SMZ yajiandaa kumshtaki Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yajiandaa kumshtaki Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Aug 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inajiandaa kumshtaki Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kwa madai aliyotoa kuwa kuna watu wanaandikishwa vitambulisho vya Uzanzibari Mkuranga mkoani Pwani na Pangani, Tanga.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari, Mohammed Juma Ame, alisema shutuma hizo ni nzito na wanampa muda wa siku saba kiongozi huyo kuthibitisha madai yake.

  “Kwa kweli ni madai mazito na kwa kuzingatia hilo, tunamtaka athibitishe, vinginevyo tunampeleka mahakamani… hivi sasa tumo katika mchakato wa kusubiri ushauri wa wanasheria, tutampeleka mahakamani akathibitishe,” alisema Ame.

  Alisema idara yake inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kusisitiza madai yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, hayana usahihi wowote zaidi ya kuipaka matope idara hiyo.

  Msimamo huo wa Serikali umekuja siku chache baada ya kiongozi huyo, kudai kumekuwa na kazi inayofanyika katika maeneo ya Mkuranga, Pwani na Pangani ya kusajili vitambulisho kwa watu wasio na sifa.

  Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alisema yeye si kikwazo cha kusitishwa kwa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura Pemba. Na kuongeza kuwa hakubaliani na matamshi ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusu idara yake kuchangia matatizo katika uandikishaji.

  Alisema badala yake tatizo ni ZEC kuwakumbatia wanasiasa na kupokea shinikizo kutoka vyama hivyo na kusahau sheria. “Tume ya Uchaguzi ndiyo inapewa mashinikizo na wanasiasa na kwa kuthibitisha hilo, katika kongamano la CUF Dar es Salaam, walitoa maazimio ambayo mojawapo ni kutaka uandikishaji usitishwe na tumeona ZEC inasitisha,” alisema Ame.

  Aliongeza kuwa kama ZEC inadai kuna tatizo katika upatikanaji wa vitambulisho ilikuwa busara kumwita na kumweleza ukweli, lakini haijafanya hivyo. Alisisitiza kwamba hakuna matatizo katika upatikanaji wa vitambulisho kwa watu wenye sifa.

  Alisema hivi sasa watu wamepungua katika shehia za Pemba ambapo katika ofisi za wilaya, kumesheheni watoto wa shule ambao wengi wao hawana sifa ya kusajiliwa kwa kuwa hawana umri wa miaka 18.

  “Kazi Pemba inakwenda vizuri na katika ofisi zetu wanaokwenda kuomba vitambulisho ni watoto wadogo, wanafunzi wakiwa na vyeti vya kughushi vya kuzaliwa…tayari kuna kesi 32 tunazichunguza za kughushi,” aliongeza.

  Aliwalaumu viongozi wa CUF kwa kuchangia wananchi wa Pemba kususa vitambulisho na katika ofisi zake kuna vitambulisho vya watu 7,887 ambavyo havijachukuliwa tangu mwaka 2005.

  Alitoa mfano wa jimbo la Konde ambapo alisema katika watu 8,947 waliopiga kura mwaka 2005 waliosajiliwa katika vitambulisho ni 9,022 huku waliojiandikisha ni 6,415, huku Mgogoni walioandikishwa vitambulisho ni 9,448 na kwenye Daftari ni 7,513.

  Juhudi za kumpata Maalim Seif kwa njia ya simu azungumzie madai hayo ya SMZ zilishindikana jana lakini Mkurugenzi wa Mahusiano na Mambo ya Nje wa Chama hicho, Ismail Jussa, alisema mpaka jana hawakuwa wamepata barua kuonesha nia hiyo ya SMZ kumshtaki Katibu Mkuu.

  “Kwa kawaida kunapokuwa na jambo kama hilo kuhusu chama chetu huwa kwanza taarifa au barua zinapitia katika idara yetu hii lakini mpaka sasa hatujaiona,” alisema Jussa. http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3396
   
Loading...