Social Media Reactions: Nape, Zitto, Tundu Lissu na wengine wampongeza Rais John Magufuli

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224








 

Attachments

  • IMG_20170524_140445_599.JPG
    IMG_20170524_140445_599.JPG
    33.7 KB · Views: 130
Ni jangiri pekee ndio anafurahi TEMBO na FARU wakiuwawa porini kwa hili alilofanya JPM atakae pinga mm namwona na kumuita ni jangiri wa maliasili na uchumi wa TANGANYIKA na nitaendelea kuamini TANGANYIKA hakuna wasomi hila kuna watu wanahold vyeti vya viwango vya elimu mbalimbali.
 
Maoni yangu kufuatia Taarifa ya Kamati ya Mruma kuhusu Mchanga wa Dhahabu

Zitto Kabwe

Leo Watanzania tumeshuhudia namna ambavyo tumekuwa tukipoteza mapato mengi kwenye sekta ya madini kufuatia Taarifa ya Kamati ya Prof. Mruma kuhusu Makanikia ya Shaba. Tarehe 8/3/2017 nilitoa yafuatayo kufuatia Amri ya Rais kuzuia kusafirisha mchanga wa madini kwenda nje ya Nchi.

"Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa (economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 hivi.

Pia tunahitaji umeme zaidi ya megawati 1500 kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama fursa (potential) ya ukanda wetu ya kuzalisha huo mchanga (copper concentrates) ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region (ukanda huu). Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo.

Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio lilitolewa na Serikali litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa.

Kwahiyo AMRI hii ya Serikali itusaidie kuuleta mezani mjadala huu kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana". Mwisho wa kunukuu.

Vile vile mnamo 26/3/2017 nilitoa maoni mengine kufuatia majadiliano juu ya manunuzi ya kampuni ya ACACIA kukwama baada ya agizo la Rais kuzuia usafirishaji wa mchanga kwenda nje ya nchi. Nilisema;

" Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni.

Tafiti zinaonyesha kuwa gharama ya kujenga ' refinery ' ya kuchenjua dhahabu hapa nchini ni USD 800m. Hivyo mapato ambayo yangepatikana kutokana na kodi ya mauzo ya Acacia yangewezesha nchi kujenga refinery na kufikia lengo la Rais la kuwa na uchenjuaji wa mchanga ule hapa hapa nchini. Rais angetulia angeweza kuua ndege wawili Kwa jiwe moja, 1) kiwanda cha kuchenjua kingejengwa nchini na 2) mchanga usingesafirishwa tena kwenda China na Japan". Mwisho wa kunukuu.

Wakati bado naamini kwamba jambo hili lingefanywa vizuri zaidi na nchi kufaidika zaidi iwapo taratibu fulani zingefuatwa, ni dhahiri kwamba Rais pengine alijua zaidi yetu na hivyo kufanya alivyoona inafaa. Taarifa ya Kamati aliyoiunda Rais inaonyesha kuwa upotevu wa mapato ulikuwa mkubwa Sana na Kwa Kweli hakuna Mtanzania mwenye uzalendo madhubuti anaweza kuthubutu kupingana na hatua Hii aliyochukua Rais.

Sisi Chama cha ACT Wazalendo kwenye Azimio la Tabora tumependekeza hatua kali zaidi za kubadili Kabisa mfumo wetu wa kuendesha sekta ya Madini Kwa 1) kuweka mikataba yote wazi 2) kuondokana Kabisa na mfumo wa Sasa wa milki ya Mali kuwa Kwa wawekezaji na kufanya milki kuwa ya Dola na wawekezaji kuwa wakandarasi tu na 3) wananchi kuwa na kauli kabla ya mali kuchimbwa Kwa kutumia kanuni ya ' free prior informed consent. Kwa vyovyote vile iwapo mapendekezo haya yangechukuliwa na Serikali tusingekuwa kwenye mjadala wa makanika kwani haki na wajibu kamwe Isingetoka Kwa dola maana wawekezaji wangekuwa makandarasi wetu tu.

Utafiti hupingwa Kwa utafiti mwengine. Kwa sasa Kamati ya Mruma na Taarifa yake Ndio rejea pekee iliyopo kuhusiana na suala la Makanikia ya madini.
Hata hivyo tunafahamu kuwa kuna kamati nyingine ambayo bado ipo kazini. Kamati hii ndio inayoshughulikia mfumo wa kusheria na kiuchumi katika sekta ya madini! Hivyo tunasubiri mapendekezo yake kama yatatoa majawabu ya matatizo yaliyopo katika sekta hii. Tunaunga mkono mapendekezo ya Taarifa hii na tunamwunga mkono Rais Kwa Hatua madhubuti atakazochukua katika kuboresha sekta ya madini. Tunataraji Rais atafanya marekebisho ya uhakika Kwa kubadili Kabisa mfumo wetu wa uvunaji wa rasilimali za madini ikiwemo mapendekezo tuliyoyatoa kwenye Azimio la Tabora pamoja na yale yaliyo katika Ripoti ya Tume ya Bomani. Muhimu zaidi ni kuhakikisha kuwa Tanzania inafaidika na rasilimali zake za madini ili kuweza kujiletea maendeleo ya watu wake.

Zitto Kabwe
24/5/2017
 
Nape kapongeza kinafki kwelikweli... Naona bado ana kinyongo!
 
Mikataba isije kuwa ina loophole ya wao kusafirisha!
Mungu amsaidie tushinde katika hili
 
Sitoi Pongezi yoyote hapo. haya yote yalikuwa yanafahamuka, isipokuwa ni siasa tu na kwa vile wanasiasa wetu wanajua mihemuko ya wabongo sasa wamewakamata. Sipendi mambo ya maigizo katika masuala yanayogusa maslahi ya taifa.
 
Sitoi Pongezi yoyote hapo. haya yote yalikuwa yanafahamuka, isipokuwa ni siasa tu na kwa vile wanasiasa wetu wanajua mihemuko ya wabongo sasa wamewakamata. Sipendi mambo ya maigizo katika masuala yanayogusa maslahi ya taifa.
Sawa umesikika, pisha njiani sasa maana safari inaendelea.
 
Back
Top Bottom