tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mwanasiasa mkongwe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwanadiplomasia, Dkt. Wilbrod Peter Slaa amesema kuwa chadema haipo kwenye uchaguzi wa mwaka huu siyo kwa ajali kwa sababu haina uchu wa madaraka kama kama vyama vingine.
Akizungumza kwa njia ya mtandao na Baraza la Kidigitali la chama hicho leo Septemba 2, Dkt. Slaa amesema ipo haja ya Chama cha Demokrasia kutekeleza katiba yake ili kuhakikisha kuwa mamlaka yanabaki mikononi mwa wananchi.
“Chama makini hakiendi kwa maslahi yake na wanachadema wamejitoa sadaka. Inabidi tuwabebe Watanzania ili watupe hayo mamlaka”.
Dkt. Slaa amesema kuwa waratibu wote wa chama hicho wana wajibu wa kuushirikisha umma kama mtu mmoja mmoja ama vikundi kama CHADEMA family akisema kuwa kwa sasa chama hicho hakitekelezi matakwa ya katiba yake.
“Nchi hii itabaki mikononi mwa CCM tusipokuwa makini na kutekeleza haya maono ya katiba yetu kwa sababu tunaenda kwa spidi ya konokono. Wakati tunazunguka kwenye no reforms no election nilikuwa naangalia hivi vikundi vipo vichache sana. Lengo letu ni kupeleka mamlaka kwa wananchi tofauti na CCM, mwenyekiti tutamheshimu”.
Ameongeza kuwa msimamo wa no reforms no election ni mtakatifu na unampendeza Mungu akisisitiza kuwa unalenga kuwanufaisha Watanzania “Ajenda ya no reform no election ilianzishwa na CHADEMA ila imekuwa ya watu wote wenye vyama na wasio na vyama pia.”