Slaa: CCM wamechanganyikiwa

Slaa: CCM wamechanganyikiwa

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechanganyikiwa ndiyo maana kinafanya hujuma kutaka kuisambaratisha CHADEMA.

Dk. Slaa alisema CCM inafanya hivyo kwani inajua fika mwisho wao wa kutawala kwa kuwadanganya Watanzania umewadia.
Alitoa kauli hiyo jana katika Ukumbi wa Vijana mjini hapa wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Singida, Morogoro na Dodoma.

Akizungumza na wajumbe wa mikoa hiyo, Dk. Slaa alisema hujuma za kutaka kuisambaratisha CHADEMA zimekuwa zikifanywa na serikali, Bunge na CCM yenyewe.

Alisema serikali kupitia vyombo vyake na kwa kushirikiana na CCM, inatapatapa kuokoteza ushahidi wa uongo kuwabambikizia kesi baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA, huku Bunge kupitia spika na naibu wake likitumia udikteta kukisambaratisha chama hicho.

"Nyie wajumbe ni mashahidi wa hili, mmesikia jinsi serikali na CCM walivyotengeneza ushahidi wa video ya kutunga kumbambikia kesi ya ugaidi Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare.

"Serikali inahaha, Bunge linahaha na CCM inahaha usiku na mchana kujaribu kuisambaratisha CHADEMA, lakini nawaambia hawawezi na mwisho wa utawala wao umekwisha," alisema Dk. Slaa na kuibua shangwe kutoka kwa wajumbe hao.

Dk. Slaa alimshambulia Spika wa Bunge Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kwamba wanaongoza Bunge kwa maelekezo ya serikali yao ya CCM ili isianguke.

"Bunge linaonesha kila dalili ya upendeleo, spika anafanya kazi kwa maelekezo, si kwa utashi wake, sio kwa kanuni, sio kwa busara zake bali kwa maelekezo ya chama na serikali yake. Hili ni jambo baya sana," alisema.

Alisema dalili za chama chochote tawala kupoteza madaraka ni pale kinapoanza kutumia dola na Bunge kutaka kubaki madarakani na kutolea mfano wa CCM kwamba mwisho wake ni 2015.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitumia nafasi hiyo kuwafahamisha wajumbe jinsi Spika Makinda alivyokosea kuhalalisha adhabu iliyotolewa na Naibu wake, Ndugai dhidi ya wabunge sita wa CHADEMA.

Mbali ya hilo, Mbowe alielezea sababu na umuhimu wa mpango huo wa kanda na kuwataka wajumbe wa mkutano huo kutambua kwamba wana kazi kubwa ya kufanya kuleta mabadiliko katika mikoa hiyo.

Mbowe alisema katika kipindi cha miaka 22 tangu CHADEMA ilipoanzishwa, ina mbunge mmoja wa kuchaguliwa na wanne wa viti maalumu katika kanda hiyo inayojumuisha mikoa mitatu.

"Miaka 22 imepita na katika kipindi hicho tumefanya kazi kubwa. Wapo watu waliojitolea hadi kupoteza maisha, wengine wamefilisika kwa kujitolea, lakini katika muda huo tuna mbunge mmoja katika majimbo 28 na wabunge wa viti maalumu watatu," alisema Mbowe.
Alimtaja mbunge wa kuchaguliwa kuwa ni Tundu Lissu wa Singida Mashariki na wabunge wa viti maalumu ni Suzan Kiwanga, Christowaja Mtinda na Christina Lissu.

Alisema hali hiyo ilitokana na chama kutofika ngazi ya chini, lakini mpango huo unalenga kupoka madaraka ya chama kutoka makao makuu ya Dar es Salaam, kuyafikisha ngazi ya kanda, wilaya, kata vijiji hadi chini.
Dk. Slaa aliongeza kuwa mpango huo utabadilisha mkakati wa mapambano kwani badala ya harakati hizo kuanzia makao makuu ya chama, zitaanzia ngazi ya kanda kushuka chini.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya katiba, Mbowe alisema msimamo walioutoa bungeni upo pale pale kwamba kama hakutafanyika mabadiliko kuhakikisha wajumbe wa mabaraza ya katiba wasiwe wajumbe wa CCM kama walivyofanya sasa, CHADEMA itajitoa katika mchakato huo ifikapo mwisho wa mwezi.

Wakati huo huo, wabunge sita wa CHADEMA waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku tano, leo wanatarajiwa kuwasha moto kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Mwanza.
Wabunge hao watafanya mkutano huo katika viwanja vya Mbugani unaotazamiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza.

Wabunge hao ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Highnes Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Ezekia Wenje (Nyamagana), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa) na Godbles Lema (Arusha Mjini).

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kuhusu mkutano huo, Wenje alisema kuwa wameamua kuionesha dunia dhuluma na ukandamizwaji wa demokrasia unaofanywa na Serikali ya CCM.
Alisema kwa muda wa siku tano nje ya Bunge watafikisha na kuonesha jinsi Serikali ya CCM ilivyojipanga kuzima hoja za maendeleo.
"Timu ya wabunge wote tuliotolewa nje tumeamua kuwasha moto wa ukombozi kwa Watanzania. Tunakwenda kuishughulikia kikamilifu Serikali ya CCM.
"Tunakwenda kuionesha nchi na dunia jinsi demokrasia, haki na usawa vinavyodhulumiwa na serikali. Moto tunaokwenda kuuwasha ni wa kueleza uozo wa kiti cha spika na wabunge wa CCM," alisema Wenje.

