Slaa apangua safu ya uongozi Chadema Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa apangua safu ya uongozi Chadema Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jan 13, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Baraza Kuu la CHADEMA mkoani hapa limepangua safu ya uongozi wa juu wa mkoa kwa kuwateua viongozi wa muda watakaokiongoza chama hicho hadi Mei.
  Kikao hicho kizito kilifanyika karibu usiku mzima chini ya usimamizi wa Dk. Slaa ambaye baadaye alitangaza safu mpya ya uongozi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nzovwe mjini hapa.
  Dk. Slaa alimtangaza Peter Mwamboneke kuwa kaimu mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya, nafasi ambayo ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Sambwee Shitambala kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM)
  Diwani wa kata ya Forest katika halmashauri ya jiji la Mbeya, Boid Mwabulanga, alitangazwa kuwa kaimu katibu wa chama hicho akichukua nafasi ya Eddo Mwamalala Makata.
  Dk. Slaa alimtaja Joseph Kasambala kuwa ameteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) mkoa wa Mbeya, akichukua nafasi ya Exavery Mwalyembe.
  Seleman Simbayanje ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu wa Baraza la Wazee wakati Tamali Mbarasya alitagazwa kuwa mratibu wa wanawake wa chama hicho.
  Juzi usiku Dk. Slaa ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Rwakatare, alihamia kwenye kikao cha Baraza la Chama hicho wilaya ya Mbeya Mjini, ambako baadhi ya wanachama walidai kwamba hawana imani na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Mjini, David Mwambigija, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako.
  Habari kutoka ndani ya mkutano huo zimeeleza kuwa wajumbe wa baraza hilo waliamua kumweka kando mzee wa upako na kisha kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
  Kwa mujibu wa chanzo chetu kura zilizopigwa zilikuwa 231 na ni kura tano tu ndizo zilizomkataa Mwambigija huku kura 226 zikimkubali.
  “Kura ya kutokuwa na imani na Mzee wa Upako ilifanyika lakini wajumbe wengi wameoyesha kumwamini na hivyo anaendelea na wadhifa wake,” kilisema chanzo chetu. Habari zimesema kuwa kufanyika kwa mabadiliko hayo, kutaongeza kasi zaidi ya utendaji kazi hasa kwa kuzingatia kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi ndani ya chama hicho

  SOURCE:TANZANIA DAIMA
   
 2. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 717
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Heko Chadema.
   
 3. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Jamaa kwa Mipango nawaaminia
   
 4. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hongereni kwa kufanya kikao cha amani.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  huko ni kutapatapa baada ya mambo kuanza kuwashinda.na bado.someni na vyanzo vingine vya taarifa mjue ukweli sio mnasoma gazeti la mbowe tz daima pekee,mnakosa mengi.
   
 6. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  viva chadema
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tuambie basi. Hilo gazeti lingine limesemaje?
   
 8. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongereni kwa kufanya mabadiliko hayo mapema kabla chama hakijaumia
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Kumbe Rwekatare yupo hivi naona siku hizi amekuwa bubu kabisaaaaaaaaa.
   
 10. L

  Luiz JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huna lolote zaidi ya unafiki tu unataka tukasome gazeti la uhuru?
   
 11. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  pole ndugu yangu...
   
 12. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,223
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Unataka tusome 'UHURU'?!!!! Siwezikupoteza muda wangu kusoma gazeti la uhuru. nipo tayari ni-cost kusafiri kwenda Mbeya kufuatilia mwenyewe habari hizi kuliko kuzipata kupitia gazeti la uhuru.
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,187
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Kumbe Slaa, yeye ndio anapanga viongozi kila sehemu hakuna uchaguzi wala nini zidumu fikra za Katibu Mkuu!
   
 14. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 880
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Soma uelewe ndio uchangie co kukurupuka tu kama magamba wenzio.
  Baraza Kuu la CHADEMA mkoani hapa limepangua safu ya uongozi wa juu wa mkoa kwa kuwateua viongozi wa muda watakaokiongoza chama hicho hadi mei. Kikao hicho kizito kilifanyika karibu usiku mzima chini ya usimamizi wa Dk. Slaa ambaye baadaye alitangaza safu mpya ya uongozi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nzovwe mjini hapa.
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante Mungu kumnyima Urais maana angekuwa anasindikizwa na ving`ora asingepata muda wa kukijenga chama ila 2015 tukichukua nchi chama kitakuwa kimeimarika
   
 16. FREDRICK KIMARO

  FREDRICK KIMARO Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leo nape kakulipa
   
 17. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Una viroba pembeni au vp? Maana unanipa wasiwasi mkuu
   
 18. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,105
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hivi unasomaga habari kwa uangalifu kweli au ukoje wewe?
   
Loading...