SMZ kumaliza zamu za wanafunzi Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakaribia kumaliza ujenzi wa madarasa 5,000 kuondoa zamu mbili kwa wanafunzi nchi nzima na kubakisha zamu moja.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipofungua rasmi Skuli mpya ya Sekondari Tumekuja iliopo Mwembeladu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 09 Januari, 2024 katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile Skuli hiyo mpya ya tumekuja ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,755 kwa wastani wa uwiano wa wanafunzi 45 kwa darasa moja, tayari wanafunzi wameshapangwa wiki ijayo kuanza masomo.

Rais Dkt. Mwinyi amempongeza mkandarasi wa kampuni ya CRJE kwa kujenga Skuli ya kisasa ambayo ina maabara tatu ya kisasa, chumba cha kompyuta, maktaba na ukumbi wa mikutano.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kujenga maghorofa katika sekta ya elimu kwa wanafunzi kutozidi 45 kwa darasa moja .

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kufanya uamuzi sahihi kwa faida ya nchi na kuyakarabati majengo ya mji mkongwe kwani ni urithi wa nchi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amesema mafanikio yaliyopatikana katika elimu ni kwa juhudi za Waalimu kwa kuongeza idadi ya ufaulu ikiwemo kutoka wanafunzi 2,000 hadi 6,000 Skuli za Msingi na matokeo ya kidato cha sita ya mwisho ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu kwa asilimia 90.

FB_IMG_1704806798495.jpg
IMG-20240109-WA0048.jpg
IMG-20240109-WA0049.jpg
IMG-20240109-WA0052.jpg
IMG-20240109-WA0053.jpg
IMG-20240109-WA0051.jpg
IMG-20240109-WA0050.jpg
IMG-20240109-WA0046.jpg
IMG-20240109-WA0041.jpg
IMG-20240109-WA0045.jpg
IMG-20240109-WA0042.jpg
IMG-20240109-WA0039.jpg
IMG-20240109-WA0040.jpg
IMG-20240109-WA0035.jpg
IMG-20240109-WA0034.jpg
IMG-20240109-WA0032.jpg
IMG-20240109-WA0033.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240109-WA0032.jpg
    IMG-20240109-WA0032.jpg
    88 KB · Views: 1
Kijijini kwetu kabla ya magu shule zilikua zinajengwa na wanakijiji wenyewe.

Wanachangishana, wenye nguvu zao wanaenda kujenga. Serikali inachangia padogo tu.

Haya mambo ya kuingia kwa zamu yaliisha zamani sana.

Ilibaki tu darasa la pili kwenda shule saa 4 na sio kwasababu ya uhaba wa madarasa ila ni utaratibu uliozoeleka hapo shuleni.

Alivoingia magu kaaminisha serikali ina hela, itafanya kila kitu iliwalemaza sana wazazi. Ule muamko waliokua nao mababu/baba zetu ukapotea kabisa.

Mzazi hata kumshonea tu mtoto uniform ikawa kazi.
 
Back
Top Bottom