SMZ Yapambana Na "Obama"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ Yapambana Na "Obama"?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Sep 15, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imedai fujo zinazoendelea hivi sasa kisiwani Pemba ni mpango maalumu na wa muda mrefu wa serikali ya Marekani.

  Kauli hiyo ya kulishutumu taifa kubwa duniani imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya kituo cha uandikishaji cha shule ya Sizini mkoami Kaskazini Pemba.

  Mwishoni mwa mwezi uliopita, Marekani ilitoa taarifa kwa raia wake ikiwataka kuwa makini na safari za kisiwani Pemba ambako ilisema kuna vurugu zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Marekani, ambayo ina tabia ya kutahadharisha raia wake kufanya ziara sehemu ambazo kuna ama kunaweza kutokea vurugu, ilieleza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura, kumekuwa na vurugu kubwa kisiwani Pemba na kuwaonya raia wake kuwa makini na mikusanyiko wawapo visiwani Zanzibar, huku ikiwataka wajiandikishe kwenye ubalozi wake mara watakapowasili Tanzania.

  Lakini SMZ ilijibu vikali taarifa hiyo ya tahadhari kwa raia wa Marekani na jana Waziri Juma alieleza msimamo wa serikali yake kuhusu kitendo hicho cha Marekani.

  "SMZ inaamini kwamba Marekani ilikuwa inajua nini kitatendeka katika kisiwa cha Pemba na ndio maana ikaanza kutoa tahadhari kwa wananchi wake mapema," alisema Waziri Juma ambaye alisema ametumwa na serikali kwenda Pemba kuangalia hali ya usalama.

  "Haiwezekani Marekani iwatake wananchi wake wasitembelee kisiwa cha Pemba halafu iwe haijui nini kitatokea katika kisiwa hicho.

  "Sisi serikali ya Zanzibar tunaamini kwamba Marekani ndio iliyopanga mpango huu maalumu wa kufanyika vurugu huku Pemba na ndio maana wakawatahadharisha raia wake mapema wasitembelee Pemba. Kama walikuwa hawajui kwa nini watoe tahadhari? Wanajua na ndio waliopanga mpango huu kwa kutafuta sababu wanazozijua wao."

  Zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura kisiwani Zanzibar limekumbwa na vurugu kubwa na awali serikali ililazimika kulisimamisha baada ya wananchi kurushiana mawe na polisi. Juzi polisi walilazimika kutumia silaha za moto kutawanya wananchi ambao walijikusanya nje ya vituo vya kujiandikishia kwa lengo la kuzuia wenzao kujiandikisha.

  Tayari nchi 14 wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani zimeshaitaka SMZ kushughulikia matatizo yaliyojitokeza kwenye zoezi la uandikishaji wapigakura ili kuufanya uchaguzi ujao kuwa huru na wa haki. Tatizo kubwa linalopingwa na wananchi wa Zanzibar ni matumizi ya kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi kama ndio sifa kuu ya mtu kuandikishwa.

  Wananchi wengi visiwani Zanzibar, ambako mkaazi ni yule aliyeishi kwa miaka mitatu mfululizo, wanadai wamenyimwa vitambulisho vya ukaazi na hivyo hawawezi kuandikishwa kupiga kura.

  Waziri huyo pia alisema ili kuondokana na masharti ya nchi wahisani, SMZ itaanza kusimamia uchaguzi wake na kuachana na ufadhili wa wahisani kwa madai kuwa uzoefu unaonyesha kuwa ufadhili huambatana na masharti, jambo ambalo alisema si jema.

  Kwa mujibu wa Waziri Juma, pamoja na kuwa nchi wahisani wanatoa fedha kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali, hakuna sababu ya nchi hizo kuingilia mambo ya ndani kwa kuwa kila nchi ina uhuru wake na inajiendesha.

  Alisema fedha zinazochangwa na wafadhili ndio zinazosababisha matatizo yanayototokea Pemba sasa kwa kuwa wafadhili huwa wana masharti yao, hivyo SMZ itaanza kusimamia uchaguzi wake hata kama italazimika kuchangishana shilingi moja moja.

  "Mtu akikufadhili ndio anakuwekea masharti anayotaka yeye lakini sisi wenyewe tutaanza kuchanga fedha wenyewe ili kusimamia uchaguzi wetu wenyewe maana tushaona hawa wanataka kutuletea maneno mengi," alisema Juma.

