoe hukumu.
Isitoshe, kuna program kibao zinazopatikana kwa bure zenye kuweza kukusaidia kuondoa virus... kuna spybot resident, kuna AVG free version.... na nyingine nyingi tu... jana tu, invisible kaweka hapa thread yenye ku-list freebies kibao, including za virus.
Naelewa umekuwa specific kwa kuuliza crack ya Kaspersky, hata hivyo program nyingi za antivirus engine zake zinafanana, na virus definitions karibu zote ziko sawa maana zinategemea website zenye database zinazokusanya new threats.
Isitoshe, kuna kuondoa virus manually, njia hii imeelezwa pahala pengi kwenye forum ya ICT, mara ya mwisho ninavyokumbuka Invisible kaitolea maelelezo kwenye ile thread ya "virus ya Odinga." Naomba ucheck...
Kingine, natumaini unaelewa na kulizingatia hili: JIEPUSHE NA WEBSITES ZA CRACKS AT ALL COSTS & BY ALL MEANS!! ZITAKUHARIBIA MASHINE YAKO. BELIEVE ME ON THIS!!!!
Naomba kumaliza kwa kukusihi ununue anti-virus program. Nasema hivi maana nina elewa kuwa nyingi hazizidi dola 40. Hela kama hii kwa program itakayokulinda wewe kwa mwaka na zaidi sidhani kama ni vibaya kuihalalisha.
I hope utasolve hilo tatizo ulilonalo. Baadae.
SteveD.