Siyo sahihi kila mradi mkubwa kuuita jina la Nyerere

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Sidhani kama nchi hii iliasisiwa na Nyerere peke yake na kwa kweli nchi hii haikujengwa na Nyerere peke yake katika miaka hiyo 60 iliyopita.

Lakini kabla ya hapo tulikuwa na baadhi ya machifu wetu na makamanda mashujaa kabisa akina Kinjekitile Ngwale, Abushiri, Kimweri na wengine ambao walipambana na ukoloni.

Leo hii almost kila mradi mkubwa unapewa jina la mwalimu ina maana Taifa hili lina uhaba wa heroes wa kuwaenzi?

1. Campus ya Mwalimu Nyerere
2. Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere
3. Chuo cha Mwalimu Nyerere
4. Barabara ya Mwalimu Nyerere
5. Ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere
6. Daraja la Mwalimu Nyerere
7. Viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere
8. Na leo bwawa la umeme linalojengwa litaitwa Bwawa la Mwalimu Nyerere

Tunampenda Mwalimu lakini tukumbuke nchi hii ina mashujaa wengi, Hebu tuanze kuenzi na wengine pia
 
Wazo zuri na wapo wengi walio hai na waliotangulia pia wenye kustahili majina yao kuwepo katika historia ya ujenzi wa nchi hii.

Labda wewe ulipenda tumhenzi nani katika ujemzi was mradi huu ? Mhe. Rais alitoa tuu pendekezo.
 
Na sisi wengine tunawaza kuanzisha chama Cha CCN
 
Sidhani kama nchi hii iliasisiwa na Nyerere peke yake na kwa kweli nchi hii haikujengwa na Nyerere peke yake katika miaka hiyo 60 iliyopita.

Lakini kabla ya hapo tulikuwa na baadhi ya machifu wetu na makamanda mashujaa kabisa akina Kinjekitile Ngwale, Abushiri, Kimweri na wengine ambao walipambana na ukoloni.
Hao machifu walijenga Tanzania au makabila yao?
 
Sidhani kama nchi hii iliasisiwa na Nyerere peke yake na kwa kweli nchi hii haikujengwa na Nyerere peke yake katika miaka hiyo 60 iliyopita.

Lakini kabla ya hapo tulikuwa na baadhi ya machifu wetu na makamanda mashujaa kabisa akina Kinjekitile Ngwale, Abushiri, Kimweri na wengine ambao walipambana na ukoloni.

Leo hii almost kila mradi mkubwa unapewa jina la mwalimu ina maana Taifa hili lina uhaba wa heroes wa kuwaenzi?

1. Campus ya Mwalimu Nyerere
2. Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere
3. Chuo cha Mwalimu Nyerere
4. Barabara ya Mwalimu Nyerere
5. Nyumba ya mikutano wa Mwalimu Nyerere
6. Daraja la Mwalimu Nyerere
7. Viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere
8. Na leo bwawa la umeme linalojengwa litaitwa Bwawa la Mwalimu Nyerere

Tunampenda Mwalimu lakini tukumbuke nchi hii ina mashujaa wengi, Hebu tuanze kuenzi na wengine pia

Unapungukiwa nini
 
Hili jambo tumeliongelea miaka mingi iliyopita

Kwa wenzetu, ''landmarks'' zina utaratibu wa kupewa majina na ''kamisheni'' maalumu
Sijui kama tuna ''kamisheni' hiyo au la, sina uhakika.

Kuna wakati jina la Nyerere linatumiwa vibaya au kisiasa.
Ramani ya bwawa ilikuwepo kabla ya Uhuru. Stiegler gorge ni M-Swiss

JokaKuu
 
Hilo jina la Kiswis kuna makabila kutamka ni shida.
 
Huko aliko anaumia sana
Mshana, unajua sasa hivi sisi sote tumekuwa kama ndezi.
Majina yanatolewa kwa watendaji ambao bado wako hai kama Daraja LA Mfugale nasi tunashangilia.
Hivi kesho tukigundua Mfugale kumbe ni fisadi kwenye hii miradi anayopewa kusimamia katupiga mamilioni ya dola na tukamfunga jee tutaendelea kuita daraja lile Mfugale?
Ni vema majina yatolewa kwa wale mashujaa wa nchi wa zamani kwani kwa sasa hakuna rekodi yao inayoweza kutolewa tena ikiwa negative.
Halafu majina haya huwa yanatolewa na kamati fulani hivi inayojadili sababu, lakini siku hizi naona kazi hiyo ameibinafsisha mwenyewe Rais.
Halafu na mtoto naibu kaanza naye kutoa mitaa nasikia mmoja kampa Samatta. RC kajigeuza baraza la madiwani!! Hopeless kabisa
 
Back
Top Bottom