  Waziri Juma alisema SMZ haitaki kuona fedha za wafadhili zinatumika kuvuruga amani na kwamba itatumia nguvu zake zote kurudisha amani iliyoanza kutoweka katika kisiwa cha Pemba.

  "Sisi ni wasimamizi wa sheria… Marekani walikuwa wanajua nini kitatokea lakini tunasema tutatumia nguvu zote katika kurejesha hali ya amani kwa sababu tunajua hii ni mbinu tu na hatutaivumilia hali hii," alisisitiza waziri huyo.

  Alisema pamoja na matatizo yote yaliyotokea, uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utafanyika kama ulivyopangwa hata kama Zanzibar nzima wataandikishwa watu 100.

  "Tunasema uchaguzi utafanyika na upo pale pale hata kama ni watu 100 wataandikishwa, hatutaacha kufanya uchaguzi kwa visingizio kama hivi kwa sababu hatutaki kufadhiliwa; uchaguzi ni wetu wenyewe," alisema Waziri Juma.

  Alisema kuanzia sasa mtu yeyote au kiongozi atakayehamasisha wananchi kufanya fujo ili kuharibu zoezi hilo, atachukuliwa hatua za kisheria.

  "Haiwezekani mwananchi anataka kutumia haki yake, halafu mwingine anamkataza kufanya hivyo. Kwa kweli kama tukimgundua kiongozi au mtu yeyote tutamchukulia hatua za kisheri kwa kuwa anachochea vurugu," alisema Hamza.

  Alisema kuwa wananchi ambao bado hawajapata fursa ya kujiandikisha, watapata fursa wakati mwingine kwa kuwa zoezi hilo litafanywa kwa awamu tatu.

  Kuhusu tatizo la vitambulisho vya ukaazi, Waziri Juma alikanusha kuwa ndilo lililosababisha kutokea kwa mvutano kati ya wananchi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) na kusababisha zoezi hilo la uandikishaji kugomewa.

  "Vitambulisho ni propaganda za kisiasa tu ambazo zinafanywa na wafuasi na viongozi wa upinzani, lakini sisi tunasema tunatumia nguvu zote katika kuhakikisha tunamaliza suala hili. Wacha wao wagome lakini tutawaandikisha wanaotaka kujiandikisha," alisema.

  Alisema hali hairidhishi lakini ameahidi kutumia nguvu za ulinzi katika kurejesha amani, na kudokeza kuwa fedha nyingi zimetumika katika kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

  "Sitaki kusema ni kiasi gani tumetumia lakini nakwambia ni fedha nyingi sana tumeshatumia na tunaendelea kutumia kw akuwa hilo si tatizo kubwa," aliwaambia waandishi wa habari..........


  SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Imefika wakati SMZ kumzuia Hamza kuwa msemaji wa kila kitu, amekuwa too much sasa, anakoelekea ni kutafuta ugombanishi wa diplomasia na mataifa makubwa, athari zake ni kubwa kuliko anavyofikiria. Upayukaji huu wa maneno yasiyokichwa wala miguu ni utaiweka pabaya si Zanzibar tu bali Tanzania kwa ujumla. Kama kauli ya tahadhari kwa Marekani hawakuitoa kwa zanzibar tu hata raia wanaotembelea Uganda na maeneo mengine yenye vurugu wamepewa tahadhari kama hiyo, waziri Juma anataka kusema kuwa Marekani pia ilijuwa nini kitatokea Uganda na maeneo mengine yenye fujo, waziri Juma aaache umbumbumbu akifikiri anawafurahisha wa kubwa zake na wakereketwa wa chama chake bila ya kujua kua anatafuta ugomvi usio walazima wa kidiplomasia.
   
 3. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa zetu tegemeo lao kubwa ni Tanganyika ndio watetezi wao lakini kama wanavyosema wazee wetu ukimzowesha mbwa mwilini ipo siku atakufuta hadi ndani ya msikiti.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Huu ni mwendelezo wa yale ambayo mtu huwa anazoea kuyafanya maana ndio yanayo define yeye ni nani. Nashangaa sana kusikia kila Tatizo la Zenj limeletwa na watu either wa bara na sasa Marekani. Ukweli wa mambo, matatizo ya zenj suluhu yake iko hapo hapo zenj. Kupoteza malengo kwa kuyasogeza matatizo kwa watu wengine sio dawa. Ni njia ya mwongo ambayo huwa fupi sana.
   
