Kwenye hzo simu kuna camera zenye kazi tofauti kama ifuatavyo;
1. Main lens: Hii ndio lens ya kawaida ambayo unayoona kwenye simu za jicho moja.
2. Ultra wide angle lens: hii inakuwezesha kuona kwa upana mkubwa zaidi. Rejea kwenye picha huko chini.
3. Telephoto lens: hii ni lens ya zoom. Utofauti wa kutumia lens hii dhidi ya zoom ya kawaida ya simu zenye lens moja ni kwamba hii inakupa picha halisi inavyoonekana na lens tofaut na simu zenye lens moja zinazo crop picha. Rejea picha chini huko
4. Depth sensor: hii ni kwaajili ya kusoma umbali wa kitu kutoka kwenye simu yako na kutengeza 3D image. Simu nyingi za bei rahisi ndio zina hii sensor. Zinatumia hii sensor kwaajili ya kuweka ile effect ya potrait moja. Kiukweli hii ni useless, kwasabab unaweza kuweka potrait effect kwa kutumia software tu na camera moja. Huwezi ona hii sensor kwenye simu za bei ghali.
5. Macro lens: hii ni kwaajili ya kuchukua picha kitu kwa ukaribu sana. Kma unavyojua kuwa ukichukua simu yako ukisogeza karibu sana na kitu inapoteza focus. Lens hii inakuwezesha kufocus vitu kwa ukaribu sana na kuoata details nzuri
6. Time of flight sensor: hii ni kma advanced version ya depth sensor. Hii haitumii picha kupima umbali bali inatumia infrared light kupima umbali. Hii utaiona kwenye simu chache sana. Utaikuta hasa kwenye Samsung za S and Note series na baadhi ya simu zingine za bei kubwa.
7. LiDAR sensor: hii ni more advanced version ya Time of flight sensor. Kwa sasa utaikuta kwenye iPhone 11 Pro series kwenda mbele ma iPad Pro 2020/2021. Hichi ni kile kidoti cheusi kidogo kuliko zile camera zingine 3 kwenye iPhones.
8. Color filter camera: hii sio popular sana. Inafanya kazi kuidentify color halisi za unachotaka kupiga picha na kupeleka hzo data kwenye software inayoweza kutengeneza color filters mbali mbali au kusaidia kuboresha rangi kwenye picha. Hii utaikuta kwenye simu kma Oneplus 8 Pro.
Hizi ndio camera zinazotumika hasa kwenye simu za sikuhizi.
Simu za bei ghali utazikuta na camera 2, 3 or 4 ambazo ni Main lens(wide angle), Telephoto, Ultra wide na Time of flight/LiDAR/Color filter/Macro lens. Hlo kundi la nne hapo huwa inategemea na brand na huwa wanakua na moja wapo kati ya hzo au wasiwe nazo kabisa.
Simu za bei ya kati za sikuhzi huwa zinakua na camera 3 hadi 5. Main lens, ultra wide, telephoto, depth sensor, macro lens. Japo kuwa hizi unaona zina camera nyingi huwa quality ya hzo camera nyingine sio nzuri.
Simu za bei za chini mara nyingi utakuta 1 au 2. Kma mbili aidha na main + ultra wide or main + depth sensor.
Mwisho wa yote ujue tu hata kama simu ina camera 5 inaweza zidiwa na simu yenye camera moja. Unakuta hzo camera 5 zote ni za quality ya chini na hii yenye moja ina camera yenye quality nzuri sana. Hvyo usirukie tu camera 5, angalia kwanza kma main camera inauwezo gani na je hizo zingine pia zina uwezo gani. Kma camera ya depth ni useless kabisa. Camera ya macro lens kwenye simu za bei rahisi unakuta ni 2MP ambayo haina quality yoyote ile. Hata hzo ultra wide na telephoto kwenye simu za bei rahisi hazina quality nzuri, quality ni mbaya kupitiliza.
Picha hapo chini inaonesha tofaut kati ya Ultra wide lens (juu kushoto), main/wide angle lens (juu kulia), telephoto 5x (chini kushoto) na Telephoto 10x (chini kulia) kutoka kwenye Samsung Galaxy S21
View attachment 1761305