babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,426
- 3,308
Rasimu mpya imepenyeswa kipengele kinachombana mtu aliyegombea Ubunge vipindi vitatu kutogombea Urais.
Kipengele ambacho kama kikiachwa
bila kufanyiwa marekebisho
kinaweza kuwabana wanasiasa
wengi ndani na nje ya CCM
wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni
pamoja na kile cha Sura ya Saba,
ambacho kinazungumzia Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kuhusu
Serikali, Rais na Makamu wa Rais,
katika sehemu ya kwanza C kwenye
kipengele cha 75 (E)
kinachozungumzia sifa za Rais
kimeeleza kuwa mtu atakuwa na
sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi
ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano ikiwa: anazo sifa za
kumwezesha kuwa Mbunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Katiba hiyo.
Wakati ikiwa hivyo katika sifa za
kuwania nafasi ya Rais, kwenye
Rasimu hiyohiyo kipengele cha sifa
za kuwania nafasi ya Ubunge
kilichopo katika sura ya tisa,
sehemu ya pili (A) inayozungumzia
kuhusu uchaguzi wa wabunge,
katika kipengele cha (2a) kimeeleza
kuwa mtu hatakuwa na sifa za
kugombea/ kuchaguliwa kuwa
Mbunge ikiwa mtu huyo aliwahi
kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu
vya miaka mitano.
Kutokana na hilo, ni wazi kuwa
viongozi au vigogo waliowahi kuwa
wabunge kwa vipindi zaidi ya vitatu
vya miaka mitano hawatakuwa na
sifa za kugombea Urais kwa sababu
tayari kipengele cha sifa za kuwania
Urais kimetaja kuzingatia sifa za
mgombea ubunge.
Kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili, umebaini
kuwa vigogo karibu wote ndani na
nje ya CCM wanaotajwa kutaka
kuwania nafasi ya Urais watakuwa
wamepoteza sifa za kuwania nafasi
hiyo endapo kipengele hicho
kitaachwa bila kufanyiwa
mabadiliko.
Vigogo hao wanaotajwa kutoka CCM
ni Waziri wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, Mbunge wa Monduli,
Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi,
Dk. John Magufuli, Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, Januari Makamba, wakati
kutoka Chadema ni Mbunge wa Hai,
Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa
chama hicho, Dk. Willbroad Slaa na
Zitto Kabwe.
Kipengele ambacho kama kikiachwa
bila kufanyiwa marekebisho
kinaweza kuwabana wanasiasa
wengi ndani na nje ya CCM
wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni
pamoja na kile cha Sura ya Saba,
ambacho kinazungumzia Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kuhusu
Serikali, Rais na Makamu wa Rais,
katika sehemu ya kwanza C kwenye
kipengele cha 75 (E)
kinachozungumzia sifa za Rais
kimeeleza kuwa mtu atakuwa na
sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi
ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano ikiwa: anazo sifa za
kumwezesha kuwa Mbunge wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Katiba hiyo.
Wakati ikiwa hivyo katika sifa za
kuwania nafasi ya Rais, kwenye
Rasimu hiyohiyo kipengele cha sifa
za kuwania nafasi ya Ubunge
kilichopo katika sura ya tisa,
sehemu ya pili (A) inayozungumzia
kuhusu uchaguzi wa wabunge,
katika kipengele cha (2a) kimeeleza
kuwa mtu hatakuwa na sifa za
kugombea/ kuchaguliwa kuwa
Mbunge ikiwa mtu huyo aliwahi
kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu
vya miaka mitano.
Kutokana na hilo, ni wazi kuwa
viongozi au vigogo waliowahi kuwa
wabunge kwa vipindi zaidi ya vitatu
vya miaka mitano hawatakuwa na
sifa za kugombea Urais kwa sababu
tayari kipengele cha sifa za kuwania
Urais kimetaja kuzingatia sifa za
mgombea ubunge.
Kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili, umebaini
kuwa vigogo karibu wote ndani na
nje ya CCM wanaotajwa kutaka
kuwania nafasi ya Urais watakuwa
wamepoteza sifa za kuwania nafasi
hiyo endapo kipengele hicho
kitaachwa bila kufanyiwa
mabadiliko.
Vigogo hao wanaotajwa kutoka CCM
ni Waziri wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, Mbunge wa Monduli,
Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi,
Dk. John Magufuli, Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya
Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, Januari Makamba, wakati
kutoka Chadema ni Mbunge wa Hai,
Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa
chama hicho, Dk. Willbroad Slaa na
Zitto Kabwe.