Aidha alisema operesheni yao hiyo wataifanya kwa kila jimbo la mbunge aliyesimamishwa bungeni.
Kwa mujibu wa Wenje, timu hiyo pia itahutubia mikutano mikubwa kwenye Jimbo la Kongwa la Ndugai na wakiwa huko watafichua uovu wa kiongozi huyo.

Mbunge wa Ilemela, Kiwia alisema uongozi wa kibabe unaofanywa na kiti cha spika kamwe hauna nia njema ya kuwasaidia Watanzania masikini.
 
M4C indio kipato cha CDM, wakiishika hela wanafufua M4C. Njaa hizi zitawaua kina Slaa.
 
Dokt wa ukweli, nimeafiki kabisa kauli hii. Hadi hivi sasa ni dhahiri kwamba CCM wamefika mahala wanahaha hakuna mfano wake; kila kitu hakishikiki kwao - mbona raha wakati yote haya wanayoyaona bado ni rasha rasha tu!!!!!!!!!!!!
 
Kweli CCM wamechanganyikiwa maana wamesahau majukumu yao ya kuiendesha nchi wameanza kuwa wapinzani.Pamoja na nia njema ya kujiandaa kuwa chama pinzani 2015 lakini haijafika, waendelee kutuletea maendeleo badala ya kupambana na upinzani.
 
Dr. Slaa hana jipya. Matamko kila siku cha maana anachokifanya hakionekani.

Sent from my hp EliteBook 8460p using JamiiForums
 
Watuwekee tena hadharani namba ya spika na naibu wake ili tuwashughulikie
 
Nataman kila mwananchi awe na akili kama yangu hainiingii akilini kuwa kuna vijana wenzangu wanaishabikia ccm. Jamani hemu tukumbuke wote jinsi viongoz wa jumuiya za ccm walivyopatikana,kuanzia uwt,uvccm na jumuiya ya wazazi. TUKUBALIANE KWA PAMOJA CCM NI JANGA
 
M4C indio kipato cha CDM, wakiishika hela wanafufua M4C. Njaa hizi zitawaua kina Slaa.

Ni ajabu sana mtu mkubwa unashindwa kujenga hoja unaamua kutukana! Lakini kwa nini unaingia wivu? Au kwa sababu ya ongezeka la wananchi katika
mikutano!
 
Dr. Slaa hana jipya. Matamko kila siku cha maana anachokifanya hakionekani.

Sent from my hp EliteBook 8460p using JamiiForums

Kama hana jipya si mnyamaze? Mbona mnahaha na kuweweseka kila jina lake linapotajwa?
Mimi si mwanachama wa CHADEMA wala hilo dude linaloitwa CCM, lakini kiukweli hakuna chama kilicho "serious" kuleta mabadiliko zaidi ya hicho mnachokigwaya - CHADEMA.
Vitendo vinavyofanywa na CCM kuihujumu CHADEMA ni sawa na kumeza vidonge vya sumu kujimaliza. Wapo wana CCM waliowahi kuonya hivyo wakaitwa wasaliti au wanachama feki! Lakini ukweli utajidhihirisha kadiri siku zinavyosogea kuelekea uchaguzi mkuu.
CCM bila kujua wanawasaidia CHADEMA kuupata umaarufu ambao pengine wasingefanikiwa kuupata!
Hebu ona, CHADEMA ndiyo ajenda katika kila kikao; kuanzia cha shina, wilaya, mikoa, Bunge na mpaka ikulu. Kiitendo CCM wamekoma kabisa kujadili maendeleo na utekelezaji wa ajenda zao na sasa wanaweweseka na Mbowe, Slaa, na kuhangaika na jinsi ya kujibu na pengine kuzipotosha hoja za CHADEMA!
Leo mnataka kutuaminisha Slaa na CHADEMA hawana jipya? Kama si kuchanganyikiwa tukuite vipi kufanya hivyo?
 
M4C indio kipato cha CDM, wakiishika hela wanafufua M4C. Njaa hizi zitawaua kina Slaa.

ATI UYU NAE NI MWANAUME LAKINI ANAISHI KWA KUITEGEMEA WALLET YA NAPE, DAH NAPE AKIANZA UFIR....JI ATAWATATAFUNA WENGi
 
CCM kinyesi kinagonga chupi kinarudi ndani yaani hofu tupu huko!
 
ATI UYU NAE NI MWANAUME
LAKINI ANAISHI KWA KUITEGEMEA WALLET YA NAPE, DAH NAPE AKIANZA
UFIR....JI ATAWATATAFUNA WENGi

Sasa hivi wanatafunwa na yule Chemba la maji taka, zamu ya nape kuwala itafika tu... Si umeona shonza alivyo tepeta na kuchoka?....
 
Back
Top Bottom