Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Mimi nikajua shida kuuubwa kumbe hako tu. Kifupi background yako haijaathiri chochote kwenye hiyo hali, hivyo usisingizie aina ya malezi uliyopata. Kama hakuna mtu mmoja wa kukusaidia, basi angalia yanayowezekana hapa.

- Jiunge na jeshi/mgambo, lengo ni mazoezi kuweka akili active maana wewe peke yako umeshindwa. Au vipi weka ratiba ya mazoezi asubuhi na jioni, au jiunge na kikundi cha mazoezi ya aerobics chochote.

- Tafuta mwanamke, bila shaka hata kutongoza huwezi ila jitoe tu ufahamu hata upate rafiki wa kike. Wanawake ni dawa nzuri ya akili ya mwanaume, Mungu aliliona hilo ndio maana akasema Adam asiishi peke yake ampatie msaidizi wa kufanana naye. Hata tusio na wanawake, ile kuongea tu au kuchat na good girl friends mkacheka huwa inaleta hali fulani nzuri kwenye mind.

- Usiisahau nafasi ya Bwana Mungu wako.

- Kula vizuri, kula mlo kamili. Ingia hata google tafuta vyakula vyenye Vitamin B6 nyingi na Magnesium nyingi, uhakikishe havikosekani mezani.

- Tafuta hobby yako ni nini, jaribu kuangalia mpira hata vibanda umiza, jaribu movies, jaribu music, kote huko uone kipi kitakutuliza akili.

NB: Kuwa mwanaume bob, jikubali. Jione hakuna mwingine kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu wangu Dr. Wansegamila kwa kunipa moyo, unaweza kunipa link ya hiko kitabu nikisome ila nisikudanganye tu, hiko kitabu sina uhakika kama kitabadili chochote kwenye maisha yangu maana nimesoma vingi na nimetoka kapa. Its like kama akili yangu ishakubali kilichotokea na haiko tayari kubadilika. naweza nikafanya changes leo ila kesho nikarudi vile vile nilivyokuwa mwanzo. Alafu hospitali nyingi wako after money so nimekata tamaa kwa hilo pia.

Tatizo lako ni wewe mwenyewe.
Kama haumini kuna chochote kinachoweza kukubadilisha obvious hakuna kitakachokubadilisha zaidi ya kifo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anza kufanya yoga.Alafu fanya kama ubongo wako ni hard drive yenye programs na files,sasa anza kidogokidogo kudelete programs na files ambazo hazina manufaa kwako.Tafuta rafiki hata mmoja tu mcheshi mchangamfu na mwenye interests zinazofanana na zako hata kama ni chache. Have long walks on the beach, jilazimishe kuface fear zako,wanasema face your fears and they will disappear.

Kwa kifupi changamoto zote ulizonazo zinatatulika sababu sio ulemavu na wala sio physical.ukihitaji msaada zaidi feel free to PM me na nitajitahidi kadri niwezavyo kukupa mwongozo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polee sanaa mkuu iyo hali ipo na zaidi inasumbua vijana hasa 20's to 30's. Mimi nilikuwa mmoja wao

Nilijitoaje huko?

1. Niliongeza ukaribu na rafiki mshikaji fulani aliyechangamka na anayependa kujichanganya na watu so muda mwingi nipo naye kwahiyo watu wake washkaji zake jamaa wote anaowajua automatically na mimi napata muda wa kusalimiana nao japo kwenye mazungumzo. Muda mwingi nipo kimya.

2. Kama ni mwanamichezo wekeza muda mwingi huko na usikose kuhudhuria whatever kind of sport you are playing

3. Tafuta msichana yeyote ambae utaweka ukaribu naye maana internal conflict utayoipata ukiwa naye itakupa kitu kipya ambacho utaona umuhimu wake kwa sasa labda siku mkiachana au mambo yakiwa sio mazuri kati yenu.

4. Kuna public places ambazo haziitaji kujielezaa mfano Kuangalia mpira, sinema, walking nk uweke muda wa kuwa hayo maeneo

5. Pombe sikushauri utumie ila mimi nilikuwa natumia na imenisaidia maana nilikuwa napata hata cha kuzungumza mbele za watu na chuo nilikuwa sikosi konyagi au k vant kwenye begi

Mambo ni mengii mda mchachee fanya maamuzii kilaaa dakika unayohisiii moyo unakataa ni ngumu sana but try na jaribu mara nyingi uwezavyo

Kila la kheri. Na pole usikate tamaa
 
Sometimes we create our destinies bila kujua, you might think kwamba ni mtandaoni tu lakini it didn't just come.

Ngoja nisome michango ya wadau tutapata tu majibu.

Mshana Jr, Heaven Sent, Sky Eclat, Da'Vinci: mnaweza kuwa na mchango hapa.
Not a right place kwa ajili ya dini; but ulichomwambia makes sense a lot. Mtu yeyote mwenye nia/kiu ya kuishi au kutaka mambo yake yafanikiwe/kuongezeka; hawezi akalifikiria jina "maiti" or anything that implicates death. Hadi yeye kujiita maiti; sio coincidence na ndiyo maana sijashangaa kukuta anatamani kujiua

Mleta mada, yes umeomba sana na Mungu anasikia sana; na inawezekana ameshakujibu; ni wewe tu kutake actions sasa. Tatizo lako litaishia huko huko kwenye kujichanganya na watu; ila ndo inatakiwa upate muongozo wa wapi uanzie

Dr Wansegamalila amejitolea kukusaidia; please accept his offer. You need someone/shrink to confide to. Mtu ambaye atatibu tatizo lako taratibu na kukuelekeza ufanye nini/ufanyaje, unaweza kupata solution ya tatizo lako kupitia yeye. It shall be well with you
 
Updates. bado sijapata msaada. Nimekata tamaa, nipo duniani kimakosa, nawaombea kwa Mungu wale mnaofurahia kuishi kwenye huu ulimwengu basi furaha yenu isikatike iwe daima. Kuna kamshahara hapa nimekapata nimeamua nianze kunywa bia na konyagi 4 kwa siku nione kama zitasaidia. bye
 
Updates: Bado sijapata msaada. Nimekata tamaa, nipo duniani kimakosa, nawaombea kwa Mungu wale mnaofurahia kuishi kwenye huu ulimwengu basi furaha yenu isikatike iwe daima. Kuna kamshahara hapa nimekapata nimeamua nianze kunywa bia na konyagi 4 kwa siku nione kama zitasaidia. bye
You are not alone.
 
Not a right place kwa ajili ya dini; but ulichomwambia makes sense a lot. Mtu yeyote mwenye nia/kiu ya kuishi au kutaka mambo yake yafanikiwe/kuongezeka; hawezi akalifikiria jina "maiti" or anything that implicates death. Hadi yeye kujiita maiti; sio coincidence na ndiyo maana sijashangaa kukuta anatamani kujiua

Mleta mada, yes umeomba sana na Mungu anasikia sana; na inawezekana ameshakujibu; ni wewe tu kutake actions sasa. Tatizo lako litaishia huko huko kwenye kujichanganya na watu; ila ndo inatakiwa upate muongozo wa wapi uanzie

Dr @wansegamalila amejitolea kukusaidia; please accept his offer. You need someone/shrink to confide to. Mtu ambaye atatibu tatizo lako taratibu na kukuelekeza ufanye nini/ufanyaje, unaweza kupata solution ya tatizo lako kupitia yeye. It shall be well with you

Dr @wansegamalila hayupo tayari nimemcheki muda mrefu, sijapata response kutoka kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom