Kutokana na taarifa za awali za msanii huyu kwamba aliachana na mumewe na sababu alizokuwa ameziweka hadharani kwamba alikuwa hampendi, kuna mwingine anampenda zaidi etc etc etc. Lakini baada ya siku chache tukasikia tena wamerudiana.
Nilikuwa napiga story na wife kuhusu maneno ya awali ya huyo msanii. na ndipo mi nikamwambia ningekuwa ni mimi huyo asingerudi na wala hata nisingetaka kumuona. Ndoa ndio ingekuwa basi. Ningemchukia zaidi kwa kunidhalilisha kuliko hata wale ambao nilikuwa nawachukia etc etc etc. Ndipo wife akaniambia ina mana ningekuwa mimi (yeye) ningemfanyia hivyo!, mi nikamjibu kwa jibu rahisi tu kwamba ndio manake. Tangu hapo naona amenisusia, najitahidi kumbeleza lakini ndio ameona kama vile simpendi. Imeshakuwa ni kususiana tu.
Katika hali kama hii kosa langu lipo wapi. Mimi ndio ungekuwa msimamo wangu huo, nisingeweza kumwambia uongo na hata hivyo ilikuwa tunapiga story tu.
Au ningemdanganya tu kumridhisha!!. Lipi sahihi!!.
Poleni akina mama wenye waume, kwa kweli mwanaume anayediskasi hawa wadada???? Let her be, its her damn life.
Kukususa kakusamehe, ningerudisha mahari yako kwenu afu nikakulipia mie mahari.
Umeonae? Sasa hapo cha kumchukiza ni kipi? Wapo kwenye story za shigongo yeye ananuna live bila chenga, khaa!Wanawake wengine akili zao ni 1-1.
Umeonae? Sasa hapo cha kumchukiza ni kipi? Wapo kwenye story za shigongo yeye ananuna live bila chenga, khaa!
Bora 1-1... yani ni 0-0.
Lakini wife wangu yupo poa na nampenda sana... Lakini ndio nimeshindwa kabisa kumuelewa kwenye hili.
itakuwa alikuwa na plan za kumkimbia big X au we waonaje hapo?.
Kabisa swahiba...na ndio hivyo keshajipatia sababu kiulaini, lol.itakuwa alikuwa na plan za kumkimbia big X au we waonaje hapo?.
Kabisa swahiba...na ndio hivyo keshajipatia sababu kiulaini, lol.
Halafu aje kurudi tena baadae au.......... Ndio itakuwa imekula kwake.
Lakini hilo hapana......... Ni vile nadhani ameona sijui simpendi kwa kufikiria kwamba ningemfanyia hivyo. Yani hata sijui nimekereka mpaka basi.
Sijakuelewa kabisa... yani ulikuwa unataka nimdanganye tu kumridhisha kama angekuwa amenifanyia huo upuuzi!!.
Aah! wanawake mmezidi bana... yani nyie mnapenda kudanganywadangaywa tu........ hampendi kuambiwa ukweli hata pale inapobidi!!.