Slaa amlipua waziri wa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa amlipua waziri wa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 31, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  na Abdallah Khamis, Mtwara
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amemtaka Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kuacha kutisha na kuwakamata wananchi wanaomuuliza maswali katika mikutano ya hadhara akidai amekashifiwa.

  Akihutubia umati wa wananchi katika Kata ya Mtimbwilimbwi na Nanyamba, Slaa alisema ni uvunjaji wa sheria na ubabe kukamata wananchi waliowapigia kura.

  Slaa alisema hayo baada ya wananchi kumwelezea kuwa, wamekuwa wakikamatwa na viongozi wa serikali na CCM wanapouliza maswali, ndiyo maana wameingiwa woga.

  Alisema Ghasia ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), anafanya vitendo hivyo kwa kuwa ana uhakika wa kutogombea tena ubunge katika Jimbo la Mtwara Vijijini baada ya kutambua kuwa hawezi tena kushinda.

  Slaa alisema maisha ya wakazi wa Mtwara Vijijini na umasikini unaowazunguka, ni aibu kwa uongozi katika miaka 50 ya uhuru, ambapo wajawazito wanalazimika kwenda hospitali wakiwa na vifaa.

  "Enzi za Mwalimu Nyerere hakukuwa na suala hilo, leo hata mtoto mdogo anajua kuwa mama yake anakaribia kujifungua kwa kuwa ni lazima atakuwa anahangaika kutafuta vifaa vya kujifungulia," alisema Dk. Slaa.

  Alibainisha kuwa, Jimbo la Karatu ambalo wananchi wake hawakuwahi kuwa na waziri kwa miaka 15 sasa, wanafikiria kuingiza maji ndani ya nyumba zao wakati Mtwara Vijijini ambayo mbunge wake ni waziri, wananchi wanatafuta maji umbali wa zaidi ya kilometa 10.Katika hatua iliyoonesha kukithiri kwa umasikini, Dk. Slaa alilishwa supu ya ngozi ya ng'ombe kama kitoweo, ambapo wananchi walidai wamefanya hivyo kwa kuwa hawana uwezo wa kununua nyama.

  Walisema hata hizo ngozi ni lazima aende mtu kuzifuata Mtwara mjini na siku inapokosekana wanajihesabia kama wamekosa nyama halisi.

  Kufuatia hali hiyo, Dk. Slaa aliwataka wananchi wa Mtwara mjini kujiepusha na kuuza uhuru wao kwa gharama ya shilingi elfu tano na badala yake wasimamie ukombozi wa kweli.

  MBOWE KUMBANA WAZIRI MKUU

  Akizungumza katika mikutano aliyoifanya katika kata za Madimba na Tangazo, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kuanzia sasa atakuwa msemaji wa wakazi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwa hawana msemaji wa shida zao hususan kuhusu zao la korosho na gesi.

  Alisema akifika bungeni swali lake la kwanza kwa waziri mkuu ni kumuuliza Serikali ya CCM inatumia sera gani kuchimba gesi katika Mkoa wa Mtwara.

  Mbowe alishangazwa na kitendo cha serikali kuweka nguzo za umeme katika maeneo yenye nyumba za nyasi, na kukiita kitendo hicho kama dharau, na kwamba ilipaswa kwanza kuhakikisha wananchi wake wana nyumba bora.

  WENJE AMVAA MBATIA

  Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) amemshambulia Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akidai amefungishwa ndoa ya mkeka na CCM, kwa kupewa ubunge wa viti maalum na Rais Jakaya Kikwete ili kumsaidia kutekekeza ilani isiyotekelezeka.

  Akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo katikati ya mji wa Mtwara juzi, Wenje alisema kitendo cha Mbatia kukubali ubunge wa viti maalumu, kimeonesha udhaifu wake mkubwa, kwamba si mpinzani wa kweli wa kupinga ufisadi na ubadhirifu unaofanywa na Serikali ya CCM.

  Hatua hiyo ya Wenje kumuita Mbatia mbunge wa viti maalumu, iliibua mvutano katika mkutano huo baada ya makundi ya watu kutofautiana, wengine wakisema hata CHADEMA kuna wabunge wa viti maalumu.

  Kutokana na mabishano hayo, ilimlazimu Wenje mwisho wa mkutano kutoa ufafanuzi jinsi wabunge wa viti maalumu wa chama wanavyopatikana na wabunge wanaoteuliwa na rais kwa mujibu wa mamlaka ya ibara ya 66 (1) (a) ya katiba ya nchi.

  "Ndugu zangu hakuna sababu ya kubishana hapa, wapo wabunge wa viti maalumu wa chama husika wanaotokana na idadi ya wabunge halali waliochaguliwa kwa kura za wananchi, na wapo wabunge wa kuteuliwa na rais kwa mujibu wa kifungu hicho, wote ni wabunge, lakini tofauti yao ni huyu ni wa rais na huyu ni wa wananchi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni Vizuri kuwapa Misukosuko Chama Tawala, hawakuwahi kushambuliwa kihalali hivyo; Walizoea kufisadi na kushiba tu
   
 3. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ipo siku CHADEMA na NCCR tutakutana tena katika meza kuzungumza, tutakumbushana mengi, ikiwa ni pamoja na hili.
  IPo siku Wenje na Mbatia mtakutana 'mjengoni', mtasalimiana; kwa kuwa wanadamu hatuna kipimo cha mioyo ni ninyi tu mtakaojua unafiki na ukweli utakaoendelea kati yenu mtakapotazamana kwenye macho.
  Mkikutana Mbowe na Mbatia, pengine halitaharibika neno, maana wakati mmoja wenu anadai atakuwa mtetezi wa wanamtwara kuhusu masuala ya bandari, mwingine amekwishasema, Korosho sasa ni sh.1200 kwa kilo kwa sababu ya jitihada zake za kuwatetea wakulima wa Mtwara. Lakini ni jambo jema kwa wanamtwara, maana sasa wana watetezi zaidi ya mmoja.
   
 4. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Aisee, naona ni ......Presha presha....... Preshaaaaa!, Nakumbuka mchaka mchaka enzi hizooo!
   
 5. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naona magamba yamebana watu nyonga duhhhhhhhhhhhh
   
 6. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yule mama sijui ana matatizo gan kwa kwel? Hawa ghasia tangu apewe uwazir anajikuta yeye ndo baba mwenye nyumbaa! Ku2pelekesha watz.. Ama kweli kaz ipo , tangu apewe gobole anaua mpaka mende na sisimiz kwa gobole
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Oh Jamani wenzetu wanamtwara kweli nasikitika sana kusikia bado wanatumia nyumba za nyasi, kweli wanahitaji mtetezi. Mkapa kweli alishindwa kuwafanya nduguze waondokane na huu umaskini? Unajua kuna umaskini na kuna ule ulio pitiliza nyumba za nyasi hadi leo? Watoto kutembea peku hadi leo? Why? Wanamtwara tuamke tuwakatae hawa mafisadi.
   
 8. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mtwara,mtwara,mtabadilika tu...maisha pia yatabadilika.hongera m4c
   
 9. R

  RC. JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushauri wa bure kwa mh.Dr.slaa naomba uepuke kunyweshwa supu za ngozi kwa kigezo cha maisha magumu,kwani hao ccm hawaaminiki kwa sumu.
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Wenje ni jembe lisiloogopa kwani linachimba popote pale na natamani hili jembe lije nyumban Tabora 2015 kugombea nasi tutaliunga mkono hili jembe la nyamagana.
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nape anasema CDM wanaleta ukusini!!!!!!!!!
   
Loading...