Smartphone ya kwanza ya bei rahisi zaidi Duniani

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
IMG_5500.jpg

Kampuni moja ya India inatarajiwa kuzindua kile kinachojulikana kuwa simu aina ya smartphone ya bei rahisi.

Kampuni ya Ringing Bells imesema kuwa simu hiyo kwa jina Freedom 251 itagharimu Rupee 500 sawa na dola 7.3,lakini vyombo vya habari nchini India vimesema kuwa itauzwa kwa Rupee 251 pekee ambazo ni sawa na dola 3.67.

Ripoti zinasema simu hiyo ina ukubwa wa 8GB na ina kamera mbele na nyuma.

India ni soko la pili kwa ukubwa la simu na lina wateja bilioni moja wanaomiliki simu.

Freedom 251 inatarajiwa kulenga soko ambalo tayari linatawaliwa na simu za bei ya chini.
1b4f5a2c-d46c-11e5-b369-6a1e536aef0c.png.jpg

Hii ndio modeli yetu ya kwanza na tunafikiri kwamba inaleta mabadiliko katika soko la simu,shirika la habari la AFP,lilimnukuu msemaji wa kampuni hiyo akisema.

Kwa sasa kampuni hiyo inanunua vifaa vya kutengezea simu kutoka nje kabla ya kuviunganisha nchini India,lakini ina mpango wa kutengeza vifaa hivyo nchini India katika kipindi cha mwaka mmoja ujao,aliongezea.

Kampuni ya Ringing Bells ilianzishwa miezi michache iliopita na hivi majuzi ilizindua simu ya be rahisi ya smartphone inayotumia mtandao wa 4G inayouzwa Rupee 2,999,chombo cha habari cha Press Trust kiliarifu
 
Hivi ni nani kati ya Burundi na Rwanda, waliingiza technology yao ya simu?
 
Back
Top Bottom