 5. s

  shabanimzungu Senior Member

  #5
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Marekani in tabia yakuvurugha mamabi kla pahali......kenya walifanya hivo hivo..halafu wanasema wao ni watu wa demokracis..........tanzania imekuwa jukwaa ya foreign policy ya america..we will pay a heavy price..i am sure we realize but Kikwete is a darling of USA...and when they do not need u they treat you like kenya.........beware.........
   
 6. C

  Calipso JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Junius mkuu, huyo jamaa anachokiongea siamini tu kama ni matakwa yake binafsi bali ni tamko la serikali nzima kwani hawa jamaa lao ni moja,wala hawajali kitu muhimu wao wanavimba matumbo yao.. MAREHEMU ALI NABWA aliwahi kusema IPO SIKU ITAKUWA KWELI
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Nini tamko la Kikwete katika kadhia nzima ya daftari huko Pemba.

  Mimi naona sasa ni kipindi muafaka kwa Kikwete kuingilia kati.
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Haya ni mawazo ya boko haram
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha kuwalaumu marekani, upumbafu wote unaotokea zanzibar ni CCM kuwakandamiza pemba. Ukitolea mfano wa issue za kenya, ni kweli kwamba US walitaka Kibaki abakie madarakani ili interests zao zilindwe kwa sababu Odinga aliwahi kusema kuwa ataondoa military base za marekani kenya akiwa rais.

  Lakini kwa zanzibar mgogoro unaletwa na CCM kwa kupanga kuwahujumu CUF maksudi. Halafu mimi nawashangaa hawa SMZ, hivi wanafikiri USA ikitaka lolote lifanyike popote duniani kuna mtu atapinga?? Unapo deal na USA, elewa una deal na EU tayari, maslahi yao wanayalinda kwa pamoja.

  ukweli nikwamba USA hawana maslahi yoyote zanzibar, isipokuwa issue ya ugaidi. Lazima waangalie nani anatawala zanzibar na ana uhusiano na nchi zipi za kiarabu, na hili ni jambo zuri tu kwani they are after peace in the region.
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa aliongea kuwa Zanjibar si swari, ndivyo alivyoutangazia ulimwengu. CUF wakamkemea sana kwamba anatangaza nchi vibaya. USA wakatoa onyo kwa wananchi wake. CUF wakatoa tamko kwamba SMZ ndiyo iliyofanya USA itoe hilo angalizo kwa raia wake. Sasa jamaa karudi kuwageuzia kibao USA. It is time kumwondoa kabisa huyu waziri asiyejua uzito wa maneno anayoyasema.

  Yeye alipoutangazia ulimwengu kuwa Zanzibar si swari alitegemea nini? tena huyu ndiye aliyetoa maneno mabaya sana kwa Waziri Mkuu Mhe. Pinda. Halafu nasikia anataka kugombea uRais.
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huyo bwana hamza hassan juma nadhani hana akili nzuri na akumbuke tu kwamba marekani ikimhitaji haichukui nusu saa wamemmaliza.
   
 12. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi siamini maneno ya wanasiasa hao visiwani. Vurugu kiini chake ni serikali yenyewe kwa kuwapangia watu aina ya serikali ya kutawala.Kama ingekuwa serikali ya watu, vurugu ingetokea wapi? Watu wamechoka kuporwa haki yao ya kujichagulia viongozi wawapendao. Vita ya wanandugu haiishi kirahisi mpaka maamuzi ya makusudi yafanyike kwa kukubali mapatano ya dhati. Ni kama Israel na Palestina.
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  Huyu Mheshimiwa wenu amesikika bbc akikanusha maneno yake, anadai mwandishi alimnukuu vibaya. Anasema Pemba hawapo wamarekani wapo wa pemba tu. Anasema hakusema kuwa USA inahusika na vurugu za Zanzibar. Jamaa anaonekana ni typical mjahidinah.
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  mfa maji haishi kutapatapa...........aliyo yasema nyerere yanaweza kutokea japo hatupendi yatokeee.......
   
 15. M

  Mulugwanza Member

  #15
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Huyu jamaa hana anachojua maana nikawaida kabisa ya mtu makini kuchukua tahadhari kabla ya janga kutokea na marekani ilichofanya kwa raia wake!
   
Loading...