Je watanzania ni mbumbumbu kiasi kwamba Dr Slaa akijieleza kwa mdomo hatutamuelewa hadi kuandamana? Je, Dr Slaa akitoa kauli ya kuibiwa kura inatosha kuandamana bila na sisi kufanya uchunguzi binafsi? Tuwe na subira tupate maelezo ya kutosha kutoka kwa wanasiasa wenyewe kabla ya kukimbilia barabarani. Kesho Ijumaa ni mapema sana kuandamana tunahitaji tafakari pana ambayo kila wananchi ataunga mkono badala ya kukurupuka.
Uchunguzi binafsi hauwezekani, tayari watu wamefanya kwa niaba ya watanzania wote na ndiyo maana chadema wameamua kupeleka rasmi malalamiko kwenye NEC lakini taarifa nilizonazo zinasema kuwa NEC wamepuuza, kwa hiyo tufanyeje? Maandamano ya amani kabisa kuuambia ulimwengu wote kuwa wezi wamechukua nchi.